Tanga: Mwalimu ajinyonga kisa wivu wa mapenzi

Tanga: Mwalimu ajinyonga kisa wivu wa mapenzi

NOMA SANA...

Haya mapenzi bwana.
pole kwa familia.
 
We ndio una shida na walimu, hujamsikia yule daktari wa kike Kibosho kule Moshi?
20240509_112737.jpg
 
Nani mwenye hela? Si afadhali ye ana kamshahara? Kudharauliwa ni we kujitakia watu wangapi waķo chini yake kiuchumi?
Pasi na shaka wewe ni teacher na ndio maana kila comment humu umeichukulia personal.

Ila angalia usije jinyonga na wewe ukishajibiwa ovyo maana mmekuwa very sensitive siku hizi.

Kaanga visheti vya kwenda kuuza darasani kesho.
 
Mwalimu Enock Peter (32) wa Shule ya Msingi Potwe wilayani Muheza mkoani Tanga, amedaiwa kujinyonga kwa kutumia shuka nyumbani kwake, wakati Kesi yake dhidi ya anayedaiwa kuwa Mpenzi wake ikiwa Mahakamani.

Leo Jumatano Julai 16, 2025, Mratibu Elimu Kata ya Pongwe, Rajabu Msuya amesema alifika shuleni kwa mwalimu huyo kwaajili ya kufanya kikao ambapo alimu wote walikuwepo kasoro mwalimu Enock.

“Nilimtuma mwanafunzi aende nyumbani kwake akamuite, lakini aliporudi akasema amegonga lakini hakuitikiwa. Baadaye mwalimu mwingine alienda naye, wakagonga bila kuitikiwa, akaamua kuchungulia dirishani ndipo akamuona mwenzetu amejinyonga,” amesimulia Msuya.

Amesema baada ya kubaini hayo, walitoa taarifa polisi na askari walifika na kuingia ndani na kukuta amejinyonga kwa kutumia shuka aliyoifunga kwenye mbao za juu ya paa la nyumba ya shule aliyokuwa akiishi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi.

Soma Pia: Geita: Mwalimu ajinyonga kisa migogoro ya kifamilia

“Katika uchunguzi wetu tumebaini marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake (jina limehifadhiwa). Waliwahi kugombana na alichana vyeti vya mwenza wake na kesi ilikuwa inaendelea mahakamani. Wakati kesi ikiendelea, ndiyo mwalimu huyo ameamua kujinyonga,” amesema.

Amesema Enock alishawahi kukamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani akituhumiwa kwa uharibifu wa mali za mwenza wake na aliachiwa kwa dhamana huku kesi ikiendelea.

Shuhuda wa tukio hilo, Abdulrazaq Kikungo amedai siku mbili kabla ya kujinyonga, Enock aligombana na mwenza wake baada ya kudai kumkuta na ujumbe wa mapenzi kwenye simu. Alimtishia kumuua kwa kisu, jambo lililomfanya mwenza huyo kukimbia.
View attachment 3408312
“Baada ya mpenzi wake kutoroka, Enock alichukua kisu na kukatakata baadhi ya vyombo, kuvunja kabati na kuchana vyeti vya chuo vya mwenza wake. Alishtakiwa polisi na alikamatwa, akaamriwa kulipa gharama za vyeti.”

Amesema wakati mvutano huo ukiendelea na kesi ikiwa mahakamani, jana ndipo waligundua mwalimu huyo amejinyonga, wakihisi chanzo ni wivu wa mapenzi.

“Baada ya ugomvi huo, Enock alikuwa hatoki nje. Mchana alikuwa anakaa ndani pekee yake, usiku kidogo ndio anaenda dukani kununua mikate au viazi."
Walimu bhana...Wengine wanajiua, wengine wanaiba mahindi na maharage!
Screenshot_20250715_080802_Instagram.jpg


Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Haya ndio madhara ya kupeleka watu shule.

Shule inafundisha mtu kuwaza sio kufikiria.

Watu wengi waliofaulu shuleni hua wanashindwa kufikiria bali wanawaza ndomana wanakua na stress hata jambo dogo wanaona kubwaa.

Mtu anaefikiria hawezi kujinyonga kisa Utelezi, dunia ni bustani ilojaa warembo hivi unaenda kujinyonga kisa pimbi mmoja.
 
Back
Top Bottom