mdhalendo
JF-Expert Member
- Dec 14, 2011
- 282
- 273
Tamko Sahara Media Group kuhusu kufungiwa vyombo vyake
Jan 17th, 2016
Manejimenti ya sahara media group ikizungumzia juu ya taarifa hizo imesema haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA ya kutakiwa kufunga vyombo vyake,
Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia tano hadi kufikia mwezi October 2015.
Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA kanda ya Mwanza, makao makuu na sahara media group limited na kukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika.
Lakini menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutangaza kuvifungia vituo vyake kupitia mkutano wa vyombo vya habari bila kujali athari za kufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma.
Sahara media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.
Menejimenti pia imelaani kwa taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki na kuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri Jumamosi na Jumapili sio siku za kazi.
Menejimenti ya star tv inawaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake, hatua thabiti zitachukuliwa ili kumaliza tatizo hili kwa sahara media group limited na TCRA Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria, Kanuni Na Maridhiano.