TANESCO Simiyu Bariadi imekuwa kero sana

kamdudu

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
2,007
1,916
Habari Wanajukwaa wa JamiiForums ?

Natumai mko salaama.

Leo ni nina kero ya muda murefu sana kutokana na umeme wa huku Bariadi Mkoani Simiyu ambao umekua ukikatika na kurudi kila wakati kutwa nzima usiku kucha kama ka mchezo flani hivi.

Yaani umeme umaweza ukawaka kama dakika 30 hivi au lisaa limoja ukakata na ukarudi hapo hapo au baada kama ya sekunde 30 au dakika moja au ukakata ukipeleka mkono kwenye switch ili kuzima kwa kuepuka kuunguza vitu ile unaenda kugusa switch umeme huo ushawaka.

Hio umekua ni kama ka mchezo kwa miaka nenda rudi tulishaunguza vitu na tukaunguza tena na Malmaka ziko kimya kama vile hakuna kinachoendelea.

Tusaidieni kupaza sauti tujue nini mbaya maana imeshakua tatizo sugu Raia hata hatuelewi nini kinaendelea huko Tanesco.

Niwatakie jioni njema Nyote.
 
Back
Top Bottom