Abdul Usanga ndiye 'producer' bora wa tamthilia kwa sasa Tanzania, Afrika Mashariki na Kati

kukumsela

JF-Expert Member
Oct 13, 2018
721
907
Kiukweli huyu jamaa anajua mnoo ameandaa tamthilia kadhaa kama vile saluni ya mama kimbo, Kombolela na sasa tamthilia ya zahanati ya kijiji.

Mwisho natoa rai kwa waongozaji wengine wa tamthilia kujifunza kwake kuanzia katika uandaaji, maudhui nk ili kutengeneza tamthilia zenye ubora ili kazi zetu za hapa ndani ziweze kufanya vizuri katika uga wa kimataifa

Naomba kuwasilisha wakuu.

Uzi tayari
 
Mama kimbo ilizoa fan sana ,sikuitazama sana sababu imekaa kike lakini ni wazi wahusika wake (producer&Director)wana talent kubwa
 
Mama Kimbo sikuwahi kuangalia naona ilikua ya wanawake zaidi ila Kombolela kuna siku niliwahi kuangalia yaan ni maisha yetu kabisa ya uswahilini.

Ilikua nzuri sana
 
Shida waigizaji wengi bongo hawajui kuigiza.. Hawalet i uhalisia ukitizama unaona kabisa huyu anaigiza...

Maongezi hayavutii, sijui wandaaji hawajui kuandika au waigizaji huwa wanapiga freestyles!?
Kabisaa mkuuu
 
Kiukweli huyu jamaa anajua mnoo ameandaa tamthilia kadhaa kama vile saluni ya mama kimbo, Kombolela na sasa tamthilia ya zahanati ya kijiji.
Mwisho natoa rai kwa waongozaji wengine wa tamthilia kujifunza kwake kuanzia katika uandaaji, maudhui nk ili kutengeneza tamthilia zenye ubora ili kazi zetu za hapa ndani ziweze kufanya vizuri katika uga wa kimataifa

Naomba kuwasilisha wakuu.

Uzi tayari
Hizo sikuwahi tazama ila ramata na ramata village yake nimemwelewa kwenye juakali hasa wale wasanii wake maria na luka na mama luka na walokole wote kwa ujumla wao mle.
 
Broo fuatilia izo tamthilia ni zamotoo
 
Kiukweli huyu jamaa anajua mnoo ameandaa tamthilia kadhaa kama vile saluni ya mama kimbo, Kombolela na sasa tamthilia ya zahanati ya kijiji.
Mwisho natoa rai kwa waongozaji wengine wa tamthilia kujifunza kwake kuanzia katika uandaaji, maudhui nk ili kutengeneza tamthilia zenye ubora ili kazi zetu za hapa ndani ziweze kufanya vizuri katika uga wa kimataifa

Naomba kuwasilisha wakuu.

Uzi tayari
Tumekusikia na tumekuelewa Abdul shnga hongera sana unafanya poa
 
Shida waigizaji wengi bongo hawajui kuigiza.. Hawalet i uhalisia ukitizama unaona kabisa huyu anaigiza...

Maongezi hayavutii, sijui wandaaji hawajui kuandika au waigizaji huwa wanapiga freestyles!?
Swala la maongezi(dialogue) kwenye movie ni suala la pande zote mbili...yaani Uigizaji na Uandishi.

Unaweza ukawa Muandishi Mzuri lakini ukawa sio mzuri kwenye dialogue...na hata kama ukaandika dialogue nzuri unakuta Muigizaji/Waigizaji hawapo tayari...kiufahamu(weledi), utayari wa muda (reharsal) n.k.

Hivyo kinachotokea ni uandishi wa kutozingatia sana eneo la dialogue hivyo Muandaaji humuachia Muigizaji uwanja wa kujinafasi (free style).

Kunahitajika mageuzi makubwa kwa upande wa Uandishi na uigizaji kufika huko..si rahisi kama ambavyo Mtu angefikiria.
 
Shida waigizaji wengi bongo hawajui kuigiza.. Hawalet i uhalisia ukitizama unaona kabisa huyu anaigiza...

Maongezi hayavutii, sijui wandaaji hawajui kuandika au waigizaji huwa wanapiga freestyles!?
Tamthiliya za kibongo chenga tupu yaan , asilimia 96 % scene ni wamekalisha mitako kwenye masofa , chumbani kitandani , au kwenye kibaraza wanaongea ikizidi Sana ofsini ... Mandhari kubadrika hamna kabisa , alaf mda wote wamejipodoa lipstic inang'aa mdomoni😳
 
Back
Top Bottom