TANGA: Mvua kubwa iliyodumu kwa siku nzima yaleta maafa

Salam wakuu,

Mpaka naandika bandiko hili Muda huu, mvua kali sana bado inashuka eneo la Tanga mjini na vijana vyake. Ni mvua ambayo Kama ikiendelea kupiga namna hii non-stop basi Kesho tutegemee mengine kwenye front pages. Haijakata tangu saa9 usiku wa kuamkia leo na hapa bado inapiga.

Maafa (ambayo hayadhibitishwa na mamlaka rasmi):

1. Mtu mmoja amoteza maisha eneo la kange baada ya kusombwa na maji
2. Nyumba tatu zimebomoka
3. Barabara ya makorora imafungwa na mamlaka ya jiji kuepusha maafa. (Hii imedhibitishwa)

Waungwana sala zenu zinahitajika kwa wana Tanga. Hii mvua tunayoiomba tunaomba iwe na kiasi...

Amen.

UPDATES:

Barabara ya kuelekea kasera imefungwa na hivyo waliopo eneo Hilo ni Kama wapo kisiwani. Ninavyoandika hapa, wanamaji na polisi wamefika kuwapa pole wahanga ambao wapo upande wa pili wa barabara, (walikuwa wanatoka mjini kwenda kasera). Na wamekwama. Kwa hesabu ya haraka hawapungui watu Mia mbili. Ni janga


Wakazi wa Sahare beach wako mbioni kufutwa kwenye ramani ya tanga ikiwa mvua hii itapiga kwa masaa mengine manne mfululizo kuanzia sasa.

Maeneo korofi Kama kwanjeka na mikanjuni Kesho watahitaji usafiri mbadala kutoka makwao. Sala zenu waungwana.

Umeme umekatika.... Kwa Hali ilivyo Nadhani kuna nguzo itakuwa imeanguka. Tusubiri tamko.
Acheni mvua itiririke ili mwaka kesho tusipate shida ya mahitaji ya vyakula, kwa wale waishio mabondeni ni lazima wapate majanga kwani kila mara huambiwa wahame lakini hawaelewi.
 
Tumeshakua isolated.. Ni kama kisiwa..hii Barbara ya Tanga beach haipitiki..naona baadhi ya watu wakihaha kuhamisha vitu..nyumba zimezingirwa na maji..nashuhudia Jirani yangu hapa akitoa msaada wa malazi kwa mama mmoja..bado ni usiku mwingi tuendelee kuomba ipungue.
 
Tumeshakua isolated.. Ni kama kisiwa..hii Barbara ya Tanga beach haipitiki..naona baadhi ya watu wakihaha kuhamisha vitu..nyumba zimezingirwa na maji..nashuhudia Jirani yangu hapa akitoa msaada wa malazi kwa mama mmoja..bado ni usiku mwingi tuendelee kuomba ipungue.
Mkuu nilisema ikipiga masaa manne non stop hapo sahare beach lazima kueleweke. Polemic asee.
 
Barabara ya kuelekea kasera imefungwa na hivyo waliopo eneo Hilo ni Kama wapo kisiwani. Ninavyoandika hapa, wanamaji na polisi wamefika kuwapa pole wahanga ambao wapo upande wa pili wa barabara,

Does it help anything, kwakweli bado tupo nyuma sana,

Yaleyale ya kule dimbwi la Mlimani city alikotumbukia mtoto na kufariki, kikosi cha uokoaji kilikwenda na gari la zimamoto na kijiti
 
Vipi maji hayajaa Amboni kwenye mapango? Hii itazuia wale wanaojificha huko au?
 
Kaka Niko donge mwisho hapa mpaka najiuliza hii ni mvua ya aina gani inagonga non stop..mbaya zaidi bora ingekua ndogo ni mvua kubwa sana..jamani mtuombee
Waambieni viongozi wa dini waombe mungu mvua iache.kama walivyoomba mvua inyeshe.
 
Vipi maji hayajaa Amboni kwenye mapango? Hii itazuia wale wanaojificha huko au?
Jamani watu wa Tanga poleni sana. Hapo ndio nyumbani nilipozaliwa na kukulia.

Mapango ya Amboni (Kiomoni) hayawezi kuathirika kwa sababu mto Mkulumuzi utabeba maji yote kwenda baharini.

NGUZO wewe sio mtu wa Kiomoni kweli? Nina swahiba wangu pale.
 
Back
Top Bottom