TAMKO:YAH:Kuvunjwa rasmi kwa uhusiano baina ya madame b na chimbuvu.

snowhite mbona hivyo aise
Dena Amsi ile ni nyumba kubwa na naruhusiwa kuwa na wa pembeni kama wanne so bado nafasi ipo usiwe na shaka dear

Wewe Mzee hebu tuheshimiane hiyo ruhusa nani katoa na lini??? Mr Rocky nataka maelezo ya kina hapa kumbe ndo ulikuwa hulali kumbe ndo unafanya madudu yako huku today no "Morning Groly"
 
Last edited by a moderator:
Wewe Mzee hebu tuheshimiane hiyo ruhusa nani katoa na lini??? Mr Rocky nataka maelezo ya kina hapa kumbe ndo ulikuwa hulali kumbe ndo unafanya madudu yako huku today no "Morning Groly"

ayaaaaaaaah!KIMENUKA TAYARI!
tatizo mumeo ya makadara ayataka yeye,ya jang'ombe ayatafta yeye,ya kipatimu ayajue yeye sasa matokeo yake ndo haya !sasa wasiwasi wangu kama kazi itafanyika kweli bila huo ubarikio!dah! af ndo mida yake hii !sipati picha ulimbalasaje aliposogeza mkono !
 
sitamani kuyaona haya yakuvunjiwa ndoa ndoa.madame B
Nakushauri kama unampenda mumeo wa zamani rudi.kama humpendi vunja ukimya dai chako talaka ni haki yawote kuomba kikatiba

Umenena vema mkiva , hata kama ndoa inavunjika lazima iwe kwa utaratibu maalum unaokubalika kisheria
 
Last edited by a moderator:
Kichwa cha habari Chahusika.
UTANGULIZI
Takribani wiki mbili zilizopita nilileta kwenu taarifa ya kutengua uhusiano batili kati cha Chimbuvu na mke wa mtu Madame B. Kathka taarifa ile niliwataka Madame B na Chimbuvu kusitisha maramoja uhusiano wao batili au la waurasmishe kwa sheria na taratibu halali za hapa chit chat.Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kujitokeza yafuatayo
i.Malalamiko yaliyofikishwa mbele ya tume yangu na ndugu Ruttashobolwa ambae ndie mume halali wa Madame B
ii.Malalamiko yaliyoletwa kwangu na wanachit chat wengi tu juu ya tabia inayokera ya Madame B na Chimbuvu ya kutoheshimu ndoa hivyo kulipaka matope jukwaa tukufu la chit chat.
iii.Barua rasmi iliyoletwa kwangu na shemeji zake Madame B ambao ni ndugu zake Ruttashobolwa wakitaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya wahusika. ndugu hao ni Judgement, Bishanga na nitonye.
iv.Hali ya sintofahamu iliyotokea hapa jamvini baada ya Madame B kudaiwa kuwatapeli kimapenzi wadau tedo na chilli.

Baada ya taarifa ile wahusika hawakuonyesha utayari wa kutekeleza maelekezo HALALI ya tume na kuendelea na uhusiano wao unaotia kinyaa.
Tangu jana tarehe 28/11/2012 nilikuwa napitia ripoti za kamati ya SCREENING ,SHERIA na ile ya MAADILI, na baada ya kujiridhisha natoa maazimio yafuatayo
i Madame B akiri kuwa yeye ni mke halali wa Ruttashobolwa kama inavyofahamika hapa na aombe msamaha kwa wana chit chat wote kwa usumbufu aliousababisha.
ii Chimbuvu atoe tamko rasmi la kuachana na Madame B na aombe msamaha kwa usumbufu aliowasababishia wana chit chat wote.
Hayo yote yafanyike kabla ya siku ya ijumaa tarehe 30/11/2012 saa tano asubuhi. Kushindwa kufanya hivyo kutapelekea hatua zifuatazo kwa wahusika zikiwa kama ni hatua za awali.
i Madame B na Chimbuvu kutopewa LIKE na mwana chit chat yeyote katika post zao.
ii.Kuto QUOTE post yoyote ya Madame B au Chimbuvu.
iii.Kuwekwa hadharani kwa picha zao ZA AIBU walizopigwa bila wao kujua.Kazi hii itafanywa na Asprin na Mtambuzi.
iv.Kusutwa hadharani wote wawili wakiwa wamevishwa kanga na kupakwa majivu. Kazi hii itafanywa na gfsonwin cacico snowhite ,FP lara 1 Ciello na Zinduna chini ya usimamizi wa malafyale watu8 huku ikifadhiliwa na Arushaone na Bishanga.
Aidha tume inampongeza sana ndugu Ruttashobolwa kwa kuonyesha busara na utulivu wakati tume ikishughulikia suala lake.
Mwisho natoa wito kwa wadau wote kusimamia utekelezaji wa maazimio na kusimamia taratibu halali zilizowekwa.
Baba V
MWENYEKITI WA TUME ZA KURATIBU MAHUSIANO NA NDOA CHIT CHAT 2012

Wafanye siri,
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nikacheki na kile kikundi cha matarumbeta na ngoma ya kibao kata kwa ajili ya shughului hii adhimu..
 
Nimerudi mamaa,ingawa jana wakati nadrive usiku nilibadilishana gari na rafiki yangu ila tulipofika njiani gari langu lililokuwa mbele lililushiwa vitu vyenye ncha kali na kumjeruhi rafiki yangu,katika purukushani wale watu walikimbia na tulimpeleka hospitali na cm yangu ilipotea ktk mazingira ya kutatanisha ila sasa suala lipo polisi,

Baba V,siwezi toa uamuzi wowote.
Kwani mpenzi wangu wa sasa Chimbuvu sijui aliko mpaka muda huu.
Anaweza akawa ametekwa na mume wa zamani Ruttashobolwa au la.
Hvyo nataka nijue usalama wake kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Nimerudi mamaa,ingawa jana wakati nadrive usiku nilibadilishana gari na rafiki yangu ila tulipofika njiani gari langu lililokuwa mbele lililushiwa vitu vyenye ncha kali na kumjeruhi rafiki yangu,katika purukushani wale watu walikimbia na tulimpeleka hospitali na cm yangu ilipotea ktk mazingira ya kutatanisha ila sasa suala lipo polisi,

Heee....
Pole mpenzi wangu.
Ndio maana kila nikipiga simu yako,nasikia sauti ya mtu aongeae kihaya.
Pole sana mpenzi.
Mimi nilijua tu.
Mpenzi wangu nifanyaje?
Ukizidi kuwa nami,wanaweza kukudhuru au hata kukuua kabisa.
 
Back
Top Bottom