AMNUT kutokana na madai yake ya longo longo kama hayo hayo ambayo kila siku mnayataka ya kutaka nchi iwe ya dini ilibidi ijifie natural death tu maana ilikutana na kisiki cha Butiama!
viliku
Au kuna jibu zaidi ya hili!
Uncle...
Mimi nilipoandika kitabu cha
Abdul Sykes sikufanya hivyo kwa nia ya
kushusha hadhi ya
Mwalimu Nyerere katika harakati za kupigania uhuru
wa Tanganyika.
Nimeandika kitabu hiki kwa nia ya kueleza historia ya TANU na harakati
za kudai uhuru kwa kuwa vitabu vyote vilivyokuwa vimeandikwa vilikuwa
vikianza na
Julius Nyerere mwaka wa 1954 TANU ilipoundwa.
Kwa kufanya hivyo historia muhimu ya African Association na TAA hadi
kufika kuundwa kwa TANU ilikuwa imepotezwa.
Nimeanza kuandika nikijua kuwa historia hii haikuwa inatakiwa kwani
kulikuwa na mradi wa TANU yenyewe wa kuandika historia yake ambao
Abdul Sykes alipewa jukumu la kuandika historia hiyo akishirikiana na
Dr. Wilbard Kleruu.
Abdul Sykes hakukamilisha kazi hii alijitoa baada ya kugundua kuwa
historia iliyokuwa inatakiwa kuandikwa si ile anayoijua yeye na
Abdul
akijua mengi katika historia ya TANU kwani baba yake alikuwa muasisi
wa African Association mwaka wa 1929.
Sasa unazungumza kuhusu ''ranking,'' sijui utafanya hivyo kwa vigezo
vipi kwani ikiwa ni historia ya TANU hakuna ushahidi mahali popote
unaoonyesha kuwa
Nyerere alifika kwa
Abdul Sykes 1952 akiwa na
''blue print,'' ya TANU.
Harakati hizi za kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika alizikuta
kwa
Abdul Sykes na kabla yake yalipita mengi na kulikuwa na wengi
katika juhudi ya kufanikisha lengo hili.
Upo ushahidi wa mchango mkubwa wa
Hamza Mwapachu katika kufikia
lengo la kuunda TANU na itoshe tu kuwa mkutano wa kumtia
Nyerere
katika uongozi wa TAA uliofanyika nyumbani kwake Nansio, Ukerewe
miezi ya mwanzo ya mwaka wa 1953 kati ya yeye
Hamza, Abdul Sykes
na
Ally Mwinyi Tambwe aliyekuwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya.
Hapa sikutaka kukurejesha nyuma 1950 kwenye TAA Political Subcommittee
ambayo wajumbe wake wake walikuwa:
Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdulwahid
Sykes, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven
Mhando na
John Rupia.
Wala sijataka kukuonyesha viongozi wa TAA ambao waliingia katika
uongozina
Julius Nyerere pale alipochaguliwa kuwa Rais wa TAA katika
mkutano uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 17 Aprili, 1953.
Viongozi hawa ni:
J.K. Nyerere, President;
Abdulwahid Sykes, Vice-
President;
J.P. Kasella Bantu, General Secretary;
Alexander M. Tobias and
Waziri
Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary;
John Rupia, Treasurer na
Ally K.
Sykes - Assistant Treasurer. Committee members
Dr. Michael Lugazia,
Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi,
C. Ongalo na
Patrick Aoko.
Sasa huwezi kufanya ''ranking,'' ya mtu mmoja lazima wawe wengi na
unaanza juu hadi unafika chini.
Ukiwa unataka kufanya ''ranking'' inabidi sasa uanze na wajumbe wa TAA
Political Subcommittee uwachanganye na hii Halmashauri ya TAA ya 1953.
Kuna wengine wamehusika sana lakini majina yao huwezi kuyaona hapo
juu mfano
Earle Seaton.
Haya ndiyo yaliyonifanya mimi niandike historia ya TANU na uhuru wa
Tanganyika kusahihisha historia iliyokuwapo.
Kuhusu AMNUT nimekwisha eleza hapa kuwa ni jina tu ''Muslim,'' ndilo
linalokufanya wewe ukiite chama cha Waislam.
Waislam chama chao kilikuwa TANU.
AMNUT iliundwa 1958 na
Ramadhani Mashado Plantan, Abdulwahid
Abdulkarim, Hamisi Hunde na
Abdallah Mohamed watu ambao hawakuwa
na ushawishi mkubwa katika siasa za wakati ule ukimtoa
Mashado Plantan.
Hayo mengine sijaona haja ya kukujibu.