Asimulia alivyojifungua kwa upasuaji katikati ya tetemeko la ardhi

Asimulia alivyojifungua kwa upasuaji katikati ya tetemeko la ardhi

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,112
Maria Florida ameeleza furaha yake baada ya kujifungua salama mtoto wake wa nne kwa njia ya upasuaji wakati tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.7 likitikisa eneo la Nusa Tenggara Mashariki mwa Indonesia.

Tetemeko hilo lilitokea Agosti 15, 2026 na kuleta madhara makubwa mashariki mwa Indonesia, likisababisha vifo vya watu wasiopungua 54, majeruhi zaidi ya 130 na kuwalazimisha maelfu ya wakazi kuondoka katika maeneo yaliyoathirika.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 39 ambaye alikuwa ameshaanza kufanyiwa upasuaji kabla ya tetemeko hilo kuanza kwenye Hospitali ya Nagekeo, amewashukuru madaktari kwa kujitoa kwao.

Alieleza kuwa madaktari wakiendelea na upasuaji huo umeme ulikatika kutokana na tetemeko, hivyo walilazimika kutumia mwanga wa tochi kuendelea na upasuaji.

Licha ya mazingira hayo hatarishi, madaktari walifanikiwa kumleta duniani mtoto wa kike aliyempa jina Gempita Soli Wona, linalohusishwa na neno la Kiindonesia linalomaanisha tetemeko la ardhi.

Mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 1.3 na kwa mujibu wa taarifa za madaktari anaendelea kuimarika kiafya. Kutokana na mitikisiko kuendelea na baadhi ya miundombinu ya hospitali kuathirika, mtoto huyo amewekwa katika mashine maalumu ya kuhifadhi joto iliyowekwa nje ya hospitali.

kujifungua.png
 
Back
Top Bottom