Tamthiliya: Challenge Made - Sehemu ya 1

winnie9999

Member
Nov 27, 2021
65
102
TAMTHILIYA: CHALLENGE MADE.
SEHEMU: 1

MUANDISHI: WINIFRIDA THOBIAS.

Usiku wa saa tano katika hospitali moja iliyopo nnje kidogo ya jiji la dar es salaam alionekana mwanamke mmoja aliyekuwa akijalibu kutoka kwa siri hospitalini hapo huku akiwa ni mjamzito wa mimba ya kama miezi nane,tisa au saba hivi.

Mwanamke huyo alikuwa akitoka taratibu sana katika hospitali hiyo huku akiwa anaogopa sana. Geti la hospitali hiyo lilikuwa mbali kidogo na jengo la maabara pamoja na hodi za wagonjwa hali iliyo pelekea mama huyo kuwakwepa walinzi wengi walio kuwa windo usiku huo katika sehemu mbalimbali ndani ya hospitali hiyo ilikuweza kufika Getini.

Lakini kwa bahati mbaya kabla ya mwanamke huyo kufanikiwa kufika getini moja kati ya madaktari wa zamu aligundua Ndani ya hodi ya wakinamama kuna mwanamama mmoja hayupo na bila ya kupoteze muda Daktari huyo alienda kuwajulisha watu waliokuwa katika chumba cha CCTV iliwaweze kumtafuta mwanamama huyo kutumia camera kabla hajatoka nnje ya hospitali kwani itakuwa hatari zaidi kwa mmiliki wa hospitali hiyo aliye fahamika kwa jina la Jackbosi.

Wafanya kazi wote wa hospitali hiyoo waliogopa sana kwani bosi wao pia atawauwa kama mwanamke huyo atafanikiwa kutoka nnje ya hospitali hiyo kwasababu mambo yaliyokuwa ya kiendelea katika hospitali hiyo ni yasiri sana na haipaswi kutolewa nnje ya eneo la hospitalini. Mkuu wa ulinzi aliamuru ulinzi uongezeke katika maeneo yote ya hospitalini haswa eneo la Getini.

Baada tu ya mwanamke huyo kuona ghafla ulinzi unaongezeka sana sehemu za Getini na pande mbalimbali za hospitalini aligundua kuwa tayari walinzi na madaktari Wameshagundua kuwa yeye anajaribu kutoroka na Kutokana na ulinzi ulivyo kuwa umeongezeke ilikuwa ni ngumu sana kwa mwanamke huyo kutoroka usiku huo hivyo aliamua kurudi ndani kwakupitia njia za siri za hospitali hiyo bila ya mtu yeyote kumuona .'kwaufupi tu nikuwa mwanamke huyo alionekana kuijua hospitali hiyo vizuri kuliko mtu yeyote alie kuwepo katika hospitali hiyoo'.

Walinzi walimtafuta sana mwanamke huyo lakini hawakuweza kumpata kwani hawakujua mwanamke huyo amejificha upande gani, madaktari waliogopa sana hivyo waliamua kumjulisha bosi wao Jack Bosi juu ya jambo lililotokea la kutoroka kwa mwanamke huyo, Jack bosi alishtuka sana na hasira zilimtawala kwa uzembe uliofanywa na walinzi pamoja na madaktari waliokuwa chini yake na bila ya kupoteza muda alianza safari ya kuelekea hospitalini huku akiongozwa na walinzi wake kutoka nyumbani kwake Masaki kuelekea katika hospitali yake ya siri baada tu ya Jackbosi kufika alianza kwa kuwagombeza vikali sana Madaktari pamoja na Walinzi wazamu wa usiku huo na kutokana na hasira ilivyo mtawala kwa wakati huo aliwapiga walinzi Wake watano risasi za miguu na bila ya huruma aliwaamuru walinzi hao wasimame kama hamna kilichotokea.

Jack bosi aliwapa masaa matatu walinzi wake Mwanamke huyo awe amepatikana kisha yeye na baadhi ya madaktari pamoja na walinzi wake walielekea katika hodi zakinamama wengine na kuwatoa wote n'je mida ya saa nane usiku na kuanza kuwatesa vikali na kuwaahidi kifo kama hawata sema mahali ambapo mwanamke huyo ameenda.

Wakati ambapo walinzi walikuwa wakiendelea kumtafuta mwanamama huyo na Jack Bosi nayeye aliendelea kuwataabisha Wakinamama wengine bila kujali wakinamama hao wamechoka na muda wowote watatakiwa kujifungua .

Baada ya mateso kuwa yamezidi kwa kinamama hao aliyekuwa kiranja wakinamama hao ambaye alifahamika kwa jina la Abi alichoka na mateso yaliyo kuwa yakiendelea hivyo alimwambia Jack Bosi aliyekuwa akipanga mipango ya kutoroka kwa grace ni jasmin jambo ambalo halikuwa la kweli kwani Abi aliamua kumsingizia jasmini kwasababu jasmini alikua akipendwa na kila mtu kuliko hata yeye ambaye ndo kiranja wakina mama hao , kwani alihisi sikumoja jasmini atachukua nafasi yake ya ukiranja.

Jack bosi baada ya kusikia hivyo kutoka kwa Abi ya kuwa jasmini ndo alipanga mipango ya grace kutoroka aliamuru haraka sana jasmini asogezwe miguuni mwake na wakinamama wengine wote wasogezwe pembeni kisha alianza kumpa mateso makali jasmini lakini jasmini hakuweza kusema chochote kwani hakuwa anajua lolote kuhusu grace kwani nikweli jasmini alikuwa rafiki wa grace lakini grace hakuwa tayari kumshirikisha mtu katika mambo yake ya hatari aliyo kuwa akiyafanya, Lakini kwasababu Jack Bosi alikuwa akimuamini sana Abi aliamua kumuua jasmini palepale na ujauzito wake baada ya kuona haongei chochote kuhusu grace alipoelekea.

Lakini wakati huohuo walinzi walirudi na kumwambia hawakumuona mwanamke huyo hospitali nzima isipokuwa kuna chumba kimoja kimefungwa na kunasauti ya mtu inasikika katika chumba hicho lakini tumeshindwa kukiifungua kwasababu kimefungwa kwa kufuri napia kinaonekana ni chumba cha siri sana kwasababu mlango wake ulikuwa umefunikwa kwa pazia jeusi .

Jack Bosi aliamuru wakinamama waongezewe ulinzi pia aliwaambia walinzi wake ya kuwa 'huyo mwanamke msimuite tena mwanamke jina lake ni grace' kisha akawaambia walinzi wake haya twendeni ikiwezekana hicho chumba kikavunjwe ili tuweze kujua huyo grace ni nani hasa'.

Jack Bosi pamoja na walinzi wake walielekea eneo ambalo mlango huo upo na kuamuru walinzi wauvunje haraka kwani yeye pia hakuwa anajua kunachumba cha siri hospitalini hapo ila hakuonyesha kuwa hajui chochote kuhusu chumba hicho mbele ya walinzi wake kwani alikuwa na Shauku ya kuweza kumjua vizuri mwanamke huyo anayejua mambo mengi kuliko hata yeye , walinzi walihangaika sana kuuvunja mlango huo lakini ilichukua muda kufanikiwa kuuvunja mlango kwani mlango huo ulitengenezwa kwa uimara sana.

Lakini baada ya kama lisaa hivi walinzi walifanikiwa kufungua mlango na wote waliokuwa katika eneo hilo walimuona grace akiwa ameshashikwa na uchungu na tayari chupa la uzazi limeisha pasuka tayari kwa mtoto kutoka na chaajabu zaidi ni kuwa grace alikuwa amefanana kilakitu na Jackbosi .

End
 
TAMTHILIA: CHALLENGE MADE
SEHEMU: 2
MUANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS

Jackbosi alishangaa sana kumuona mtu anaefanana nayeye katika hospitali ambayo yeye pamoja na washirika wenzie wamekuwa wakifanya uchafu wao, Jackbosi alitamani kumuuliza maswali mengi sana grace lakini muda haukuwa rafiki kwasababu tayari mtoto alikuwa ameshaanza kutoka tumboni mwa grace hivyo Jackbosi ilimbidi awafukuze walinzi wote kisha amsaidie grace kujifungua na kwabahati nzuri grace alifanikiwa kujifungua salama na kupata mtoto wakike jambo ambalo lililomfanya grace atabasamu nakusahau shida zote alizokuwa akipitia wakati alipokuwa amebeba ujauzito wa mtoto huyo.

Jackbosi alimsafisha mtoto huyo na kumwambia grace hongera umepata mtoto wa kike, grace alimuangalia Jackbosi kwa hasira na kumwambia huyo mtoto unauhakika ni wangu ?. Jackbosi hakumjibu chochote grace alichofanya ni kuamuru walinzi wamchukue mtoto wampeleke hodini na grace apelekwe ofisini Kwake kwa mahojiano zaidi . Lakini Kabla ya Jackbosi kufika ofisini kwake na grace simu ya Jackbosi iliita na aliye kuwa akipiga alikuwa anaitwa Mr.Kivuli ambae huyo ndo msimamizi wawanachama wote wanaoshirikiana kuendesha shuhuli zote zinazo fanyika hospitalini hapo. Jackbosi aliongea na Mr.kivuli faragha na alipomaliza kuongea na simu aliwaambia walinzi wake waongozane nae pamoja na grace kuelekea hodini ataongea na grace atakaporudi kwasasa anahitajika kwenda kufanya jambo muhimu.

Lakini kabla hajaondoka Jackbosi alienda kuwaambia wakinamama wote hodini akiwemo grace kuwa atakae jalibu kutoroka wakati huu sitamuua yeye tu bali wote mtakufa kwenye mikono yangu kumbukeni hilo. Wakina mama wote walijenga chuki na grace kwani waliamini kama sio yeye kujalibu kutoroka jasmini asinge kufa lakini pia vitisho visinge kuwepo kila wakati . Hata hivyo grace huwa hajali kabisa kutengwa na wakinamama hao kwasababu sikuzote wamekuwa wakifanya hivyo japo grace hakuwa anajua nini haswa kiliendelea hodini alipo kuwa akijalibu kutoroka, mpaka pale ambapo Ade alipo muuliza mlinzi kama watapata nafasi ya kumzika jasmini na mlinzi akamjibu ucjali kuhusu yeye ameshakufa jali kuhusu wewe ambae kama si leo ni kesho utakuwa umekufa ' kisha mlinzi alicheka sana na kuondoka zake.

Wote waliogopa sana lakini mwanamke mmoja kati yao aliuliza 'hivi inawezekanaje jasmini apigwe risasi halafu tusione damu hata tone baada ya mwili wake kuondolewa pale' ?, Ade aliwaambia kwa hasira hayatuhusu tufanyeni kazi zinazo tuhusu kama vile kuhakisha tunajifungua salama na kukabidhi watoto wakiwa hai la sivyo chakula hatuta pata na ndugu zetu wataisha wote.wakinamama walinyamaza nakumtupia maneno ya lawama grace japo grace hakuonekana kujali chochote na ndio kwanza alijifunika kwa shuka lake na kuwaambia 'mda wenu wakutamba huwa ni mchana na ndio maana nyie niwaongeaji sana na usiku mnakuwa mmechoka sana lakini mimi usiku ndio muda wangu mzuri nandio maana nawekeza akili yangu yote mchana ili usiku niwe macho kwaajili yenu wote' .

Ade alimuangalia sana grace nakuongea moyoni mwake ya kuwa 'grace Leo haijalishi nini kitatoke lakini lazima tutatoka wote kwasababu natamani kujua kwanini ulinishawishi kuja hapa halafu unaonekana haujali kabisa kuhusu mimi'.

Jackbosi alipo kuwa njiani akielekea kwa Mr.Kivuli simu yake iliita na alipo pokea Mr. Kivuli alimpa kazi ya kwenda airport kumpokea muwekezaji wao mpya, Jackbosi alimwambia Mr.kivuli sawa nimekuelewa na hapohapo akampa amri mlinzi wake ageuze gari waelekee airport. lakini chaajabu wakati Mlinzi wa Jackbosi anabadili muelekeo wa gari yao ili waelekea airport kumpokea muwekezaji mpya gari iliyo kuwa nyuma yao nayo ikaonekana kuwafuatia kwa nyuma na alipokuwa akipunguza mwendo nayo pia ilipunguza mwendo kama wao, Jackbosi alipata hisia mbaya alihisi pengine ni wapinzani wenzao wa kibiashara hivyo aliamuru gari isimamishwe kisha akachukua bunduki yake nakuweka risasi pia akawaambia walinzi wake Msitoke nnje ya gari kisha yeye akalifuata gari lile kwani nalo lilisimama baada tu ya gari ya Jackbosi kusimama.

Jackbosi aliwasogelea na kuwanyooshea bunduki lakini alipo waangalia watu waliokuwa ndani ya gari hiyo aligundua wote ni wazee hivyo alipasua tu magurudumu ya gari Lao kwa bunduki bila kuongea chochote na kuwafanyia chochote kisha akarudi kwenye gari yake kuelekea airport. baada ya magurudumu ya wazee hao kupasuliwa kwa bunduki waliwasiliana na mtu na kumpa taarifa ya kilicho tokea haikupita mda pikipiki nne zililetwa kwaajili yao na hapo ndo safari yao ikaamza rasmi tena kumfuata Jackbosi kwani kwa namna yeyote ile Jackbosi anahitajika na bosi wao.

Jackbosi alipofika airport alimpokea muwekezaji kwa heshima na kumuomba aongozane na mlinzi wake yeye kunamajukumu muhimu anahitajika kuyafanikisha , muwekezaji alikubaliana nayeye kwani hata hivyo mkutano wa uwekezaji ulikuwa siku inayofuata na yeye alihitaji kupumzika kwani alikua amechoka sana na safari, Jackbosi alimpakazi moja ya mlinzi wake ampeleke muwekezaji huyo nyumbani kwake yeye ili na yeye akaongee na grace.

wakati mlinzi wake anaanza safari ya kumpeleka muwekezaji huyo nyumbani kwa Jackbosi na Jackbosi naye alianza safari kuelekea hospitalini akiwa katikati ya safari ghafla mbele yake alishtuka kuona pikipiki nne mbele ambazo zilimzuia yeye kuendelea na safari yake , Jackbosi alimuamuru mlinzi wake asimamishe gari kisha akatoka nnje kuwafokea kwani alihisi ni watu wanaojifunza kuendesha pikipiki kwenye Barabara kubwa na kama kawaida yake aliwaambia walinzi wake wasimfuate. Alipokuwa akikaribia pikipiki hizo madereva wa pikipiki wote walivua kofia za pikipiki na hapo ndipo jackbosi aligundua ni walewale wazee aliowadharau awali na hapo ndipo aliona kumbe wapo serious hivyo moja kwa moja aliwauliza 'mnataka nini kwangu' ? , lakini hawakumjibu walimpiga na kitukizito kichwani na palepale akapoteza fahamu kisha watu hao wakampigia bosi wao simu kumjulisha kwamba kazi imeisha. Chakushangaza zaidi ni kuwa walinzi wa Jackbosi nao walikuwa pamoja na watu waliomteka Jackbosi kwani baada ya Jackbosi kupoteza fahamu wao walili sukuma gari la Jackbosi sehemu ambayo mtu hawezi ona kisha wakafuatana na watekaji tena wakiwa na furaha.

Mida ya saambili kama kawaida grace aliiba mavazi ya mlinzi kisha akavalia kama mlinzi na akambusu mtoto wake kisha akawaambia wakinamama usiku mwema na nisameheni kwasababu nafanya hivi kutokana na nyie hamuwezi kufunga midomo yenu, wote walimuangalia kwa hasira lakini grace hakujali alitoa dawa mfano wa vumbi na kuwapulizia wote na hapohapo wakapitiwa na usingizi mzito kisha akawalaza vizuri na kuanza kutoka nnje na kila alipopita safari hii alipuliza dawa nakupiga kamera za ulinzi risasi kisha akachukua pikipiki inayotumikaga kuchukua mahitaji muhimu ya hospitalini na alipofika Getini alifunguliwa geti bila kikwazo chochote kwani alikuwa amevalia kofia ya pikipiki pamoja na Miwani hivyo ilikuwa ngumu walinzi kujua ni grace na kabla ya kutoka aliwapulizia dawa walinzi wa Getini kisha akatoka nakufunga geti ili watakapoamka wasihisi kitu chochote kibaya.

Alipo toka tu Getini na pikipiki alienda nayo umbali mdogo tu kisha akaificha sehemu ya msituni kidogo na yeye akaanza kutembea kwa miguu umbali kidogo tu kisha mbele yake kulikuwa na Magari manne ya kifahali na walinzi wasiopungua Kumi na wote baada ya kumuona grace waliinamisha vichwa vyao chini na kumwambia grace unaendeleaje bosi.



USIKOSE KUSOMA SEHUMU YA 3 HAPO KESHO ILI UWEZE KUJUA JE GRACE NI NANI ? NANI KWANINI ANAONEKANA NI MTU MZITO MWENYE PESA ZAKE LAKINI BADO YUPO NDANI YA HOSPITALI YENYE MATESO KIASI KILE? NA JE JACKBOSI KWANINI KATEKWA PIA KWANINI YEYE ANAFANANA SANA NA GRACE ? NA JE KUNA KAZI GANI GANI INAYOFANYIKA HOSPITALINI AMBAYO WATU WA N'JE HAWATAKIWI KUJUA ?
ASANTENI SANA.
 
TAMTHILIA: CHALLENGE MADE
MUANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS
SEHEMU: 3 $ 4
WhatsApp: 0746115688

Baada ya walinzi hao kuuliza hali ya bosi wao grace, grace aliwaambia yuko powa na hawana muda wa kupoteza inabidi waelekee mahali mzigo ulipo. Baada ya kusema hivyo grace akaingia kwenye gari pamoja na walinzi wake na safari yake ilianza na kwenda kukomea kwenye jumba moja kubwa la kifahali ambalo lina kila aina ya vitu ambavyo kila binadamu angetamani kuvipata. Grace alishuka kwenye gari na kuingia ndani ya nyumba hiyo walinzi wake wakiwa nyuma yake mda wote.

Moja kwa moja grace alielekea kwenye chumba kilichokuwa maalumu kwaajili ya mziki na kuamuru walinzi wake wamletee mzigo wake , bila ya kuchelewa walinzi wake walimleta Jackbosi mbele yake na wale wazee wanne ambao Jackbosi aliwapuuzia awali walikuwa mbele yake na kutoa nywele bandai za mvi walizo kuwa wamevaa, jambo lililo mfanya Jackbosi ashangae sana na kuogopa lakini wakati yupo kwenye mshangao alishtushwa na sauti ya mtu aliemuita grace bosi jambo lililo mfanya akacheka sana na kumwambia grace kama huto jali nimiminie kinywaji, grace alimimina kinywaji na kumpatia Jackbosi kisha akawaamuru walinzi wote wa muache pamoja na Jackbosi kwani wanamazungumzo muhimu sana .

Walinzi wa grace Walitoka na baada ya Jackbosi kuona walinzi wote wamesha ondoka alisimama na kumpiga ngumi ya uso grace lakini grace hakuweza hata kutikisika kwa ngumi jiwe aliyo pokea kutoka kwa Jackbosi kwasababu mwili wake yeye ni sawa na chuma kwani unamazoezi ya kutosha na umeshazoea maumivu ya ngumi, Jackbosi baada ya kuona hata mkono wake tu nao umeshindwa kumpiga grace aliamua tu kumuuliza grace huku akiwa anatabasamu aliuliza ' wewe ninani Grace?

Grace alimwambia naitwa grace na hicho ndo kitu muhimu unacho paswa kujua kwasasa kwasababu ukijua hata kidogo kuhusu mimi nakuapia tuta kupoteza. Jackbosi alimwambia grace najua kunakitu unataka kutoka kwangu sijui ninini, lakini unapaswa kujua bila kuniambia wewe ninani siwezi kukwambia chochote. lakini grace alimwambia Jackbosi vip kama nikikwambia nataka wamama wote waliopo katika hospitali unayo miliki, pamoja na wale ulio waficha huku ukiendelea kumdanganya Mr.Kivuli ya kuwa umewaua ? Tafadhali Jackbosi kwa amani tu naomba unifanye mimi kuwa wewe ili niweze kuwasaidia watu wote ulio wahifadhi ukidanganya umewaua ili waweze kuishi maisha yao ya amani.

Jackbosi alimuangalia sana grace na kumuuliza ni kitu gani unajua zaidi ? Baada ya swali hilo kutoka kwa Jackbosi grace alimuuliza pia, 'unajua kwanini watoto wanaolelewa katika hospitali yako wakifika umri wa miaka ishirini wanapelekwa nnje ya nchi na wazazi wao wanachukuliwa na Mr.kivuli na huwaonagi tena mbele ya macho yako? Jackbosi hakuwa na jibu juu ya swali la grace ila grace alimwambia moja kwa moja ya kuwa wewe unahusika pia kwa kinacho tokea kwa watoto hao sema nakuhurumia kwasababu hujui chochote.

Jackbosi huwa hapendi kudharauliwa hivyo baada ya kuona grace anamwambia hajui chochote alimwambia wakinamama unao waona pale tuna wasaidia kukuza mimba zao na kuwapa watoto wao malezi bora na k kila wanacho hitaji pia watoto wao wanapofikisha umri wa miaka ishirini bosi wangu na baba yangu pia Mr. kuvuli anawatafutia nafasi za kwenda kusoma nchi za nnje na huko ndo wenyewe wanapotelea hivyo huna haja ya kunilaumu mimi wala bosi wangu kwani sisi huwa tunafanya kama Msaada kwani wazazi wao hawawezi kukizi mahitaji ya watoto wao.

Grace alicheka sana na kumwambia Jackbosi pole sana kwasababu ya kila kitu ulicho danganywa na kugeuzwa kuwa kama mtoto mdogo anaetii amri bila kujua watu wangapi mpaka sasa anawapoteza kwa kosa la yeye kutii amri zilizoleta madhara makubwa kwenye maisha ya watu wengi sanaa. Jackbosi alimuangalia sana grace lakini grace alimwambia watoto wote ambao ulikuwa ukiambiwa wanapelekwa nchi za nnje ni uongo mkubwa sana kwani kitendo chawewe kuwafuatiliaga viza, kuwakatia tiketi za ndege na kuwasindikiza airport unawapelekea vifo vyao karibu kama ulikuwa hujui basi mimi leo na kwambia watoto hao wanapotoka nnje ya Tanzania wanaenda kuwa marehemu na mama zao hugeuzwa Kuwa machizi tena wasio tibika. Jackbosi alimuangalia sana grace na kumuuliza 'grace unamaanisha nini wewe shetani ?

Grace alipata hasira baada ya Jackbosi kumuita shetani alikupasua glass yake ya kinywaji kwa mkono wake na kusababisha mkono wake kutokwa na damu sana lakini yeye alikuwa hajali na alichofanya ni kumshika mkono Jackbosi na kumwambia leo inabidi wewe ujifunze kitu kuwa mimi na wewe nani shetani na nani malaika. Moja kwa moja grace aliingia na Jackbosi katika chumba ambacho kilikuwa kimejaa wakina mama ambao wanaupungufu waakili na kila mmoja alikuwa amebeba mdoli mkononi akidai ni mwanae, Jackbosi alijikuta akimwaga machozi na kumuuliza grace 'hii inamaanisha nini' ? na hapo ndipo grace alimshika tena mkono Jackbosi na kumuingiza chumba ambacho kinamzee mmoja ambae umri wake umeenda sana hata kupumua kwenyewe ni shida kwake hivyo anatumia mashine kupumbua na mwili wake ulikuwa haufanyi kazi kabisa na jina lake mzee huyo lilikuwa Steven, Jackbosi alizidi kushangazwa sana na maneno ya grace lakini hakuwa na chakufanya zaidi ya kumuuliza tena na tena 'wewe ni nani grace' ? Na mbona unajua mambo mengi ya kutisha hivi?

Grace hakumjibu chochote Jackbosi ila alimuuliza 'kwanini kama bosi wako Mr.kivuli anafanya kazi ya kusaidia watu wenye shida bado anajificha wakati wachungaji, vituo vya yatima na watu wengine wote wanaotoa Msaada wote pamoja na vituo vyao tunaishi nao kwenye mwanga kwanini yeye yupo Gizani tu'? Jackbosi alimwambia grace kama huwezi kuwa muwazi bhasi niue au unitoe nnje ya nyumba yako kwasababu sijazoea methali na mafumbo. Grace akamwambia Jackbosi Mr.kivuli hawasaidii wamama unao waona katika eneo lile la hospitali bali wale wamama ndo wanao kufanya wewe pamoja na yeye muonekane watu wazuri na wenye pesa za kutosha . Wakinamama wote unao waona hapa ndani leo hii walidanganywa wametafutiwa kazi nchi za nnje pamoja na mawakala bandai wa Mr.kivuli na kuahidiwa mishahara mizuri ambayo kwa maisha magumu walio kuwa wanaishi wasinge weza kupata pesa kama hizo hata kama wangeamua kujitoa kufanya kazi usiku na mchana .

Mr.kuvuli alijifanya kuwa mwema kwao kwani kabla hajawachukua alikuwa akiwasaidia ndugu za wakinamama hawa kwenye mambo muhimu kama kuwapa fedha za upasuaji kwa wagonjwa walio nao, na ada za watoto wao kwa wenye watoto ambao wameshindwa kuwaendeleza na masomo kwasababu ya kushindwa kulipa ada, pia kuwapelekea magunia ya vyakula mbalimbali hali iliyo pelelekea wakina mama hawa kushawishika na misaada hiyo na kukubali kutafutiwa viza ili wakafanye kazi nnje ya nchi watengeneze pesa kama Mr.kivuli alivyowaambia . Lakini baada ya viza kukamilika kwakuwa Mr.kivuli tayari alikuwa amejenga uaminifu kwa nduguzao pamoja na wakinamama hawa, ndugu zao hawakuwa na wasiwasi walikabidhi ndugu zao kwa Mr.kivuli na kusaini mikataba ambayo ilimlinda yeye na kumfanya asiusishwe na kurudi au kutokurudi kwa wakina mama hawa.

Kilichofuata baada ya kuwachukua moja kwa moja aliwapeleka kwenye hospitali unayoiangalia wewe kwa sasa na kwakutumia madaktari wake ambao kwasasa wote nimesha waua aliwapandikiza wanawake hawa mbegu za wanaume wasio wajua na kwabahati nzuri au mbaya siku alipokuwa akiwapandikiza mbegu hizo wakinamama hawa mwanamama mmoja alikosa mbegu za kupandikizwa hivyo alimuomba mlinzi wake mmoja amsaidie kutoa mbegu halafu atampa pesa za kutosha, kwasababu mlinzi huyo alikuwa na shida alilizika na kutolewa mbegu kitendo ambacho kilimpelekea yeye kupoteza nguvu zake za kiume maishani mwake na mwanaume mwenyewe ndo mzee huyu unae muona anaitwa Steven,Jackbosi alishangaa sana,

Lakini grace alimwambia Jackbosi baada ya wakinamama hawa kupandikizwa mbegu aliwaambia cha umuhimu ni kuhakisha wanazaa watoto wakiwa salama na kwakuwa hakuna aliejua nini kitawatokea baada ya kujifungua wakinamama hawa hawakuwa na shida walilea mimba na kufanikiwa kupata watoto wao na kwabahati nzuri mwanamke aliyepandikizwa mbegu za Steven alifanikiwa kupata watoto wakike mapacha na mwanamke huyo alikuwa akiitwa Maria ambae aliwapenda sana wanae kuliko chochote na ukizingatia pia yeye alikuwa ndio mwanamke pekee anaemjua baba wa watoto wake.

Miaka mitano baada ya wakina mama hawa kupata watoto , sikumoja wakati Maria alipokuwa akipita ofisini alimsikia Mr.kivuli akipanga mipango ya kuwalea watoto wao mpaka watakapofikisha miaka ishirini kisha atawapeleka nchi Za nnje kuwatoa viungo vya ndani kama figo,ini,pamoja na moyo ilikuweza kuingiza mamilioni ya pesa.

Maria alichukia sana na kwabahati nzuri Steven Naye alimsikia Mr.kivuli pamoja na rafiki ake mmoja aliye kuwa mbunge wakipanga mipango mibaya juu ya watoto hao . Maria na Steven waliamua kuwatorosha watoto wao pamoja na yeye lakini maria hakuona ni busara kuondoka yeye na kuwaacha wanawake wenzie hivyo aliwapa siri ya kinachoendelea pale ili waweze kukubaliana nae na watoroke lakini mwanamke mmoja alieitwa Elizabeth alimuona maria ni muongo naana taka kupata vyeo nakuonekana mwema kwakila mtu hivyo aliwajaza wenzake ujinga na wote wakakataa kutoroka maria hakuwa na jinsi alimuomba Steven atafute usafiri saa tisa usiku wao watatoroka.

Steven aliandaa kila kitu na muda ambao maria alikuwa anatoroka walinzi hawakuwepo upande wa Getini hivyo alifanikiwa kutoka yeye pamoja na wanae salama kabisa lakini baada ya kuingia ndani ya gari maria alijisikia vibaya kuwaacha wenzie hivyo aliamua bora arudi tu ndani kuwaokoa wakina mama wengine au angalau hata mmoja lakini alipo ingia ndani wote walikataa na alipo kuwa akirudi Getini ili aondoke moja ya walinzi wa zamu siku hiyo alimuona na kumpigia risasi ya mguu kisha akafungiwa chumba cha adhabu na chumba chenyewe ni kile chumba cha siri ambacho wewe ulidai ni chumba cha kuhifadhi vifaa kitu ambacho sio kweli kwani chumba kile kilikuwa chumba cha adhabu na ulifichwa kwasababu usingekubali kusimamia hospitali ya baba yako feki , Jackbosi alibaki alimuangalia tu grace huku mate ya kimdondoka kama maji ya tiririkayo katika maporomoko ya milima ya usambala .

Grace aliendelea kwa kusema siku iliyo afuata ilikuwa ndio kiama cha maria kwani alitolewa mbele ya wenzie kwa lengo tu la yeye kupewa adhabu za kawaida na kuendelea kuishi hospitalini hapo hata kama watoto wake walitoroshwa, lakini Maria alimwambia Mr.kivuli unajisikiaje kuwadanganya wakinamama hawa kwakuwapa matumaini ya kuwalea watoto wao halafu baada ya hapo wewe na muheshimiwa mbunge mna wasafirisha nnje na kuwatoa viungo muhimu vya miili yao na kuwatupa kwenye bahari za ugenini wawe chakula cha mamba ?. Mr.kivuli alishtuka sana nakumuua palepale maria kwakumpiga risasi ya kichwa kisha akawaambia wakinamama kwakuwa mmeshajua kazi iliyo waleta hapa pambaneni muifanye yasiyo wahusu yasiwasumbue kabisa kwasababu mkifanya tofauti sio hao watoto wenu tu bali wote mtapotea.

Elizabeth alijisikia vibaya sana baada ya kujua maria alikuwa sahihi na toka siku hio amebakia kujilaumu kwa kifo cha maria na ndio maana mpaka sasa pamoja na kuwa amechanganyikiwa ila kila mara amekuwa akilia 'maria usife nisamehe na twende wote'. Jackbosi alishtuka sana na kumwambia grace ilikuaje wakinamama hawa wakatoroka na je watoto wamaria wako wapi ? Grace alimwambia Jackbosi baada ya kifo cha maria wanawake walijalibu sana kutoroka na watoto wao lakini kila walipo kamatwa waliuliwa mpaka wakabakia wakinamama hawa kumi ambao baada ya watoto wao kufikisha miaka ishirini Mr. Kivuli aliwachukua na kuwapeleka nnje ya nchi kisha akachukua video za watoto wao wakifanyiwa upasuaji mpaka wanapo kufa na bahari ambayo miili yao utupwa na kuliwa na Samaki kisha akawaonyesha wakinamama hao na baada ya kuwaonyesha video hiyo wakinamama wote walifanyiwa upasuaji nakuwekewa chip kichwani mwao ambazo zimewafanya kuwavichaa na kupoteza kumbukumbu kila dakika na endapo utahitaji kuondoa chip hizo kifo ndo matokeo na ndio maana mpaka leo hakuna aliye jalibu kutoa chip walizo nazo kichwani kwani ndo uhai wao, pia grace alimwambia wakina mama hawa walifika hapa kwa msaada wa Steve kwani Mr.kivuli baada ya kazi yake kuisha kwa wanawake hawa aliamuru usiku Wamanane wote wakatelekezwe barabarani na kwakuwa wana muda mrefu maisha yao yamekuwa ndani naukizingatia akili zao hazipo sawa itakuwa rahisi kwa wao kugongwa na magari na kufa kama Ajali.

Baada ya Steve kusikia mpango huo alimuomba Mr.kivuli ruhusa siku hiyo kisha akaenda kutega mahali ambapo wanawake hao wali mwagwa na baada ya walinzi wote kuondoka aliwachukua na kuwapeleka kwake na hapo ndo alianza kuishi nao nakuacha kufanya kazi rasmi na Mr.kivuli bila ya kumpa taarifa yeyote jambo lililo mfanya Steven kuchomwa sindano na Mr.kivuli miaka kumi baadae walipokutana nae katika soko la hisa kwenye kampuni kubwa ya usafirishaji ya GRAJA ambayo Steven ndo alikuwa mwenyekiti.

Jackbosi alimuuliza grace vipi mbona huja niambia kuhusu watoto wa maria ? , grace akamwambia Jackbosi usiku ule watoto wa maria walifanikiwa kutoroshwa na hao ndio watoto pekee ambao tokea hospitali ile kuanzishwa wako hai japo walitenganishwa kwani walipo kuwa na miaka kumi na miwili Mke wa Mr. Kivuli alienda kumtembelea Steve hospitalini nakujua watoto wake wote ni wagonjwa sana na malipo ya hospitalini yalikuwa makubwa kuliko uwezo wake hivyo mke wa Mr. Kivuli aliahidi kumsaidia Steven watoto wake ila kama atakubali kumkabidhi mtoto wake mmoja yeye amchukue na kumfanya binti yake yeye, ilikuwa ngumu mwanzoni kwa Steven kufanya hivyo lakini baada ya hali ya wanae kuwa Mbaya siku hadi siku alikubali sharti la mke wa Mr. kivuli kwani ilikuokoa maisha ya watoto wake wote wawili ilimbidi mmoja amtoe kwa hao mashetani wawili na kwabahati nzuri Mr. kivuli hakukataa kabisa alikubaliana na Wazo la mkewe kwani alijua kabisa kuishi na mtoto huyo itamsaidia kwani Steven hataweza kutoboa siri za biashara zake huko baadae ikitokea wamegombana kwani ndio njia pekee ya kumlinda mwanae na ndio maana hata Steven alipo wachukua wakinamama na kuacha kazi haku mshitaki popote Mr. Kivuli kwasababu ya mwanae na kwabahati nzuri mke wa Mr. Kivuli na Mr.kivuli walimpenda sana mtoto huyo naukizingatia walikuja kugundua hawawezi kupata mtoto na kwataratibu hivi sasa mtoto huyo wanaanza kumrithisha uchafu wao jambo ambalo siwezi kukubali kwani yeye hana damu chafu kama wao na ndio maana leo nakuomba unipe nafasi yako na wewe uchukue nafasi yangu.

Jackbosi alisimama huku akiwa Ametoa macho na kumuuliza grace unamaanisha nini ? Grace kwasauti akamwambia mimi ni grace Steven na wewe ndio Jack Steven hilo jina la Jackbosi wamekupa wao na maanisha wewe ni mdogo angu mimi na huyu mzee aliye lala hapo ni baba yako na wale mashetani walio kulea ndio walio muua mama yako na kumfanya baba yako kilema na kuonekana mzee sana kwa sababu ya maradhi na kuharibu maisha yawakinamama kibao na kusababisha vijana kibao kuzaliwa , kukua vizuri na kupewa kila kitu halafu mwisho wa siku wanauliwa ugenini na kuwa chakula cha samaki.

USIKOSE SEHEMU YA 5 & 6 KESHO.
 
TAMTHILIA: CHALLENGE MADE .

MUANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS.

SEHEMU: 5 $ 6.

WhatsApp no: 0746115688 .

Baada ya grace kumaliza kuongea, Jackbosi alihuzunika sana, machozi yalitiririka usoni mwake kiasi cha kuufunika Uzuri wake. lakini grace hakuwa na muda tena wakukaa kuongea nae, aliwaambia walinzi wake wamrudishe Jackbosi hospitalini baada ya lisaa limoja na kisha yeye alichukua pikipiki na mlinzi wake mmoja nakuelekea eneo ambalo aliificha pikipiki ya hospitalini kisha akaichukua pikipiki hiyo na kuelekea hospitalini, lakini pia mlinzi wake alirudi nyumbani. Grace alipofika getini walinzi bado walikuwa wapo kwenye usingizi mzito hivyo alifungua geti na kuingia ndani kisha akarudisha pikipiki mahali alipo kuwa ameitoa na kuingia ndani, na hata chumbani kwa wakinamama hakukuwa na yeyote aliyeamka hivyo alioga na kubadili nguo zake kisha akaelekea kitandani. Baada ya kama masaa mawili hivi Jackbosi alirudi hospitalini na kwenda kuangalia hodi ya wakinamama ilikuhakikisha kama grace amerudi, na kwabahati nzuri kweli grace alikuwa amesharudi na amelala lakini aliharibu kamera zote za CCTV jambo ambalo hata Jackbosi alipoona tu alijua kabisa huyu ni grace ndio kafanya hivi. Baada ya Jackbosi kumaliza kukagua alichukua gari pamoja na walinzi wapya kwani alihisi walinzi wake waliuliwa baada ya tukio la yeye kukamatwa, jackbosi alianza safari ya kuelekea nyumbani kwake Masaki na kwakuwa barabarani kulikuwa na foleni sana, Jackbosi alilichelewa kufika kwake alifika mida ya saa tisa usiku jambo ambalo lilimkera sana Mr.kivuli kwani muwekezaji wao mpya alikuwa nyumbani kwa Jackbosi, lakini Jackbosi alimtelekeza nyumbani hapo na mlinzi wake tokea alipompokea .
Asubuhi na mapema Jackbosi alijiandaa ili kuongozana na muwekezaji huyo mpaka mahali ambapo kutakuwa na mkutano wa uwekezaji napia muwekezaji mpya atasaini mikataba rasmi .
Lakini Jackbosi aliwaalika waandishi wa habari ili aone baba yake atafanya nini baada ya kuwaona waandishi hao, Jackbosi aliongozana na muwekezaji mpaka eneo la tukio na walipofika walishuka kwenye gari lakini Jackbosi akasimama mahali ambapo waandishi walikuwepo na waandishi walipomuona jackbosi kasogea karibu yao walianza kumuhoji kuhusu biashara zao za familia Jackbosi aliwajibu ziko powa lakini baada ya kumuona Mr.kivuli karibu na waandishi Jackbosi alibadilisha mada na kuanza kuelezea kuhusu uwekezaji mpya unaoenda kufanyika siku hiyo, waandishi walipouliza muweke zaji wenu mpya katika kampuni yenu ya Culture Company anaenda kuwekeza upande gani mana kampuni yenu ni kubwa na ina matawi mbalimbali na yanahusika na shughuli mbalimbali, Jackbosi alimuangalia Mr.kivuli kisha akataka kujibu hospitalini kama baba yake alivyo mwambia awali lakini kabla hajajibu Mr.kivuli alimuwahi nakumtoa katikati ya waandishi wa habari na kumsogeza pembeni kisha akamuuliza Jackbosi ninani alie waleta waandishi hawa ? Jackbosi alimjibu ni mimi kwani kunashida gani baba, nimewaita ili wapinzani Wetu katika biashara Waone ni jinsi gani tumepiga hatua kushinda wao. Mr.kivuli hasira zilimtawala mpaka alianza kutetemeka kisha akamwambia Jackbosi hata siku moja hukuwahi kuona waandishi katika matukio yangu wewe ninani wakuwaalika hapa leo ikiwa unajua vizuri kuwa cjawahi hitaji waandishi katika shughuli zangu tokea zamani , Jackbosi aliita 'baba' lakini Mr.kivuli alimwambia haraka kawatoe hao wajinga wako nnje ya eneo hili au kama unapenda sana mitandao kawaambie wakusaidie kukutafutia mchumba mana unamiaka '30' na bado hujaolewa na sio kuleta maswali juu ya nnacho kifanya kwasababu hayupo na hakuna mwenye ruhusa ya kuwepo katikati ya shughuli zangu na sina kumbukumbu kama kunaaliejifanya mjanja kwangu akaishi hata kama awe mtoto wangu. Jackbosi alimtuma mlinzi wake akawaondoe waandishi wote na kwakuwa yeye ndo aliwaita hawakuleta shida kabisa juu ya kuondoka kwani hata hivyo hawakuwa waandishi wa kweli ni vijana tu wa mtaani .
Baada ya waandishi kuondoka Jackbosi alielekea chumba ambacho ndo wawekezaji wote wanaendelea na kikao na alipofika walinzi wa mlangoni Hawakuweza kumzuia kwasababu yeye ni mtoto wa Mr.kivuli, alipo ingia ndani Jackbosi alishangazwa sana kwa kitu alichokuwa anakiona kwenye kikao hivyo alibakia tu kuzunguuka na kuwaangalia watu wanaoshirikiana na Mr.kivuli huku akiwa ametoa macho yake yote kwa washirika hao. Mr.kuvuli alichukia sana kwani siku zote Jackbosi hakuruhusiwa kuingia kwenye kikao lakini siku hiyo aliingia tena bila ruhusa ya mtu. Washirika wa Mr.kivuli waliogopa sana na kuanza maongezi ya chinichini lakini Mr.kivuli aliwatoa hofu kwakuwatambulisha kuwa Jackbosi ni mtoto wake na ndio msimamizi wa hospitalini kisha akamwambia Jackbosi asalimiane na washirika wake. Jackbosi aliwapa mkono washirika hao wa baba yake kwa uoga mkubwa kwani hakuwa anaamini watu alio kuwa anawaona sehemu hiyo . Baada tu ya Jackbosi kumaliza kuwapa mkono alichukua kiti ili na yeye akae lakini kabla hajakaa Mr.kivuli alimwambia Jackbosi inakibidi uende hospitalini kwa sasa. Jackbosi alitoka na kuingia kwenye gari yake lakini mlinzi alipotaka kuendesha gari Jackbosi alimwambia leo ntaendesha mimi, mlinzi alirudi kiti cha nyuma na kumuachia jackbosi aendeshe gari . Jackbosi alivuta kwanza mafuta kisha akaliendesha gari kwa kasi yaajabu bila kuhofia chochote .
Lakini kwa upande wa pili Mr.kivuli alikuwa anazindua biashara yake mpya ya kusafirisha madawa ya kulevya kwakutumia vijana wenye majina makubwa nchini kama wasanii, waandishi wa habari, wanafunzi wanaosoma nchi za nnje lakini pia hadi viongozi na wagonjwa wanao enda kutibiwa nnje ya nchi wote watatumika kwa kazi hiyo na yule muwekezaji kumbe hakuwa muwekezaji kama Jackbosi anavyojua bali ni mtengenezaji wa madawa hayo ambaea anaaminika na anauwezo mzuri katika kazi kama hiyo na ndio maana wao walimtoa nchi za nnje na kumuingiza rasmi kwenye biashara yao kwasababu anaaminika sana katika kazi hiyo na kwamajina alikuwa anitwa james. james aliwaahidi kufanya kazi nzuri na watu wote walilizika na kukubaliana na Mr.kivuli kwa kazi nzuri na kwakuwa maelewano yalienda vizuri Mr.kivuli aliwaalika nyumbani kwake kwa part ya kupongezana kwakufungua project yao mpya . Wakati huo Jackbosi alipata Ajali kutokana na kuendesha gari kwa kasi sana lakini kwa kuwa alikuwa hajaumia sana alimlipa fidia aliegongana nae na moja kwa moja alienda mpaka hospitalini na aliposhuka ndani ya gari aliwataarifu walinzi kuwa anahitaji muda wa kuwa mwenyewe baada ya hapo Jackbosi alienda ofisini kwake lakini alipofungua mlango ndani alimkuta grace akiwa amekaa kwenye kiti chake huku akizunguka zunguka, Jackbosi hakumuongelesha kabisa grace bali alikaa kwenye kochi lake huku akiwa anatetemeka sana . Kama kawaida grace alicheka sana na kumwambia mambo madogo tu uliyokutana nayo unatetemeka halafu bado kichwani kwako unampango wakuwasaidia wakinamama ulio waficha kule mafichoni hivi kweli utaweza?. Jackbosi alisimama huku akitetemeka kwa hofu kisha akamwambia grace huwezi pambana na Mr.kivuli kwasababu timu aliyo nayo inamfanya astawi kila siku hivi unajua ana Mawaziri, wabunge na wafanya biashara wakubwa kibao, hivi wewe ninani hasa wakuweza kumzuia Mr.kivuli ? grace alijitetemesha kwa utani na kumwambia Jackbosi haya njoo tujifiche sasa wote chini ya meza ili wasituone, grace kwahasira akamwambia tena Jackbosi unaogopa vyeo vyao tu wakati bado hujaona waliyokuwa wanayaongelea hivi ukijua si unaweza kuzima wewe au kufa kabisa kwa presha. Jackbosi alimuangalia grace lakini grace alimwambia unapochelewa kunikabidhi majukumu yako ndio jinsi ambavyo mambo yanazidi kuharibika kwasababu leo rasmi wamefungua project mpya na unajua inahusu nini ' grace akacheka na kumwambia samahani nilisahau umefukuzwa katika chumba cha mkutano kabla ya project kuwekwa mezani basi ngoja mimi nikuhadithie japo sikuwepo eneo la tukio .
Ukweli ni kuwa baba yako na kwa upande mwengine bosi wako Mr.kivuli kaandaa project mpya kubwa sana ya kuhakisha anawaharibia maisha vijana wote waolipiga hatua lakini pia wanafunzi waliopata nafasi za kusoma nnje ya nchi na alivyo kuwa hana aibu hata punje safari hii anampango wa kuwatumia hadi wagonjwa wanaoenda kupokea matibabu nnje ya nchi kwa kuwatumia kusafirisha madawa yake ya kulevya na atakaekuwa anatengeneza madawa hayo nakuyapaki ni james mtu ulie kuwa jana ukimuhangaikia na kumuita muwekezaji na kibaya zaidi kwa watakao safirisha madawa hayo kupitia miili yao upasuaji utafanyikia hapahapa hospitalini kwako mpendwa Jackbosi mpigie makofi baba yako mlezi mana this time ameuwa . Jackbosi alisimama na kumwambia grace inatosha sasa acha uongo wako, grace alicheka sana na kumwambia ukweli una uma sana mdogo wangu kipenz kisha alisimama na kuplay kitu kwa kutumia kompyuta ya Jackbosi kisha akawasha projector na hapo ndipo grace aliona yote yaliyo kuwa yakiendelea kwenye mkutano ule kuanzia yeye alipo fukuzwa mpaka baba yake alipo weka project yake mpya ya madawa mezani na jinsi watu walivyoungana nae na kufurahi huku wakisifia biashara hiyo kwani itawaingizia pesa kibao. Jackbosi alisimama kwa hofu na kumwambia grace nashindwa hata kuelewa wewe na baba nani mbaya zaidi kwa sababu wewe siku zote upo kila alipo na unamiaka '30' tu! Hivi huoni kama wewe ni hatari zaidi kwa umri ulio nao na unayo ya fanya kuliko hata Mr.kivuli ? grace alicheka tena sana lakini Jackbosi alitoa bunduki nakumyooshea grace , grace aliogopa sana lakini Jackbosi hakurudi nyuma alimpiga risasi grace halafu akatupa chini bunduki na kuanza kulia mwenyewe 'nimemuua dada yangu mimi' lakini ghafla grace alicheka sana na kusimama Jackbosi alishangaa sana kwani bunduki yake iliitoa milio wa risasi kabisa alipo mpigia grace lakini grace alimwambia ningeweza kukuachia uniue mdogo wangu lakini nilibadilisha bunduki kwasababu nilijua kabisa nikifa mdogo wangu kipenzi atahuzunika sana na kujilaumu na ndio maana nilikuwekea bunduki feki lakini kama ulivyoona inaviwango sawa naya ukweli si ndio dogo, jackbosi kabla hajamjibu grace Mr.kivuli alimpigia simu na kumwambia njoo nyumbani leo kuna part kwaajili ya project yangu mpya ya kutengeneza dawa kwaajili ya raia wasioweza kupata dawa kwa hela, Jackbosi alichukia sana kuona baba yake bado anamdanganya na kwahasira alikata simu na kuizima kabisa kisha akamkaba grace na kumwambia nipe bunduki yangu ya kweli leo naenda kummaliza yule mzee. grace alicheka sana na kumpa bunduki Jackbosi lakini kabla hajaondoka Daktari aliingia ofisini kwake na grace nae aliificha kwani hakutaka mtuyeyote kujua kuhusu ukaribu uliopo baina yake na Jackbosi, Daktari aliyeingia alimpa taarifa Jackbosi kuwa wakina mama wote kumi wanahitaji kujifungua lakini kwa bahati mbaya sita ndo tunaweza kuwasaidia wanne hatuwezi kwasababu wanahitaji upasuaji na kama unavyojua madaktari wa upasuaji hakuna,. Jackbosi alimwambia Daktari tangulia nakuja ngoja nifanye mawasiliano na madaktari wanao weza kunisaidia . Daktari alimjibu sawa na kuondoka. grace alitoka alipo kuwa amejificha na kumuangalia Jackbosi anavyojalibu kuwasiliana na madaktari anao juana nao lakini kwa bahati mbaya simu zao hazikupatikana. Jackbosi alijawa na hofu sana lakini grace alimwambia Jackbosi mimi nitawafanyia upasuaji wakinamama wote, Jackbosi alimuangalia grace na kumwambia kumbuka huu sio utani hili linahusu maisha ya watu tafadhali kaa mbali na mimi kwa sasa. grace alimjibu ya kuwa natumaini na wewe unakumbuka kuwa mimi huwa sina michezo na maisha ya watu, hivyo twende tukawasaidie wakinamama hao.

USIKOSE SEHEMU YA 7 & 8
 
Tuko sambamba. Ila maneno yote haya watunzi huwa mnawazaa au kuna visa mliona
Kunabaadhi ya tungo nizakufikilika tu hivyo zina chukua kiasi kikubwa cha mawazo ya mtunzi kuliko visa alivyoona . Lakini tungo nyingi zinazo husiana na mambo mbalimbali hasahasa yanayo kuwa yapo na yanaisumbua jamii hutokana na visa ambavyo mtunzi anaona lakini pia mawazo yanahusishwa kwasababu mawazo yamsaidia mtunzi kupata picha juu ya tungo anayo tunga.
Samahani sijui kama majibu yangu yamekutosheleza mpendwa ila huo ndo mtazamo wangu mimi kama mtunzi wa TAMTHILIA hii ya CHALLENGE MADE.
 
Kunabaadhi ya tungo nizakufikilika tu hivyo zina chukua kiasi kikubwa cha mawazo ya mtunzi kuliko visa alivyoona . Lakini tungo nyingi zinazo husiana na mambo mbalimbali hasahasa yanayo kuwa yapo na yanaisumbua jamii hutokana na visa ambavyo mtunzi anaona lakini pia mawazo yanahusishwa kwasababu mawazo yamsaidia mtunzi kupata picha juu ya tungo anayo tunga.
Samahani sijui kama majibu yangu yamekutosheleza mpendwa ila huo ndo mtazamo wangu mimi kama mtunzi wa TAMTHILIA hii ya CHALLENGE MADE.
Nimekuelewa mpendwa
 
TAMTHILIA : CHALLENGE MADE.
MUANDISHI : WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS.
SEHEMU : 7 $ 8.
WhatsApp: 0746115688.
Grace aliwaomba wauguzaji wawili wamsaidie katika upasuaji, kisha wakandaa chumba cha upasuaji haraka na kuanza kufanya upasuaji huo. Grace alionekana kuwa mtaalam sana katika suala zima la upasuaji kwani ndani ya masaa mawili alimaliza upasuaji kwa wanawake wote wanne na kufanikiwa kuwaokoa wanawake wote wa nne pamoja na watoto wao. Madaktari walishangaa sana kazi aliyofanya grace lakini Jackbosi kwake aliona ni kawaida kwani grace kilasiku amekuwa akimshangaza na jambo jipya. Baada ya upasuaji kuisha Jackbosi alijiandaa ili kuweza kwenda kwake kujiandaa na shughuli ya Mr.kivuli . lakini kabla hajatoka grace akamwambia Jackbosi usijalibu kufanya kitu chochote kibaya,nakuomba sana ukifika katika part muunge mkono baba yako kama unavyofanyaga kila mara kwasababu ukionyesha uadui kwake atakuua na hasara taifa ndo litapata kwasababu nchi inahitaji watu kama wewe kuliko watu kama Mr.kivuli jitahidi sana urudi, kwani mimi nitakuwa nakusubiria hapa na nnaimani Thabiti kuwa utakuja. Grace aliongea kwahisia sana kiasi cha kumtoa machozi Jackbosi lakini pia Jackbosi alimwambia grace nnamengi sana ya kujifunza kutoka kwako kwanini nikafe leo ntarudi ucjali. Baada ya Jackbosi kuondoka grace alirudi ndani ya hodi anayoishi yeye pamoja na wakinamama wengine na kuanza kumnyonyesha mwanae . mwanamke mmoja alimwambia grace kiukweli bado cjajutia kitendo cha wewe kunitoa kwangu na kunileta hapa kwasababu siku zote upo kwaajili yetu nakumbuka uliapa hutagusa tena kisu kumfanyia mtu upasuaji lakini kwaajili yetu leo umegusa kisu tena na kunawatu wanne wamepona pamoja na watoto wao yote ni kwasababu yako ubarikiwe sana japo sitaacha kukulaumu kwa kifo cha jasmini.
Grace aliwaangalia wakinamama wote kisha akawaambia 'ukweli ni kuwa Jackbosi sio muuaji na wala hakumuua jasmini kwani bunduki aliyo mpigia jasmini ilikuwa na sindano tu ya kumfanya azimie kwa wakati ule na alifanya vile kwasababu flani hivi ambazo siwezi waambia kwasasa lakini leseni tu yeye si adui yeti bali Mr.kivuli'. Ade alimuuliza grace jasmini yupo wapi ? Lakini grace alimwambia Ade usijali kabisa jasmini amekusamehe ila hata sikumoja usimtoe tena mwenzako kafara kwa sababu ya wengine kama hamna mpango wa kumuokoa . Ade alilia sana lakini grace alimsihi anyamaze lakini pia aliwaambia wakinamama wote kwapamoja msisahau kwanini tuko hapa lakini pia hongereni kwakujifungua salama na muwatunze watoto wenu kwasababu hilo ni moja ya jukumu lenu pia nnaimani hata waume zetu wangekuwepo leo wangesema hivyohivyo watoto wetu ni nijukumu letu hivyo tuwatunze. Wakinamama wote waliojifungua kawaida walisogea alipokuwa grace kisha wakakumbatiana. Upande wapili Jackbosi alienda kwake kujiandaa kisha akaelekea nyumbani kwa baba yake kwaajili ya part ya kujipongeza kwa kufungua project mpya iliyo andaliwa na baba yake mlezi Mr.kivuli. lakini Jackbosi alipofika kwenye part baba yake alimtambulisha tena binti yake na wakati utambulisho unaendelea James alinyoosha mkono na kuuliza ' Mr.kivuli binti yako ameolewa' ?. Mr.kivuli alimwambia james hapana kiukweli hajaolewa bado vipi kwani james, james alimwambia unabinti mrembo sana hongera huku akimtazama Jackbosi kwa matamanio, Watu walicheka sana na part ilikuwa inaendelea na kila alie jisikia kunywa alikunywa vinywaji vya kutosha kwani vinywaji vilikua vya aina mbalimbali na vyakula vya kutosha. Jackbosi alienda kukaa na mama yake kwani alikuwa amemkumbuka sana na alikuwa anamuda mrefu hakwenda kumtembelea. lakini mama yake alipo muona tu alianza hapohapo kumsisitiza Jackbosi kuwa unapaswa kuolewa kwani umri wako umeenda sana lakini kama kawaida Jackbosi alimuahidi tu mama yake ataolewa tu asijali . Ulipofika muda wa kucheza mziki James alimuomba Jackbosi acheze nae lakini Jackbosi alimkatalia, jambo ambalo lilimfanya james kushikwa na hasira na kuanza kumzalilisha Jackbosi kwa kumshika makalio kwa lazima mbele ya Jackbosi waliokuwepo katika sherehe hiyo wakiwemo wazazi wake , kitu kilichopelekea kila mtu aliehudhulia part hiyo kucheka akiwemo James mwenyewe , wakati james amekaukia kucheka Jackbosi alimpiga teke zito la sehemu za siri na kuondoka zake akiwa amemuacha james chini akiugulia maumivu . Mr.kivuli alimuita Jackbosi lakini Jackbosi hakugeuka nyuma na alipofika kwenye gari aliwasha simu yake na kumtumia ujumbe baba yake kumuomba msamaha kwa tabia yeyote mbaya ambayo ameonyesha kwa namna moja au nyingine itakuwa imeharibu part yake lakini part iliisha salama na wageni wote walielekea majumbani mwao .
Usiku wakati Mr.kivuli na mkewe walipo kuwa kitandani mke wa Mr.Kivuli alimwambia mumewe aongeze umakini na James kwasababu akiendelea kumzalilisha mwanangu nitamuua kwa mkono wangu.
Mr kivuli kwakuwa anampenda sana mke wake alimuahidi mke wake kuwa ataongea na james na anaimani James ata muelewa.
Hospitalini wakati wakinamama wote wamelala grace alimfunika mwanae na kumuacha akiwa amelala kisha akaelekea sehemu ambayo kumehifadhiwa vinywaji kisha akatoa chupa mbili za red wine na akazima taa zote na kuwasha tochi ndogo yenye mwanga mdogo sana, Kisha grace akawa anakunywa mvinyo huo machozi yakimtoka huku akiwa ameshikilia picha ya mumewe alie fahamika kwa jina la adrew. Wakati yuko pale Jackbosi alimsikia akilia na kumfuata kisha akamwambia ' ckujua kuwa wewe ni bingwa sana wakulia gizani '. Lakini grace alimwambia Jackbosi kwanini uko hapa ? Jackbosi alimwambia hapa pia si kwangu, kuna tatizo mimi kuwa hapa ? Grace alimwambia hapana niliogpopa tu kwasababu huna kawaida ya kulala hospitalini.
Jackbosi Alimuelezea grace kila kilicho tokea kwenye sherehe jinsi ambavyo james alimvunjia heshima, lakini grace alimwambia inabidi baadhi ya vitu uzoee kutoka kwa huyo james kwasababu yeye kazi yake ni madawa tena upande wa kutengeneza naamini kabisa anaweza kuwa mtumiaji mzuri pia na ndio maana Anatabia za ajabu sema usiruhusu akuzoee kabisa kaa nae mbali hana akili kabisa hata kuua Kwake inaweza kuwa kawaida .
jackbosi alikubaliana na grace kuwa james sio mtu wa kuaminika kabisa ni wakukaa nae mbali lakini Jackbosi aliona picha aliyokuwa ameishika grace na grace alipoona Jackbosi ameiona aliificha lakini haikusaidia kwani grace alikuwa tayari ameshaiona hivyo alimuuliza grace, 'samahani grace kwani ulishawahi kuolewa'? Grace alimwambia ndio lakini kwasasa hayupo tena . Jackbosi alimgusa bega na kumwambia pole sana kwasababu inavyoonekana ulimpenda sana hata hivyo Ungelijabu angalau kumuomba Arudi kwako kuliko kulialia mwenyewe muda kama huu . grace alimwambia Jackbosi najalibu sana kuomba arudi kwangu lakini inavyoonekana haiwezekani tena yeye kurudi kwangu. Jackbosi alimwambia grace kwani ameshaoa huko alipo ? Grace alimwambia sio yeye tu hata mimi siwezi olewa na mtu mwingine zaidi yake . Jackbosi alimuangalia grace na kumwambia mapenzi ni hisia mama pengine utapenda tena . Lakini grace akasema kama ningefuata hisia basi nisingefika nilipo . Jackbosi akacheka sana na kumwambia ndio maana amekuacha. Lakini Grace akamwambia Jackbosi 'Andrew asingejalibu kuniacha hata kama ningetaka' . Jackbosi alimwambia lakini tayari kakuacha na kwannavyo kuona kila siku unageuka kuwa shetani sijui kama ataweza kurudi .
Grace alimwambia Jackbosi awezi kurudi hata akitaka kwasababu yeye pamoja na wanaume wa wanawake hao unaowaona hapa walikufa na kutuachia watoto kama zawadi na baba yako mlezi Mr.kivuli anahusika yaani hakuweza kutufikilia watu wao wakaribu hata kidogo , Grace aliendelea kwa kumwambia hao wanawake kuna madaktari kati yao kuna waandishi na kuna Mwanasheria mmoja na mwengine alikuwa mama tu wanyumbani na mimi nilikua Daktari na rafiki yao ambaye walikuwa wakinisaidia kuhakikisha nawapatia haki watu wote walio umizwa na baba yako kwa kutumia sheria lakini mpaka leo hakuna haki iliyo Tendaka kama ulikuwa hujui basi leo ni miezi nane tangu waume zao na mume wangu wafe walipo jalibu kunisaidia mimi kwa kazi yao ya uandishi habari, lakini baba yako hakufikilia angalau hata mara moja alitengeneza pancha kwenye magurudumu ya gari walilokuwa wanatumia siku hiyo na kusababisha milele tusione nao, na kibaya zaidi mume wangu alikuja Mzima hospitalini kwangu lakini alikufa nikiwa najalibu kumfanyia upasuaji kutoa chupa iliyo zama kifuani , na kibaya zaidi kati yetu wote kumi na moja Ade tu ndo alibahatika kumzika mpendwa wake lakini sisi wengine wote tulibakia kwenye mshtuko kwa muda wa wiki moja na kuja kuonyeshwa matuta tu yaliyo funika miili ya waume zetu.
Tokea hapo Dr.grace alikufa akazaliwa mtu mwingine mpya asiyetaka kuonewa tena na aliye amua kuitafuta haki kwa njia zake mwenyewe akiwa na mimba ya mwezi mmoja tu na wale wamama wa nyumbani, wananasheria , madaktari na waandishi wakachukulia kama hawakuwahi kuwa watu katika hii dunia wakajipa jina la kuwa mashetani kwa wakati huo kwasababu tu wanaamini kila kitu kikiwa sawa watu watawaona wao kama malaika . Mpendwa Jackbosi 'challenge made us', lakini kwa baba yako challenge zime muharibu kabisa ukichanganya na tamaa ya mali Aliyonayo na ndoto ya kuwa mtu maarufu ndo zimemuharibu nakuuharibu mfumo Mzima wa maisha yake. sisi sio kama yeye sisi tunajenga alipobomoa yeye kwa njia tulizozichagua wenyewe .
Baada ya grace kumwambia hayo Jackbosi alielekea kulala bila hata ya kumuaga grace.
alipofika chumbani alikagua wakinamama wote kama wakosawa kwakuwapima homa kwa mikono yake pamoja na watoto wao kisha akaelekea kulala , lakini kumbe wanawake hawakuwa wamelala na baada ya yeye kuwapima na kuwabusu kama ishara ya kuwatakia usiku mwema . Wakinamama walitokwa na machozi sana ndani ya mashaka waliyo kuwa wamejifunikia kwani walijua chuki waliyo tengeneza awali juu ya grace wakihisi anawatelekeza na kusahau upendo wote alio nao juu yao haina faida kwani yeye bado anawapenda sana tu! .
Ade aliumia zaidi kwani yeye alikuwa rafiki wa karibu sana na grace hata kabla ya matatizo yaliyo wakuta lakini hofu ilimfanya amuone grace kama msaliti jambo ambalo alimkosea sana grace kwani yeye bado alimpenda kwa kipimo kilekile .
Asubuhi na mapema Jackbosi aliingia kwenye hodi ya wakinamama na kuwaambia inabidi mjiandae muondoke haraka sana katika hospitali hii baba anakuja hapa anataka kuanza rasmi project yake ya madawa ya kulevya hivyo ondokeni haraka kwani madawa si mazuri kwa watoto wenu . lakini wakinamama hao walimuangalia Jackbosi kwa hasira, kisha Ade akamwambia grace inabidi utafute mtu wakuchukua nafasi yako ili Mr.kivuli asihisi vibaya kwani wewe na Jackbosi mnafanana sana akiona jinsi Mnavyo fanana itampa mashaka na ukizingatia anajua kabisa Steven alikuwa na mapacha na iko wazi Jack alinunuliwa tu kwa Steven .
Jackbosi aliwashangaa sana huku akijiuliza ni watu au wanyama mana wanawake hao kwanza hawajali kuhusu wao wala watoto wao, ameamua kuwatorosha ili wawe salama lakini wao wamekataa na ndio kwanza grace na wakinamama wanamuomba amuachie jasmini angalau kwa muda kidogo.
Jackbosi alishangazwa sana na umoja wao pia akawakubalia na kuwatolea jasmini alipokuwa amemficha na Wote walikuwa na furaha kumuona jasmini yuko powa kwani waliambiwa tu na grace yupo hai lakini hawakuwahi kumuona tangu usiku ule .
Baada ya muda kidogo mlinzi alikuja kumpa taarifa Jackbosi kuwa Mr.kivuli amesha wasili, na hapo ndipo wakinamama wote walitoka nnje na Mr.kivuli alifurahi sana kuona wana afanya nzuri kisha akawaambia kwa afya zenu mnaweza hata kupata watoto wazuri tena na tena na wamisaidie tena na tena ukizingatia na elimu watakayo enda kupokea nchi za ugenini watakapomaliza masomo yao ya sekondari , wakina mama walicheka sana huku wakimuangalia kwakumtamani.
Mr.kivuli aliwaambia twendeni wote nikaone mtoto wakila mmoja wenu inaonekana watakuwa wazuri sana ,basi wakinamama waliongoza njia mpaka mahali ambapo watoto wao walikuwa wamelala na Mr.kivuli aliwakagua watoto wote lakini alipofika kwa mtoto wa grace alitamani kumshika lakini alipojalibu kumshika mtoto jasmini aliumshika kwanguvu mkono wa Mr.kivuli uliokuwa unajalibu kumshika mtoto wa grace jambo lililo mfanya kila mtu aliyekuwepo eneo lile kuduwaa .

USIKOSE SEHEMU YA 9-10.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom