Jana majira ya 20:00hrs nilianzisha uzi TANESCO SINA HAMU NAO. Katika uzi huo, nilishangaa na kuhoji kwa nini kama Chama tawala cha CCM kikiwa na mikutano ya live ambayo wanalenga umma wa tanzania ufuatilie kupitia runinga na redio umeme unashinda kuanzia asubuhi hadi jioni saa 18:00hrs? Nilihoji
1. Je mitambo inapona ccm wakiwa live na wakiwa offline inakufa tena?
2. Je umeme unakuwa wa kutosha ccm wakiwa live lkn wakiwa na mikutano ya kimya kimya mitambo inakuwa na umeme mdogo hivyo kulazimisha uwepo wa mgao?
3. Tumesikia utetezi kuwa mitambo ya gas iliyowashwa ina nguvu sana hivyo kulazimu kuiwaisha taratibu ili bomba zisipasuke. Je kukiwa na live coverage ya ccm, umeme wa kuwasha tanzania nzima unatoka wapi?
4. Na kwa nini mara baada ya kumaliza mikutano yao ya live coverage, umeme unazimwa hadi usiku wa manane na asubuhi hata fursa ya kusikia magazeti tunanyimwa?
Nasikitika kuwa uzi huo tangu jana modes hawajauruhusu kuwa hewani lkn kupitia uzi wako nilichoandika jana nimekiweka hapa.
Kifupi mie naamini ni janja ya TANESCO na seriakali ili waweze kuiba kiasi kikubwa cha pesa. Itakumbukwa migao ya umeme huambatana na uwashaji wa mitambo ya dharura inayolipwa pesa nyingi sana kwa siku.
Naamini kamati za bunge za 2016, zitakuja na taarifa moja ya ufisadi wa kutisha. tusubiri tu muda utimie
[FONT=Calibri,Arial,Helvetica,sans-serif][FONT=Calibri,sans-serif]kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi ambayo ilisababisha upungufu wa umeme kwenye mikoa yote iliuongwa kwenye gridi ya taifa. Baada ya kuanza kuwasha mitambo hiyo Septemba 19, 2015 upungufu huo umeanza kuimarika kwa baadhi ya mikoa. Mitambo yote ya gesi iliyokuwa imezimwa haiwezi kuwashwa mara moja kwa kuwa kitaalam itafyonza gesi haraka na kuleta vacuum kwenye bomba lenyewe. Kumbuka bomba hili ni kubwa la nchi 36 na urefu wa kilometa 487. Hivyo Tanesco tunawasha mtambo mmoja baada ya mwingine ili kumonitor presha ya gesi kwenye bomba. Kazi hii itakamilika mwishoni mwa Oktoba ambapo tutakuwa tumewasha mitambo yote jumla ya megawati 335.[/FONT][/FONT]