Tamko Sahara Media Group kuhusu kufungiwa vyombo vyake

Tamko Sahara Media Group kuhusu kufungiwa vyombo vyake

Naona wachangiaji wa hii thread niu UKAWA !
Pole sana kwa maumivu ya uchaguzi mkuu
Star TV itakuwa hewani kama kawaida
 
Hoja yao ya kulipa kwa dola sijui kama ina mashiko hao wengine wanalipa kwa hela ya Zimbabwe ??? Nendeni bungeni mkabadilishe hizo sheria za ajabu sio jambo linapowakuta wakubwa mnaanza kulia lia
 
Kwa taarifa hii ya Sahara ni kweli wanadaiwa.Ni vema wakawa na tabia ya kulipa kodi ili kuepuka usumbufu na kuwapa wasiwasi wateja wao.Hata hivyo ni vema TCRA nayo ikazingatia sheria.Kudai Sahara walipe kodi in US dollars wakati wote tuko Tanzania sio sahihi na kwa kweli inashusha thamani ya shillingi yetu.Niseme pia kwamba haikuwa uungwana kuwapelekea taarifa Sahara over the weekend huku wakijua kwamba kufanya hivyo kunawapunguzia muda wa kutekeleza amri yao.Ni vema tukapenda kusaidiana kuliko kukwamishana.
Tamko Sahara Media Group kuhusu kufungiwa vyombo vyake.
Jan 17th, 2016
Manejimenti ya sahara media group ikizungumzia juu ya taarifa hizo imesema haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA ya kutakiwa kufunga vyombo vyake,

Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni miatano hadi kufikia mwezi October 2015.

Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA akanda ya Mwanza, makao makuu na sahara media group limited nakukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika.

lakini menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutanagaza kuvifungia vituo vyake kupitia kutano wa vyombo vya habari bila kujali athari zakufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma.

Sahara media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.

Menejimenti pia imelaani kwa taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki nakuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri jumamosi na jumapili sio siku za kazi.

Menejimenti ya star tv inawaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake, hatua thabiti zitachukuliwa ili kumaliza tatizo hili kwa sahara media group limited na TCRA Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria, Kanuni Na Maridhiano.
 
Ni jambo la aibu serikali kupitia TCRA kutoza ada kwa dola.
 
Kwani mlifikiri mkiwapigia debe ccm ndo hamtachukuliwa hatua za
Kisheria haya sasa ile miziki mliyokuwa mkipiga
Wataisoma namba sasa
Someni ninyi wenyewee...
 
Hawa majamaa ata mabenki yangekuwa chini yao ni watu ambao kesho wanaweza kukurupuka na kusema na benki ya MNB isifungue ofisi zao zote nchini kisa wana mgogoro nao bila ya kujali athari kwa wateja wanaotumia hizo huduma wala impact ya uchumi.

Hivi Star TV imeajiri watu wangapi Tanzania ambao TRA inachukua PAYE pia na hiyo mishahara inayotumika katika kuchochea uchumi, kwa miezi mitatu TRA inapoteza kiasi gani cha kodi ya faida kutoka kwa hawa jamaa za faida ya biashara kwa kutokuwa hewani, jamii inakuwa deprived vipi kupata habari, wafanya biashara wanaotangaza wanaathirika vipi.

Unataka kuniambia huyu jamaa anayetoa haya matamko anaelimu yoyote ya biashara kweli wakati anapewa kusimamia kitengo cha biashara haya ndio mambo tunayoyalalamikia mtaalamu anatakiwa kutoa technical advice sio kuendesha taasisi zilizokaa kibiashara sitashangaa kusikia jamaa ana li Phd sijui ya mambo engineering za communication mambo ya biashara hanayo ufahamu nayo ata chembe ndio logic ya mtu anaeweza amua vitu kama hivi tu.
 
Kwani Rates za TPA na TRA nazo si zipo kwenye mfumo wa USD..

Waache kulialia na visababu uchwara Wakalipe kodi, zile anasa za dr dhaifu zishaamia Msoga..
 
kwani n wao tu wanalipishwa kwa USD?

mbona media zingine wanalipa?

hizi ni unnecessary excuses.walipe alafu wa channel madai Yao kwa utaratibu unaoeleweka

alafu mkuu stop this business ya kutetea wakwepa kodi

Hujajibu swali uliloulizwa.

Kwa nini media house yoyote ile Tanzania ilipishwe kwa USD wakati BOT ishakataza?

Utasemaje unnecessary excuse wakati rate ya dollar to Tsh ina affect fedha zinazolipwa?

Serikali dunia nzima zinakubali wafanyabiashara walio nyuma katika malipo ya kodi zao kama wameonyesha nia ya kulipa kodi na wamelipa zaidi ya 75% ya kodi zao.

Hiyo hata IRS hawawezi kukufungia, watakufungiaje wakati wakikufungua wanaikosa hiyo 25% na wakikubaliana kufanya kazi nawe wanaipata hiyo 25% ?

Serikali hii inavyofanya ni kama vile kufungia biashara ni kitu cha muhimu zaidi ya kukusanya %25 iliyobaki kwenye deni la ada.
 
Hoja yao ya kulipa kwa dola sijui kama ina mashiko hao wengine wanalipa kwa hela ya Zimbabwe ??? Nendeni bungeni mkabadilishe hizo sheria za ajabu sio jambo linapowakuta wakubwa mnaanza kulia lia
Ukweli kwamba wengine wanalipishwa kwa USD hauondoi ukweli kwamba hilo ni kinyume na sheria.

Hakuna sheria inayosema watu walipe ada kwa USD. Kama ipo iweke hapa.

Bank of Tanzania ineshakataza malipo haya kwa USD.

Kama hujui kitu nyamaza, usijitie kujua usichojua.
 
Wafungiwe tu nilikuwa nawapenda lakini kampeni zilivyoanza niliichilukia sana na hata matangazo ya biashara yangu nilihamisha.walikuwa hawabalance mambo kama wenziye itv
mnafiki mkubwa wewe kwa hiyo itv ndiyo walikuwa wana balance habari
 
Ni jambo la aibu serikali kupitia TCRA kutoza ada kwa dola.
Ni makosa ya serikali kutofuatilia madeni yake kwa wakati. Mbona wafanyakazi serkalini wanakatwa kodi kabla ya mshahara.
 
Kwahiyo pesa ya kulipa ilikuwepo au!kama menejiment imetoa hayo maelezo nina wasiwas na menejiment yenu.
 
Tamko Sahara Media Group kuhusu kufungiwa vyombo vyake.
Jan 17th, 2016
Manejimenti ya sahara media group ikizungumzia juu ya taarifa hizo imesema haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA ya kutakiwa kufunga vyombo vyake,

Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni miatano hadi kufikia mwezi October 2015.

Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA akanda ya Mwanza, makao makuu na sahara media group limited nakukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika.

lakini menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutanagaza kuvifungia vituo vyake kupitia kutano wa vyombo vya habari bila kujali athari zakufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma.

Sahara media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.

Menejimenti pia imelaani kwa taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki nakuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri jumamosi na jumapili sio siku za kazi.

Menejimenti ya star tv inawaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake, hatua thabiti zitachukuliwa ili kumaliza tatizo hili kwa sahara media group limited na TCRA Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria, Kanuni Na Maridhiano.
Taasisi za serikali inakuaje zinatoza ada zake kwa dola,ukienda TFDA napo unapigiwa hesabu za dola,ukienda Tanroads faini kwa dola etc nashindwa kuelewa kabisa
 
Wacheni na nyinyi muisome namba.
Hivi kituo chenu cha Star TV si ndiyo kilikuwa kikijifanya kimbelembele kwa kutoa 'ofa' ya kurusha mikutano yake yote ya Magufuli aliyokuwa akiifanya mikoani?

Hata hivyo nimeamini kweli Magufuli hasomeki, nakumbuka alipofanya mkutano wa kufunga dimba kampeni zake pale jijini Mwanza, Magufuli alim_5wita juk🙂@aani mmiliki wa t, Media Anthony Diallo na kumwahidi pale gzys kuwa kutokana na kazi kubwa ya 'kumbfdzaeba' iliyofanywa na szèKCDTVARZZG vyake vya habari, akamuahidi pale pale uwanjani kuwa pindi atakapoingia Ikulu, hatamsahau kwenye 'ufalme' wake.
Kumbe Magufuli kumkumbuka kwake kwenye ufalme wake alikomuahidi Diallo kumbe ndicho hicho kibano cha TCRA?!
 
Tundu lisu alisema a vigelegele hivi ni vya wasioelewa. Ukweli nikwamba ni maigizo tu wala hakuna kitu kama hicho labda el ndo angeifungia star tv
 
Back
Top Bottom