TANESCO Mtwara, walipeni vibarua posho zao kwa wakati

Twasha

Senior Member
Oct 26, 2015
170
133
Kilio cha vibarua kufanyishwa kazi ngumu badala yake kutolipwa kwa wakati posho zao. MKOJO WA MBWA)

Wahusika fuatilieni then wasaidieni ndugu zetu.
 
Tumepokea taarifa tafadhali tunafatilia
Ndugu Mpendwa Mteja wetu

Tumefuatilia malalamiko husika, na mrejesho ni kama ifuatavyo: -

1. Mkoa wa Mtwara hauna wafanyakazi wa kazi maalumu (STE) wanaofanya kazi za ufundi ambao wameajiriwa na TANESCO moja kwa moja.

2. Kiuraratibu ikitokea uhitaji wa wafanyakazi wa kazi maalumu, Mkoa husika huingia mkataba na Serikali ya Kijiji / Mtaa ambao kazi zitatekelezwa.

3. Kazi zikikamilika Serikali ya Kijiji / Mtaa husika hulipwa kulingana na mkataba walioingia.

4. Kwa sasa STE wanaofanya kazi huko (Mtwara) ni wale wanaoajiriwa na Vijiji na hakuna malipo yeyote ambayo TANESCO inadaiwa. Kimsingi Mkoa wa Mtwara haudaiwi na vijiji tulivyofanya navyo kazi.

Kwa maelezo haya kama bado utahitaji ufafanuzi zaidi tafadhali tutumie taarifa zifuatazo hata inbox

1.Jina Kamili

2.Wilaya

3.Kiasi unachodai

4.Kazi uliyofanya

5.Namba ya simu

Kwa hatua zaidi

TANESCO Makao Makuu

25/08/2021
 
Fatilieni vizuri labda ni wale vijana wanaochimba mashimo na kusimika nguzo mitaani,kuna siku niliwaona huko mtwara wapo kwa makundi maeneo ya komoro
 
Tumetoa ufafanuzi hapo kuwa hakuna tatizo hilo na wala hakuma anayedai sasa kama yupo atusaidie taarifa kamili na sisi tutazifanyia kazi mara moja.Inapendeza sana kutoa taarifa sahihi ili kuacha kuchafua taswira ya TANESCO kwa kuwa kutoa taarifa zisizo na ukweli sio uungwana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom