Maganga Mkweli
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 2,089
- 829
mkuu hizi ndio wanaita visioni twente twente 2020.......... Jamani sio kila jambo mnaliweka kisihasa daah wakati mwngine naingia uoga na uwezo wa wawakilishi wangu huko mjengoni ............mhando mtamuonea bure mtu wa watu. Nchi hii inaendeshwa kisiasa mno. Bila political will and support tanesco haiwezi kufanya chochote wala haiwezi kuthubutu kwenda huko unakokusema ili ikadai madeni. Zitapigwa simu na mwishowe waziri wa nishati atampigia mhando na kumuamru kuachana na hayo mambo ya kudai idara nyeti!
Nasema tena kwamba generator ziondolewe maofisi ya serikali: Kazi zisifanyike na posho zisilipwe. Generator ziondolewe kwenye nyumba za serikali. Generator ziondolewe ikulu. Generator ziondolewe kwenye nyumba za mawaziri wote ili watoto wao waone adha ya kulala bila viyoyozi wawalilie baba zao na mama zao. Wake/waume walie kwa kuwa usiku hawakulala usingizi mororo, kesho wakienda kwenye mkutano wa baraza la mawaziri watakuwa wana mawazo ya kutatua tatizo la umeme. Kuondoa generator kwa mhando ni tamko lisilo na chembe ya tija hata kidogo.