Ushasema mtu binafsi, ingekuwa ya umma sawa. Hapo ni mwenyewe anapanga cha kufanya, hakuna anayemtolea fungu la kumpa kwenye biashara zake hadi uje ulalamike. Hata hiyo hoteli ni hivyohivyo, ushasema ni binafsi.
Hizo ni kama shule za kidini za kikristo, hakuna anayewapangia cha kufanya maana ni binafsi. Mabinti hata wa kiislamu wakiingia wanaambiwa hakuna hijabu na wawe kichwa wazi, hakuna mwislamu aliyewahi kuja kulalama hilo. Nazo ni za mtu binafsi ameweka udini kwenye biashara. Mbona hamsemi?
Hoteli uliyoitaja ina sheria za kiislamu, kama zilivyo shule zenu na baadhi ya taasisi kuwa na sheria za kikristo na hazilalamikiwi.