TANESCO kutoa mikataba ya uunganishaji umeme kwa makampuni binafsi

Wawe makini tu na quality ya kazi, umeme na porojo ni kuleta majanga, Tz ajali za moto sababu ya miundombinu ya Tanaesco ni chache, hivyo privatizations isitumike kama uchochoro wa kupunguza ubora.
 
Nadhani itarahisisha kwa kuwa kampuni itapewa list ya waliolipia na kwa eneo husika aidha mtaa ama kijiji, uundwaji wa shirika lingine changamoto itakuwa hii hii. Labda TANESCO wapewe nafasi ya kuajiri wafanyakazi ili kazi ziende chap chap na hili liende sambamba na uharakishaji wa kuagiza vifaa kama meter, transformer, nyaya na nguzo
Tatizo la ucheleweshaji linatokana na kukosekana vifaa + fedha. Hizo kampuni zitazokua zinafanya kazi hazitahusika na kununua vifaa.
 
Kwa nini?
Mashirika ya umma hayana usimamizi mzuri kwa hawa subcontractors kwa kuwa subcontractor s wengi huwa ni sehemu ya uongozi wa shirika.
Mfano; bandari ilitoa contract kwa ticts ili kupunguza mzigo upande wa container lakini huko ticts kuna maajabu mengi na delays kuliko bandari kwenyewe. Ila hawakua na namna sababu ticts ilikua ya watu flani juu.
Atcl walitoa contract ya kufanyiwa matengenezo na hao subcontractor Ila mwisho wa siku hakuna matengenezo na pesa ikalipwa.

Kama bado management haipo vizuri, hizi subcontract ni kazi bure na kitakua kichaka tu cha kujifichia huko.
 
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema linatarajia kuanza kuzipa kandarasi kampuni binafsi kazi ya kuunganisha umeme, ili lenyewe lijikite kwenye uzalishaji na usafirishaji wa nishati hiyo muhimu.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Maharage Chande wakati wa mkutano wa Tanesco na wadau uliofanyika juzi jijini hapa na kusema hatua hiyo na nyingize zitasaidia kumaliza tatizo la watu kuchelewa kuunganishiwa umeme.

“Watakaopewa kazi ya kuunganisha umeme watalipwa kwa ‘commission’ kulingana na kazi itakayofanywa na tutakuwa tunafuatilia na kubaini iwapo kutakuwa na ucheleweshaji na kuchukua hatua. Lengo ni kumaliza changamoto ya kuchelewa kuunganisha umeme,” alisema Chande bila kufafanua lini hasa wataanza.

Hata hivyo, Chande alisema wameanza majaribio na pindi wakapoanza rasmi suala la kuunganishwa umeme litakuwa si shida tena, kwani urasimu utapungua.

“Pamoja na kwamba tunaendelea na hilo kwa utaratibu huu wa sasa tunatarajia walioomba kuunganishiwa umeme wote wataunganishwa ndani ya miezi sita ijayo,” alisema.


Chanzo: Mwananchi
Ni mawazo ya kifisadi. Mi nilidhani watoe kibali cha kampuni binafsi kufua umeme na kuuza kwa wananchi. Hiyo ya kusema subcontracting uunganishaji wa umeme utapelekea kupandisha gharama ya uunganishaji na ya umeme, na pia hao subcontractors hawataweza kabisa kujitegemea na watategemea kila kitu toka TANESCO. Yaani hili wazo ni la kulipinga kwa nguvu zote na la kifisadi maana yake kila subcontractor atatatakiwa kutoa rushwa ya 10% kwa Maharage Chande na Akina Makamba wataunda vikampuni vyao ili wapige cha juu. Hilo wala siyo suluhisho ni wale wala rushwa na mafisadi wenye kufaidika watafurahia. Mungu hili wazo life na atakaye likomalia yeye aondoke kabisa maana litaumiza watanzania.
 
Umeelewa kweli?
nimeelewa kwamba wanawapa tenda kampuni binafsi ya kuunganisha umeme kwa raia sawa, na wao wakijikita kuzalisha na kusafirisha umeme...Hoja yangu ni kuwa wanarahisisha kuwaunganishia umeme kwa haraka, lakini pia nasema huo umwamba wa wao kuzalisha na kusafirisha pia tunataka uishe atleast kuwe na ushindani sio kila kitu kinachohusu umeme washike wao.. najua ni ngumu ila sio mbaya tukijaribu
 
Should outsourced or even privatise the whole services..private kuna uwateja, accountability, ufanisi na fast response...Tanesco ya sasa ni Taka x2
Wewe unakimbilia kuandika bila kutafakari na kuelewa.
 
nimeelewa kwamba wanawapa tenda kampuni binafsi ya kuunganisha umeme kwa raia sawa, na wao wakijikita kuzalisha na kusafirisha umeme...Hoja yangu ni kuwa wanarahisisha kuwaunganishia umeme kwa haraka, lakini pia nasema huo umwamba wa wao kuzalisha na kusafirisha pia tunataka uishe atleast kuwe na ushindani sio kila kitu kinachohusu umeme washike wao.. najua ni ngumu ila sio mbaya tukijaribu
Bado hujaelewa
Kila kitu bado kinafanywa na kitafanywa na Tanesco. Bado kuunganishiwa umeme utaunganishiwa na Tanesco Ila watakua na subcontractors
 
nimeelewa kwamba wanawapa tenda kampuni binafsi ya kuunganisha umeme kwa raia sawa, na wao wakijikita kuzalisha na kusafirisha umeme...Hoja yangu ni kuwa wanarahisisha kuwaunganishia umeme kwa haraka, lakini pia nasema huo umwamba wa wao kuzalisha na kusafirisha pia tunataka uishe atleast kuwe na ushindani sio kila kitu kinachohusu umeme washike wao.. najua ni ngumu ila sio mbaya tukijaribu
Kuelewa tu hakutoshi. Inatakiwa uende mabali zaidi na kujua pros nad cons za huo utaratibu. Fanya angalau research ndogo na usipende kukimbilia ku-type tu bila kutafakari mambo kwa undani.
 
Wajikite kwenye kuzalisha na kusafirisha? Kwahiyo ule mpango wa akina Ngeleja wa kuligawa shirika vipande vitatu ndo unaanza kutekelezwa? Generation, Transmission na Distribution?

Wao waweke kampuni zao Generation, Transmission iachwe kwa serikali kuu, Distribution pia iendeshwe kwa ubia, kwakuwa mkopaji mkubwa wa umeme ni serikali, basi Distribution atashindwa kukusanya mapato effectively, hivyo pesa zitakuwa zikichotwa serikalini kuilipa Generation.

Transmission itachakaa kwa ghafla kwa kukosa matengenezo, Distribution itakuwa dhoofu lihali, mgao utakuwa bab'kubwa!

Watumishi wa shirika waliwahi kuupiga chini huo mpango kwakuwa IPP's zote ni za kipigaji na zikidaiwa kumilikiwa na wao, Symbion, Songas, IPTL, Kilwa Energy, Dowans, Greenbird n.k

Solar na majenereta itakuwa ni biashara nzuri, kila la kheri TZ
 
Back
Top Bottom