kasambalakk
Senior Member
- Apr 2, 2011
- 126
- 17
hili wazo zuri sana lazma [HASHTAG]#tanesco[/HASHTAG] wataipokea tu jinsi walivyojipanga..Heri ya Pasaka kwenu pia. Hongereni kwa jitihada zenu pamoja na kuwa mnafanya kazi katika mazingira magumu sana yanayosababishwa na mikataba ya kifisadi.
Msikae kimya kuhusu kuendesha shirika kwa hasara kubwa inayosababishwa na TANESCO kununua unit moja ya umeme kwa shilingi 544 na kuuza unit hiyo moja kwa shilingi 279.
Hili ni la kushughulikia haraka ipasavyo ili kuhakikisha uwepo wa TANESCO kwa miaka mingi ijayo vinginevyo mtapotea katika anga za Tanzania na hivyo kuzuka vikampuni uchwara ambavyo vitatulangua sana Watanzania na umeme kuwa wa bei kubw sana na hivyo Watanzania wengi kushindwa kumudu gharama kubwa.
Pia muangalie uwezekano wa kujikita kwenye umeme wa jua ambao bila shaka unaweza kushusha sana gharama zenu za uendeshaji kwa kiasi kikubwa.
I hope to see you on this forum every now and then to share your ideas with your fellow Tanzanians and also to learn from us.
Happy Easter Sunday.
