TANESCO kumaliza tatizo la umeme Tanga kufikia Machi 2023, waelezea kuzalisha umeme kwa njia ya jua

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeweka wazi mipango yake ya kumaliza tatizo la umeme kwa asilimia 100 Mkoani Tanga kufikia Machi 2023, huku kukiwa na mikakati ya kuzalisha umeme kwa njia ya jua kufikia mwishoni mwa mwaka huu (2022).

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa amezungumzia jinsi changamoto ya mabadiliko ya Tabia Nchi yanavyochangia changamoto kwa TANESCO, akisema:

“Dunia sasa ina wimbi na changamoto ya mabadiliko ya Tabia Nchi, mmoja wa wahanga wakubwa ni TANESCO. Tafsiri pekee tuliyonayo ni changamoto ya upatikanaji wa maji ambayo tunaitegemea kama sehemu ya uzalishaji umeme.”

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usafirishaji Umeme wa TANESCO, Abubakari Issa ameeleza kuwa Shirika hilo linafanya maboresho ya laini ya umeme kutoka Ubungo kwenda Chalinze kisha Tanga ikiwa ni juhudi za kuboresha upatikanaji wa umeme maeneo hayo.

Issa amesema “Hii laini ina uwezo wa Megawati 75, tunaenda kuifanyia maboresho ya kuiongezea uwezo kuwa na Megawati 150, ambayo ni mara mbili ya kiwango kilichopo sasa, hii kazi itafanyika katika awamu tatu.

“Awamu ya kwanza ya Chalinze kwenda Mlandizi tumeikamilisha, ahadi yangu ni kuwa hadi kufikia Machi 2023 tatizo la umeme litakuwa limemalizika kwa wakazi wa Tanga.”

Akizungumzia ahadi hiyo, Meya wa Jiji la Tanga, Abrahaman Shiloo amesema hatua zinazofanywa zinaonesha kuna mwanga mzuri wa kuondoka kwenye tatizo la kudumu la upungufu wa umeme Nchini.

Upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Martin Mwambene amesema TANESCO imejidhatiti kuhakikisha wana vyanzo mchanganyiko, akigusia mpango wa kuanza kuzalisha umeme kwa njia ya jua maeneo ya Kishapu Mkoani Shinyanga pindi itakapofika Desemba 2022.
 
View attachment 2398734

Wameweza?
 
Back
Top Bottom