Tamthiliya: Challenge Made - Sehemu ya 1

Well done!! Kitu inazidi kunoga John John, anatatizo la wivu anaona Kama kawahiwa flani ivi[emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji173][emoji173][emoji173]sasa hivi nakuongezea shahuku my[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

#asante kwakuwa na mimi[emoji120][emoji120][emoji120]
Kwenye whatsapp unakuwa na glup la story
 
TAMTHILIA : ZAWADI.

MWANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS

SEHEMU : 14 $ 15

WHATSAPP NO: 0746115688.

baada ya john John kugundua ya kuwa Zawadi anaumwa, haraka alifanya mpango wakumpata daktari na kuanza safari ya kwenda kumsaidia Zawadi, lakini kwabahati mbaya walichelewa kwani walimkuta zawadi ameshajifungua tena akiwa mwenyewe na mtoto yuko pembeni analia wakati yeye amepoteza fahamu kutokana na kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua. haraka Daktari alimsafisha mtoto nakumbeba, John John na yeye akambeba zawadi na kuanza rasmi safari yao ya kutoka kisiwani na kwenda mjini kumpeleka zawadi hospitalini, walipofika hospitalini zawadi alipata matibabu na baada ya muda zawadi alipata nafuu, na alipo amka alimuuliza Daktari aliyekuwa akimuhudumia ' samahani wewe ninani, na hapa nime fikaje mana nakumbuka mara ya mwisho nilikuwa kwetu'. Daktari akamwambia kweli mara ya mwisho ulikuwa kwenu , na sisi tulikuja kukuchukua kwasababu ulimpigia simu moja kati ya maafisa wetu ukaomba msaada kwani muda wako wa kujifungua ulikuwa ushafika na hapo ndio mimi na John John tukakufuata kwalengo la kuja kukusaidia wakati wa kujifungua lakini kwa bahati nzuri tukakukuta umesha jifungua na mtoto wako alikuwa salama. Shida ilikuwa kwako kwani tulikukuta umepoteza fahamu na kukuhudumia kwapele ilikuwa ngumu kwasababu ulihitaji huduma bora zaidi na uangalizi wa hali ya juu na ndio maana mimi pamoja na John John tulikuchukua na kukuleta hapa.
Zawadi aliwaambia Daktari natumaini wazazi wangu hawajui kuhusu mimi Daktari. lakini Daktari akamwambia Zawadi utatusamehe kwasababu kwa hali tuliyo kukuta nayo kule, hakukuwa na jinsi yeyote ya kuepuka kuwaambia wazazi wako ukweli, hivyo John John aliwaambia na hivi sasa wako karibu kufika hospitalini pamoja na John John. Zawadi alimbeba mtoto na kumwambia Daktari yeyote atakae kuulizia mwambie mimi nimetoroka na mwanangu. Kabla Daktari hajamjibu sauti ya mtu kutoka mlango ilisikika ikimwambia zawadi lakini hujatoroka bado na tumefika. Zawadi alipogeuka nyuma kuangalia ninani aliye kuwa pale na ndipo alipomuona Mfalme na Malkia mbele ya macho yake, na palepale wakamkumbatia na kumwambia pole binti yetu kwa yote uliyo yapitia, wala usijifiche na mtoto wako eti kwasababu ulibwakwa kwani kwapamoja tutamlea kwa upendo atakuwa na siku moja mwanao atakuja kukusaidia jivunie yeye wala usimtenge na ulimwengu. Zawadi akilia sana na kumwambia Malkia pamoja na Mfalme ya kuwa Kamwe siwezi kumtenga kijana wangu nitamlea vizuri atakuwa na heshima na adabu lakini pia atakuwa mtoto anayetenda matendo mema sitaruhusu afe kama baba yake bali atakufa kama shujaa.
John John alitabasamu baada ya kuona ujasiri wa zawadi , lakini pia akampa taarifa Zawadi ya kuwa rais nataka kumuona na nimuhimu sana kwayeye kwenda iliakapate kuimba msaada juu ya mahitaji yote ambayo watu wake watahitaji kwasasa. Malkia na Mfalme walimwambia Zawadi na kabla hujaenda huko inabidi ukakutane na watu wako ili ujue wanahitaji nini, na baada ya hapo unaweza tu kwenda na kupeleka mahitaj hayoo kwa muheshimiwa rais. Zawadi alishangaa sana na kumuangalia john John kisha akawauliza Malkia pamoja na Mfalme mmewezaje kumuelewa John John kwaharaka hivyo kwasababu mnajua kilakitu kuhusu huku tayari kwannavyo waona. Malkia akamwambia Zawadi ni Mwaka sasa binti yangu tumejifunza mambo mengi sana kwasasa na tunatamani kufidia ualifu wote walioufanya mababu zetu juu ya ndugu zetu wenyewe bila ya wao kujua na hata hivyo kunataarifa mpya natamani kukwambia binti angu, Zawadi akamuuliza ni taarifa gani mama ,"ukweli ni kuwa Zawadi sisi kwasasa tunajua kusoma na kuandika lakini pia watoto wote wameanzishwa hule chini ya usimamizi wa John John akiongozwa na serikali.
Zawadi alimuangalia sana John John nakumwambia asante san, japo mimi nimefundishwa hayo yote na kaka yangu japo ni jambazi ila nampenda sana na natumaini ipo siku mtampa nafasi ya kutoka nnje akiwa kabadilika tabia. John John alimuangalia sana Zawadi na kumwambia sio dhambi kumpenda jambazi unaweza kumsubiria ukipenda, lakini Zawadi akamwambia tatizo sijui utamuachia lini mana unahasira nae sana. John John alimwambia zawadi ungemficha basi siku ile na ukabakia nae kulekule kisiwani si ni raha sana kumuona. Zawadi alicheka sana na kumwambia John John mbona kama unachuki sana na mimi lakini John John akamwambia kiasi tu. Mfalme aliingilia katikati ya ugomvi wao kwakuwaambia mtoto amelala na msipo acha kelele zenu ndo ataamka na asilale tena, kisha Malkia na Mfalme wakatoka nnje ya chumba alichopo zawadi huku wakiwa wanacheka kwasababu waligundua kuwa John John amesha mpenda binti yao zawadi na anawivu na kila kitu hata visivyo kuwa na maana. Lakini wakati John John amekaa katika chumba kile na zawadi na wote wakiwa kimya huku wakiangaliana kwa hasira Daktari aliingia na kumwambia zawadi ya kuwa mtoto anaitwa nani ? Zawadi akamuuliza Daktari chagua tu wewe unaweza kumuita John au jina lako pia sio mbaya. John John alimuangalia Zawadi lakini hakuongea chochote na ghafla aliingia afisa ambae ni rafiki wa karibu sana na Zawadi na alipo ingia tu alimuangalia mtoto na zawadi moja kwa moja bila kugeuka nyuma hivyo hakujua kuwa bosi wake yuko pale. Daktari aliuliza kwahiyo nikamuandikishe mtoto kwajina la john, afisa alimuuliza zawadi kwani umempa jina la john mtoto . Zawadi akamwambia mi nimemwambia Daktari achague jina la John au la kwake mwenyewe ampe mwanangu. afisa alicheka sana na alipo geuka alimuona bosi wake John John na hapo ndo zawadi akamuuliza kwani we unaonaje au nikosa pia kumuita mwanangu John . afisa alimwambia itapendeza sana akiitwa John John John , zawadi alicheka akijua ni utani wa kawaida lakini John John aliwauliza kwani mimi ndio baba wa mtoto mpeni majina ya baba yake lakini zawadi akamwambia nilikuwa nakutania tu mbona unaonekana kuchukia? John John hakumjibu Zawadi alichofanya aliondoka eneo lile na Daktari akamuuliza zawadi 'kwahiyo aitwe John?' lakini zawadi alimwambia hapana kisha akamuuliza rafiki yake yule afisa unaitwa nani kwani , afisa akawambia naotwa elius Steven na zawadi akamwambia Daktari basi mwanangu aitwe Steven lakin elius akamwambia bora aitwe Jofrey elius Steven, mimi nikae kama baba yake kwasababu baba ake hatumjui jina. Zawadi alifurahi sana na kumshukuru elius kisha akamwambia Daktari kamsajili kwa majina hayoo. Daktari alienda na kujaza kadi y mtoto ili waweze kuruhusiwa wakiwa na kadi hiyooo. Baada ya usajili Daktari alirudi hodini ili kumpa Zawadi kadi ya mtoto lakini mlangoni alikutana na John John na alimpa taarifa zawadi anavaa hivyo Daktari huyo alimpa John John kadi ya mtoto na baada ya dakika chache Zawadi alitoka pamoja na mtoto na safari ya kumpeleka zawadi katika nyumba ambayo watu wote waliotoka katika Ufalme wa Wetu wanaishi hapo , Nabaa ya kufika mahali hapo watu walifurahi sana baada ya kumuona Zawadi na mwanae, kisha wakamuomba msamaha Zawadi kwasababu mara ya mwisho walimuacha kisiwani wakiwa na kinyongo nae , kwani walihisi kuwa anawageuka wote kwasababu ya John John. lakini zawadi aliwaambia yeye amewasamehe na hawakufanya kosa pia kutilia mashaka matendo yake kwa sababu pale ndo nyumbani kwao hivyo anapotokea mtu wa kuwashawishi waache kuishi kwao na waende kwa watu wasio wajua lazima wawe vile. Mtu mmoja akamwambia Zawadi wewe una moyo wakitofauti sana lakini pia wewe ni muelewa kwasababu pamoja na sisi kuwa wabaya kwako siku zote unatuelewa sana nakupenda sana Zawadi wetu. Zawadi alimsogelea mtu yule na kumbusu kisha akamwambia nakupenda pia wewe na kila mtu hapa. Lakini mtu mwengine akasema Zawadi unamiaka ishirini kwa sasa lakini du kama mzee vile kwa majukumu unayobeba, zawadi akamwambia toka ujue kuhesabu sasa, akamjibu na hesabu hadi Nyota. Watu walicheka sana kwa furaha huku machozi yakiwamwagika jambo lililo mfanya john John kumwaga machozi kwa sababu kweli wao wanaishi vizuri zaidi ya maisha waliyo kuwa wanaishi wakina Zawadi awali lakini chaajabu wakina Zawadi wanaelewana hata wanapokoseana, na maisha yanaendelea tena kwa furaha wakati huo huku walipo wao John John mtu akikosewa na mtu anakuchukulia uadui kabisa na mwingine anapokukosea anasahau kabisa kuna kuomba msamaha.
Zawadi aliwaambia sasa tunalia nini, tufute machozi na tupange sasa kesho naenda kumwambia ni rais . Watu walimwambia Zawadi angalau ungepumzika kwanza, lakini zawadi aliwaambia ntapumzika pale sisi tutakapo kuwa nauhakika wakuishi na kuendesha maisha yetu bila ya tabu yeyote.
Watu walifurahi sana na moja kati ya watu hao alimwambia Zawadi mi naona sio vibaya kama tutaendelea kuishi kule kwetu wakati serikali ikiendelea kutufanyia mabadiliko kule, lakini mwingine alimwambia Zawadi baadhi ya watoto hapa uwaoni kwasababu wanaenda shule jambo ambalo kule kwetu ni ngumu kwa watoto kupata elimu kwasababu hakuna shule, lakini mwingine akamwambia Zawadi hatuwezi kuitegemea serikali kwakila kitu tunahitaji na Sisi kufanya kazi kuziendesha familia zetu hatuja zoea kukaa tu muda wote .
Zawadi aliwaambia sawa mimi nimewasikia wote na hio kesho nikifanikiwa kukutana na rais nitahakikisha hoja zene wotee zinamfikia. Basi wote walikubaliana wakaendelea na shughuli zao za kila siku na John John nayeye aliondoka na kuelekea nyumbani kwake. Lakini alipofika aligundua kuwa ameondoka na kadi ya mtoto wa zawadi na alichofanya alichukua kadi ile nakuiweka juu ya redio yake na kumjulisha Zawadi kwa ujumbe mfupi kwanjia ya simu kuwa kadi ya mtoto wake yupo nayo. Zawadi akamjibu sawa kesho mpe baba wa mtoto ataileta mana wewe unaonekana hutaki kuja kabisa huku ni kazi tu ndo inakufanya ulazimike kuja karibu yetu na ndio maana kila mara tu unakasirika unapo niona usijali hivi karibuni tutakuwa mbali kabisa na macho yako na kazi yako itakuwa imeisha na Sisi, utapata kazi mpya kwa watu utakaovutiwa nao . John John aliusoma ujumbe wa zawadi lakini hakuweza kumjibu chochote na alibakia tu kujiuliza 'hivi ni kweli Zawadi hajui kama na mpenda au anafanya kusudi?"
John John aliamua tu bora alale mana kuchart na zawadi kunamfanya apate hasira tu. Lakini wakati John John yupo usingizini alikumbuka zawadi alimwambia kadi ya mtoto ampe baba wa mtoto na hapo ndo usingizi wote ulikata na kisha John John akawasha taa na kuuchukua kadi ya mtoto ili ajue huyo baba wa mtoto anaetakiwa kumpa kadi ninani?

USIKOSE SEHEMU YA 16 NA 17
 
Hapa zawadi alipofikia anataka kunigombanisha na boss ananipaje mtoto kienyeji hivi? Ila boss wangu nae akili Hana anamnunia mrembo wakati anamuhitaji mpuuzi kweli huyu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…