TANESCO kutoa mikataba ya uunganishaji umeme kwa makampuni binafsi

Kubinafsisha ndio tulifeli toka awamu ya mwinyi na mkapa
ni bora twende hivi. Haya mashirika ukibinafsisha tu ndio yanakufa moja kwa moja. Tuliwahi kuwapa shirika Net group solution kwa lengo unalosema. Ila mwisho wa siku tulikoma.
Kama maharage kashjndwa kusimamia, basi tutafute mkurugenzi mwingine
Kuna namna iliyobora...we have to explore that namna ila hakuna kinachofanikiwa chini ya serikali.
 
Ufisadi na rushwa ni mambo yanaongoza kuliko faida na ufanisi
 
Tanesco na Maji ni idara za kifalæ sana.. yani sijui wanafanyaje kazi.
 
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema linatarajia kuanza kuzipa kandarasi kampuni binafsi kazi ya kuunganisha umeme, ili lenyewe lijikite kwenye uzalishaji na usafirishaji wa nishati hiyo muhimu.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Maharage Chande wakati wa mkutano wa Tanesco na wadau uliofanyika juzi jijini hapa na kusema hatua hiyo na nyingize zitasaidia kumaliza tatizo la watu kuchelewa kuunganishiwa umeme.

“Watakaopewa kazi ya kuunganisha umeme watalipwa kwa ‘commission’ kulingana na kazi itakayofanywa na tutakuwa tunafuatilia na kubaini iwapo kutakuwa na ucheleweshaji na kuchukua hatua. Lengo ni kumaliza changamoto ya kuchelewa kuunganisha umeme,” alisema Chande bila kufafanua lini hasa wataanza.

Hata hivyo, Chande alisema wameanza majaribio na pindi wakapoanza rasmi suala la kuunganishwa umeme litakuwa si shida tena, kwani urasimu utapungua.

“Pamoja na kwamba tunaendelea na hilo kwa utaratibu huu wa sasa tunatarajia walioomba kuunganishiwa umeme wote wataunganishwa ndani ya miezi sita ijayo,” alisema.


Chanzo: Mwananchi

Kwanini sasa tu wasibinafisishe TANESCO ikaeleweka moja kuwa wameshindwa kujiendesha, manake sasa hivi hadi magari ya kazi wanakodi private.

Ama ieleweke tu wafanye kama kwenye simu kuwe ni soko hulia halafu tuone. Otherwise ni mwendo wa kugawiana tenda tu kupitia utatu upigaji engineering za akina maharage, mafuru (mafish) na mchechuu for a sake of awamu ya 4 na 6
 
Usinipangie chakuelewa huu ni mtazamo huru
Unajua kusoma kwa ufahamu? Nimekupangia saa ngapi cha kuelewa? Nimekuambia hujaelewa, na sijakupangia uelewe nini! Ukisema 1 na moja ni tatu ukiambiwa siyo jibu hakika hujapangiwa!
 
Shida ni management tu na Wala sio ku-subcontract kwa kampuni. Kwa kuwa ndio mwanzo wa kutengenezwa kampuni flani za ujanja.
Ikiwa Tanesco wanakiri hawana uwezo tena wa kuunganisha umeme basi liundwe shirika lingine lifanye hiyo kazi wao wabaki kwenye uzalishaji
Sasa mpaka uunde shirika jingine tena uanze kuajiri! Mbona ni rahisi zaidi kuuza hiyo kazi kwa watu wanaoweza kuifanya kwa haraka tena unamuuzia mpaka wafanyakazi.

Pia ni njia nzuri ya kupunguza tatizo la ajira.
Kimfano kampuni zitakazopata hiyo tenda anaweza kuamua kupiga kazi usiku na mchana.
 
Tatizo kubwa na sababu ya watu kuchelewa kupata huduma TANESCO ni Moja tu, FEDHA, tanesco wasipotatua uhaba wa fedha hai subcontractor watafeli sana, Mana najua wengi uwezo wao utakuwa mdogo, wakiwa na Feza za kutosha wanaweza kumudu kuungia watu umeme Ila huna hela hao subcontractor watatoa pesa mfukoni mwao.

Hapa wanapenda kufeli, Bora Kitengo Cha kuungia wateja umeme kipelekwe kwa Wakala wa Umeme Vijijini(REA) sababu Hawa wameonesha ufanisi wa Hali ya juu
 
Hii mbinu imewahi kutumika miaka ya nyuma, bado tulifeli. Tatizo la Tanesco bado lipo kweye usimamizi.
Hao subcontractor sio kwamba watakua wanajitegemea, Bali kila kitu watakuaa wanafanya chini ya Tanesco. wao ni kutumwa tu kuungaanisha umeme Ila mengine yote bado yatakua chini ya Tanesco.
Tuliwahi kuyapa makampuni makubwa kazi ya kusaidia kuzalisha umeme kwa Tanesco. Najua unajua kilichotokea
Shida ni kwamba hapa tulipo hakuna unafuu, huo usimamizi unaoutamani hauwezi kuja hivi karibuni. Tusubiri tuone huu utaratibu mpya utakuwaje. Kuwe na vigezo vilivyo wazi na nini kitatokea vigezo vikivunjwa. Maana sasa hivi hakuna mtu yeyote anayewajibika kwa yoyote. Hata kama utaratibu mpya unaweza kuwa mbaya, sijui kama utazidi ubaya wa sasa
 
Subcontracting ni nzuri kiasi na inaweza kufast track process ya wateja kuunganishwa ila tujue pia lazima Issue ya quality tuiangalie kwa Jicho kali sana, hawa Contractors wengi watakaopewa hizo kazi watakuwa na mikono ndani ya shirika ivo kupelekea, wasimamizi kushindwa kuwawajibisha wakikuta kazi hazina ubora ivo maelekezo yatatoka juu na wasimamizi hawatakuwa na namna bali kupitisha izo kazi, Tuna mifano hai ya kazi Za REA zilivokuwa Chini ya Ubora, Na Wakandarasi tayari wameshapewa Certificate of Acceptance and Completion
 
Huyo Sub Contractor mwenyewe lazma itakuwa kampuni ya Waziri na vibaraka wake wa kizungu! So hela yote watakayojilipa % inaingia kwake tena.
Kama watafanya kazi kwa ufanisi, acha tu wale pesa 😂😂😂. Maana mateso ya sasa hivi hayana nafuu
 
Shida ni kwamba hapa tulipo hakuna unafuu, huo usimamizi unaoutamani hauwezi kuja hivi karibuni. Tusubiri tuone huu utaratibu mpya utakuwaje. Kuwe na vigezo vilivyo wazi na nini kitatokea vigezo vikivunjwa. Maana sasa hivi hakuna mtu yeyote anayewajibika kwa yoyote. Hata kama utaratibu mpya unaweza kuwa mbaya, sijui kama utazidi ubaya wa sasa
Unasema hapa tulipo hakuna unafuu, Sasa Kama hakuna unafuu hao subcontractors watasimamiwaje?
Hao hawapo independent, kila kitu kinabaki kuwa chini ya tanesco
 
Kama watafanya kazi kwa ufanisi, acha tu wale pesa . Maana mateso ya sasa hivi hayana nafuu
Kadri wanavyokula ndio ubora wa kazi nao unaoungua. Tatizo la Tanesco hadi Sasa ni pesa, Sasa wakila si itakua ndio kufeli moja kwa moja?
 
Shida ni management tu na Wala sio ku-subcontract kwa kampuni. Kwa kuwa ndio mwanzo wa kutengenezwa kampuni flani za ujanja.
Ikiwa Tanesco wanakiri hawana uwezo tena wa kuunganisha umeme basi liundwe shirika lingine lifanye hiyo kazi wao wabaki kwenye uzalishaji
Naunga mkono hoja wapewe private contractors

Umeme utafungwa kwa spidi kubwa kuliko.sasa
Wafanyakazi hao wala Rushwa wa Tanesco waliokuwa wakiendekeza rushes ndio wabunge umeme wakatafute kazi zingine za kufanya halihitajiki shirika linginr la umma

Private wapewe hizo kazi kama wanaolipwa kwa commission atakimbiza kazi haraka iishe apewe chake

Hilo naunga mkono
 
Back
Top Bottom