TANESCO: Taarifa kwa Vyombo vya Habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO: Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Aug 17, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuuarifu umma kuwa mitambo mipya ya kuzalisha umeme ya Megawati 100 iliyoahidiwa bungeni na Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa William Ngeleja, imewasili nchini leo [12 August] na kazi ya kuifunga inaanza mara moja. Mitambo hiyo iliyokodiwa kutoka Kampuni ya Aggreko ya Mombasa (Kenya), itafungwa katika maeneo ya Ubungo na Tegeta jijini Dar es Salaam ambapo kila kituo kitazalisha Megawati 50.


  Umeme wa mitambo hiyo utaingia kwenye gridi ya Taifa mapema Septemba 2011. Mitambo hiyo itakayotumia mafuta itapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la mgawo wa umeme nchini kwa kuzingatia ukweli kuwa mitambo ya Jacobsen Electro Supply kutoka Sweden itakayozalisha Megawati 100 nayo imeshaanza kufungwa Ubungo. Awali TANESCO ilikuwa ikikabiliwa na upungufu wa Megawati 260.

  Hivyo kuwasili kwa mitambo ya Aggreko, kuwashwa mitambo ya IPTL inayozalisha Megawati 100, kutumika kwa Mitambo ya Symbion ya Megawati 112 na kuendelea kufungwa mitambo ya Jacobsen kunaipa TANESCO nafasi kubwa ya kumaliza tatizo la mgawo wa umeme mara baada ya kazi ya ufungaji wa mitambo hiyo itakapokamilika.

  TANESCO inapenda kuwahakikishia Watanzania kwamba inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa Mikoa yote iliyounganishwa katika gridi ya Taifa inapata umeme wa kutosha, sambamba na kupanua huduma ya usambazaji umeme kwa wateja wapya.

  Imetolewa na:
  Ofisi ya Mahusiano
  Tanesco: Makao Makuu

  http://www.tanesco.co.tz/index.php?option=com_remository&Itemid=214&func=startdown&id=381
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Bla bla
  Mpaka tutakapouona umeme umekuwa wa uhakika bado hizo ni taarifa tuu
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mi huwa navutiwa na hesabu na FIGA za megawati,hadi raha
   
 4. G

  GATZBY Member

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Habari za namna hiyo hazijaanza leo.
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  ... I love this this song !!!
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hiyo mikataba ya umeme wa dharura ndiko wanakojichimbia na ufisadi wao. Tutajua baadae how much is the cost.
   
 7. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  shukurani wa taarifa mkuu
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ningependa huo wimbo uwe unapigwa kila siku
  Mpaka bibi na babu kijijini wanajua hizo hesabu za magewatt japo hata umeme hawana
   
 9. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Tatizo kuu TANESCO haiaminiki tena kwani porojo zimezidi!!!!!
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kuanzia kuileta mpaka inafungwa na kununua mafuta ya kuitumia wanajua wameshakula ngapi
  na je mbona hatuambiwi ikiondoka au mkataba wa dharura ukiisha tunarudi kule kule au inakuwaje
   
 11. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwani megawati ndo nini wengine hatujui mi nachojua kuna volts za umemE au na je megawati zinaweza kutoa volti ngapi nahtj msaada
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  sina uhakika na habari hii mana cijaisikia kokote zaid ya hp jf. JE MTOA HOJA WE NI MFANYAKAZI WA TANESKO?UMEPATAPATAJE HABARI HII?
   
 13. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,108
  Likes Received: 7,366
  Trophy Points: 280
  Megawati inatokana au ni kifupi cha neno
  "Mgawo wa Dhati",
  Yaani watu wanapanga live kutugaia Mgao kwa dhati kabisa, bila hata kuoneana huruma,
  Umeelewa sasa??
  Kama hujaelewa ni-PM
   
 14. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Watuhakikishie je, gharama za umeme hazitapanda???????????K Kuendesha magenerator ya mafuta Haya ndiyo mambo yatakayo fukuza wawekezaji nchini kwetu, hata kama unataka kufunga kiwanda chochote kuzalisha kitu chochote kibiashara, gharama za umeme zitakutimua. Bora ukafunga kiwanda Rwanda unauhakika wa umeme wa bei nafuu, wachumi watanielewa!!!!!!!!!!
   
 15. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mbona kenya nao wanalalamika na mgao,halafu Aggreko ndo wanahamisha mitambo kutoka kenya!au ndo tunaletewa mabomu tu
   
 16. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Same song different tune
   
 17. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  mkuu MW kinachotakiwa ni sisi kununua hayo majenereta tuwenayo kuliko kukodi mbona rada na ndege ya raisi tumeweza hawa bwana wanaboa ni bora tusiwe na wizara ambayo haitatui matatizo ya watu wake..

  chengine hawa wah. huko bungeni naona wamelala mbaya hadi wengine wameshakata network nini kinaendelea tz na huyu ngereja naona anafikiria kimasaburi zaidi..
   
 18. only83

  only83 JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Sawa mkuu.......nadhani ni kawaida yenu..ngoja tuone..
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  Kwa kweli huu wimbo wa megawati umeimbwa sana na tanesco pamoja na wizara ya nishati na madini.
  Ukimsikiliza ngeleja anavyotaja megawati,ukija huku tanesco nao wanavyotaja megawati kweli raha mustarehe.
   
 20. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwani tatizo lilikuwa mitambo au ni ukame?
   
Loading...