Tamthilia ya Zahanati Kijijini

kukumsela

JF-Expert Member
Oct 13, 2018
721
907
Wakuu habarii,

Kiukweli naomba nianze kukiri kuwa Mimi binafsi sio Mpenzi wa Tamthilia/Filamu za hapa nyumbani Almaarufu kwa Jina la Bongo Movie na hii inatokana na Tamthilia/Filamu zetu kuwa na Ubora Mdogo Jambo ambalo Limetufanya kuvutiwa zaidi na Uamthilia za Ughaibuni.

Siku Moja Majira ya saa 1 Usiku Nilipokosa cha kufanya Nikiwa Sebuleni Nilikutana na Tamthilia tajwa hapo juu ikiwa inaonyweshwa kupitia Channel ya Sinema Zetu inayopatikana katika King'amuzi cha Azam.

Kiukweli baada Kuiangalia Nilivutiwa mno na Tamthilia hiyo huku nikivutiwa zaidi na Wahusika wake walivyovaa Uhusika , Ubora wa Sauti na Picha sambamba na Mazingira/Manthari waliyoigizia kwakweli hongera Director kwa kazi nzuri.

Mwisho nahitimisha kwa kusema kuna haja sasa kwa Bodi ya Filamu hapa Nchini kuwapiga Msasa Waongozaji wa Tamthilia na Filamu hapa Nchini kuhakikisha wanaandaa Kazi zenye Viwango vya Kimataifa pamoja na kutunga Story zenye kuakisi Maisha ya Watanzania walio wengi ili ziweze kupata nafasi ya kuonekana katika Majukwaa Mbalimbali ya Kimataifa kama vile Netflix,Amazon Video, Prime Video, Fubo Tv, Hbo Tv, AppleTv +,Acorn Tv,Disnep +, Hulu nk.

Nawasilisha
KUKUMSELA.
 
Kwahiyo nawe kuna manesi wanaishi na kufanya vile kwenye zahanati ipi nchi hii. Wameongeza sana Mbwembwe na kuua uhalisia wake bro.
Ndiyo maana ya sanaa
Lazima mbwembwe ziongezwe tupate comedies lakini uhalisia upo pale pale

Wapo wauguzi washirikina
Wapo wanaofitiniana makazini
Wapo wasio na passion na kazi zao
Wapo wasio na weledi na kazi zao

Wapo wauza dawa wasio na taaluma
Na wapo wenyeviti/watendaji wanaochukulia vijiji ni mali zao binafsi

Sanaa sanaa sanaa!
 
Nimecheka sana kosa moja yaan Jay voice ana vitujo saana
Unaiangalia
Umeona anavyomwambia naa aweke mkia kule mbele 🤣

Mimi Cathy ananiboa.
Ameharibu mchezo wote,, huwezi kuwa na mwanamuziki amepoa vile utadhani anaimba nyimbo za kuabudu.
 
Back
Top Bottom