Tanga miaka ya themanini lazima ulowee

madala mujipa

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
1,417
860
Amani iwe juu yenu
Ni mwaka 1980 niliingia mkoani tanga nikitokea mkoani kilimanjaro ndio kwanza nimetoka kuoa mke wangu mzuri

Dhumuni la kwenda tanga ni kufuata nazi za kibiashara kupeleka arusha na mwanza wakati huo nazi zilikua ni bidhaa adimu kwa mikoa hiyo

Nikapanda treni jioni nikafika tanga asubuhi,nikashuka pale stesheni nikaulizia lilipo soko kuu kuna mtu mmoja alikua amepakia ndizi kwenye mkokoteni kwa harakaharaka zile ndizi nilizigundua si za kula ni za kutengenezea mbege

Akaniambia mimi naelekea sokoni sema mimi nitakua kasi ila fuata njia hii utanikuta sehemu moja nimepunzika nakusubiri nikakubali kweli nilitembea mwendo kama dakika tano namkuta yule msukuma mkokoteni ameegemea mkokoteni huku akivuta sigara iliosokotwa kwa karatasi la gazeti,nilipomfikia akaniambia mgosi umefika eeh sema sasa hapa ni barabara ya saba inabidi unisukume ili nisikuache tufike pamoja nikasema sawa nitafanyaje nami nataka kufika sokoni

Kama dakika tano tena tukawa tumefika barabara ya kumi na mbili sokoni ngamiani yule mwenyeji wangu akaniambia mgosi hapa ndio mwisho wa safari tumefika mimi napaki palee ukiwa na shida utaniona hapa na palee ni stendi utakuta washona viatu na wapiga kiwi ni mangi wenzako mgosi sawa,kabla hajamaliza ikaita kijana wa kahawa akaniambia sasa kama anitania mangi kahawa uamke nikamuambia hapana,nionyeshe kijihoteli nijibanze nipate chai maana tangu nimekula jana akacheka kiutani ila akarudia kusema napenda kukuita mgosi twende pale kwa mama mwanamtama ukaonje chai iliopikwa kama pilau

Mmhhh kufika pale si hoteli ni uwani mwa nyumba,tulivyoingia tu yule mwenyeji akasema mama mwanakombo mpe chai mgeni wangu huyu mimi nitakuja kumchukua baadae,yule mama akajibu sasa na kulipa utalipa wewe au mwenyewe akajibu mwenyewe yule mama akasema nyoo ungesema utalipa ningekupa unyumba mchana kweupe mbuzi anakula majani

Akanikaribisha yule dada si mama kama yule anavyomuita ila si unajua tena,haya mgeni utakula nini ipo chai na maandazi,mkate wa kumimina ,chapati,vitumbua na half keki,maharage,kunde,choroko na mbaazi zote nazi,nipe chapati na maharage

Nikala nikalipa pesa yule dada akasema mchana na jioni pia napika karibu tena nikasema asante,sasa si umsubiri mgosi wa ndima kasema atarudi njoo ukae hapa ananionyesha sehemu anayokaa yeye akimaliza kuhudumia nikakaa kutokana na ile shibe na usiku sijalala nikaanza kusinzia

Yule dada kuona vile akaniambia vipi mgeni umefika hii asubuhi nikamjibu ndio,sasa umetoka wapi kwani nikasema moshi oooh wewe ni mchaga ndio wa kibosho sawa wewe ni mangi njoo huku ndani hapa ni nyumbani kwetu ila wazazi wangu wapo kule barabara 20 pumzika hapa akija mgosi wa ndima atakuamsha si unajua kazi zake za mkokoteni yawezekana kapata mzigo,nikakata shauri soko nimeshaliona na hapa nimeshapata pa kupunguza usingizi ni poa pia ila akili nyingine inauliza ukiibiwa akili ya usingizi ikasema wewe lala upo salama

Nikajilaza pale ukumbini yule dada alipa mto duuh usingizi mwana haramu kuja kushtuka ni saa nane mchana,fasta nikajipapasa nikajikuta poa maana hiyo pesa kuifikia pia ilikuwa kazi nina mapensi ya kodrai kama mawili nimeyavaa ndio nikavaa suruali juu,nikatoka kule uwani yule dada akasema mangi umeamka mgosi amekuamsha mpaka nikamwambia akuache naona umechoka sana,..ndio dada,nionyeshe msalani nenda mlango ulee akanielekeza kwa kidole..mimi sawa

Nikaingia mle chooni mmh nakuta kuna kibao cha mbuzi na korokoro nyingine nafsi inajiuliza isije kuwa ni chumba usiku kuna mtu kapangishwa,

Haya utakula nini sema nimekufunikia wali na samaki wa nazi ukimaliza twende hapo sokoni nikuache kwa mgosi na mimi ninunie mahitaji ya jioni,akaniletea chakula wakati ninakula na sijakaa kule green stand nipo vip akaingia mtoto...akauliza mama huyu ni nani yule dada akasema huyu ni mjomba wako mangi anakaa huko moshi..mjomba shikamoo na mimi utanichukua moshiii eeh wacha nikamwambie kisua na sisi tuna mjomba wetu mangii

Nikacheka kidogo lakini kwa aibu si unajua meno yote hina...nikamwambia dada nimemaliza akaingia ndani akatoa glasi akanipa maji,akavaa vazi lake jeusi la kufunga kidevuni baadae niligundua ndio baibui si kama haya ya kihindi

Basi tukafika sokoni hatukumkuta mgosi ila akampa maagizo mzee mmoja...mzee mwanyiro huyu ni mgeni wetu akija mgosi utamshtua na wewe kaka pale nyumbani si unakumbuka..nikajibu ndio..dada akaongeza muda huu huyo mgosi saa hizi yupo kwenye vibanda vya gongo..

Nikabaki na mwanyiro kulingana na biashara niliofuata yaani kama yule dada alijua,mzee mwanyiro akaniuliza mimi ni mwenyeji wa wapi nikamjibu na dhumuni langu,akaniambia vyema kwa kuwa umeletwa na mwanangu nisubiri kama siku tatu twende pangani zinakotoka nazi ili nikienda nikapate faida nzuri

Nikafurahi na ushauri wa mzee,mgosi alirudi muda ukawa umekwenda ni time za kufunga soko,aaah mgosi na wewe ugenini unalala vile na umekubali kuingia ndani umekwisha wewe huku anacheka,lakini nilimuona akiwa juu ya sayari nyingine

Basi twende kwa mwanakombo upate cha jioni tukalale palee stend kwenye banda la kusubiri wageni..mgosi sina chumba nimeacha mke na watoto bumbuli lushoto kuja kutafuta kwenye mji wa wadigo..najiuliza sasa nitaenda kulala pale bandani wakati nina pesa

Tukafika pale nyumbani...yule mmh dada mmhh teh mgosi kumbe ndivyo ulivyo hivyo umemchelewesha baba wa watu,majibu ya kilevi sasa haya ndio nishamleta hivyo tena na ameniambia hana pa kulala si unajua mimi nalala wapi sema usimlaze ukumbini unakolaza wasambaa wako wa kahawa...eehehehe mgosi unavisa wewe mwenyewe si anamdomo mpaka umsemee..mwaya kaka achana na mgosi wa ndima kesha utwika huyo akaniita halo mangi akaninong'oneza nakwenda kwa wahaya nishaunganisha hapo pa kulala hakuna shaka mimi sawa

Nilikuwa nimevaa raizoni zangu nikavua nikaletewa mkeka nikaletewa chakula kimefunikwa kwenye kawa limeandikwa dondoa taratibu ni zako zabibu..nikamaliza dada akaniuliza hays mgeni wewe leo utaenda kulala wapi..sikuwa na jibu zaidi ya nionyeshe loji ya karibu..dada akafikiria kama sekunde kumi akasema haya inuka nifuate

Niliingizwa kwenye chumba chenye harufu nzuri juu ya kitanda japo mwanga wa chemli ulikuwa hafifu kutokana na nyumba kutounganishwa umeme lakini niliweza kuona maua ya waridi yaliomwaga kiufundi pale kitandani..mhh nikajisemea makubwa haya mtu utalalaje hapa

Nikawa nimekaa kwenye kiti pale chumbani..haya mangi vua hizo nguo zako ukajimwagie maji uondoe mavune na uondoe harufu ya huko moshi alinitania kidogo...mmh nikatoa suruali mtihani ni zile pensi za pesa unaona aibu haya kanga hii hapa..akaniambia kaka ya mombasa hii haivaliwi hovyo hovyo nikaiangalia naona ina picha ya jipanzi kubwa

Basi akaniambia naona unaogopa haya twende na makaptura yako kama askari wa mzungu nikafika kule chooni nakuta vitu vimeongezeka na kuwekwa taa ya kibatari..nikamwambia haya pisha nioge akaniambia teeh mangi una umri gani,hebu vua hayo magwanda yako,kishingo upande nikavua..haya nenda pale kakojoe nikatii amri

Nikaambiwa haya simama hapa naye akatoa kanga yako nikaona mapigo moyo yamesima maneno ya mgosi yangonga umekubali kuingia ukumbini umekwisha..akachukua kikombe kukubwa kuna ndoo tatu kubwa za plastic akatoa maji katika zile ndoo mbili akajaza moja na nyingine akafanya hivyo

Akanimwagia yale maji eeeh yana uvuguvugu na harufu ya kuvutia hakyanani baba angu sijawahi oga hivyo akaanza nipaka sabuni na dodoki akanisugua akaniambia haya kaa hapa nikakaa kwenye kile kibao cha mbuzi akaniwekea kisahani kwa chini mhh narogwa sasa na yeye akakaa upande wake akaanza kusugua nyayo zangu

Kumaliza pale akanifunga kaka ya kishingo shingo nikabebwa kama mtoto na nguo zangu ameshika yeye mpaka chumbani akaniambia kaa hapo,akafungua sanduku lake la mbao akatoa kajimkebe na akachukua mkeka na mto akatindika akaniambia lala hapo kwenye mkeka nikashukuru akaniambia mmh mangi huko kwenu hanyoi akanitoa ile kanga

Akaanza kuninyoa huku nikihisi aibu hii habari hata mtu mmoja kule moshi sijawahi msikia nayo,baada ya hapo kuna vijiti akachukua akaanza kusugua na kijiwe akaanza kutia kwenye kisahani cha chai akanipaka usoni na mwilini huku akiendelea kunisugua nilihisi raha ilioje

Baada ya hapo akaniambia haya lete hizi nguo zako tuziroweke ili kesho ufue nikaona amechukua raizoni zangu akazitupa juu ya dari,akaanza kufanya hesabu zake za biashara mimi bado nipo pale kwenye mkeka nimelala hakuzificha zile zake mbali aah na mimi nikaona nimkabidhi yeye aziweke,basi akamaliza nikaona sasa yale maua yanaondolewa kitandani ile kanga nikavuliwa duuh kwa kuwa mimi ni mwanaume rijali mpini umekongooka

Nikataka kuparamia kama kule kwetu moshi akaniambia aaah mbona huna staha mara unataka kama kudandia mi sijui ndio najua hilo dada yule ndio akawa mwalimu wangu,ilipofika asubuhi duuh nguo zipo kwenye maji nitafanyaje mara namsikia mgosi wee mwanakombo mgosi yupo wapi..akajibu yupo ndani duuh si ndio amefika huyo nitamcheki baadae kuna mzigo napeleka soko la uzunguni..nikaa mle ndani nikaletewa chai kawa limeandikwa mkarimu mgeni,nikanywa nikisubiri nguo zikauke

Zilipokauka nikavaa nikaenda kwa mzee mwanyiro kidogo mara mgosi nae akafika vipi rafiki yangu mambo jana danga chee haya twende huku..tukatembea kama hatua tatu.. akaniambia mwanakombo amenipa pesa ukanunue nguo ubadili

Nikamjibu sawa nikaenda kujichagulia vinyuli vipadeo vyangu kwa wahindi,siku ya ahadi ya mzee mwanyiro kulinyesha mvua isiyo na kipimo barabara zote zikawa hazipitiki nikaona nimjulishe yule dada dhumuni langu akaniambia kama itashindikana kwenda baba yake ni dereva wa treni atafanyiwa mpango wa kazi railway,na moshi asirudi tena kwakuwa amenipenda ile mvua ilinyesha kama wiki nzima na ndio ikawa mwisho wa biashara na kulowea tanga nikafunga ndoa na mdigo,nikapata machotara yangu.

Nasikitika hivi sasa nikisia tanga hakuna mapenzi tena lakini wengi walioingia kipindi hicho hawakutoka

Aksanteni usipime tanga ya zama hizo
 
Mwaka 2003 kwa mara nakanyaga Tanga nilikwenda kwenye mradi wa Malaria nikpangiwa kituo Muheza nikapiga kama mwezi ivi then nikahamishiwa Tanga mjini huu mradi nilitakiwa nikae miezi 3 tu nirudi zangu Dar ila yaliyonikuta kule niliapa lazima nikafanye kazi milele Tanga,kaka Tanga mapenzi yapo mpaka kesho na sio wa bara tu yanayowakuta hata sisi wa pwani pia mfano mimi mpaka naenda Tanga nilikua sijawi kuishi bara ila nilivurugwa ila bahati yangu nilikua bado kijana sana ndio naanza hustle hua nikipata nafasi naenda TA nakaa hata wiki ni kati ya sehemu ninazozipenda.
 
Mwaka 2003 kwa mara nakanyaga Tanga nilikwenda kwenye mradi wa Malaria nikpangiwa kituo Muheza nikapiga kama mwezi ivi then nikahamishiwa Tanga mjini huu mradi nilitakiwa nikae miezi 3 tu nirudi zangu Dar ila yaliyonikuta kule niliapa lazima nikafanye kazi milele Tanga,kaka Tanga mapenzi yapo mpaka kesho na sio wa bara tu yanayowakuta hata sisi wa pwani pia mfano mimi mpaka naenda Tanga nilikua sijawi kuishi bara ila nilivurugwa ila bahati yangu nilikua bado kijana sana ndio naanza hustle hua nikipata nafasi naenda TA nakaa hata wiki ni kati ya sehemu ninazozipenda.
Ni kweli kule karakana ya gari moshi na bandarini kulijaa walowezi wengi tu kweli walituteka
 
Yule ndio nilimsahau tena mke anastazia nilikolea wali nazi maharage ya kupaka unani weweee ah
Be proud of your wife no matter what.......ulimuoa kwa kuwa ulimuona she was perfect for you......yani kwa kuwa ulibebwa ndo umuache mdada wa watu....not fair
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom