Tamko la wakristo kuhusu machafuko na hali ya vitisho Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la wakristo kuhusu machafuko na hali ya vitisho Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magobe T, Jun 1, 2012.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Sisi Maaskofu, Mapadre, Wachungaji na Waumini tunaoishi Zanzibar, tumekutana leo tarehe 30 Mei 2012 kufutia hali ya machafuko, uvunjifu wa amani, uchomaji wa Makanisa, uharibifu wa mali za Kanisa na vitisho dhidi ya Wakristo na mali zao.

  Tumekutana na tunatoa tamko baada ya muda mrefu wa kimya na uvumilivu tuliosafiri nao kwa takribani miaka 11, kwa kumbukumbu zetu tangu mwaka 2001. Tunajua na tunauambia umma wa wapenda amani kuwa matukio ya tarehe 26 hadi 28 Mei 2012 ni matokeo ya mahubiri na mihadhara ambayo imekuwa ikiendeshwa iliyolenga kwa makusudi kuutukana na kuukashifu Ukristo hapa visiwani Zanzibar na hivi kupandikiza hofu miongoni mwa waumini wa dini ya Kikristo. Tunashawishika kusema kuwa ufadhili na ushawishi wa vurugu na vitisho hivi vina udhamini wa ndani au nje ya nchi yetu.

  Tumefikia hatua hiyo baada ya matukio mbalimbali yaliyokuwa yanafanywa dhidi ya Kanisa na mali zake tangu mwaka 2001 hadi hivi majuzi yalikuwa yakitolewa taarifa kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa visiwani Zanzibar lakini ushirikiano umekuwa mdogo na kwa sehemu kubwa dhaifu sana. Kwa maelezo na vielelezo ni kwamba, jumla ya makanisa yasiyopungua 25 yamevunjwa na kuchomwa moto tangu mwaka 2001, pamoja na ahadi za Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo yote yaliyopata kutolewa taarifa hakuna hata moja lililothibitika wahusika kukamatwa, kufikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua za kisheria. Kumekuwa pia na vitendo vya kuchoma magari huko Pemba na hapa Unguja, na Serikali kwa upande wake imeshiriki hata kupora ardhi na majengo ya Kanisa hapa Unguja na huko Pemba.

  Tumebaini pia hasa baada ya matukio ya vurugu za tarehe 26 hadi 28 Mei 2012 kuwa kuna mikakati ya makusudi ya kuwafanyia Wakristo vurugu. Mikakati hiyo inajumuisha mambo kama vile kuchoma Makanisa zaidi, kuharibu mali za Makanisa yakiwemo mashule, vituo mbalimbali vya Kanisa vinavyotoa huduma za kijamii hapa Visiwani.

  Mkakati au mpango huo umepangwa na unakusudiwa kutekelezwa kati ya tarehe 1 na 2 Juni, na tarehe 8 na 9 Juni mwaka huu. Tunazo taarifa tunazoweza kuzithibitisha kuwa baadhi ya Wakristo wamekuwa wakitumiwa jumbe za simu za mkononi (SMS) zikiwatisha na kuwataka waondoke visiwani humu mara moja hata kama ni wazawa.

  Sehemu ya pili ya mkakati ni kuwasaka Wakristo nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kuwaangamiza, kuwabaka na kuwalawiti.

  Chakusikitisha zaidi ni pale ambapo baadhi ya walinzi wa Usalama wa raia hasa Polisi wenye asili ya hapa Visiwani Zanzibar kusikika wakisema kuwa wataunga mkono vurugu kila zitakapotokea.

  Kufuatia maelezo hayo yote, Sisi Maaskofu, Wachungaji, Mapadre na waumini tuliokutana leo, tunapenda kwanza kutoa neno la shukrani kwa uongozi wa Serikali kwa ushirikiano iliyotuonyesha kufutia matukio ya hivi majuzi, na hasa kwa kupewa fursa za kukutana na viongozi na kusikilizwa.

  Tunatamka kuuelezea umma wa wapenda Amani wote tukisema, tumechoswa kuishi na kuchukuliwa kama raia wa daraja la pili katika nchi yetu. Tunaonya kuwa hatuko tayari tena kuvumilia vitendo vya uvunjaji wa amani na haki zetu na tabia za kufanywa tuishi kwa hofu.

  Kadhalika tunaiomba seriakli yetu ituhakikishie usalama wa maisha yetu, mali zetu pamoja na majengo yetu ya ibada.

  Wito wetu kwa viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini ni kuwa, kila mmoja anawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa kwa mujibu wa sheria za nchi na kwmba kila mmoja ahubiri kwa lengo la kukuza amani, utulivu na usalama wa kila mtu na mali zake.

  Mwisho, tunapenda kuhitimisha tamko letu kwa kuwaalika wakristo wote kuiombea nchi yetu amani, utulivu na mshikamano ambazo ni tunu tulizoachiwa na waasisi wetu.

  Ni imani yetu pia kwamba viongozi wetu wataendeleza wajibu wao na mamlaka waliyopewa na Mungu pasipo upendeleo wa aina yoyote.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Zanzibar.

  Kwa niaba ya Wakristo wote;

  Ni sisi Maaskofu wenu

  1. Michael Hafidh
  Askofu wa Kanisa Anglikana Zanzibar

  2. Augustine Shao
  Askofu wa Jimbo Katoliki Zanzibar

  3. Pastor Timothy W. Philemon
  Makamu Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji wa Makanisa ya Pentekoste Zanzibar


  SOURCE: Kiongozi [Toleo Na: 22 Juni 01-07,2012 (uk 2)].
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Hoja legelege,

  Kwani hamjamsikia Dr. shein, au ndo kutafuta umaarufu?
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  kwanini tuliungana kwanza,aaah
   
 4. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 837
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Amina.
   
 5. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tuko pamoja makamanda! People's Power!!!!!!!!! Mpaka kieleweke!
   
 6. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Tena ikiwa Dr. Shein keshasema basi watu wote wakae kimya, hata wewe hukupaswa kuweka post hii, au unatafuta umaarufu?
   
 7. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kama ungesoma vizuri na kuelewa tamko lilitolewa lini na Dr Shein alijibu lini ungeweza kuchangia vizuri zaidi. Au ulitaka kuchangia kwanza ndipo usome ili uelewe tamko la maaskofu lilitolewa lini? Kwa kukuelewesha Dr Shein aliongea na waandishi wa habari kuhusu kile alichokisema baada ya maaskofu kutoa tamko lao na si wao kutoa tamko baada ya Dr Shein kuongea na waandishi wa habari kuhusu vurugu za Zanzibar. Tujifunze kusoma na kuelewa kabla ya kujibu kitu chochote na siyo kujibu kwanza na kuelewa baadaye.
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Unachanganya mambo. Any itaku-cost sana kutopata vema Elimu dunia na mda wako mwingi kuutumia kwenye vyuo vya dini
   
 9. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Ni vigumu mtu yeyote kunishawishi vinginevyo kama serikali ya Zanzibar haina mkono wake kwa kupitia mlango wa nyuma kuhusiana na ghasia hizi huko Znz.

  Maana isingekuwa hivyo tusingefikia hapa yalipofikia mambo haya. Polisi waliofunzwa japo kwa kiwango cha chini tunao. Maafisa usalama tunao. Misikiti ya kuwakutanisha waumini wa kiisilamu karibia kila kona ya Znz ipo. Iweje masheikh wasilijue jambo hili mapema? Ati leo wanatoa matamko. Hawa uamsho, wanasali misikiti gani na chini ya sheikh yupi.

  Polisi na maafisa usalama je bado mnastahili kuendelea na ajira zenu baada ya kushindwa kubaini chanzo cha haya yanayotokea. Pamoja na watu wanaosema hawa waliofanya haya ni wahuni, mimi bado nakataa na kusema kuwa ni mpango kabambe wa watu "wazito" waliojificha nyuma ya pazia.
   
 10. m

  mvunjamiwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 455
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Sawa kabisa.
   
 11. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ngoja ni reserve comments zangu kwanza maana mtu unaweza kusema kitu ambacho unaweza kukijutia baadaye...
   
 12. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli usiopingika kuwa kuna baadhi ya viongozi wa serikali ya Zanzibar na vyombo vya dola Zanzibar vinashabikia vurugu hizo. Kitu cha kushangaza kwa nini usiwekwe ulinzi maalum kwenye makanisa na hasa ukizingatia kuwa mahubiri ya uamusho hivi sasa ni kuuangamiza kabisa ukristo katika Zanzibar. Mahubiri yanawahamasisha waislamu kutokuwa na ushirikiano wa namna yo yote na wakristo iwe katika sherehe za furaha au misiba!
   
 13. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  heeee hizi akili za KIMAGAMBA NA za mijitu iliyokosa akili kabisa!
   
 14. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Jamani wanaosema "waliofanya vurugu Zanzibar si wa kikundi cha uamsho na si waislamu kwani waislamu hawawezi kuiba wala kunywa pombe..." wana maana gani? Ina maana mtu akiwa Mwislamu hawezi tena kutenda mabaya kwa utashi wake? Aina hii ya "reasoning" ngeni kwangu! Je, ndivyo tunavyoona mitaani tunamosihi? Ni kama kusema vilevile Mkristo au mwumini wa dini nyingine hawezi kutenda mabaya! Conclusion ni kwamba waliofanya hivyo hawana dini yoyote! Are we fair to ourselves and other people?
   
 15. r

  ralphjn Senior Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  You are right,I think SUK is behind the scene.
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa nikiwaamini sana viongozi wa dini ya kikiristo. lkn sasa ni more propaganda. Utadhani risala hii imeandikwa na Nape (msemaji wa ccm) na sio viongozi wa dini.

  Tuache propaganda hata mambo ya dini.
   
 17. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,329
  Likes Received: 2,635
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa na hilo neno "legelege" sijui kiswahili ndio kimeishia hapo sheikh!
   
 18. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Kazi ya watu wa usalama kutaka kupatikane uharali wa wazanzibar kutozungumzia muungano ndicho kinachotafutwa hapo. It was inside job, kama kwani hayo makanisa hayajaanza kuwepo juzi hapo zenj na kama ni uamsho hawajaanza kazi hiyo juzi mbona hata siku moja hukusikia kanisa limechomwa? Fitina hiyo ambayo usalama wanaitekeleza siyo kwani hawalitakii taifa kheir.

  Hivi niambie kama polisi wasingeenda kumkamata yule Imam, wakapotezea tu juuu kwa juu kungetokea nini? lakini inaonekana kwakuwa ilikuwa ni plan wasingeweza kuuacha kutekeleza hayo. Mungu ndiye muumba na ndiye anaona yote yaliyo nyuma ya pazia. kiukweli uislam haufundishi wala hauungi mkono suala la chuki kwa asiye kuwa muislam mpaka pale huyo asiyekuwa muislam atakapogundulika kuwa adui wa dhati kwa waislam, otherwise ndio maana hata kupanga mmepanga kwenye nyumba za waislam na wala hawana tatizo na nyie.

  Pia naamini kuwa ukristo haufundishi mkristo kumchukia muislam au yeyote asiye mkristo lakini cha ajabu sana wachungaji wengi sana kwa sasa ktk ibada zao huchukua muda mwingi kuwatukana waislam wawapo ktk misa zao, na hata siku moja sijasikia serikali ikiwakataza. kama huamini nenda pale kwa gwajima kawe. Jamani haya mambo kama kweli tuko na dhati ya kuyarekebisha basi tuseme ukweli na tusitete upofu.
   
 19. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwani Shein ye ndo Mungu akiongea wengine ndo wasiongee?
   
 20. t

  thatha JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  people power haijafika zanzibar?
   
Loading...