TANESCO wanataka ninunue transformer

🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mimi pia niliambiwa hivyo Wilaya ya kibaha,eneo linaitwa Boko Mnemela.Niliambiwa ninunue transfoma ili waniwekee umeme
 
Kisa cha muwekezaji mzawa wa kiwanda kidogo cha kubangua korosho mtwara nae alizungushwa miaka mitatu wakimdai anunue transformer hadi JPM alipofika kwenye ziara ngoma ikabuma kwahiyo visa hivyo ni vingi sana na havipendezi, bado bado mambo hayajakaa sawa
 
Unakumbuka wakati wa kununua nguzo? Ni mambo kama hayo, ila ni wajibu wa Tanesco
 
Kwa wale tuliolipia laki 3 kuunganisha umeme wakati bei elekezi ya elf 27 ilishatamkwa na waziri, ni lini tutarudishiwa chenji zetu au walau kupewa fidia ya unit za umeme.........
 
Kusema ukweli niliambiwa kwa mdomo sio kwa barua, sikuwahi kupewa barua
Ni vigumu kusaidiwa kama huna vielelezo. Cha kufanya, anza mchakato upya; waandikie barua yakuomba kuunganishiwa umeme, ukiambatanisha na michoro ya umeme wa jengo lako
 
Kosa lilianza kwenye uchaguzi wa saiti ya ujenzi wa mradi wako. Ungepata ushauri kabla. La sivyo kama miradi wa umeme ulikukuta!
 
Hicho kichwa Cha habari nimecheka kinoma[emoji1], hiv mkuu unajua bei ya transformer? Yan hao wahuni kama hawatak kukuletea umeme wakwambie tu
Wanataka hela ya ku brashia kiatu hao
 
Kitaalamu hauwezi kujibu swali kwa ujumla wake bila kujua ukweli wa taarifa husika, kujibu hivyo ni blabla ambayo taasisi yenye wataalamu kama yetu haiwezi kukurupuka kujibu bila taarifa kamili
Mbona unajibu kimipasho wewe na hao wataalamu mnafanana tabia, changamoto ya mteja unaita blah blah aisee!?
 
Mbona unajibu kimipasho wewe na hao wataalamu mnafanana tabia, changamoto ya mteja unaita blah blah aisee!?
Tafadhali pitia tena maelezo yetu ukiyasoma vizuri utaelewa tulichomaanisha, mteja aliyelalamika tumeshawasiliana naye Dm Na tumefikia pazuri
 
Mpaka sasa hakuna taarifa kamili za kuweza kudhibitisha hilo hivyo tunaomba uvumilivu na lugha nzuri ili kuendela kuheshima watoa huduma.
tutaheshimu vip kama wenyewe hawaheshimu wateja?
 
tutaheshimu vip kama wenyewe hawaheshimu wateja?
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…