Tamthiliya: Challenge Made - Sehemu ya 1

Tamthiliya: Challenge Made - Sehemu ya 1

Hapa zawadi alipofikia anataka kunigombanisha na boss ananipaje mtoto kienyeji hivi? Ila boss wangu nae akili Hana anamnunia mrembo wakati anamuhitaji mpuuzi kweli huyu
kazi huna tenaa
 
TAMTHILIA: ZAWADI

MWANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS

SEHEMU YA : 16 NA 17 .

WHATSAPP NO: 0746115688.

John John alifungua kadi ya mtoto wa Zawadi na hapohapo hakutaka kuongea zaidi ya kuichana tu na maisha mengine yaendelea.
Asubuhi na mapema john John alipitia katika duka la suti akanunua suti kwaajili yake na zawadi kisha yeye akaivaaa yakwake dukani hapohapo na suti kwaajili ya Zawadi alienda nayo mpaka nyumbani anapoishi zawadi na kumpa suti ile ili avae, lakini cha ajabu alimkuta Zawadi amevaa mavazi ya ngozi ambayo alikuwa akivaa kabla ya wao kupata elimu juu ya mabadiliko.
John John alimuomba sana Zawadi avae mavazi aliyo mpatia lakini Zawadi alimwambia asante ila leo siwezi vaa mavazi tofauti na mavazi ambayo yata mtambulisha zawadi ninani .
Lakini John John alikuwa mgumu sana kuelewa kwasababu alikuwa amesha nunua mavazi kwaajili ya zawadi lakini wazazi wa Zawadi walimuomba John John amuelewe Zawadi. Baada ya muda John John alimuelewa tu Zawadi na hatimaye wakaanza safari yao ya kuelekea ikulu. Baada ya muda walifika ikulu na kwasababu walikuwa wageni maalimu kwa muheshimiwa rais walikaguliwa na moja kwa moja walipelekwa mpaka mahali ambapo muheshimiwa rais alikuwa amekaa, na baada tu ya wao kufika mahali ambapo rais alikuwepo John John aliombwa kuondoka kwani muheshimiwa alikuwa na maongezi muhimu na Zawadi.
Zawadi alimwambia muheshimiwa rais juu ya kila kitu ambacho watu wake wanataka na muheshimwa akamwambia zawadi ni ngumu kuwaruhusu watu wako warudi kule ni hatari wewe mwenyewe umejionea, hata hivyo Sisi tunaliweka kwanza pembeni eneo lile tutakacho fanya hatuta lifanyia chochote eneo lile kwasasa zaidi ya ulinzi na baada ya miaka kumi serikali italigeukia tena eneo lile na kuandaa mpango wakuanzisha hoteli kwaajili ya watu kupumzikia hasa hasa watalii na wakati huo wafanyakazi watakao pata kipaombele ni wakazi wote wazamani waeneo lile ambao ni nyie.
Kwasasa kuna nyumba zinajengwa kwaharaka sana na hivi tunavyoonge ziko hatua ya mwisho na nyumba hizo ni kwaajili ya watu wako kwani kila kaya itakabidhiwa nyumba pamoja na shamba likiwa na hati ya kuonyesha umiliki wao na watoto watasoma chini ya serikali na wazazi wao hawata sumbuliwa ada wala pesa kwaajili ya daftari kwasababu hilo ni jukumu la serikali ikiwemo na wao kupata kazi . lakini pia nimesikia habari kuhusu wewe ya kuwa uliokotwaga tu pembeni ya bahari nampaka sasa huna kumbukumbu yoyote juu ya wazazi wako na kutokana na hilo serikali imejitolea kukusaidia wewe kuwatafuta wazazi wako mpaka pale utakapo wapata.
Zawadi alimwambia muheshimiwa rais nashukuru sana kwahilo, lakini hilo suala la Wazazi wangu ungeachana nalo tu muheshimiwa kwani ni miaka kumi na nne imepita walilia na kusahau lakini nilio nao sasa hata walie hawata weza kusahau , hivyo sitaki kabisa kuondoka kwao kwani umri wao umeenda sana haipaswi kuwa na msongo wa mawazo tena hasa mama yangu.
Rais alimwambia zawadi naamini sikumoja utahitaji kujua kuhusu wao na utakapohitaji tu niambie. Zawadi alimwambia inawezekana nitakuja kweli kutamani kukutana na wewe hata kama sio kwaajili ya wazazi wangu lakini itakuwa ngumu kwasababu wewe unalindwa sana na watu wakawaida kama sisi hakuna ruhusa ya kukuona tutakavyo hata tukitaka. muheshimiwa rais alimuangalia sana Zawadi na akavutiwa nae kweli kwasababu ni binti wa umri mdogo ila haogopi kitu. rais alimuita John John na kumpa amri ya kumpokea zawadi kama mfanyakazi mwenzake na muheshimiwa akampa zawadi cheo kama cha john john. Zawadi alimuangalia sana muheshimiwa na kumuuliza hii ina maanisha mini mana mimi sielewi chochote kuhusiana na kazi za John John kwasababu sijapata hata elimu. Muheshimiwa rais alimuuliza Zawadi kama ni kwaajili ya nnchi yako miaka mitatu haitoshi kuwa mtu hatari kuliko John John aliye fanya kila njia mpaka akaweza kuwatoa nyie kisiwani jambo ambalo watu kibao walilikatia tamaa na watu wakaendelea kuteseka.
Zawadi alimwambia muheshimiwa rais naweza kufanya hivyo kwaajili ya watu wangu, nipe kazi muheshimiwa. Rais akachukua faili pembeni la mkataba wakazi na kumpa zawadi asaini na kumuapisha rasmi zawadi kama afisa usalama wa nnchi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, na kazi yake ya kwanza ni kuhakikisha ndani ya miaka mitatu chini ya usimamizi wa John John anakuwa hatari kuliko John John na kisha alikabidhiwa kitambulisho cha kazi rasmi kisha wakapeana mkono na rais na kisha Zawadi akamuaga rais lakini rais akawaambia hamtaweza kuondoka mpaka mpate mlo pamoja na mimi.
Basi zawadi na John John walishiriki mlo mmoja pamoja na rais na baada ya hapo wakasimama ili kuondoka lakini chaajabu Zawadi alipogeuza macho yake ukutani mwa Nyumba anayoishi rais alikutana na picha ya rais pamoja na John John tena muheshimiwa akiwa amemkumbatia John John kama vile mtu wake wa karibu. zawadi alishangaa sana lakini hakutaka kumuonyesha mtu yeyote kuwa yeye ameona hilo hivyo alizuga kwa kumpa mkono rais kisha wakatoka na John John akamrudisha zawadi mpaka anapoishi na kisha John John akakaa kusikiliza maoni ya watu wa Zawadi juu ya ofa ya rais na kwabahati nzuri hakuna yeyote aliyoonyesha kupinga, wote walifurahi kwani maisha yao hayatakuwa magumu kama walivyo zania . Zawadi hakuweza kuwaambia juu ya kazi yake mpya kwasababu ni siri yake yeye na Taifa.
John John aliaga na kuondoka lakini Zawadi akamwambia naomba nisamehe kwasababu mimi ni jukumu lako tena lakini John John alimwambia usijali, lakini unatakiwa kujua nimekupata miaka mitano hivyo uwe naheshima na kingine na weza kuwa kaka au rafiki kama ukitaka Zawadi na kusikiliza. lakini zawadi alicheka na kumkumbatia kisha akamwambia siwezi kuwa na kaka kichaa kama wewe hata kama umenipita umri, wewe utabakia kuwa kama rafiki tu. john John alicheka na kumtupia zawadi kijiwe kisha akapakia kwenye gari na kuanza safari rasmi ya kwenda nyumbani kwake kwani ilikuwa ni weekend. lakini wakati Zawadi anarudi ndani alishangaa kusikia honi za gari tena na alipogeuka alikuwa ni John John hivyo akamuuliza wewe tena. lakini John John akamwambia nilisahau kukupa tu taarifa kadi ya mwanao imechanika ila usijali kwasababu mpya inatengenezwa na kesho itakufikia kisha akafunga vioo vya gari na kuondoka. wakati gari ya John John inaondoka Zawadi alipogeuka nyuma chap kwani kunakitu alihisi na kweli alipogeuka aliwakuta watu wote walikuwa wanawachungulia madirishani. Zawadi alicheka sana nakuingia ndani huku akicheka lakini alipoingia tu ndani mama yake alimwambia John John anaonekana anakupenda sana lakini Zawadi hakumjibu mama yake chochote zaidi ya kuwaaga kuwa anaenda kumuangalia mtoto wake.
Asubuhi ilipo fika zawadi na watu wake waliendelea na shughuli zao lakini ghafla walikuja watu wakiwa wamebebelea mabahasha na kuwataarifu kuwa wameagizwa kutoka katika ofisi ya rais kwenda kuchukua majina yao ili waweze kuandaliwa hati za makazi yao na hivi karibuni nyumba zao zitakuwa tayari na wao wataachia nyumba wanayoishi kwasasa na kwenda kuishi katika miji yao. wote walifurahi sana na kujiandikisha majina yao na kisha watu hao wakaondoka . Zawadi alipokuwa ndani akimbembeleza mwanae alikumbuka picha aliyoiyona kwa muheshimiwa rais lakini alipofikiliaa kuuliza kwa yule rafiki ake Zawadi aliogopa hivyo ilimbidi amzuge tu rafiki yake kwasababu alikuwa amesha mpigia simu.
Siku iliyofuata Zawadi alitafutwa na elius na elius aliomba wakutane kwasababu kunajambo muhimu anataka kuongea nae. Zawadi alimwambia elius sawa tukutane lakini tutaonana wapi au utakuja nyumbani? Elius akamwambia zawadi nitakuja kukuchukua hapo nyumbani mida ya saa 10 mchana, zawadi alikubaliana na elius na elius akakata simu . Mida ya saa nane zawadi alikuwa akijiandaa ili gari iliyo tumwa na elius ikija kumchukua yeye awe tayari amesha jiandaa, baada ya muda kweli Zawadi alijiandaa na alivaa suti aliyo kuwa ameletewa na John John. lakini kabla ya Zawadi kuondoka John John alikuwa amekuja ilikuongea nae kuhusiana na kazi lakini alishangaa kumuona Zawadi akiwa amependeza sana tena amevalia suti aliyo mletea . John John alimuuliza 'Zawadi unaenda wapi'?. Zawadi akamwambia kunasehemu naenda mara moja, John John akamwambia sawa mi nilikuja kukwambia tu ya kuwa mtoto atakapo fikisha umri wa miezi sita itabidi umuache na bibi na babu yake ili mazoezi yaanze, kwani tunamiaka mitatu tu pekee japo mambo ya wewe kujifunza ni mengi. Zawadi alimwambia sawa na palepale gari ilkuja kumchukua zawadi . John john alimruhusu zawadi tu atangulie kisha yeye akasalimiana na Mfalme , Malkia pamoja na watu wengine kisha akawaaga. Lakini watu walimuomba akae japo angalau kidogo ila John John aliwaambia hapana kunakazi muhimu naenda kumalizia hapa nilikuja maramoja tu ili kumpa Zawadi taarifa muhimu Mfalme na Malkia hawakuwa na jinsi zaidi ya kumruhusu John John .
John John alipotoka tu alianza kuifuatilia gari iliyokuwa imemfuata Zawadi ili aweze kujua zawadi anaelekea wapi , lakini gari ilikwamia kwenye hoteli moja ya kifahali, jambo lililo mfanya John John ashtuke sana kwani zawadi ni mgeni hivyo ni ngumu kwayeye kwenda pale mwenyewe. Na kweli baada ya muda alimuona elius akiwa anampokea Zawadi na kuingia nae ndani ya hoteli hiyo, Machozi yalimtoka sana John John lakini baada ya muda aliona bora aondoke arudi zake kazini kwani alihisi ni ngumu sana kumpata zawadi kwasababu zawadi anampenda sana elius na sio yeye.
Lakini upande wapili elius alikuwa amemuita Zawadi ili kumjulisha kuwa baada ya week kutakuwa na kumbukumbu ya John John ya kuzaliwa na wao kama wafanyakazi wamepanga kumfanyia sherehe ya kuzaliwa bila ya yeye kujua na yeye wanamuhitaji katika sherehe hiyo. Zawadi alikubaliana na elius kuwa yeye atahudhulia katika sherehe hiyo wala asijali, kisha wakapata chakula na dereva akamrudisha zawadi nyumbani kwao.
John John alikuwa akikosa amani kila anapo muona elius kwani yeye alikuwa anampenda sana Zawadi lakini ukaribu ulipo baina ya elius na zawadi ulimfanya aamini kuwa wawili hao wanamahusiano ya kimapenzi. hivyo alikuwa akijitenga nao sana ili kuweza kuacha ukaribu nao na hata Zawadi alipokuwa akimtumia ujumbe wa kumjulia hali alikuwa hamjibu kabisa akiamini kuwa atamtoa moyoni akifanya hivyo jambo ambalo lilikuwa ni gumu sana kwake.
Kweli siku zikaenda na siku ya kuzaliwa ya John John ikawadia , na usiku huo John John alipokuwa anarudi kwake alikuta mlango umefunguliwa wakati yeye aliufunga, na hapohapo ndio John John aliingia akiwa ameshika bunduki huku akiwa na wasiwasi sana lakini alipo washa taa ghafla aliona watu wakiwa wamejaa na wote kwapamoja wakamuimbia wimbo kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa. John John alifurahi sana lakini baada tu yakumuona elius na Zawadi furaha yake ilikatika kwani kila anapo muona elius yupo pamoja na Zawadi imani yake inamwambia kuwa wawili hao ni wapenzi . Zawadi aligundua hilo kuwa John John baada ya kumuona tena furaha yake yote imetoweka, ila zawadi hakuwa na jinsi alichofanya ni kukaa mbali na macho ya John John.
Na kweli John John furaha yake ilirejea na wakakata keki watu wa kala na kunywa lakini kabla ya sherehe kufungwa elius alimwambia John John ongea hata neno moja basi kabla ya kulala na John John alisimama na kuwashukuru wotee kwakujali kuhusu yeye, lakini elius alimwambia John John hakuna kitu chochote unataka kusema zaidi lakini John John alimwambia mimi sina chochote cha kumwambia yeyote .
Elius alivyoona John John kasema hana cha kumwambia yeyote yeye alipiga goti na kutoa pete katika mfuko wake na kumuita zawadi kisha akamwambia nakupenda sana zawadi kama huto jali kuwa namimi siku zote za maisha yangu, naomba ni kuoe tafadhali kuwa mke wangu.......

USIKOSE SEHEMU YA 18 NA 19
 
Back
Top Bottom