Tamthiliya: Challenge Made - Sehemu ya 1

Tamthiliya: Challenge Made - Sehemu ya 1

TAMTHILIA : ZAWADI.

MWANDISHI:WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS.

SEHEMU YA : 8 $ 9.

WHATSAPP No: 074611566.

Zawadi aliwaangalia sana wazee wa jadi, kisha akawaambia ' hivi wazee wangu kosa la huyu binti mdogo zawadi nilipi ?'. Mana kunawakati nahisi kama nyie mkipata nafasi mnaweza kuniua kabisa. Haya sasa maovu yenu hatimaye yako wazi tumiue,mchapwe viboko au mtajitosa baharini kama mlivyo tamani iwe kwangu ? . Kiukwel wazee wangu mnanishangaza sana mana wakati mimi na jalibu kujenga sikuzote mnakesha kubomoa.Sasa basi inatosha leo mimi naomba adhabu yenu niamue mimi kama binti Mfalme, lakini kwa ruhusa yako Mfalme wangu wa himaya hii ya Wetu pamoja na Malkia wangu. Mfalme alisimama pamoja na kumwambia Zawadi ' mimi kama Mfalme wa himaya ya wetu nakuachia leo binti yangu Zawadi jukumu la kutoa hukumu si kwa wazee hawa wa jadi tu! ,bali kwakila atakae tenda kosa linalo hitaji adhabu, na kesi zote za Ufalme huu wa Wetu tunakuChia wewe '. ( Mfalme na Malkia wakasimama na kuingia katika ufalme huku wakiwa wamemuachia jukumu la kutoa hukumu zawadi). zawadi aliwaangalia sana wazee wa jadi huku kelele za wakazi wa Ufalme wa wetu zikimlazimisha yeye kuwahukumu kifo wazee hao. Lakini Zawadi alinyoosha mkono wake juu ilikupata utulivu wa watu hao na kisha akawaambia wazee wote ya kuwa ' kati yenu hakuna atakae guswa kwa kupigwa na hata jani la mpapai ,niki-maanisha hamta chapwa viboko , hamta nyongwa wala kutengwa kwasababu hiyo ndo adhabu kubwa kwangu kwenu' . Baada ya Zawadi kusema maneno hayo alisimama na kuwaaamuru walinzi waweze kuwaachia Wazee hao wa jadi kisha yeye akaelekea zake katika jumba la kifalme. Familia za wazee hao wajadi zili watenga na kuwaona kama maadui zao kwani hata maramoja hawakuwafikilia wao walipo kuwa wakifanya vitendo vyao vya ajabu ambavyo wao wenyewe walidai ndo sababu ya njaa kijijini hapo.
Zawadi alipoingia tu katika jumba la kifalme moja kwa moja alielekea katika chumba cha Mfalme na Malkia na alipoingia moja kwa moja alienda kukaa katika miguu ya Malkia na kumwambia, ' mama nimechoka sana'. Mailkia akamwambia Zawadi ' pole sana binti yangu kwani unayopitia sasa najua yanafanya ukate tamaa kabisa lakini kumbuka kitu kimoja maishani mwako unatakiwa kuwapenda tu, mpaka siku moja wakupende wewe tu na waache kusikiliza maneno ya watu wengine na wasiutilie tena mashaka upendo wako kwao , nanaamini ipo siku binti yangu wewe na wao mtaungana kutoka moyoni na hakuna atakae kutilia mashaka tena wakati huo ukifika kuwa mvumilivu tu binti yangu'. Zawadi alilia sana lakini baba yake alimwambia ' zawadi nini maana yako kuwaachia huru wazee wa jadi ikiwa sheria zote zinaruhusu kabisa kuwapeleka kuzimu?' Zawadi alicheka sana huku machozi ya yakimtoka na kumwambia baba yake, ' Ni kweli kabisa ningeweza kuamuru wanyongwe na kwa muda huu wangekuwa pengine wamesha sahaulika na wao pia ingekuwa nafuu kwao kwasababu wangekuwa wamepumzika mbali na hasira za watu. Lakini mimi nimewapa nafasi ya kuishi wazee wa jadi ambayo ni uchungu sana kwao, kwasababu watoto wao hawataki hata kuwasikia, wake zao wanawaona wao kama wasaliti wasio wa jali wao, ndugu zao wanawaona wao kama mfano wa nyoka na watu wa Wetu hawatamani hata kuzisikia sauti zao na ukizingatia hali wanayo ipitia kwasasa, imani yao inawaambia kabisa ni kwasababu ya miti waliyoikata wazee wa jadi ili kusababisha mimi nionekane mbaya kwao na Kwa hali kama hiyo wataona bora wangekufa na hapo sasa ndo watatakiwa kujifunza kuwa watu . Mfalme alicheka sana na kumwambia binti yake hakukuwa na makosa mimi kuwa na wewe kama binti yangu. Malkia alimbembeleza Zawadi na zawadi akapitiwa na usingizi hapohapo. Wakati zawadi yupo katika usingizi aliota yupo yeye pamoja na Mfalme na Malkia wanachemsha kitu ambacho kinafanana sana na mizizi ile aliyoipita sikuile wakati wakutafuta miti kwaajili ya ngalawa na kisha wakaila huku wakiwa wanacheka sana , na hapohapo Zawadi akashtuka toka ndotoni muda wa saa kumi na mbili hivi jioni nm bila kupoteza muda zawadi akawaambia walinzi wake nifuateni pamoja na vifaa vya kuhifadhia chakula , walinzi walimshangaa sana lakini hawakuwa najihisi zaidi ya kutii na moja kwa moja Zawadi akaelekea na walinzi mpaka eneo ambalo lilikuwa na mihogo ambayo wao kwakipindi hicho waliichukulia kama mizizi, zawadi aliwaamuru walinzi hao wakate mihogo hiyo ya kutosha na kisha wakaelekea nayo katika jumba la kifalme na walipofika zawadi akachukua kipande kimoja cha muhogo na kuingia nacho mpaka mahali ambapo Mfalme na Malkia walikuwa wamekaa kisha akawaonyesha, Mfalme na Malkia kwanza walishangaa ni mzizi wa aina gani unachakula kiasi hicho na nimlaini , lakini zawadi akawaelezea ndoto aliyoota na hapo ndo Mfalme na Malkia wakamwambia ni sawa lakini kabla ya kupeleka kwa watu inabidi kujalibu kwanza isije ikawaletea madhara. Zawadi alimwaambia Mfalme mimi ndo nitakuwa wakwanza kujalibu lakini Malkia pia akasema nitajalibu pia na pamoja na Mfalme na walinzi wote walikuwa tayari kujalibu kwasababu wote walikuwa wakimuamini sana Zawadi, basi kwapamoja walichuna majani ya mihogo ambayo wao waliita mizizi na kisha wakaiweka jikoni na kutia maji na wakafunika kwa majani. Baada ya muda kidogo tu harufu iliyo toka katika chungu iliwafanya watu kutokwa na mate midomoni mwao bila taarifa kwani kila mtu alivutiwa na harufu hiyo, na hapo ndo wapishi na zawadi walichungulia mihogo na kugundua imesha iva na hapo ndo walinzi ,Mfalme,Malkia, Zawadi pamoja na wapishi wakala na kufurahia sana lakini walikubaliana hakuna kutoa taarifa nnje mpaka pale asubuhi wote watakapo amka wazima ndo watajua mizizi hiyo haina madhara na watu wengine watapata nafasi ya kufurahia .
Asubuhi na mapema Zawadi aliamka na kumtembelea kila mtu kujua hali yake na aligundua wote walinzi yeye na wapishi ni wazima hivyo watu walifurahi kwani wajua kabisa tabu ya chakula 'byebye' kwani mpaka mizizi iliyokuwa msituni iishe samaki na matunda vitakuwa vimesha rejea lakini Zawadi aliwaambia wasitoe taarifa nnje mpaka wajue hali ya Mfalme na Malkia . Zawadi alielekea katika chumba cha Mfalme na Malkia kisha akagonga Hodi lakini Malkia aliitiki sauti ya chini na hapo ndo zawadi aliogopa sana, nakuingia haraka katika chumba hicho cha Malkia pamoja na Mfalme na alipoingia Malkia na Mfalme walikuwa wamelegea sana jambo lililo mfanya zawadi kulia na kuwaambia ni makosa yangu hamkutakiwa Kula mizizi ile ngoja nikamuite Daktari sitaruhusu kitu kibaya kiwatokee nyie. lakini wakati zawadi anataka kutoka nnje Malkia na Mfalme walicheka sana na kumwambia tuko salama na kila mtu unapaswa kujua ya kuwa mzizi ile ni chakula umefanikiwa binti yangu hakuna njaa tena katika ufalme huu wa Wetu .
zawadi alicheka kwa furaha huku machozi yakimtoka na kumrukia baba yake . Baada ya muda mbiu ilipigwa na watu walikusanyika kisha zawadi pamoja na wapishi wakawafundisha watu jinsi ya kutengeneza mizizi hiyo lakini pia Zawadi aliwaelekeza na wazee wajadi ili wasaidiane kuwafundisha watu. Baada ya muda mihogo ilikuwa tayari na kila mtu alifurahia na tokea hapo njaa ili sahaulika katika Ufalme huo wa wetu na wazee wa jadi walielekea katika ufalme na kumuomba Mfalme, Malkia pamoja na Zawadi msamaha na walisamehewa na kila mtu aliendelea na majukumu yake ya awali. siku,miezi na hatimaye ikapita miaka kumi baadae ambapo zawadi akatimiza umri wa miaka kumi na nane.
Siku moja wakati Zawadi anacheza na maji baharini pamoja na mabinti walika lake walitokea wadada wawili na wakaka watano waliokuwa wamevalia suti jambo ambalo lili mfanya zawadi pamoja na wenzake wawashangae sana ukizingatia wao walivyo vaa na watu hao walivyo vaa ni tofauti kabisa. mabinti walio kuwa wanacheza na zawadi walikimbilia msituni ili kuweza kurudi katika ufalme na kutoa taarifa juu ya watu hao. Zawadi alipokuwa kwenye mshangao watu hao walimteka na kumpeleka katika boti Lao la kisasa kisha waka washa boti nakuondoka. Wakati wasichana wanarudi na walinzi walikuta bangili ya zawadi tu lakini zawadi alikuwa ameshatekwa.
Watu walio mteka zawadi walimchukia na kwenda kumfungia katika chumba kimoja ambacho kilikuwa na kila kitu ambacho binadamu anahitaji na baada ya zawadi kuamka alishtuka sana kwani watu hao walikuwa wamemtoa nguo alizo nazo na kumvalisha mavazi ya kisasa, zawadi alishangaa sana na kuanza kupiga kelele na hapo ndo watu wale waliingia ndani na kumwambia ' mambo vip zawadi', zawadi alishtuka sana na kuwauliza nyie ni wakina nani na mmenijuaje.......

USIKOSE SEHEMU YA 10 $ 11
 
TAMTHILIA: ZAWADI

MWANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS

SEHEMU YA : 10 $ 11

WHATSAPP NO: 0746115688.

Baada ya zawadi kuuliza maswali hayo moja kati ya wanawake waliokuwa wamemteka alimwambia zawadi ' sisi tunaomba utusaidie' zawadi alishtuka sana baada ya mwanamke huyo kuomba msaada kutoka kwake jambo ambalo lililomfanya zawadi ashangae kwasababu akiwaangalia watu walio mteka ni bora zaidi yake na ndipo zawadi akawauliza ' kunakitu gani ambacho mimi naweza kuwasaidia nyie kwasababu mnaonekana mpo vizuri kuliko mimi lakini pia hata mlivyo vaa ni tofauti kabisa na mimi pamoja na watu wangu'. Yule mwanamke akamwambia zawadi sisi sio watu wa baya kwani wewe huoni hilo? ' zawadi aliwaambia siwezi sema wewe ni mtu mbaya au mzuri kwakukuangalia kwasababu watu hubadilika na pia naomba mnirudishe milipo nitoa kwasababu mimi cjui hata nyie ni wakinanani japo ndo hivyo mimi pamoja na nyie tunaongea na kusikilizana. Mwanamke yule alimwambia zawadi ndio sisi na nyie tuna sikulizana kwasababu lugha tunayo tumia ni moja na pia sisi ni watu wa nnchi moja. Zawadi alicheka sana na kisha akamwambia mwanamke huyo 'kwani huyo lugha ninani na Nchi ndo kitu gan?' Mwanamke huyo alicheka pia na kumwambia zawadi kubali kutusaidia na sisi tutakufanya wewe uelewe mambo mengi kama vile sisi ni wakina nani na kwanini tumekuchukua bila ruhusa ya Mfalme na Malkia wako.
Zawadi akawauliza inamaanisha baba yangu na mama yangu lakini moja kati ya watu waliomteka zawadi akamwambia 'hapana Mfalme wa Wetu pamoja na Malkia sio wazazi wako hata sisi tunalijua hiloo', Zawadi alishtuka sana na kuwauliza mmejuaje hayo mambo nyie? lakini kabla ya zawadi kujibiwa kiongozi wa watu walio mteka zawadi wakaingia na moja kwa moja akamwambia zawadi; Kwamajina naitwa John-John-yohana nimzaliwa wa arusha, na pia ni Afisa Usalama wa nchi hii ya Tanzania ambayo ndani ya nchi yetu kuna sehemu moja ambayo watu wamejitenga na kutengeneza himaya yao inayo fahamika kama himaya ya wetu na hapo ndo wewe unaishi, watu wa kule wanaishi chini ya uongozi wa ufalme kama sisi tunavyoishi chini ya uongozi wa rais, tofauti kubwa ya kule na huku ni kuwa nyie hamtumii pesa wala hamvijui vitabu( John akachukua pesa na kitabu akaweka mezani) kisha akamwambia lakini pia zawadi kule kwenu nyie kunakupindi mnaishi kwa shida sana mkiamini hamna chakula zaidi ya samaki,mihogo pamoja na baadhi ya matunda vitu ambavyo sio kweli vyakula vya kula nyie ni vingi sana kama mngejitahidi kutuelewa msingepata shida ya vyakula kwasababu mngetoka kule polini na kuja huku mjini kuishi pamoja na sisi na serikari ingechukua uangalifu juu yenu .
Lakini Zawadi alimwambia John nashukuru sana kwa kukutana nanyie naombeni mnirudishe kwetu, lakini john john hakumsikiliza Zawadi bali yeye alimwambia unakumbuka mizizi iliyo wasaidia kipindi kile ambacho njaa imeukumba ufalme Wa Wetu? Zawadi alimwambia ndio lakini umejuaje? John John akamwambia kile ni chakula na sio mizizi bali inaitwa mihogo John akachukua 'laptop ' na 'kuplay' video iliyo kuwa inaonyesha jinsi ambavyo mihogo inapandwa na aina mbalimbali ya kupika kisha akamwambia mihogo ile iliyo wasaidia kipindi cha njaa haikujiotea tu yenyewe bali serikari ndo iliandaa mpango wa kupanda mihogo ile ili wakati wa njaa ukifika watu wa ufalme wa Wetu waweze kufaidika nayo na kweli wewe ulikuja baadae ukaiona na kweli watu wakapona na njaa( John John akamuonyesha zawadi video ya watu wakiwa wanapanda mihogo ile kimya kimya usiku na mwanga wa pochi tu katika eneo ambalo Zawadi aliiiona mihogo hiyo ) .
Zawadi akauluza sasa kwanini nyie huwa mnakuja kwenye ufalme wetu kwa siri, lakini pia mlikuwa wap sikuzote msiniambie hayo yote halafu leo ndo mniambie.
John John akamwambia zawadi 'kukwambia wewe kipindi hicho ilikuwa ngumu kwasababu umri wako ulikuwa mdogo sana, lakini pia watu wa ufalme wenu ni hatari sana na ndio maana sisi huja kimyakimya kwasababu ikitokea wakakuona na sio mtu wao zawadi unayo pokea ni kifo tu.
zawadi akamwambia John John 'hapana watu wangu hawana kawaida hiyo kwa wageni , mimi pia nilikuwa mgeni kipindi hicho na walinilea na kunipa kila kitu iweje leo nyie mniambie kuwa wanaweza kuwauwa wageni. John John hana kawaida yakuongea sana alichofanya 'aliplay' video za matukio yamauaji ya watafiti mbalimbali waliowahi kuuwawa pamoja na askari wa ufalme wa Wetu, kisha akamwambia zawadi mwanzoni serikari haikujua kuwa kwenye kisiwa kile kuna watu wanaishi na hawajui kuwa kuna watu wengine kama wao.
lakini mtu mmoja aliyekuwa anaitwa james alifanya utafiti wake nakugundua wapo watu wanaishi kwakuutambua ufalme tu na sio serikari, wala hawajui biashara,nnchi , kusoma , wala mlokamili lakini pia uvaaji wao ni tofauti kabisa na watu wengine jambo lililomfanya mtafiti huyo kuomba nafasi ya kukutana na rais ili kuweza kuongea nae juu ya 'issue' hiyo.
haikuwa rahisi kwa mtu huyo kuaminika na kupewa nafasi ya kumuona rais kwani ilimchukua miaka miwili na mwishoe kweli alifanikiwa na kumuonyesha rais ushahidi wa picha alizo piga katika ufalme wa Wetu lakini muheshimiwa rais aliona nijambo la kumaliza tu mara moja kwa kumtuma muwakilishi wake akatoe amri ya watu wote waliokuwa katika kisiwa hicho watoke wakakae katika makazi ya watu wengine kwasababu mazingira wanayoishi sio mazuri na katika msitu ule kuna wanyama wakali hivyo ni hatari kwa wao kuishi sehemu kama ile.
Na Kweli muwakilishi alitoka huku na kwenda kutembele eneo lile lakini matokeo yake watu wa kule walimuua na kumtupa baharini kwasababu walimuona kama ni mtu mbaya jambo ambalo lililomfanya rais aanze kuchukulia sasa serious juu ya jambo hilo kwasababu watu kama wanaua bila ya kujali lolote ni hatari kwasababu ufalme wao ukiwa na nguvu hawashindwi kuleta vita, jambo ambalo litakuwa sio sahihi ukizingatia sisi wote ni watu wamoja tunatofautiana kitu kimoja nyie hamja pokea mabadiliko lakini sisi tumepokea mabadiliko, na ndio maana uvaaji wetu na uwazaji wetu ni tofauti na sisi .
Zawadi alimwambia John John nitaaminije hivi vitu unavyo nionyesha kuwa ni watu wa kweli ? Kama kawaida John John akamvuta Zawadi na kumsimamisha pembeni ya kitanda kisha akampiga picha kupiti laptop yake kisha akamwambia zawadi njoo uone , zawadi alishangaa sana kuona mtu kama yeye na hapo ndo alibakia kuduwaa nakuwaambia naomba kurudi nyumbani sitaki kusikia kitu kingine chochote, John John alijalibu kumuelezea mambo mengi lakini zawadi aliziba masikio na kumwambia anahitaji wampeleke nyumbani kwao , hataki kusikia mambo mengine zaidi. lakini John aliwaambia hamna kumrudisha mpaka aelewa kwamba baadhi ya maadui wanaweza kutumia maeneo hayo ambayo wao wanakaa, na kwakuwatumia hao wanaweza kuwashawishi kuteketeza nchi yao wenyewe kwasababu tu ya uelewa wao mdogo.
Zawadi hakutaka kuelewa hayo na alipoona hakuna mpango wakupelekwa popote aliamua kususa kula na kila chakula alicholetewa hakukigusa hali iliyopelekea Zawadi kuanza kukosa nguvu na afya yake kudhohofika jambo lililo mfanya John John kuwapa ruhusa vijana amri ya kumpeleka Zawadi karibu na kwao kisha wao warudi, lakini kabla zawadi hajaondoka John John alimwambia ' binti mzuri nyie ni wachache sana hamuwezi kuwafikia hata chambe idadi ya watu wanaoishi huku hivyo siwezi ruhusu hata maramoja watu wengi waje kuangamia siku moja kwaajili yenu hivyo na kupa siku kumi na tano uwe umesha tuelewa na kuungana nasisi kuwashawishi watu wako, tofauti na hapo tutawaangamiza nyie wachache kwa faida ya wengi kwasababu hata babu zenu waliwaangamiza vijana ambao walijito kwaajili ya wengi hivyo safari hii itakuwa zamu yenu tutawatoa nyie wachache kwasababu ya wale watu wengi. Baadhi ya maafisa usalama wengine wakamchukua zawadi na kumrudisha kama walivyo ambiwa japo zawadi alikuwa tayari amezimia.
Asubuhi ya siku iliyofuata zawadi alizinduka kutoka katika usingizi mzito aliokuwa amelala na alipofungua tu macho alimuona Malkia na hapo ndo alimuuliza mama kwani naota au, lakini Malkia alimuangalia zawadi na kumwambia ' huoti mwanangu na kila mtu anawasiwasi na wewe kwani baada tu ya wewe kutekwa babayako alipata mshtuko na hivi tunavyoongea bado amepoteza fahamu namshukuru mungu angalau umepatikana na leo umepata fahamu, naamini yeye pia ataamka kwani watu wapo nnje siku ya pili hawajala wanamuombea yeye pamoja na wewe mpone.
Zawadi alishtuka sana na kumwambia Malkia ' kwanini unaruhusu watu hao kuishi na njaa kwasababu yangu na baba huoni unawatesa.
malkia alimwambia zawadi hiyo ndo sheria yetu pale ambapo Mfalme , Malkia au Binti Mfalme anaumwa hakuna mtu hataruhusiwa kula. Zawadi alishangaa sana na kumwambia Malkia haya mama basi kawaambie wale chakula basi kwasababu mimi nimesha amka lakini Malkia alimwambia siwezi fanya hivyo Mpaka pale ambapo Mfalme ataamka laasivyo mizimu itatuadhibu na hata ukiwaambia wale chakula mwanangu hawatakula.
Zawadi alishtuka sana na moja kwa moja ilibidi akasaidiane na Daktari kuhakikisha hali ya Mfalme inakuwa sawa kwasababu bila ya Mfalme kupona maisha ya watu wengine yanakuwa hatarini, juhudi za zawadi pamoja na Daktari ziligonga mwamba na hapo ndo zawadi aliamua kwenda mahali ambapo walikubaliana na John John akibadili mawazo aende usiku karibu na bahari kutakuwa na mtu wake ambae atamfikisha kwake na kweli zawadi alienda eneo hilo na alipofika kweli alikutana na mtu na akamuelezea hali halisi ya baba yake na mtu yule akamuahidi zawadi amsubiri mahali hapo mpaka pale atakapo rudi, na kweli zawadi bila ya woga alikaa eneo hilo la baharini mpaka mida ya saa tisa hivi usiku na ndipo mtu huyo alikuja na dawa kwaajili ya ugonjwa wa Mfalme na kumpa zawadi ili akampe Mfalme.
Mida ya saa kumi usiku zawadi alifika katika ufalme na kumwambia Daktari wa ufalme ampishe kidogo, na baada tu ya Daktari huyo aliondoka na kumpisha zawadi, kisha Zawadi akampa Mfalme dawa aliyoletewa na baada tu ya dawa kumpenya katika koo la Mfalme haikupita muda Mfalme akaamka na hapo ndo zawadi akatoka nnje na kuwaambia wapishi wapike chakula kwaajili ya watu lakini baada ya chakula kuiva watu wengi walikuwa amepoteza fahamu na hapo ndo zawadi akakiri kuwa kunaumuhimu wa yeye kumsikiliza John John kwasababu baadhi ya mambo yanayoendelea katika ufalme yalikuwa hayapenyi katika ubongo wake kabisa.
USIKOSE SEHEMU YA 12 NA 13
 
TAMTHILIA: ZAWADI.

MWANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS

SEHEMU YA : 12 $ 13.

WHATSAPP NO :0746115688.

Baada ya kupona kwa Mfalme, Zawadi alikumbuka ahadi aliyoiweka kwa moja kati ya afsa usalama aliyekuwa chini ya john John na hapo ndo alianza kuwaza kwasababu siku zote Zawadi anapotoa ahadi huwa anatimiza, lakini kwa ahadi aliyoitoa kwa John John ilikuwa ikimpa mashaka sana lakini hakuwa na jinsi kwani giza lilipoingia Zawadi alienda katika eneo ambalo ndo amekuwa akikutana na afisa yule wa usalama ambae yupo chini ya John John lakini ajabu safari hii John John ndo alikuwepo yeye mwenyewe katika eneo lile. Zawadi alishangaa sana lakini hakuwa na haki ya kuhoji hayo yote, alichofanya ni alimwambia tunaweza kwenda sasa mana baba yangu ameshapona ni muda wa mimi kuitimiza ahadi yangu. Lakini John John akamwambia huwezi kwenda popote Zawadi kwasababu kazi yako utaifanyia hapahapa, zawadi alishtuka sana na akamuuliza John John "ni kwanjia gani ntaweza kufanya kazi hiyo hapa kwetu ?' John John akamwambia zawadi cha kwanza inakubidi ujalibu kuwa hadithia vitu vizuri ambavyo wewe umekutana navyo kule, lakini pia waelezee jinsi watu wakule wanavyo jali na kuwathamini watu wengine ili tuone kama watabadili fikra zao na kutaka kuishi na wenzao . Zawadi alikubaliana na John John na kweli siku iliyofuata zawadi alipoulizwa na Mfalme juu ya yeye kutekwa yeye alielezea Uzuri tu alio kutana nao kule alipopelekwa na kuwasifia sana watu wakule lakini Mfalme akamwambia ' inawezekana watu hao kwao nipazuri sana lakini mioyo yao ni michafu zaidi kwasababu kama wangekuwa ni watu wazuri kwanini wakuteke inabidi uache tu habari hizo Zawadi mana pengine watu wakijua wanaweza hata kuku tenga.
Zawadi aliyasikiliza sana maneno ya baba yake na hapo ndo aligundua kweli ni ngumu kubadilisha ufahamu wa watu wao na baada ya zawadi kugundua hilo alimwambia John John juu ya msimamo wa baba yake lakini John John alimshawishi angalau atafute watu wakumuunga mkono juu ya jambo hilo ili iwe ngumu kwa watu wanaotaka kumpinga.
Kweli Zawadi akaanza kuwashawishi watu wanao mzunguka hasahasa vijana kama yeye, lakini vijana hao walimchukulia yeye kama msaliti na kusambaza taarifa za kuwa zawadi anampango mbaya na watu wa Ufalme wa Wetu kwa sababu amekuwa akiwashawishi watu kuweza kumuamini na kuwaamini wageni walio mteka yeye, jambo lililo wafanya watu kuweza kumtenga na kumuona mbaya na wala hajali kuhusu wao yeye anachojali ni wageni hao na sio watu wake.
Mfalme alijisikia vibaya sana aliposikia Uvumi huo kuhusu Zawadi, na hapo ndo akamwambia zawadi ' kitendo cha mimi kukukataza wewe kuacha kuendelea kuongelea habari za watu usio wajua vizuri ulikichukuliaje, kwasababu nikama vile unajali sana kuhusu hao zaidi yetu na ndio maana unajalibu sana kuwashawishi watu ili wawakubali watu waliokuteka na wawapende kama unavyo wapenda wewe lakini mimi hujaniweka wazi kabisa lengo lako ninini juu ya watu hao. Lakini pia kama walikuachia kwa masharti niambie tu ili tujue jinsi gani tunatimiza sharti lao na si kuwatumia watu wako kwa faida yao.
Zawadi alijisikia vibaya na kuona hayo yote yanayo mtokea ni kwasababu ya John John kama si yeye baba yake asingethubutu kuongea maneno makali hivyo juu ya binti yake, hivyo zawadi alienda moja kwa moja mpaka wanapo kutana na John John na baada tu ya John John kufika mahala hapo zawadi alimwambia sipo tayari kushirikiana na nyie kwasababu kila nnavyojiweka karibu na nyie napata tabu tu zaidi.
John John alichukia sana kwasababu aligundua kuna baadhi ya maadui wakubwa tu nchini wamekuwa wakienda kujificha katika maeneo yao jambo ambalo ni hatari sana kwa nchi hasa pale ambapo baadhi ya watu wa Zawadi wakiungana na makundi hayo.
Lakini upande wapili zawadi baada ya kurudi katika ufalme alibakia kuwa mpweke sana kwasababu kila mtu katika ufalme wa Wetu alikuwa akimchukia yeye kwa kampeni alizo kuwa akiwafanyia watu wa mjini. John John na yeye baada ya kuona mambo yanazidi kuwa magumu, na magaidi wanazidi kuingia katika kisiwa kile na kutoka kila siku alijua kabisa jambo hilo litakuwa shida kubwa baadae hivyo alicho kifanya alitafuta nyumba moja kubwa sana na kuanza kuwateka watu wa ufalme wa Wetu kidogokidogo na kuwaweka katika nyumba hiyooo na kuwapa elimu zaidi juu ya mambo mbalimbali waliyo kuwa hawayajui. Kilasiku watu walipokuwa wakitekwa lawama zote alikuwa akipewa zawadi jambo lililo mfanya zawadi akose marafiki lakini pia kutengwa na familia yake nzima yaani Mfalme, Malkia na watu waliokuwa wamesalia katika Ufalme huo wa wetu. Zawadi alipoona kila siku watu wake mwenyewe wana mtenga alienda katika eneo ambalo mara nyingi watu wa john John huwa wanakaa hapo , lakini kwa bahatimbaya sio John John wala watu wake walikuwa wakipatikana katika eneo hilo na kibaya zaidi aliporudi katika ufalme siku hiyo watu wote walikuwa wametekwa kama wengine, lakini chaajabu kunawatu tofauti na wafanyakazi wa John John walikuwa wakiwatafuta watu wa ufalme huo na kwambali aliwasikia wakiwa wanakili juu ya mpango wao wa kuwachukua watu wao na kuwatumia watu hao kuigeuka nnchi yao, na hapo ndo zawadi aligundua kuwa ni vizuri watu wake kuondoka katika eneo lile na wala hata hakujisikia mnyonge tena kama awali bali alichukua maamuzi ya kujilengesha kwa majambazi wale na kweli wakaingia katika mpango wake na wakamteka na baada ya muda kidogo wote wakampenda na kumuamini zawadi kwa kila jambo na zawadi akapewa cheo cha usimamizi wa eneo lile na alipoona watu wapale hawamtilii tena mashaka alienda tena kujalibu kukaa katika eneo lile la baharini na kwabahati nzuri siku hiyo John John alikuwepo na alipomuona zawadi alimkumbatia na kumwambia inabidi twende wote kwasababu mahali hapa sio salama tena, lakini zawadi akamwambia John John usijali kabisa mimi nitakuwa katika eneo hili kukusaidia kuwakamata hawa majambazi kwasababu wanavyo onekana ni watu hatari sana na bila ya kuwa waangalizi jambo lolote baya laweza tokea, bora mimi wamenielewa ntaendelea kuwa nao mpaka mtakapo wakamata. John John hakutaka kuniacha pale Zawadi lakini kwakuwa zawadi aliomba sana John John ilimbidi aondoke japo kiukweli alionekana ameanza kuvutiwa sana na zawadi kwasababu jinsi alivyokuwa anawasiwasi na alivyo mkumbatia haikuonyesha kuwa ni wasiwasi wakawaida kwani alikuwa na Shahuku sana ya kumuona zawadi lakini upendo uliakisi kwa namna ambavyo alimuangalia zawadi aliweka wazi juu ya hisia zake kwa zawadi.
Zawadi alifurahi sana kuona angalau John John anaonyesha kumjali sana kwani binafsi awali alihisi kuwa John John aliwachukua watu wote nakuamua kumtelekeza yeye kwa makusudi jambo ambalo sio kweli kwani John John anamjali sana na kumthamini na ndio maana bila kujali alirudi tena kisiwani kwaajili yake tu lakini pia akampa na nafasi ya upendeleo ya yeye kuweza kusikia sauti za wazazi wake kupitia simu jambo lililo mfanya Zawadi afurahi sana.
Sikumoja wakati zawadi akielekea zake kulala katika himaya hiyo ya majambazi , moja kati ya jambazi aliwatuma watu wake, wakaenda kumteka zawadi na kisha wakampeleka kwake na yeye akambaka Zawadi bila huruma, jambo lililo pelekea mkuu wa majambazi hao kumuua jambazi yule kwani yeye pamoja nakuwa ni jambazi ila alikuwa akimchukulia zawadi kama dada yake wakike hivyo hakufurahishwa na kitu kile kilicho tokea. lakini pia baada ya zawadi kubakwa Zawadi alitawaliwa sana na hasira kiasi cha kuamua kuwauza majambazi hao kwa muda mfupi na kweli baada ya muda wa miezi sita zawadi akaongea na mmoja wa maafisa wale wa Usalama wa Taifa na kumpa taarifa zote kuhusu majambazi hao na jinsi ya kuweza kuvamia himaya yao John John alishangaa kwanini Zawadi hakutaka kukutana na yeye, lakini hakujali sana kwani alihisi zawadi hakutaka tu kumsumbua, lakini baada ya mfanyakazi wake kukutana na zawadi aliporudi kwa bosi wake alibakia kumuonea huruma tu John John kwa alicho kiona kwa Zawadi, lakini John John alipo muona afisa wake amerudi na hana raha alimuuliza 'zawadi yuko sawa?" Na afisa huyo alimjibu ndio yupo sawa lakini, John John alishtuka sana na kumwambia malizia lakini ninini, na ndipo afisa huyo akamwambia muheshimiwa zawadi ni mjamzito kwasasa na mimba yake ni kubwa. John John alishtuka sana na kukosa nguvu hata za kusimama kisha akamwambia afisa huyo amekwambia ni ya nani? Afisa huyo alimjibu tu kuwa kweli ni mjamzito lakini hataki kuongelea kuhusu mimba yake kabisa . John John alichukia sana na kumtuma afisa wake apeleke habari makao makuu ili wakavamie haraka.
Kweli baada ya muda watu walijipanga na kwenda kuvamia eneo hilo na kumkamata mkuu wa majambazi hao pamoja na watu wake na kisha wakaingizwa kwenye boti kupelekwa mjini kuhukumiwa kwa ujambazi wao, lakini baada ya boti ya waalifu hao kuondoka boti iliyofuata ilikuwa niya maafisa pamoja na zawadi , lakini chaajabu Zawadi aligoma kuingia kwenye boti hiyo na kuwaambia nyie mnaweza kwenda tu hakikisheni wanaadhibiwa wale ni watu hatari sana. John John alipata hasira sana na kumuuliza 'hivi wewe huelewi maana ya twende au, unataka tufanyejee tukufunge pingu ndo utaungana na sisi au vip . Zawadi alimwambia hapana nyie nendeni mimi ntaishi hapa na sitasababisha matatizo yoyote niaminini. Lakini mmoja kati ya maafisa usalama akamwambia zawadi twende kwani huniamini c tulisha ongea lakini zawadi alimwambi nimebadili mawazo , john akamwambia Zawadi kwani wewe upoje, kati yetu hakuna alie kwambia uwe na mahusiano na majambazi haya sasa wamekupa mimba wanaenda jela sisi tupo hapa tu kukusaidia unatuona wajinga hutaki kuongozana na sisi kwanini lakini unafanya hivyo.
zawadi alijisikia vibaya kwa maneno makali yaliyotoka katika kinywa cha john john na hapo ndo zawadi alikimbilia msituni ili kurudi katika himaya yao ili akakae huko huko ambako watu hawata muhukumu kwalolote lile lililotokea maishani mwake, John John alishangazwa sana na tabia ya Zawadi lakini kwasababu alikuwa na hasira nae juu ya mimba aliyokuwa ameibeba aliwaambia maafisa usalama tuondokeni lakini moja kati ya maafisa hao aliomba kubakia pale na zawadi lakini John John aliwaambia ni amri wote tunaondoka na kweli wakaondoka na kumuacha Zawadi pale. Zawadi alikuwa ni binti jasiri kwaaina flani hivi ya kutisha kwasababu aliishi katika msitu bila hata kuhofia kitu chochote japo alikuwa akishinda kulia na kulala kulia kila alipokuwa akiliangalia tumbo lake.
Sikumoja wakati John John alipoenda kumuhoji jambazi mkuu, jambazi huyo alimuuliza kwanza hali ya zawadi, lakini yeye alimwambia kabakia kule mliko mkuta awali. jambazi huyo alichukukia sana na kumwambia John John nyie hamna huruma kabisa nyie mnamuacha binti wawatu kule na nimjamzito pamoja na yeye kumisaidia, lakini John alimwambia hatukumtuma akafanye umalaya kule ilikuwa ni kufanya kazi tu ya nyie kukamatwa. jambazi huyo akamkaba shingo John John na baada ya watu kuja kumtoa mikono jambazi yule shingoni maw John John , jambazi huyo akamwambia John John hata sikumoja usimtukane zawadi kwasababu ntaakuua unamuita malaya wakati kama sio yeye kujitoa kumisaidia nyie kutukamata sisi, leo angekewa hajabakwa na kupata ile mimba lakini kwasababu yenu yote yametokea halafu mnamlaumu, mashetani wakubwa nyie. mtu hakuwa analala pamoja na mimba yake , anafanya kazi ngumu yote nyie mfanikiwe halafu leo kwenu hana thamani, kweli nimeamini nyie ni watu wabaya sana msio faaa kabisa hata kuwa na rafiki kama Zawadi.
John John alishtuka sana baada ya kusikia maneno hayo na hapo ndo akatoa amri jambazi huyo aingizwe gerezani kisha akamfuata afisa aliyekuwa karibu sana na zawadi kimawasiliano kisha akamwambia niambie kila kitu kuhusu mimba ya Zawadi, na hapo ndo afisa huyo alimwambia John John kweli zawadi alibakwa na aliembaka aliuliwa na jambazi tulie mkamata kwasababu yeye siku zote anamchukulia Zawadi kama dada kwake.
wakati John John anagundua hilo zawadi akampigia simu afisa huyo huku analia akimpa taarifa juu ya kuumwa kwake....

USIKOSE SEHEMU YA 14 $15
 
Back
Top Bottom