Ndugu Mpendwa Mteja wetu
Tumefuatilia malalamiko husika, na mrejesho ni kama ifuatavyo: -
1. Mkoa wa Mtwara hauna wafanyakazi wa kazi maalumu (STE) wanaofanya kazi za ufundi ambao wameajiriwa na TANESCO moja kwa moja.
2. Kiuraratibu ikitokea uhitaji wa wafanyakazi wa kazi maalumu, Mkoa husika huingia mkataba na Serikali ya Kijiji / Mtaa ambao kazi zitatekelezwa.
3. Kazi zikikamilika Serikali ya Kijiji / Mtaa husika hulipwa kulingana na mkataba walioingia.
4. Kwa sasa STE wanaofanya kazi huko (Mtwara) ni wale wanaoajiriwa na Vijiji na hakuna malipo yeyote ambayo TANESCO inadaiwa. Kimsingi Mkoa wa Mtwara haudaiwi na vijiji tulivyofanya navyo kazi.
Kwa maelezo haya kama bado utahitaji ufafanuzi zaidi tafadhali tutumie taarifa zifuatazo hata inbox
1.Jina Kamili
2.Wilaya
3.Kiasi unachodai
4.Kazi uliyofanya
5.Namba ya simu
Kwa hatua zaidi
TANESCO Makao Makuu
25/08/2021