Tanesco yailipa REX Attorneys zaidi ya bilioni 7... Wapi sheria ya manunuzi??

na mwenzake pia ni Mkono& Mkono advovates ambaye akishachota Mabilioni anakwenda na vimilioni na kutoa msaada jimboni kwakwe halafu tunashangilia kuwa huyu ndiye mbunge makini maana haongei Bungeni bali kuwa na vitendo kumbe vitendo vyenyewe ni kutugaiwa kiduchu cha fedha zetu anazotuibia, hivi tumelogwa??
Tumelogwa ndio, na wachawi ni sisi wenyewe!.
 
serikali legevu,ujambazi wa wazi wazi,REX attorneys ni njia ya kuibia watanzania kama ilivyokuwa mkono and co.
taasisi ya umma inatumia wanasheria wa bei kubwa,kwani office ya mwanasheria mkuu haina wanasheria wa kutetea taasisi za umma,au ndio tuseme wanasheria wa serikali ni vilaza wote.siamini ktk hilo
hapa kilichofanyika ni maandalizi ya kukwapua mabilioni ya pesa za watanzania
 
akitangaza kufutwa kwa mkataba wa Dowans waziri mkuu alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kupata ushauri wa kitaalamu toka Rex attorney ambao wamebobea kwenye mikataba ya kimataifa,baada ya Tanesco kushindwa kesi Rex attorney hao hao ndiyo waliiambia Tanesco hamna jinsi zaidi ya kulipa lakini wakati wanaipa ushauri serikali na pia kuitetea Tanesco rex attorney ndio walioiandkia barua Dowans barua ya dhamana ili kupata mkopo benki.kisheria ili jambo halikubariki.Waziri mkuu ni mwanasheria,mnadhimu mkuu wa serikali ni mwanasheria hivi wameshindwa kuona hilo tatizo.
hii kampuni ni ya kitapeli na inatakiwa ifunguliwe mashitaka kwa kuipotosha Tanesco ingawa naona watendaji wake wanazidi kupewa vyeo na juzi juzi tumesikia mmoja wao akiteuliwa kuwa bodi memba wa bodi ya kahawa wakati huo huo kampuni hiyo hiyo inahusika na kusimamia uuzwaji wa jengo la KNCU
na bado wanatudanganya na mradi wao wa kuchangia madawati
 
Hapa kwetu inaonekana kila chombo cha udhibiti wa mienendo na maadili kiko likizo.Kwa yeyote ambaye akifuatilia mwenendo wa hawa Rex Attormeys atakubaliana na mimi ya kuwa kuna tuuma nyimgi zinazoelekezwa kwao kuhusu ukiukwaji wa maadili ya kazi zao; kwa mfano katika suala la Dowans, ulitolewa ushahidi uliothibitisha kwamba wanasheria hao wamekuwa wakishauri kwa wakati tofouti Dowans na Tanesco juu ya suala lile lile. Baya zaidi ushauri ambao wamekuwa wakitoa kwa Tanesco umekua ukilemga kufaidisha Dowans. Dhahiri kitendo hicho ni ukiukwaji mkubwa wa "professional ethics". Hivyo ilitegemewa chama cha wanasheria Tanzania kingeliingilia kati ili kubaini undani wa jambo hilo, lakini mpaka sasa kiko kimya. Kama hiyo haitoshi hivi karibuni mwanasheria mmoja kutoka kampuni hiyo aliteuliwa na rais kuwa mwenyekiti wa kampuni anayoishitaki yeye mwenyewe kwa niaba ya mteja fulani. Pamoja na jambo hilo kupingwa kwa nguvu zote na baadhi ya wabunge hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na chama hicho,
 
Back
Top Bottom