TAMTHILIA: ZAWADI.
MWANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS
SEHEMU YA : 12 $ 13.
WHATSAPP NO :0746115688.
Baada ya kupona kwa Mfalme, Zawadi alikumbuka ahadi aliyoiweka kwa moja kati ya afsa usalama aliyekuwa chini ya john John na hapo ndo alianza kuwaza kwasababu siku zote Zawadi anapotoa ahadi huwa anatimiza, lakini kwa ahadi aliyoitoa kwa John John ilikuwa ikimpa mashaka sana lakini hakuwa na jinsi kwani giza lilipoingia Zawadi alienda katika eneo ambalo ndo amekuwa akikutana na afisa yule wa usalama ambae yupo chini ya John John lakini ajabu safari hii John John ndo alikuwepo yeye mwenyewe katika eneo lile. Zawadi alishangaa sana lakini hakuwa na haki ya kuhoji hayo yote, alichofanya ni alimwambia tunaweza kwenda sasa mana baba yangu ameshapona ni muda wa mimi kuitimiza ahadi yangu. Lakini John John akamwambia huwezi kwenda popote Zawadi kwasababu kazi yako utaifanyia hapahapa, zawadi alishtuka sana na akamuuliza John John "ni kwanjia gani ntaweza kufanya kazi hiyo hapa kwetu ?' John John akamwambia zawadi cha kwanza inakubidi ujalibu kuwa hadithia vitu vizuri ambavyo wewe umekutana navyo kule, lakini pia waelezee jinsi watu wakule wanavyo jali na kuwathamini watu wengine ili tuone kama watabadili fikra zao na kutaka kuishi na wenzao . Zawadi alikubaliana na John John na kweli siku iliyofuata zawadi alipoulizwa na Mfalme juu ya yeye kutekwa yeye alielezea Uzuri tu alio kutana nao kule alipopelekwa na kuwasifia sana watu wakule lakini Mfalme akamwambia ' inawezekana watu hao kwao nipazuri sana lakini mioyo yao ni michafu zaidi kwasababu kama wangekuwa ni watu wazuri kwanini wakuteke inabidi uache tu habari hizo Zawadi mana pengine watu wakijua wanaweza hata kuku tenga.
Zawadi aliyasikiliza sana maneno ya baba yake na hapo ndo aligundua kweli ni ngumu kubadilisha ufahamu wa watu wao na baada ya zawadi kugundua hilo alimwambia John John juu ya msimamo wa baba yake lakini John John alimshawishi angalau atafute watu wakumuunga mkono juu ya jambo hilo ili iwe ngumu kwa watu wanaotaka kumpinga.
Kweli Zawadi akaanza kuwashawishi watu wanao mzunguka hasahasa vijana kama yeye, lakini vijana hao walimchukulia yeye kama msaliti na kusambaza taarifa za kuwa zawadi anampango mbaya na watu wa Ufalme wa Wetu kwa sababu amekuwa akiwashawishi watu kuweza kumuamini na kuwaamini wageni walio mteka yeye, jambo lililo wafanya watu kuweza kumtenga na kumuona mbaya na wala hajali kuhusu wao yeye anachojali ni wageni hao na sio watu wake.
Mfalme alijisikia vibaya sana aliposikia Uvumi huo kuhusu Zawadi, na hapo ndo akamwambia zawadi ' kitendo cha mimi kukukataza wewe kuacha kuendelea kuongelea habari za watu usio wajua vizuri ulikichukuliaje, kwasababu nikama vile unajali sana kuhusu hao zaidi yetu na ndio maana unajalibu sana kuwashawishi watu ili wawakubali watu waliokuteka na wawapende kama unavyo wapenda wewe lakini mimi hujaniweka wazi kabisa lengo lako ninini juu ya watu hao. Lakini pia kama walikuachia kwa masharti niambie tu ili tujue jinsi gani tunatimiza sharti lao na si kuwatumia watu wako kwa faida yao.
Zawadi alijisikia vibaya na kuona hayo yote yanayo mtokea ni kwasababu ya John John kama si yeye baba yake asingethubutu kuongea maneno makali hivyo juu ya binti yake, hivyo zawadi alienda moja kwa moja mpaka wanapo kutana na John John na baada tu ya John John kufika mahala hapo zawadi alimwambia sipo tayari kushirikiana na nyie kwasababu kila nnavyojiweka karibu na nyie napata tabu tu zaidi.
John John alichukia sana kwasababu aligundua kuna baadhi ya maadui wakubwa tu nchini wamekuwa wakienda kujificha katika maeneo yao jambo ambalo ni hatari sana kwa nchi hasa pale ambapo baadhi ya watu wa Zawadi wakiungana na makundi hayo.
Lakini upande wapili zawadi baada ya kurudi katika ufalme alibakia kuwa mpweke sana kwasababu kila mtu katika ufalme wa Wetu alikuwa akimchukia yeye kwa kampeni alizo kuwa akiwafanyia watu wa mjini. John John na yeye baada ya kuona mambo yanazidi kuwa magumu, na magaidi wanazidi kuingia katika kisiwa kile na kutoka kila siku alijua kabisa jambo hilo litakuwa shida kubwa baadae hivyo alicho kifanya alitafuta nyumba moja kubwa sana na kuanza kuwateka watu wa ufalme wa Wetu kidogokidogo na kuwaweka katika nyumba hiyooo na kuwapa elimu zaidi juu ya mambo mbalimbali waliyo kuwa hawayajui. Kilasiku watu walipokuwa wakitekwa lawama zote alikuwa akipewa zawadi jambo lililo mfanya zawadi akose marafiki lakini pia kutengwa na familia yake nzima yaani Mfalme, Malkia na watu waliokuwa wamesalia katika Ufalme huo wa wetu. Zawadi alipoona kila siku watu wake mwenyewe wana mtenga alienda katika eneo ambalo mara nyingi watu wa john John huwa wanakaa hapo , lakini kwa bahatimbaya sio John John wala watu wake walikuwa wakipatikana katika eneo hilo na kibaya zaidi aliporudi katika ufalme siku hiyo watu wote walikuwa wametekwa kama wengine, lakini chaajabu kunawatu tofauti na wafanyakazi wa John John walikuwa wakiwatafuta watu wa ufalme huo na kwambali aliwasikia wakiwa wanakili juu ya mpango wao wa kuwachukua watu wao na kuwatumia watu hao kuigeuka nnchi yao, na hapo ndo zawadi aligundua kuwa ni vizuri watu wake kuondoka katika eneo lile na wala hata hakujisikia mnyonge tena kama awali bali alichukua maamuzi ya kujilengesha kwa majambazi wale na kweli wakaingia katika mpango wake na wakamteka na baada ya muda kidogo wote wakampenda na kumuamini zawadi kwa kila jambo na zawadi akapewa cheo cha usimamizi wa eneo lile na alipoona watu wapale hawamtilii tena mashaka alienda tena kujalibu kukaa katika eneo lile la baharini na kwabahati nzuri siku hiyo John John alikuwepo na alipomuona zawadi alimkumbatia na kumwambia inabidi twende wote kwasababu mahali hapa sio salama tena, lakini zawadi akamwambia John John usijali kabisa mimi nitakuwa katika eneo hili kukusaidia kuwakamata hawa majambazi kwasababu wanavyo onekana ni watu hatari sana na bila ya kuwa waangalizi jambo lolote baya laweza tokea, bora mimi wamenielewa ntaendelea kuwa nao mpaka mtakapo wakamata. John John hakutaka kuniacha pale Zawadi lakini kwakuwa zawadi aliomba sana John John ilimbidi aondoke japo kiukweli alionekana ameanza kuvutiwa sana na zawadi kwasababu jinsi alivyokuwa anawasiwasi na alivyo mkumbatia haikuonyesha kuwa ni wasiwasi wakawaida kwani alikuwa na Shahuku sana ya kumuona zawadi lakini upendo uliakisi kwa namna ambavyo alimuangalia zawadi aliweka wazi juu ya hisia zake kwa zawadi.
Zawadi alifurahi sana kuona angalau John John anaonyesha kumjali sana kwani binafsi awali alihisi kuwa John John aliwachukua watu wote nakuamua kumtelekeza yeye kwa makusudi jambo ambalo sio kweli kwani John John anamjali sana na kumthamini na ndio maana bila kujali alirudi tena kisiwani kwaajili yake tu lakini pia akampa na nafasi ya upendeleo ya yeye kuweza kusikia sauti za wazazi wake kupitia simu jambo lililo mfanya Zawadi afurahi sana.
Sikumoja wakati zawadi akielekea zake kulala katika himaya hiyo ya majambazi , moja kati ya jambazi aliwatuma watu wake, wakaenda kumteka zawadi na kisha wakampeleka kwake na yeye akambaka Zawadi bila huruma, jambo lililo pelekea mkuu wa majambazi hao kumuua jambazi yule kwani yeye pamoja nakuwa ni jambazi ila alikuwa akimchukulia zawadi kama dada yake wakike hivyo hakufurahishwa na kitu kile kilicho tokea. lakini pia baada ya zawadi kubakwa Zawadi alitawaliwa sana na hasira kiasi cha kuamua kuwauza majambazi hao kwa muda mfupi na kweli baada ya muda wa miezi sita zawadi akaongea na mmoja wa maafisa wale wa Usalama wa Taifa na kumpa taarifa zote kuhusu majambazi hao na jinsi ya kuweza kuvamia himaya yao John John alishangaa kwanini Zawadi hakutaka kukutana na yeye, lakini hakujali sana kwani alihisi zawadi hakutaka tu kumsumbua, lakini baada ya mfanyakazi wake kukutana na zawadi aliporudi kwa bosi wake alibakia kumuonea huruma tu John John kwa alicho kiona kwa Zawadi, lakini John John alipo muona afisa wake amerudi na hana raha alimuuliza 'zawadi yuko sawa?" Na afisa huyo alimjibu ndio yupo sawa lakini, John John alishtuka sana na kumwambia malizia lakini ninini, na ndipo afisa huyo akamwambia muheshimiwa zawadi ni mjamzito kwasasa na mimba yake ni kubwa. John John alishtuka sana na kukosa nguvu hata za kusimama kisha akamwambia afisa huyo amekwambia ni ya nani? Afisa huyo alimjibu tu kuwa kweli ni mjamzito lakini hataki kuongelea kuhusu mimba yake kabisa . John John alichukia sana na kumtuma afisa wake apeleke habari makao makuu ili wakavamie haraka.
Kweli baada ya muda watu walijipanga na kwenda kuvamia eneo hilo na kumkamata mkuu wa majambazi hao pamoja na watu wake na kisha wakaingizwa kwenye boti kupelekwa mjini kuhukumiwa kwa ujambazi wao, lakini baada ya boti ya waalifu hao kuondoka boti iliyofuata ilikuwa niya maafisa pamoja na zawadi , lakini chaajabu Zawadi aligoma kuingia kwenye boti hiyo na kuwaambia nyie mnaweza kwenda tu hakikisheni wanaadhibiwa wale ni watu hatari sana. John John alipata hasira sana na kumuuliza 'hivi wewe huelewi maana ya twende au, unataka tufanyejee tukufunge pingu ndo utaungana na sisi au vip . Zawadi alimwambia hapana nyie nendeni mimi ntaishi hapa na sitasababisha matatizo yoyote niaminini. Lakini mmoja kati ya maafisa usalama akamwambia zawadi twende kwani huniamini c tulisha ongea lakini zawadi alimwambi nimebadili mawazo , john akamwambia Zawadi kwani wewe upoje, kati yetu hakuna alie kwambia uwe na mahusiano na majambazi haya sasa wamekupa mimba wanaenda jela sisi tupo hapa tu kukusaidia unatuona wajinga hutaki kuongozana na sisi kwanini lakini unafanya hivyo.
zawadi alijisikia vibaya kwa maneno makali yaliyotoka katika kinywa cha john john na hapo ndo zawadi alikimbilia msituni ili kurudi katika himaya yao ili akakae huko huko ambako watu hawata muhukumu kwalolote lile lililotokea maishani mwake, John John alishangazwa sana na tabia ya Zawadi lakini kwasababu alikuwa na hasira nae juu ya mimba aliyokuwa ameibeba aliwaambia maafisa usalama tuondokeni lakini moja kati ya maafisa hao aliomba kubakia pale na zawadi lakini John John aliwaambia ni amri wote tunaondoka na kweli wakaondoka na kumuacha Zawadi pale. Zawadi alikuwa ni binti jasiri kwaaina flani hivi ya kutisha kwasababu aliishi katika msitu bila hata kuhofia kitu chochote japo alikuwa akishinda kulia na kulala kulia kila alipokuwa akiliangalia tumbo lake.
Sikumoja wakati John John alipoenda kumuhoji jambazi mkuu, jambazi huyo alimuuliza kwanza hali ya zawadi, lakini yeye alimwambia kabakia kule mliko mkuta awali. jambazi huyo alichukukia sana na kumwambia John John nyie hamna huruma kabisa nyie mnamuacha binti wawatu kule na nimjamzito pamoja na yeye kumisaidia, lakini John alimwambia hatukumtuma akafanye umalaya kule ilikuwa ni kufanya kazi tu ya nyie kukamatwa. jambazi huyo akamkaba shingo John John na baada ya watu kuja kumtoa mikono jambazi yule shingoni maw John John , jambazi huyo akamwambia John John hata sikumoja usimtukane zawadi kwasababu ntaakuua unamuita malaya wakati kama sio yeye kujitoa kumisaidia nyie kutukamata sisi, leo angekewa hajabakwa na kupata ile mimba lakini kwasababu yenu yote yametokea halafu mnamlaumu, mashetani wakubwa nyie. mtu hakuwa analala pamoja na mimba yake , anafanya kazi ngumu yote nyie mfanikiwe halafu leo kwenu hana thamani, kweli nimeamini nyie ni watu wabaya sana msio faaa kabisa hata kuwa na rafiki kama Zawadi.
John John alishtuka sana baada ya kusikia maneno hayo na hapo ndo akatoa amri jambazi huyo aingizwe gerezani kisha akamfuata afisa aliyekuwa karibu sana na zawadi kimawasiliano kisha akamwambia niambie kila kitu kuhusu mimba ya Zawadi, na hapo ndo afisa huyo alimwambia John John kweli zawadi alibakwa na aliembaka aliuliwa na jambazi tulie mkamata kwasababu yeye siku zote anamchukulia Zawadi kama dada kwake.
wakati John John anagundua hilo zawadi akampigia simu afisa huyo huku analia akimpa taarifa juu ya kuumwa kwake....
USIKOSE SEHEMU YA 14 $15