TANESCO wanataka ninunue transformer

TANESCO wanataka ninunue transformer

MKARASINGA

Senior Member
Joined
Jun 9, 2018
Posts
149
Reaction score
237
Habari, Mimi ni mkazi wa Morogoro vijijini. Biashara yangu ni ya kukoboa zao(silitaji kwa sababu binafsi) ni mwaka wa tatu sasa nafuatilia kuwekewa umeme katika kiwanda hichi kidogo maana natumia diesel lakini gharama nnazopewa ni zaidi ya milioni kumi, ikiwemo na kununua transform.

Wataalam hili suala limekaaje maana nashindwa kuelewa. NINUNUE transformer kivipi wakati ni wajibu wa TANESCO kutupatia huduma kwa malipo husika ya huduma hi.. na ugumu wa kuwekewa umeme unakuja wapi jamani. MSAADA
 
Habari, Mimi ni mkazi wa Morogoro vijijini. Biashara yangu ni ya kukoboa zao(silitaji kwa sababu binafsi) ni mwaka wa tatu sasa nafuatilia kuwekewa umeme katika kiwanda hichi kidogo maana natumia diesel lakini gharama nnazopewa ni zaidi ya milioni kumi, ikiwemo na kununua transform
Kama utakumbuka Maelekezo ya Serikali hapo awali hakuna mteja anayepaswa kununua kifaa chochote cha kumfungia umeme bali ni jukumu la TANESCO kusogeza miundombinu ya umeme kwa wateja wake, tafadhali tusaidie taarifa zifuatazo

Jina

Namba ya Simu

Wilaya

Na kiasi ulichodai kuambiwa ulipie ili tukupatie ufafanuzi kwa taarifa kamili

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

MAKAO MAKUU
 
Kama utakumbuka Maelekezo ya Serikali hapo awali hakuna mteja anayepaswa kununua kifaa chochote cha kumfungia umeme bali ni jukumu la TANESCO kusogeza miundombinu ya umeme kwa wateja wake, tafadhali tusaidie taarifa zifauatazo...
Kwa hiyo Meneja wa wilaya husika hajui huu utaratibu?
 
Mimi pia naona hawataki. Ila kwanini wakatae ikiwa ni jukumu lao na Mimi ni haki yangu kupewa huduma hiyo.
 
TANESCO majibu ya huyu mteja wa transformer mngeyaleta hapa jukwaani...
 
Back
Top Bottom