TANESCO Mwanza, kuna mgao rasmi unaendelea?

Leo usiku mzima mkoa wote wa Mwanza hauna umeme. Tangia saa 12 jioni. Na hakuna taarifa yo yote. Huyu meneja atumbuliwe haraka. Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu anataka wana mkoa wa Mwanza wamchukie kipenzi wao.


Ni kweli, lakini bado kuna watu wanatetea upuuzi, umeme unakatwa bila taarifa, taarifa ikitoka ni vizuri watu tunachukua hatua mapema.
 
Ndio mana tumeacha kuimba ule wimbo wa Tanzania ya viwanda
 
Mkuu tatizo hili haliko Mwanza tu,lipo hata mkoa wa Morogoro.Umeme umekuwa ukikatika Morogoro kati ya saa 10 jioni na saa 12,tena bila taarifa.No,TANESCO ipo shida.
 
Leo 17/03/2020 ndo funga kazi,wamekata kata hadi kero!
Saivi tuko gizani toka saa 1.40 jioni saivi ni saa 2.45 usiku gizaa.
Wapigie huduma kwa wateja usikie majibu yao..." Hata sie hatuna umeme vumilieni tu utarudi".... Enzi za awamu ya nne japokuwa kwa sasa ni mgao wa kinya kimya.
Kalemani sijui analijua hili!
Au wamesambaza sana umeme wa REA kiasi umeme hautoshi lazima kuwe na mgao wa kimya kimya......
In general TANESCO especially Mwanza is boring.
Jana tarehe 16/3/2020 muda wa saa 130 usiku ghafla umeme ulikatika hapa Mwanza. Umeme umerudi mnamo saa 1.40 leo asubuhi tarehe 17/3/2020. Ni vema tukaelezwa sababu za kukatika kwa umeme usiku mzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mpendwa mteja wetu

Tunakuomba utusaidie taarifa kamili za eneo na namba yako ya simu hata inbox kwa ufatiliaji na hatua zaidi

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunashukuru kwa taarifa tafadhali tusaidie namba yako ya simu kwa hatua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulia huyu ndugu yako amekuwa ni mzigo, kwanini kila siku saa moja umeme ukatwe? hakna majungu, yeye afanye majukumu yake aone kama ataguswa. Sisi tunataka umeme hayo mengine atafahamu yeye na ndugu zake.
Juzi walikata saa moja usiku ukarudi saa moja asubuhi, ni zaidi ya kero bado saa sita mchana wakakata mpaka saa kumi ndio ukarudi tena
 
Leo usiku mzima mkoa wote wa Mwanza hauna umeme. Tangia saa 12 jioni. Na hakuna taarifa yo yote. Huyu meneja atumbuliwe haraka. Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu anataka wana mkoa wa Mwanza wamchukie kipenzi wao.
Je ulitoa taarifa ofisi yetu ya Mwanza? Tunakusihi unapopata hitilafu tupigie simu au pitia TANESCO APP au mitandao yetu ya kijamii kwa kuonyesha taarifa kamili za eneo simu wilaya na tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je ulitoa taarifa ofisi yetu ya Mwanza? Tunakusihi unapopata hitilafu tupigie simu au pitia TANESCO APP au mitandao yetu ya kijamii kwa kuonyesha taarifa kamili za eneo simu wilaya na tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani karibu mji mzima umeme unakatika Tanesco inakuwa haina habari hadi ipigiwe simu na individuals? Lazima kutakuwa na kitu hakijakaa vizuri kimfumo.
 
Yaani karibu mji mzima umeme unakatika Tanesco inakuwa haina habari hadi ipigiwe simu na individuals? Lazima kutakuwa na kitu hakijakaa vizuri kimfumo.
Kwanza mvua zinazoendelea mnaziona
Pili miundombinu ya tanesco nichakavu kipindi hiki nguzo zinaanguka line zinakatika nadhani ni kuwapa mda wakafuatiria meneja nae anaishi mwanza na watumishi wote wa tanesco wanaishi mwanza cdhani kama watajiweka nawao gizani huyu meneja nimpiga kazi na anajiwa wajibu wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mji Kama mz umeme kukata hata saa moja Ni hasara Sana,nimekaa huko mwaka Jana hii Hali haikuwepo au tuseme tatizo Ni mvua au?
 
Tunashukuru kwa taarifa tafadhali tusaidie namba yako ya simu kwa hatua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo hata mkipewa namba za simu hazitawasaidia isitoshe ni ishu inayowaadhiri watu wengi si individual issue kusolve so nice kweli kata yetu ya Nyasaka centre ikifika saa 12 jioni umeme unakatika kurudi ni asubuhi saa 1 au pia tunatoka majumbani kwa tochi kama vile mnatupimia umeme huu ni upuuzi mnafanya utafikiri tunatumia umeme wa jenereta kumbe Hydro inaonyesha umeme wa bwala la nyerere ukikamilika mtaendelea kuhujumu jitihada za Mheshimiwa.....
Mnaboa sana Tanesco siku mkizingua nitawaweka wazi wahujumu Tanesco Mwanza waliomuhujumu mama Eng. Assey list yao ipo hapo tutaua hii cancer
 
Ninaweza kuamini unayosema hapa.

Lakini hata yeye mwenyewe (Meneja), ashindwe hata kutoa taarifa tu kwa wananchi wake waelewe sababu za umeme kukatika?

Hilo ndilo lingekuwa jambo lake la kwanza kujihami na hao wanaomhujumu unaowasema.

Angalia huo ni udhaifu kwa upande wake. Akiacha wapiga majungu ndio wapaaze sauti huku yeye akiwa kimya; na huku yeye ndiye boss.
Sijui umenielewa?
 
Hapa wameshakata ndo tunakesha giza hawa popo wanna shida sana ila ngoja tutaelewana tu
 
Sawa lakini kwa nini msitoe taarifa kwa wateja wenu? Mbona zamani mlikuwa mnatoa taarifa? Au siku hizi huyo afisa mahusiano anafanya kazi gani?

Halafu mbona leo kulikuwa hakuna mvua lakini umeme umekatika tena kuamzia saa 1 usiku? Na hatutegemei kwamba utarudi hadi asubuhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…