TANESCO, mgao huu una sababu gani tena?

TANESCO, mgao huu una sababu gani tena?

Aunt yangu huuza juice za matunda maximum lita 20 kila cku,na ni mwanachama wa ccm mwenye kadi.. Nilifanya juhudi kubwa kumshawishi aipigie kura ukawa kwa mgombea Lowassa aliishia kunifukuza eneo lake la biasha. Jana kanipigia cm nipite kwenye kibanda chake cha juice na nikakuta kainama kwenye meza ya kuuzia juice. Alionekana ana mawazo na maumivu makali sana. Nikajua kapatwa na msiba..
Nikamuuliza aunt vipi?
Akanijibu huku akionesha vipande vya kadi yake ya ccm ikiishirizia kuungua katka jiko.
Nikashangaa sana,ila kwa hasira akaniambia, tangu mwez wa 9 uingie kila cku anauza lita 5 tu. Lakini kilichomuumiza zaidi ni juice yake niliyoishuhudia ikianza kutoa harufu ya kuharibika baada ya umeme kukatika tangu asubuhi mpaka usiku.
"Sina hamu na CCM na serikali hii isiyojali maisha ya watu" shangazi aliongea kwa uchungu.. Ckumjibu ila kwa jinsi maneno aliyoongea jana kura moja ya ccm imepotea.
 
Kinachonishangaza jumuia ya wafanyabiashara na wenye viwanda iko kimya,jumuia za kiraia kama twaweza wako bize NA siasa,hatujui wagonjwa wanakufa kiasi gani kwa kukosa umeme kwenye vyumba vya operesheni NA ICU,mambo mengi yamekwama

Mkuu umeongea kitu cha maana Sana kuhusu huo umoja Wa wenye viwanda na hizo jumuia za kiraia, huku kwenye mahospitali yetu nadhani ndio Furaha kwao maana itabidi wapate sababu za kupiga ulaji Agha khan ,regency, kwa kisingizio kwamba Mwananyamala au temeke hospital hakuna umeme
 
Kwa ufupi,nimewauliza baadhi ya wanafanyakazi wa Tanesco kuhusiana na hii issue wakaniambia huko kuwashwa kwa mitambo,mara matengenezo ni sababu tu ya kudanganya wananchi.Shirika lipo ktk hali ngumu kifedha kujiendesha kutokana na CCM kuchota pesa kwa ajili ya kampeni zake zinazoendelea kwa sasa.

Kwa hiyo ndo sababu ya kusema hali itakuwa nzuri mwishoni mwa October?kwamba ccm watalipa deni baada ya goli la mkono
 
na kweli...nina ukweli maana tanesco people wamekua kama miungu...tatizo lolote ukiripoti hata kama taarifa za kuripoti ziko sahihi lazima wasumbue...tumeambiwa umeme sasa tatizo hakuna tena...lkn maneno na utekelezaji ni tofauti...maneno ya ahadi ni mengi....kwa watanzania lazima tujiulize...why too much blaa blaa no reality acition...kazi kiduchu blaaa blaaa nyingi na unyang'anyi rushwa kwa kwenda mbe...people we should change our atittude top officers to lower work mates
 
Kama waziri anazikwa halafu rais hahudhurii,yuko marekani,sembuse kifo cha mtaji wa mlala hoi au Mtoto wake
 
Ccm hoyeeee.umeme wa gesi huo wakuu Mwaka huu mtaisoma no chagueni ccm
 
Kuishi Tanzania ni kazi! Unaweza punguza life span kwa mawazo.
 
Hizi ni hujuma za wazi zidi ya serikali ya Ccm
 
[FONT=Calibri,Arial,Helvetica,sans-serif][FONT=Calibri,sans-serif]kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi ambayo ilisababisha upungufu wa umeme kwenye Mikoa yote iliuongwa kwenye gridi ya taifa. Baada ya kuanza kuwasha mitambo hiyo Septemba 19, 2015 upungufu huo umeanza kuimarika kwa baadhi ya mikoa. Mitambo yote ya gesi iliyokuwa imezimwa haiwezi kuwashwa mara moja kwa kuwa kitaalam itafyonza gesi haraka na kuleta vacuum kwenye bomba lenyewe. Kumbuka bomba hili ni kubwa la nchi 36 na urefu wa kilometa 487. Hivyo Tanesco tunawasha mtambo mmoja baada ya mwingine ili kumonitor presha ya gesi kwenye bomba. Kazi hii itakamilika mwishoni mwa Oktoba ambapo tutakuwa tumewasha mitambo yote jumla ya megawati 335.[/FONT][/FONT]


mwishoni mwa October!
yaani baada ya uchaguzi?
hamna kudanganyana kama watoto hapa!
dawa ni kuwapiga chini ccm hamna namna nyingine!
 
Huo utakuwa ni uwongo wa kupitiliza, kwa kuwa tayari tulishaelezwa na Mkurugenzi wa TANESCO Mramba kuwa baada ya kukamilika kwa uungwanishaji wa bomba la gesi toka Mtwara na mitambo ya Kinyerezi na Ubungo kuwashwa na hivyo kuongeza megawati 330 kwenye gridi ya Taifa, mgao wa umeme utakuwa historia.

Sasa mgao wa umeme unaoendelea hivi sasa unazidi kuthibitisha pasipo shaka yoyote kuwa serikali ya CCM imekuwa ikitumia uwongo wa kutisha katika uendeshaji serikali yao.

Ndiyo maana kwa uwongo huu wa wazi waliousema watendaji wa TANESCO, ambalo ni shirika la Umma ndani ya serikali ya CCM kunaongeza sababu za wapiga kura wa nchi hii kuvitumia 'vichinjio' vyao vya kupigia kura hapo Oktoba 25 mwaka huu kuwang'oa toka madarakani hawa CCM ambao kipindi hiki cha miaka zaidi ya 50 ya kututawala, kimewafanya wawe wanelewa madaraka kupindukia.

na ndio maana walisema hawata waruhusu watu wengine kamwe waingie ikulu, hiyo ni kwasababu wanajua kuna mambo ya kutisha ndani ya makabrasha...
 
Umeme umekuwa donda sugu.tatizo ni chanzo cha maji uzalishaji umepungua sana.mengine siasa .tunasubiri mvua inyeshe mabwawa yajae maji. Magufuli akiingia madarakani tatizo la umeme litabaki kuwa.historia
 
Mitambo ya ges haiwez kuwasha kama unavyo fikil et yote tu kwa pamoja iwake itasababisha vacuum kwenye bomba so wanacho fanya nikuwasha moja baada ya nyingine nazan baada ya kuwa wamewasha ma bomba yote tatizo litatulia
 
Wametoa sababu kwamba mitambo inaendelea kuwashwa tuvumilie mpaka Oct 20, sasa sijui Mtwara imegeuka NASA maana hiyo mitambo inayoendelea tu kuwashwa mpaka Oct 20 itakua sio ya Gesi peke yake kutakua pia na mitambo ya Ku launch rockets
Ha, ha, ha.
 
Tanescrow ni ng'ombe wa maziwa aliyekamuliwa mpaka akatoa damu. Sasa wana mpango ageuke ng'ombe wa mayai..
maybe
 
Back
Top Bottom