Tamko Sahara Media Group kuhusu kufungiwa vyombo vyake

Tamko Sahara Media Group kuhusu kufungiwa vyombo vyake

kutetea wakwepa kodi na ada za leseni kisa ni wa chama chetu au kabila letu halikubaliki. wahusika wakalipe kodi na wakatumikie adhabu...
 
kutetea wakwepa kodi na ada za leseni kisa ni wa chama chetu au kabila letu halikubaliki. wahusika wakalipe kodi na wakatumikie adhabu...
 
Nimepata private message ya Diallo on the matter, Magufuli na serikali yake wanachemka sana.

Diallo analipa hela nyingi kuliko the rest of media houses in the lake zone combined, amelipa 75% ya deni lake, na kulikuwa na makubaliano ya kulipa zote.Isitoshe, wanalipishwa kwa USD kinyume na maagizo ya BOT.

July to October tu mwaka 2015 wanadai wamelipa Sh 210 m.

Kwa kawaida, mtu anayefanya biashara na uongozi, mdeni hafungwi kwa kutolipa deni kama ameonyesha nia ya kulipa deni, analipa deni kila mwezi na kashalipa zaidi ya 75% ya deni.

Kama haya madai ni ya kweli, serikali ya Magufuli inazidi kuniaminisha kwamba inafanya kazi kwa pupa.

Zaidi, hizi ada ziko juu sana kiasi kwamba zinakuwa anti business. Katika structuring ya kodi na ada, ukiweka kodi na ada za juu sana unaweza kuua ng'ombe anayekupa maziwa kwa kumkamua mpaka damu. Isitoshe, ada za juu sana zinaweza kuwapa watu ushawishi wa kutafuta mianya ya kukwepa ada.
Wewe kama ni staff wa hiyo tv wacha mfungiwe maana anaye nufaika ni diwaloo nawe unaambulia makombo
 
Tundu lisu alisema a vigelegele hivi ni vya wasioelewa. Ukweli nikwamba ni maigizo tu wala hakuna kitu kama hicho labda el ndo angeifungia star tv
Tweeeeeeeeeee tweeeeeeee tweeeeeeee tweeeeeeeeee
 
azam tv na star tv zimetoka kupendwa na watu wengi,, tofauti na itv inategemea watu wa kaskazini tu
 
Sahara media siyo media ya kitaifa...labda ya kikabila ..wafungiwe na iwe fundisho KWA wengine, wameingia katika list of shame on tax evasion ...media yenye most low profile journalists....
 
Ingekuwa ada ziko juu angetoa free airtime kwa ccm? He's as corrupt as most ccm affiliated businemen... To hell to hell,mwambie akalipe kodi... Ada eti inalipwa kwa dollar.. So what...anadhani media business ni sawa na kuchunga ng'ombe?
 
Ada ya masafa na leseni ni shilingi milioni mia tano kwa mwaka?
seriously?
Same problem again and again...tunakosea sana kuchanganya siasa na biashara. Kama wafanyabiashara wangetumia platform yao vizuri na kutafuta majawabu ya changamoto za kibiashara nje ya ulingo wa kisiasa, mambo mengi yangekuwa tofauti sana.

Kitu serious kama hiki kilidharaulika sababu siasa ilikuwa inaziba sheria kuchukua mkondo wake. Wafanya biashara wengi walikuwa wanaamini kwa kukifadhili chama hawatakiwi kutoa kodi stahiki.

Leo hii mambo yanawakuta kwa suprise...pole zao wote.

Kama tunajitakia mema na kuitakia mema nchi yetu, biashara zisiendelee kuchanganyika na siasa na kukosa uadilifu wa kuzifanya biashara hizo. Imagine Star TV miezi mitatu bila kuonekana kwa watumiaji wake??!!!

Dawa ya deni ni kulipa...maana hakuna namna
 
Huo utetezi ndio jamaa walikuwa wanapiga goli la mkono!
Maana baada ya hapo tcra wangeomba radhi kuiweka startv na RFA ktk list, bahati mbaya muandishi kakosea kujitetea na amekoroga mambo!
Wangeng'ang'ania wamelipa basi wange back date tu tarehe ya malipo! Kosa hilo la kusema wamepewa siku 2 hivyo hawakuweza kulipa on time! Hilo ndilo lilioharibu hili bao la kisigino!
nimethibitisha bila shaka kwamba hamjalipa ada ; maelezo yenu tu ni kitanzi , sasa haya ndio madhara ya kutumika bure wakati wa uchaguzi , poleni sana , maana hakuna kulipa tena hadi pale miezi mitatu itakapoisha , mlipewa muda lakini mliuchezea kwa kampeni za bure .
 
Tamko Sahara Media Group kuhusu kufungiwa vyombo vyake.
Jan 17th, 2016
Manejimenti ya sahara media group ikizungumzia juu ya taarifa hizo imesema haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA ya kutakiwa kufunga vyombo vyake,

Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni miatano hadi kufikia mwezi October 2015.

Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA akanda ya Mwanza, makao makuu na sahara media group limited nakukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika.

lakini menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutanagaza kuvifungia vituo vyake kupitia kutano wa vyombo vya habari bila kujali athari zakufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma.

Sahara media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.

Menejimenti pia imelaani kwa taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki nakuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri jumamosi na jumapili sio siku za kazi.

Menejimenti ya star tv inawaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake, hatua thabiti zitachukuliwa ili kumaliza tatizo hili kwa sahara media group limited na TCRA Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria, Kanuni Na Maridhiano.
Poleni sana Sahara Media Group. Tatizo kubwa la viongozi sasa hivi ni kila mmoja kutaka asikike na ili kufanya hivyo kila kitu watafanya kwa kustukiza ili waonekane wako kazini. Ni jambo la kushangaza kwa jambo kubwa kama hilo badala ya kuwaletea taarifa kwa maandishi wanakwenda kuongea na waandishi wa habari ili waonekane na wasikikike.
 
ndo hapo sasa na ndiomaana pesa yetu inazidi kudrop kila kukicha, dola inazidi kupanda
La ajabu serikali hiyo hiyo utasikia inawazuia watoa huduma wengine kutoza kwa dola. Hata mitandao ya simu zamani ilikuwa inatoza kwa dola serikali ikaingilia kati na kuzuia kumbe yenyewe nayo inaidharau shilingi yake kwa kutoza kwa dola. Ajabu!
 
Kuweka rekodi sawa tu (kwa kadiri ninavyojua na kwa uzoefu wangu):

Suala la kutoza kwa USD: Hakuna sheria inayozuia kutoza kwa USD. Tutofautishe kutoza na kulipa (au kukubali malipo). Tozo inaweza kuwa kwa currency yoyote, lakini mlipwaji hana haki ya kukataa kulipwa kwa shilingi kwa sababu shilingi ya Tanzania kwa transactions za ndani ndio "legal tender". Kwa hivyo mtozaji anaweza kutoza bidhaa/huduma/kodi/Ada kwa kutumia USD lakini mlipaji ukitaka unaweza kulipa equivalent amount ya Shilingi kwa kuzingatia exchange rate za BoT (au benki husika au rate nyingine ambayo wahusika wanaweza kukubaliana nayo). Kwa wale mnaoingiza magari au bidhaa kutoka nje mnaweza kuwa mashahidi wa jinsi kodi inavyokokotolewa kwa dola na malipo yanafanyika kwa shilingi.

Kwa hivyo Sahara hawana hoja mahususi katika hili la USD kwa sababu hakuna sheria iliyovunjwa (actually hivyo viwango vya Ada vipo kisheria/kikanuni kabisa na katika USD). Na kwa wote wanaoomba leseni au wenye leseni zitolewazo na TCRA viwango hivyo vipo wazi kabisa na havijaanza mwaka jana au huu. Kwa nini malalamiko yaje sasa? Lakini generally, inaweza kujengwa hoja na kupitisha sheria ya kuzuia utozaji kwa currency tofauti na Shilingi. Lakini kwa sasa, hiyo sheria haipo.
 
Back
Top Bottom