Jamani wadau wa JF nimefuatilia kwa makini mjadala wenu kuhusu hiki chuo chetu kipya cha Tanzania International University(TIU). Nataka kuwahakikishia na kuwaondoa wasiwasi kuwa hiki chuo kipo na Mipango ya kukianzisha ilianza toka 2010 kwa ku-prepare curriculum, kujenga majengo nakufanya vitu vingine ambavyo vitafaa kwa chuo kuweza kukubalika na TCU lakini pia kuwezesha kutoa elimu bora ya chuo kikuu pindi TCU watakopo ruhusu chuo kianze ku-enrol wanachuo. Kwahiyo basi naomba kuwahakikishia wanaJF na watanzania kiujumla kuwa chuo kipo Kimara Mwisho njia ya kwenda Bonyokwa nafasi za kazi zilizotangazwa ni za Kweli hakuna utapeli wowote mtu anayejiona anafit kwenye post yeyote kati ya zile zilizotangazwa atume maombi yake; kwani chuo kinahitaji wahadhiri wa ngazi zote toka ma-professor hadi ma-tutorial ili kiwe na uwezo wa ku-enrol student mwaka huu. Ndugu za wanaJF na watanzania wote tuachane na maneno mbovumbovu yasiyokitakia chuo hiki kimpya TIU maendeleo. Mwisho kabisa nawaweke link ya TCU inayoonyesha chuo hiki kimesajiliwa kwa REG No CR1/028 ila kinasubiri kuanza ku-enrol wanafunzi baada ya kuajili wa2 wenye sifa nzuri kama nyie http://www.tcu.go.tz/images/pdf/Recognised_Universities_Colleges_Centres.pdf baada yakufunguka angalia no 20. WanaJF jitokezeni ombeni kazi kwani hizi kazi pia zimetangazwa katika mitandao ifuatayo http://www.brightermonday.com/jobs/default.asp?bmed=tz na http://www.zoomtanzania.com/sectionoverview?ParentSectionID=8&CurrentPage=3&SortBy=MostRecent waweza zi-copy link hizi na kuzi-paste kwenye browser bar. Kuhusu website yetu ambayo ni main page iko katika kutengenezwa baada ya mwezi mmoja kila kitu kuhusu chuo chetu hiki kipya TIU kitakuwa pia kinapatikana humo. Niwatakieni WanaJF wote kazi njema.
"We Build the Kingdom"
Huu ndo msemo wa wana-Tanzania International University (TIU)
KARIBUNI SANA
"We Build the Kingdom"
Huu ndo msemo wa wana-Tanzania International University (TIU)
KARIBUNI SANA