moneytalk
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 8,040
- 16,870
ubarikiweTAMTHILIA : CHALLENGE MADE.
MUANDISHI : WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS.
SEHEMU: 15 $ 16.
WHATSAPP : 0746115688.
Grace alihamia rasmi nyumbani kwa Mr.kivuli na Jackbosi alihamia nyumbani kwa grace . grace alimkabidhi Jackbosi kampuni na biashara zote za familia na kumwambia kila kitu ni cha kwetu na sio cha kwangu tu , kwasababu utafutaji wa baba haukuwa kwaajili ya binti mmoja tu bali binti zake wote wawili yaani grace na Jack ndio maana hata kampuni aliita Graja. mimi naenda kwa Mr.kivuli kutafuta uhuru wako mdogo wangu pamoja na mimi na watu wote wanaoteseka kwaajili ya Mr.kivuli na pia kila mtu ajue kuwa wewe ndio Jack mtoto wa mzee wetu Steven na mimi ndio dada yako na Mrs.kivuli ndo mama yetu, kwasababu amekupenda wewe kama mwanae mimi sina tatizo nae kabisa kwasababu furaha yako mdogo wangu ndo ya dada yako kumbuka hilo . Grace alipoondaka Jackbosi alianza rasmi kusimamia kampuni na kwakuwa yeye alisoma biashara alipofika tu hatua ya kwanza alifuta project zote ambazo hazina faida na kupunguza wafanyakazi wasio kuwa na ulazima na kila mfanyakazi aliyekuwa anamfukuza alimlipa fedha za kujikimu Siku hiyohiyo aliyoondoka.
Mr.kivuli yeye hakuweza kujua hata kama pale nyumbani wanaishi na grace kwani hakuwahi kukaa na Jackbosi muda mrefu kiasi cha kujua huyu ni grace na huyu ni Jackbosi.
Baada ya wiki moja rasmi wakinamama wale walio saini mkataba na Mr.kivuli walienda kuanza kazi na Mr.kivuli aliwagawanya katika kila biashara zake akaweka mwanamama mmoja. Kwasiku za mwanzoni kila mwanamama alisimamia vizuri wafanyakazi waliokuwa chini yake lakini hawakuruhusu kabisa mtu yeyote kuona sura zao pamoja na kazi nzuri waliyofanya. Kwabahati nzuri Ade alibahatisha kufanya kazi katika eneo ambalo ndo madawa ya kulevya yanapotengenezwa na james lakini pia huyohuyo james ndo alikuwa kiongozi wa eneo hilo kwa upande wa utengenezaji. Lakini kwabahati nzuri pia Ade aligundua hakuna madawa yaliyo toka nnje ya eneo lile kwani ilikuwa ni ngumu kwao kusambaza amigo kwani James ni mgeni alihitaji mwenyeji kwanza iliasome ramani na ndio maana Ade akaajiliwa ili aandae mpango wa madawa hayo kusafirishwa nnje ya nchi na kusambazwa kwa watumiaji wadogowadogo.
Upande wa grace yeye alijiweka karibu sana na Mr.kivuli na kumfanya amuamini sana kiasi cha yeye kumruhusu kuingia katika chumba ambacho kinanyaraka na karatasi mbalimbali za mikataba yake pamoja na viongozi wa siri ambao walikuwa kwenye mtandao wa Mr.kivuli.
taratibu Mr kivuli alimuamini grace kuwa ni Jackbosi na wafanyakazi alio waajili na baada tu ya wote kupata imani ya Mr.kivuli walipanga Siku ili wakutane wapange mpango wa mwisho wa kumuangusha sasa Mr.kivuli , ambae wao waliamini ndie kiongozi wa biashara zote hizo chafu. Walipo kutana siku hiyo watu walishangaa sana kuona kumbe grace na yeye anateam ya viongozi wa kubwa wa nchi ambao wao ni waaaminifu na wanaopenda nchi yao kiasi cha kujitolea kuungana na grace pamoja na Mrs.kivuli ili waweze kupata uhuru wa nnchi na vijana kwa ujumla kwasababu biashara haramu za Mr.kivuli ziliwalejenga zaidi vijana. kwapamoja walikubaliana kwanza kabisa kuteketeza biashara zote zinazo mhusu Mr.kivuli.
kisha kupata nyaraka za watu wanaoshirikiana nae ili kuweza kuwatishia waweze kutoa ushahidi juu yake ili ahukumiwe, halafu bila ya wao kujua wakati wanatoa ushahidi ndio watakuwa wamejiangamiza pia. wakinamama wanaofanya kazi katika vituo vya Mr.kivuli walipanga mipango ya kuweza kuteketeza sehemu hizo, na baadhi ya wafanyakazi wa Mr.kivuli waliamua kuwasaidia kwani hata wao hawakufurahia kufanya kazi katika biashara zake lakini yeye aliwalazimisha na kuwatishia kuteketeza ndugu zao kama watakataa na hio ndio sababu ya wao kufanya nae kazi hivyo walivyogundua kuna mtu anahitaji kumteketeza Mr.kivuli waliungana nae kwani walikuwa wamesha choka na wanahitaji uhuru wao .
Basi siku moja wakati Mr.kivuli yupo katika Tafrija na wafanyakazi wake mtu mmoja alimtumia ujumbe afungue WhatsApp kuna zawadi yake na Mr kivuli alipofungua aliona jinsi biashara zake zinavyo teketea kwa moto na pia aliwaona wale wakinamama walio vaa maski wakiwaongoza wachomaji wa biashara hizo. Mr.kivuli alipokuwa akijiuliza ni wakina nani hasa hawa wakinamama na kwanini wanafanya hivi wakati niliwaajili na kuwapa pesa nzuri tu, palepale kwenye video wakinamama walivua maski huku wakimcheka sana Mr.kivuli kisha kwapamoja wakamwambia Mr.kivuli wewe ni binadamu tu na kama ulihisi wewe ni mungu bhasi ulikosea sana kwani toka mwanzo ulipaswa kujua wewe ni binadamu tu. Kisha wakinamama kwa pamoja wakavaa maski na kuondoka katika eneo lile .
Mr.kivuli akawagawanya wafanyakazi waliokuwepo katika Tafrija hiyo haraka ili waende sehemu mbalimbali za biashara zake kwani alihisi pengine labda ni utani tu na mambo ya kuedit ili kumkatisha tamaa yeye.
Lakini baada ya muda mchache mfanyakazi wa kwanza alipofika eneo la tukio alimpigia bosi wake video call kumuonyesha kuwa kweli moto umewaka na hakuna jinsi ya kuokoa chochote, baada ya taarifa hizo grace na Mrs.kivuli waliwaambia wageni wote waondoke Tafrija imeghairishwa kisha wakaiingia ndani pamoja na Mr.Kivuli,
wote walikuwa wamekaa kwenye kochi kusubiri taarifa mpya kutoka kwa wafanyakazi walioenda kuangalia maeneo yaliyo bakia na baada ya muda kidogo James alimpigia simu Mr.kivuli na kumpataarifa ya kuwa biashara zote zimeteketea kilichobakia ni majivu tu hakuna cha zaidi.
Hapohapo Mr.kivuli alianguka kwa presha, ndani ya wiki moja alikuwa akiamka analia ntakuwa masikini mimi kisha anazimia, madaktari walijalibu kumuhudumia kwa kadiri walivyoweza na kweli hali yakuzimia zimia ikapotea kabisa na madaktari waka ahidi siku inayo fuata watamruhusu Mr.kivuli. Wakati Mr.kivuli anaugulia hospitali grace alichukua nyaraka zote za siri nakuzificha lakini pia akayapa taarifa mabenki yote aliyokopa kuwa Mr.kivuli kafirisika na hivi karibuni atatoroka hivyo mabenki yote yakaungana na Siku iliyofuata wakati Mrs.kivuli na grace wanamchukua Mr.kivuli kumpeleka nyumbani Mr.kivuli alipofika nnje ya hospitali akaona kulikuwa na mnada wa live kwenye tv uliokuwa ukionyesha jinsi nyumba, magari na mali nyingine za Mr.kivuli zinavyo pigwa mnada na hapo ndo Mr.kivuli alianguka tena na kurudi hodini.
Lakini upande wa Jackbosi bila kumpa taarifa mtu yeyote aliongea na Daktari bingwa wa nchizannje wamasuala ya ubongo na kumueleza afya za wakina mama wote waliochanganyikiwa na akamuelezea pia kuhusu chip walizonazo na Daktari alimpa taarifa Jackbosi anauwezo wakuwasaidia kwasababu upasuaji wao una asilimia sabini na tano za wao kuishi , baada ya jibu hilo Jackbosi alimuuliza Daktari anahitaji kiasi gani lakini Daktari akamwambia nataka wapone tu kwasababu kwa stori uliyo ni hadithia kuhusu wao mimi pia ni muathirika, kwani nililetwa huku kutolewa viungo tu lakini moja kati ya madaktari aliniokoa na kunisomesha mpaka sasa mimi ni Daktari bingwa na nafanya hivi kwaajili ya watu wote walio uwawa kwa amri ya Mr.kivuli kwani sisi ni ndugu tulikua pamoja na kupendana sana kama si yeye naamini tungekuwa pamoja mpaka sasa . wakati grace anammaliza Mr.kivuli taratibu kwa Jackbosi nayeye Daktari aliwasili jijini dar es salaam na kuwafanyia upasuaji wakinamama wote na akafanikiwa kutoa chip kwa wakinamama wote na wote wakatoka katika upasuaji salama lakini pia akaanza kumtibu Steven taratibu taratibu na kweli nafuu ilianza kuonekana.
Mr.kivuli alipo amka kwenye mshtuko wa safari hii alimwambia ukweli wote grace akijua ni Jackbosi kuhusu biashara alizo fanya , Mr.kivuli bila kujua grace alikuwa anamrekodi kwa kamera aliyokuwa ameivaa kama kifungo katika shati lake lakini kikubwa zaidi alimpa siri ambayo hata grace alikuwa hajui kuwa yeye sio bosi wa hizo biashara bosi wake alikuwa ni mstaafu mmoja wa Udaktari ambae anaduka dogo tu la madawa la kuizugia serikari na pia akawaambia mtaa alipo ili wakamwambie anahitaji msaada wake lakini kwa bahati mbaya grace ,Mrs.kivuli pamoja na wakinamama walipoelekea mahali ambapo Daktari huyo yupo walikuta msiba kwani Daktari huyo alijinyonga baada ya kujua mambo yameharibika ili familia yake isimchukulie yeye ni jambazi na kweli japo wakina grace waliwaambia ndugu zake ukweli wa mzee huyo lakini ndugu hawakuamini kwani hawaku wahi kuona dalili yeyote kwa mzee huyo ya kuonyesha anafanya biashara hiyooo.
Wakina grace waliona hamna haja ya kuwalazimisha watu, kwanza kashajiadhibu mwenyewe na kwaupande mwingine bado Mr.kivuli ndo hatari zaidi kuachiwa huru kwani yeye ndo alikuwa mpangaji mkuu na msimamizi wa biashara hizo hivyo akiwa huru mambo yataharibika hivyo grace pamoja na Mrs.kivuli walimua kumfungulia mashtaka Mr.kivuli kwa kujihusisha na biashara za madawa, na viungo vya binadamu mashtaka ya madawa yalipelekea james kukamatwa .
wakati Mr.kivuli yupo hospitalini alishangaa kwenye tv kuona mkewe na grace wamemshitaki yeye tena bila woga hapo ndo Mr.kivuli akili alimjia akavua nguo za hospitalini na kutoroka hivyo polisi walipo kuwa wakimtafuta hospitalini ili akamjibu mashtaka Hawakumpata.
grace nae alimwambia Mrs.kivuli asiwe na wasiwasi kwani Mr.kivuli hana pakwenda chaumuhimu ni kuwalaghai washirika wake , na kweli grace akakutana na washirika mbalimbali wa mr.kivuli na kuwaonyesha ushahidi wa kuwamaliza kama hawatatoa ushahidi dhidi ya Mr.kivuli na kweli washirika wake wote baada ya kuona ushahidi huo hawakuwa na jinsi walikuwa tayari kusimama mahakamani kama mashahidi . Usiku mmoja polisI walipo kuwa katika windo walimuona Mr kivuli akiwa amepitiwa na usingizi chini ya gari la kubeba mataka na hapohapo wakamkamata na baada ya mwezi kesi ilipelekwa mahakamani na mashahidi wa kwanza walikuwa ni wakinamama waliokuwa na grace hospitalini ambao ushahidi wao ulikataliwa kwani mahakama ilishindwa kuamini kua kweli Mr.kivuli anapandikiza mbegu kwa wakinamama kwani wao watoto walikuwa ni wawanaume zao ambao wanadai wameuwawa na Mr.kivuli, hivyo mahakama ili mwambia grace atafute ushahidi mwingine. grace akawashawishi viongozi walioshirikiana nae na kweli waliwasili mahakamani na kutoa ushahidi lakini baada ya grace kutoa ushahidi mwingine wa video ambayo ilikuwa inaonyesha hadi wao walikuwa pamoja na Mr.kivuli mahakama ili kataa kuwaamini pia kwani waliamini grace kuwatishia kwani ni ngumu mtuhumiwa kutoa ushahidi wa kujizulu bila sababu za msingi hivyo hakimu aliomba utulivu mahakamani na kumwambia grace kama hana ushahidi wa kueleweka kesi itafungwa mana hapangilii ushahidi hivyo Mr.kivuli atahukumiwa kwa makosa yenye ushahidi tu na makosa yenye ushahidi yalikuwa madogodogo tu ambayo anaweza epuka kwa faini tu .
grace alichoka kwani alikuwa hajui atapatia wapi ushahidi mwingine wakuwafanya Mr.kivuli na wenzake wasitoke jela kabisa lakini ghafla hakimu kabla hajatamka hukumu Jackbosi aliingia akiwa na wakinamama wale walio kuwa wamechanganyikiwa tena wakiwa wazima pamoja na Steven na Daktari yule ambae ni ushahidi tosha wa suala la upandikizaji wa mbegu kwani yeye pia mamayake alipandikizwa tu mbegu hivyo yeye hamjui hata baba yake zaidi ya mama yake, lakini pia anajua hadi hospitali wanayotolewagwa vijana hao viungo baada ya kutolewa nchini na Mr.kivuli.
hakimu alimuuliza wewe ni nani na Jackbosi alimwambia muheshimiwa hakimu mimi naitwa jack Steven ila maarufu kama Jackbosi na hawa unao waona mbele yako ni waathirika waliotokana na huyo Mr.kivuli yaani namaanisha baba yangu mlezi.
Mr kivuli alishangaa sana kwani aliyekuwa akimuhisi kama Jackbosi ni grace lakini pia alijua ni ngumu kupona tena kwa ushahidi aliokuwa nao Jackbosi hivyo alimwambia muheshimiwa hakimu inatosha , kwasasa naomba tu nafasi ya kuongea kidogo, muheshimiwa hakimu akampa Mr.kivuli nafasi aliyo itaka na Mr kivuli kwanza akakubali shutuma zake na kumwambia hakimu hata hawa viongozi kweli wanahusika na taratibu akawageukia viongozi wale pamoja na wafanya biashara wakubwa tu na wengine ni viongozi hadi wa dining ambao alikuwa wanaoshirikiana nao kisha akawaambia wakubwa Inatosha hakuna njia ya kutoka tena na wote wakainamisha vichwa chini kwa aibu . Mr kivuli akamuomba hakimu tena nafasi ya kuongea japo kidogo na hakimu alimpa tena nafasi, Mr.kivuli akasema nashukuru sana wote nyie mlioshirikiana kuhakikisha leo najuta kwa ubinafsi na tamaa zilizo kuwa zina niandama, lakini pia nashukuru kwani nyie mmenifundisha kuwa changamoto zinaweza kujenga usipo jali ujenzi huo utachukua muda gani, mimi umaskini tu ulinifanya nikaogopa kabisa kupambana nikashawishiwa na Daktari john ambae ni marehemu kwasasa nakwapamoja bila kujali tukatumia uhai wawatu wengine kama pesa kwetu, mpaka sasahivi najiuliza kama umaskini tu umenifanya nikawa mtu mbaya hivi je ingekuwa ndugu zangu ndo wamepitia waliyo yapitia ndugu zenu sijui nchi yangu leo ingekuwa inapambana na mtu wa namna gani, kisha mr.kivuli akatoa bunduki aliyokuwa ameificha na kuisalimisha kwa askari wakaribu yake kisha akasema nilitamani mambo ya kiwa magumu nijipige risasi nifie mbali ili aibu isinipate lakini nimegundua hata nijikatekate vipande kama nyama cwezi lipa madhambi niliyo tenda hivyo muheshimiwa hakimu naomba nipe adhabu itakayo wafanya watu waogope kabisa kufikilia kufanya nilicho kifanya mimi. kisha Mr.kivuli akamwambia Jackbosi ahsante sana wewe pamoja na dada yako grace kwa mlicho kifanya pamoja na mke wangu kaeni mkijua sijawachukia wala sinakinyongo na nyie nisameheni sana kama inawezekana na nawapenda sana kuanzia sasa kwani mmenifundisha upendo ananguvu kiasi gani . Baada ya maneno hayo Mr.kivuli alihukumiwa kunyongwa pamoja na washirika wake wote.
grace aliendelea kuwa Daktari na kumlea mwanae, lakini pia Jackbosi aliolewa na Daktari yule na alipata watoto wake wawili , wakinamama waliendelea nashughuli zao kwa wale waliokuwa na taaruma zao na wengine waliajiliwa katika kampuni ya Graja chini ya usimamizi wa mwenyekiti Jack steven
MWISHO.
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app


