Mangi flani hivi
JF-Expert Member
- Jan 2, 2016
- 2,026
- 3,104
Salam wakuu,
Mpaka naandika bandiko hili Muda huu, mvua kali sana bado inashuka eneo la Tanga mjini na viunga vyake. Ni mvua ambayo Kama ikiendelea kupiga namna hii non-stop basi kesho tutegemee mengine kwenye front pages. Haijakata tangu saa9 usiku wa kuamkia leo na hapa bado inapiga.
Maafa (ambayo hayadhibitishwa na mamlaka rasmi):
1. Mtu mmoja amoteza maisha eneo la Kange baada ya kusombwa na maji
2. Nyumba tatu zimebomoka
3. Barabara ya Makorora imafungwa na mamlaka ya jiji kuepusha maafa. (Hii imedhibitishwa)
Waungwana sala zenu zinahitajika kwa wana Tanga. Hii mvua tunayoiomba tunaomba iwe na kiasi...
Amen.
UPDATES:
Barabara ya kuelekea Kasera imefungwa na hivyo waliopo eneo Hilo ni Kama wapo kisiwani. Ninavyoandika hapa, wanamaji na polisi wamefika kuwapa pole wahanga ambao wapo upande wa pili wa barabara, (walikuwa wanatoka mjini kwenda kasera). Na wamekwama. Kwa hesabu ya haraka hawapungui watu Mia mbili. Ni janga
Wakazi wa Sahare beach wako mbioni kufutwa kwenye ramani ya Tanga ikiwa mvua hii itapiga kwa masaa mengine manne mfululizo kuanzia sasa.
Maeneo korofi kama Kwanjeka na mikanjuni kesho watahitaji usafiri mbadala kutoka makwao. Sala zenu waungwana.
Umeme umekatika. Kwa Hali ilivyo Nadhani kuna nguzo itakuwa imeanguka. Tusubiri tamko.
Gari la magazeti ya Mwananchi lasombwa na maji Tanga

Mvua kubwa iliyonyesha mfulilizo kwa siku mbili,imevunja baadhi ya nyumba jijini Tanga. Na nyumba kadhaa kujaa maji, kimo cha kifuani. Mvua hiyo iliyonyesha kwa nguvu zaidi wakati wa usiku na upepo mkali, uliyosababisha, baadhi ya nyumba kuezuliwa mapaa.
Mitaa ya Tanga beach, kiboi, usagara, mzingani, nyumba nyingi zimefinikwa na maji,na wakazi wake kuokolewa na wasamaria wema, kwa kutupiwa kamba za kuwatoa majumbani. Maduka ya maeneo ya barabara ya jamaa na nyumba za maeneo hayo, maji yaliwaangilia mpaka ndani. Wakazi wa maeneo hayo, walikuwa wakionekana, wakitoa maji, kutoka kwenye nyumba zao, kwa kutumia ndoo.