Tamthilia ya Bibi Titi Mohammed na Prof. Emmanuel Mbogo

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,020
2,000
Tuesday, 20 December 2016
TAMTHILIA YA BIBI TITI MOHAMED NA PROF. EMMANUEL MBOGO

Hapo chini ni kidokezo kaniandikia rafiki yangu Tamim Faraj kuhusu kitabu cha Bi. Titi Mohamed ambacho alikuwa kamaliza kukisoma na kimemgusa sana. Kaniandikia ili nami nikisome. Chini ya saa moja kitabu kikawa kimenifikia nyumbani na chini ya saa moja nyingine nikawa nimemaliza kuisoma tamthilia nzima ya Bi. Titi iliyoandikwa na Prof. Emmanuel Mbogo:
''Asalaam Aleykum,
Nimekisoma kijitabu (61 pages) cha tamthilia juu ya Bibi Titi - tiled: MALKIA BIBI TITI MOHAMED by Prof. Emmanuel Mbogo.
Ni kizuri.
Ni script iliyo capture vizuri a short history on the role of Bibi Titi katika kuupigania uhuru wa Tanganyika. pazia la tamthiliya linafunguka jela ya Isanga alikofungwa Bibi Titi na kufungwa huko baada ya uhuru kupatikana.

Setting imepangwa kumuonesha Bi Titi akiwa jela na daftari ambalo anaandika historia ya harakati za uhuru.

Zubeda askari jela baada ya kujua anachoandika Bi Titi, anamuomba kutumia historia aliyoiandika Bi Titi ili kuandaa igizo kwaajili ya kuazimisha sherehe za uhuru Disemba.

Anamueleza Bi Titi kawaida ya jela kufanya hivyo kila mwaka. Hivyo amamshawishi wafanye mchezo kwa mujib wa alichokiandika katika daftari lake na kumuomba Bi Titi ashiriki pamoja na wafungwa wenziwe.

Mwisho pazia linafungwa kwa Zubeda kurudishia daftari la na pia kumpa barua ya taarifa ya kutolewa gerezani.''

Tamim
***********************************************************************************
Kitabu kinaanza mwaka wa 1970 kwa kumuonyesha Bi. Titi akiwa Gereza la Isanga Dodoma, moja ya magereza magumu Tanzania. Kabla yake mwaka wa 1953 mwanasiasa mkubwa sana Tanganyika sehemu za Maziwa Makuu, Ali Migeyo alifungwa gereza hilo na Waingereza kwa kosa la kufanya mkutano wa siasa Kamachumu bila idhini ya serikali. Miaka 17 baadae mpigania uhuru Bi. Titi yuko kifungoni kwa kuhusika na kesi ya uhaini kutaka kuiangusha serikali aliyoipigania wakati wa kudai uhuru.

Akiwa hapo gerezani Bi. Titi anaandika historia ya uhuru wa Tanganyika na anaeleza ushirikiano wake na Nyerere wakati wakiwa katika ofisi ya TANU New Street. Bi. Titi anaeleza katika mswada wake, anaoandika jela vipi yeye na wenzake walipita mtaa kwa mtaa kueneza TANU.

Kitu cha ajabu Gereza la Isanga wanamuomba Bi. Titi watumie historia yeke ile kufanya onyesho la historia ya uhuru wa Tanganyika.

Bi. Titi akiwa katika moja ya matawi ya TANU Dar es Salaam tawi hili lilikuwa Magomeni Mapipa nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu 1955

Picha ya Mwandishi aliyopiga Viwanja Vya Mnazi Mmoja mwaka wa 1966 nyuma yake ni barabara iliyokuja kujulikana baadae kama Titi Street kwa kumuenzi Bi, Titi Mohamed na ukivuka barabara hiyo linaloonekana ni Soko la Kisutu maarufu kama ''Soko Mjinga.''

Tamthilia hii ya Bi. Titi Mohamed ni kazi ya kupigiwa mfano kwani naamini hii ni tamthilia ya kwanza ambayo imejaribu kuhadithia historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuwataja wale ambao waliupigania uhuru wa Tanganyika. Kurasa za mwanzo Mwandishi anamleta Schneider Plantan akizungumza na Boi Selemani kuhusu TANU.

Bwana Boi akimlalamikia Schneider kuwa mkewe Bi. Titi hatulii nyumbani kwa ajili ya shughuli za TANU kiasi imekuwa yeye ndiyo mfuaji wa nguo zake na mpishi wa chakula chake.

Boi Selemani alikuwa dereva wa taxi.

Schneider yeye ana historia ndefu katika siasa za Tanganyika. Yeye ndiye aliyesimama kidete kuwaleta vijana wasomi katika TAA ili kuwaondoa wazee waliokuwa wamechoka na kuifanya TAA isifanye siasa za maana kwa ajili ya ukombozi wa Tanganyika.

Hii ilikuwa mwaka wa 1950.

Sasa TANU ilipokuja kuasisiwa mwaka wa 1954 Schneider ndiye aliyemleta Bi. Titi katika TANU pamoja na wenzake akina Tatu Bint Mzee na wanawake wengine kuja kukipa nguvu chama.

Tamthilia inaanza mwaka wa 1955 wakati Bi. Titi na wenzake wako katika hekaheka ya kuhamasisha wananchi kujiunga na TANU na wakati huo ndiyo safari ya Julius Nyerere kwenda UNO inatayarishwa.

Boi katika mazungumzao yake na Schneider anatabiri kuvunjika kwa ndoa yake na mkewe Bi. Titi kwa ajili ya TANU na anamtupia lawama zote rafiki yake Schneider Plantan kwa kumpeleka mkewe TANU.

Boi analalamika hadi kufikia kusema, ''Titi mwanamke wa Kiislam. Kasoma madrasa....Bibi Titi kapanda jukwaani...hana baibui...''

Bi Titi Mohamed na Julius Nyerere wakihutubia wananchi Uwanja wa Jangwani 1955

Kulia ni Bi. Titi Mohamed, Clement Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Julius Nyerere na nyuma ya Nyerere ni Maria
Nyerere, Rajab Diwani na John Rupia

Kitabu hiki, ''Malkia Bibi Titi Mohamed,'' ukikianza hukiweki chini hadi umekimaliza.
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,020
2,000
Bibi Titi walielewana sana na Rais Nyerere, nadhani hata kitendo cha Nyerere kumuweka gerezani ali kifanya tu, ki protocal but these two loved each other so much.

*no publication
Iceman,
Hapana Nyerere na Bi Titi walitofautiana mwaka wa 1963 tatizo likiwa
East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ambayo Nyerere alitaka
kuipiga marufuku Tanganyika na akawa anatafuta kuungwa mkono
ndani ya TANU NEC.

Katika moja ya mkutano walitoleana maneno na hapo ndipo ugomvi
ulipoanzia.

Bi. Titi kaeleza haya katika mahojiano na gazeti la Rai 20 September
1994.

Unaweza ukasikiliza habari hii hapo chini:
Blogger
 
Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,629

Ahsante sana Mohamed Said
Nimekuelewa kwenye chanzo, lakini nimeshindwa kusikiliza hiyo attachment. Kwa kuwa niki ingia ina niletea vitu sivijui. Hivo nasumbuka kuipata.

Lakini ninavo jua mwisho wa siku Rais Nyerere ndio ali mfanya bibi titi atoke jela na baada ya hapo hapakuwa na maneno tena kati yao. Nadhani na Nyumba zake alimrudishia.
Pia naskia kuwa ugomvi wao hasa hasa ni ule wa azimio la arusha. Kuhusi suala la umiliki wa mali.
point yangu kubwa ni Rais na Bi Titi walipishana baadhi ya misimamo tu ila bondi yao ilikuwa kubwa.
Hawa wazee hata uki waangalia walikuja kuelewana na waliridhia kuwa tofaut zao ndogo ndogo ziliwatenganisha kidogo. Walikuwa wana chemistry ya asili.

Nitafurahi kama uta nirekebisha nilipo kosea ahsante
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Tuesday, 20 December 2016
TAMTHILIA YA BIBI TITI MOHAMED NA PROF. EMMANUEL MBOGO

Hapo chini ni kidokezo kaniandikia rafiki yangu Tamim Faraj kuhusu kitabu cha Bi. Titi Mohamed ambacho alikuwa kamaliza kukisoma na kimemgusa sana. Kaniandikia ili nami nikisome. Chini ya saa moja kitabu kikawa kimenifikia nyumbani na chini ya saa moja nyingine nikawa nimemaliza kuisoma tamthilia nzima ya Bi. Titi iliyoandikwa na Prof. Emmanuel Mbogo:
''Asalaam Aleykum,
Nimekisoma kijitabu (61 pages) cha tamthilia juu ya Bibi Titi - tiled: MALKIA BIBI TITI MOHAMED by Prof. Emmanuel Mbogo.
Ni kizuri.
Ni script iliyo capture vizuri a short history on the role of Bibi Titi katika kuupigania uhuru wa Tanganyika. pazia la tamthiliya linafunguka jela ya Isanga alikofungwa Bibi Titi na kufungwa huko baada ya uhuru kupatikana.

Setting imepangwa kumuonesha Bi Titi akiwa jela na daftari ambalo anaandika historia ya harakati za uhuru.

Zubeda askari jela baada ya kujua anachoandika Bi Titi, anamuomba kutumia historia aliyoiandika Bi Titi ili kuandaa igizo kwaajili ya kuazimisha sherehe za uhuru Disemba.

Anamueleza Bi Titi kawaida ya jela kufanya hivyo kila mwaka. Hivyo amamshawishi wafanye mchezo kwa mujib wa alichokiandika katika daftari lake na kumuomba Bi Titi ashiriki pamoja na wafungwa wenziwe.

Mwisho pazia linafungwa kwa Zubeda kurudishia daftari la na pia kumpa barua ya taarifa ya kutolewa gerezani.''

Tamim
***********************************************************************************
Kitabu kinaanza mwaka wa 1970 kwa kumuonyesha Bi. Titi akiwa Gereza la Isanga Dodoma, moja ya magereza magumu Tanzania. Kabla yake mwaka wa 1953 mwanasiasa mkubwa sana Tanganyika sehemu za Maziwa Makuu, Ali Migeyo alifungwa gereza hilo na Waingereza kwa kosa la kufanya mkutano wa siasa Kamachumu bila idhini ya serikali. Miaka 17 baadae mpigania uhuru Bi. Titi yuko kifungoni kwa kuhusika na kesi ya uhaini kutaka kuiangusha serikali aliyoipigania wakati wa kudai uhuru.

Akiwa hapo gerezani Bi. Titi anaandika historia ya uhuru wa Tanganyika na anaeleza ushirikiano wake na Nyerere wakati wakiwa katika ofisi ya TANU New Street. Bi. Titi anaeleza katika mswada wake, anaoandika jela vipi yeye na wenzake walipita mtaa kwa mtaa kueneza TANU.

Kitu cha ajabu Gereza la Isanga wanamuomba Bi. Titi watumie historia yeke ile kufanya onyesho la historia ya uhuru wa Tanganyika.

Bi. Titi akiwa katika moja ya matawi ya TANU Dar es Salaam tawi hili lilikuwa Magomeni Mapipa nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu 1955

Picha ya Mwandishi aliyopiga Viwanja Vya Mnazi Mmoja mwaka wa 1966 nyuma yake ni barabara iliyokuja kujulikana baadae kama Titi Street kwa kumuenzi Bi, Titi Mohamed na ukivuka barabara hiyo linaloonekana ni Soko la Kisutu maarufu kama ''Soko Mjinga.''

Tamthilia hii ya Bi. Titi Mohamed ni kazi ya kupigiwa mfano kwani naamini hii ni tamthilia ya kwanza ambayo imejaribu kuhadithia historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuwataja wale ambao waliupigania uhuru wa Tanganyika. Kurasa za mwanzo Mwandishi anamleta Schneider Plantan akizungumza na Boi Selemani kuhusu TANU.

Bwana Boi akimlalamikia Schneider kuwa mkewe Bi. Titi hatulii nyumbani kwa ajili ya shughuli za TANU kiasi imekuwa yeye ndiyo mfuaji wa nguo zake na mpishi wa chakula chake.

Boi Selemani alikuwa dereva wa taxi.

Schneider yeye ana historia ndefu katika siasa za Tanganyika. Yeye ndiye aliyesimama kidete kuwaleta vijana wasomi katika TAA ili kuwaondoa wazee waliokuwa wamechoka na kuifanya TAA isifanye siasa za maana kwa ajili ya ukombozi wa Tanganyika.

Hii ilikuwa mwaka wa 1950.

Sasa TANU ilipokuja kuasisiwa mwaka wa 1954 Schneider ndiye aliyemleta Bi. Titi katika TANU pamoja na wenzake akina Tatu Bint Mzee na wanawake wengine kuja kukipa nguvu chama.

Tamthilia inaanza mwaka wa 1955 wakati Bi. Titi na wenzake wako katika hekaheka ya kuhamasisha wananchi kujiunga na TANU na wakati huo ndiyo safari ya Julius Nyerere kwenda UNO inatayarishwa.

Boi katika mazungumzao yake na Schneider anatabiri kuvunjika kwa ndoa yake na mkewe Bi. Titi kwa ajili ya TANU na anamtupia lawama zote rafiki yake Schneider Plantan kwa kumpeleka mkewe TANU.

Boi analalamika hadi kufikia kusema, ''Titi mwanamke wa Kiislam. Kasoma madrasa....Bibi Titi kapanda jukwaani...hana baibui...''

Bi Titi Mohamed na Julius Nyerere wakihutubia wananchi Uwanja wa Jangwani 1955

Kulia ni Bi. Titi Mohamed, Clement Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Julius Nyerere na nyuma ya Nyerere ni Maria
Nyerere, Rajab Diwani na John Rupia

Kitabu hiki, ''Malkia Bibi Titi Mohamed,'' ukikianza hukiweki chini hadi umekimaliza.
Sasa hivi nnamtumia ujumbe Ami Faraj anitumie kopi japo kwa email.

Shukran Alama.

Unajuwa Almarhum kaka'ke Faraj Tamim aliitwa "Alama" Tamim?
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Ahsante sana Mohamed Said
Nimekuelewa kwenye chanzo, lakini nimeshindwa kusikiliza hiyo attachment. Kwa kuwa niki ingia ina niletea vitu sivijui. Hivo nasumbuka kuipata.

Lakini ninavo jua mwisho wa siku Rais Nyerere ndio ali mfanya bibi titi atoke jela na baada ya hapo hapakuwa na maneno tena kati yao. Nadhani na Nyumba zake alimrudishia.
Pia naskia kuwa ugomvi wao hasa hasa ni ule wa azimio la arusha. Kuhusi suala la umiliki wa mali.
point yangu kubwa ni Rais na Bi Titi walipishana baadhi ya misimamo tu ila bondi yao ilikuwa kubwa.
Hawa wazee hata uki waangalia walikuja kuelewana na waliridhia kuwa tofaut zao ndogo ndogo ziliwatenganisha kidogo. Walikuwa wana chemistry ya asili.

Nitafurahi kama uta nirekebisha nilipo kosea ahsante
Unaambiwa tofauti zilianza 1963 kwa sababu ya Nyerere kutaka "kupiga marufuku" EAMWS, wewe unasema azimio la Arusha ambalo lilikuja 1967.

Au hujamsoma vizuri Alama Mohamed Said alivyokujibu?

Tafadhali rudia kusoma majibu yake.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Huyo ndiyo mwanamke wa Dar.

Allah amghufirie maghf.iran kathiran na atughufirie na sote.

Utotoni niliitwa Titi, kwa unene wa utotoni niliokuwa nao walinipa "nickname" kutokana na jina la huyu bibi mwenye enzi, she was a symbol ya wanawake mahodari.

Hawa ndiyo wanawake wa kuandikwa historia zao kwa wino wa dhahabu.
 
ISIS

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
91,509
2,000
Huyo ndiyo mwanamke wa Dar.

Allah amghufirie maghf.iran kathiran na atughufirie na sote.

Utotoni niliitwa Titi, kwa unene wa utotoni niliokuwa nao walinipa "nickname" kutokana na jina la huyu bibi mwenye enzi, she was a symbol ya wanawake mahodari.

Hawa ndiyo wanawake wa kuandikwa historia zao kwa wino wa dhahabu.
Ni kweli na ni mfano wa kuigwa lakini sio kwenye siasa bali biashara kwani nchi yetu ni tajiri sana. ..kweli utashangaa maana jana nilikuwa na wahindi fulani. ..yaani tukiweza kuhamisha mawazo yetu tukayaweka kwenye kutafuta biashara. ..itakuwa safi sana. .maana mawazo ndiyo kila kitu....MAMA YETU BIBI TITI AMESHATUFUNGULIA MLANGO WA UHURU. .ni juu yetu sasa kutafuta vipawa na hekima ili tuweze kufanya biashara za nguvu. ....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom