TAMKO la UVCCM Arusha 25/5/2011 SOMA UJIONEE!

UVCCM Arusha: Lowassa, Chenge, Rostam ng`okeni
Na John Ngunge
26th May 2011

B-pepe

Chapa

Maoni
Millya adaiwa ni kibaraka

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa

Hali si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha, na lile zengwe lilioanza wiki iliyopita likimtaka Katibu wa chama mkoa, Mary Chatanda, ang’oke limejibiwa kwa nguvu miongoni mwa makundi yanayokizana huku lawama zikielekezwa kwa viongozi watatu waandamizi.

Msuguano huu unaakisi harakati za kuwania kiti cha ubunge jimbo la Arusha Mjini ambacho chama hicho kilipoteza na kuchukuliwa na Godbless Lema (Chadema), huku mgombea wa CCM, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Batilda Buriani, akiangushwa.

Jana wanachama wa Umoja wa Vijana (UVCCM), waliibuka na kutoa madai mazito juu ya uchaguzi huo, huku wakitaka mapacha watatu wenye shutuma za ufisadi ndani ya chama hicho watimuliwe haraka kukinusuru chama hicho.

Waliwataja mapacha hao kuwa ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa huo, James Ole Millya, naye ametakiwa kuachia ngazi akidaiwa kuwa ni kibaraka wa mafisadi.

Viongozi wa UVCCM ngazi ya mashina, matawi, kata na wilaya zote za mkoa wa Arusha, pamoja na wanachama wa umoja huo, jana walikutana na waandishi wa habari ambapo walitoa tamko zito kuhusu masuala makuu sita waliyodai yanakivuruga chama hicho mkoani hapa.

Hata hivyo, kikao hicho hakikuhudhuriwa na Mwenyekiti wa umoja huo Mkoa, Millya pamoja na katibu wake Abdallah Mpokwa.

Akisoma tamko hilo jana, Ali Babu, aliyejitambulisha kuwa ni Mjumbe wa Baraza la Vijana wa Wilaya ya Arusha, alisema wanaunga mkono uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kwa kuona umuhimu wa kuifanyia kazi kwa vitendo falsafa ya kujivua gamba.

“Tunaipongeza na kuiunga mkono Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwamba mafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chama chetu mbele ya umma wa Watanzania ... kwa mantiki hiyo, tunatamka kwa kauli moja kwamba mapacha hao watatu wa ufisadi ambao ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge na vibaraka wao wafukuzwe mara moja kwa maslahi ya CCM na Watanzania,” alisema.

Pia alisisitiza kuwa Chenge aondolewe kwenye Kamati ya Maadili ya CCM mara moja na wakati huo huo, Lowassa afukuzwe kwenye uenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Umoja wa Vijana wa CCM Taifa haraka iwezekanavyo.

Azimio lingine ni kutaka Millya ambaye walidai kuwa ni kibaraka mkuu wa mafisadi mkoani hapa afukuzwe ili apate muda wa kuwatumikia mafisadi.

Katika tamko hilo, vijana hao walisema wameshaandika barua yenye kumbukumbu namba ARS/Malalamiko/01 kwenda CCM Makao Makuu kuelezea namna Millya alivyo mnafiki, mfitini, mwongo na namna asivyojali maslahi ya vijana wa UVCCM mkoa wa Arusha.

Aidha, walitoa onyo kwa mbunge wa viti maalum (Vijana), Catherine Magige, wakimtaka aache kutumia fedha za mafisadi kuwagawa vijana wa Arusha kabla hawajatumia haki yao ya kikanuni ya kumsimamisha ubunge.

Vijana hao katika tamko lao, walikiomba chama chao kiwafukuze makatibu wa UVCCM kutoka wilaya za Monduli, Arumeru, Longido na Karatu kwa kushiriki maandalizi ya maandamano haramu na kwa kukataa wito wa chama wa kwenda kutoa ushahidi wa malalamiko kuhusu mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa.

Walisema kitendo hicho cha kukataa wito wa chama ni dharau na ukosefu wa maadili.

Walisema ili kulinda hadhi ya CCM mkoa wa Arusha, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Onesmo Nangole, ajiuzulu mara moja kwa madai kuwa anafanya kazi za Lowassa.

“Kitendo cha yeye kufanya kazi ya mafisadi na si CCM, kimesababisha tupoteze majimbo mawili kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2010,” tamko hilo lilisema.

Kadhalika, vijana hao katika tamko hilo walimuunga mkono Katibu wa CCM mkoani hapa, Mary Chatanda, kuwa ni mpiganaji na ni lulu ya CCM mkoa, kwa sababu amefanya mengi ya maana na wana CCM makini, wazalendo na wanaojali maslahi ya chama hicho wanatambua hilo.

Walimuunga mkono na kumtambua rasmi Mrisho Gambo kuwa ni mjumbe halali wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa kuwakilisha Mkoa wa Arusha ambaye alitangazwa kufukuzwa wadhifa wake baada ya kikao cha UVCCM kilichokaa wilayani Longido, hivi karibuni.

“Tunamuunga mkono kwa ujasiri wake, umahiri wake na uzalendo wake wa kupambana na ufisadi ndani ya chama na Tanzania kwa ujumla,” alisema.

Wakizungumza baada ya mkutano huo, Chacha Mwita Hamed, alisema anaunga mkono tamko la vijana kuhusu ufisadi.

“Vijana wametoa tamko zuri dhidi ya viongozi wao wa chama mkoa. Madai kwamba Chatanda ameuza jimbo la Arusha sio ya kweli,” alisema

Alidai kuwa Lowassa alijiingiza kwenye kampeni za Dk. Batilda Buriani jambo ambalo liliwaudhi sana wanachama na wapiga kura jimboni hapa na iwapo asingefanya hivyo huenda Buriani angeshinda.

Kwa upande wake, Odilia Abraham, alisema hawana imani na Millya na hawamtaki.

MILLYA AOMBA UCHUNGUZI

Akizungumza na NIPASHE, Millya alikanusha kuwa kibaraka wa mafisadi mkoani hapa na akasema hawezi kukumbatia mafisadi.

Aliiomba Sekretariati ya CCM Taifa kutuma kamati teule mkoani hapa kuchunguza tuhuma mbalimbali za kupoteza jimbo, lakini alisema kwa maoni yake sababu kubwa ya kupoteza jimbo ni hujuma za baadhi ya wanachama.

Kuhusu Lowassa, alisema anamheshimu na kumpenda kiongozi huyo mstaafu kwa maelezo kuwa ni mwanachama mwadilifu wa CCM mkoani hapa.

Alisema vijana waliotoa kauli hiyo hawana nguvu kwa sababu hawawakilishi vijana wa mkoa wa Arusha, isipokuwa kata chache.

Alisema vijana waliotoa tamko hilo ni wale ambao walihusika katika kulipoteza jimbo hilo wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.

Alisema anashangaa kusikia akituhumiwa kuwa ni kibaraka wa mafisadi wakati huu, na akahoji walikuwa wapi kutoa tuhuma hizo mapema.

“Inaonekana kuwa sasa hivi wameshikwa pabaya…sasa watu wazima wakishikwa sehemu mbaya unaweza kufahamu maumivu yake,” alisema.

MWENYEKITI MKOA: NI UPUUZI

Mwenyekiti CCM Mkoa wa Arusha, Nangole alisema madai yaliyotolewa na vijana wa CCM, ya kumtaka ajiuzulu kwa sababu anafanya kazi ya fisadi ni upuuzi, kwa sababu taratibu za chama haziruhusu kufanya kazi ya mtu.

“Mimi ninafanya kazi ya CCM mkoa na sio kazi ya mtu, yaani Lowassa...na pia sifanyi kazi chini ya UVCCM, hivyo hawana uwezo wa kunishinikiza nijiuzulu...kwa kifupi hizo ni siasa za chuki za Arusha,” alisema.

Hata hivyo, alisema vijana hao wote ni wake, akimaanisha wale walioandamana wiki iliyopita na hao waliotoa tamko jana, hivyo anangalia taratibu za kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo la kutoelewana kwa pande mbili hizo.

Alisema madai kwamba mkoa wake umepoteza majimbo mawili sio hoja yenye nguvu ya kumtaka ajiuzulu kwa sababu ipo mikoa mingine ambayo imepoteza majimbo matano.

Alisema anafanya kazi kwa mujibu wa taratibu za chama na hawezi kukurupuka katika utendaji wake wa kazi.

Hivi karibuni, baadhi ya vijana waliotajwa kuwa ni wa UVCCM walifanya maandamano hadi CCM Mkoa wakimtaka Chatanda ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa ajiuzulu kwa madai ya kukiangusha chama hicho katika uchaguzi mkuu uliopita.
CHANZO: NIPASHE
0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
 
Friday, 27 May 2011 00:22

Waandishi Wetu
TAMKO la baadhi ya vijana wa UVCCM, Mkoa wa Arusha kutaka mafisadi wafukuzwe, limezidi kukivuruga chama hicho baada ya Katibu Mkuu, Wilson Mukama kusema hawezi kujiingiza 'kichwa kichwa' kuzungumzia suala hilo, huku baadhi ya watuhumiwa wakikataa kulizungumzia.Akizungumza na gazeti hili jana, Mukama alisema CCM inafuatilia kwa karibu mgogoro huo, lakini haiwezi kuuzungumzia sasa kwa kuwa hajapata taarifa rasmi kutoka umoja wa vijana.

Kwa mujibu wa Mukama, UVCCM ni jumuiya halali ya chama tawala yenye mamlaka kamili ya kuzungumzia matatizo yake, hivyo yeye kusema chochote itakuwa ni kuingilia kazi za jumuiya hiyo.

“Chama chetu kina utaratibu wake, UVCCM ni jumuiya ndani yake, hayo yaliyotokea kule Arusha siwezi kuyazungumzia, ila kesho (leo) tuna kikao, hivyo wao vijana watatupa taarifa zao,” alisema Mukama, huku akisoma ujumbe mfupi wa simu (sms) alioandikiwa na katibu mkuu wa umoja huo, Martin Shigella kuwa watatoa taarifa ya yaliyotokea Arusha.

“Suala la Arusha tunalifuatilia kwa ukaribu sana, ila utendaji tunawaachia wao (UV-CCM), nasi tukishapata taarifa zao ndio tutaweza kulizungumzia suala hilo, ila kwa sasa mtafute Shigella,” alielekeza Mukama.
Alipotafutwa kwa simu jana kuzungumzia tuhuma hizo, Shigella alisema kuwa hawezi kutolea ufafanuzi kwa kuwa alikuwa nje ya nchi kikazi.

“Sikuwapo nchini, kwa hiyo sitaweza kuzungumza lolote, kuna mtu alikuwa akikaimu nafasi yangu, hivyo nikipata maelezo kutoka kwake nitakuwa tayari kuzungumza, nitafute kesho (leo),”alisema Shigella.

Beno Malisa asikitika
Naye makamu mwenyekiti wa umoja huo taifa, Benno Malisa alisema wamesikitishwa na kauli zilizotolewa na vijana wenzao wa Arusha, hivyo watatuma kamati ya maadili kwenda kuzungumza na makundi yanayolumbana.

“Hivi karibuni Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM itakaa na kutoa uamuzi, lakini ni baada ya Kamati ya Maadili itakayotumwa kuzungumza na wanachama wanaolumbana huko Arusha kuleta ripoti makao makuu ya umoja wetu,”Alisema Malisa.

Akizungumzia adhabu wanazoweza kupewa wanachama wa umoja huo, Malisa alisema adhabu hizo zitatokana na aina ya makosa watakayokutwa nayo.

“Suala hili liko ndani ya uwezo wetu na tutalifanyia kazi na kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni za UVCCM, kama kutakuwa na makosa makubwa zaidi yatapelekwa ngazi za juu zaidi,”alisema Malisa.

Juzi, UVCCM Mkoa wa Arusha waliuomba uongozi wa juu wa chama tawala kuwafukuza uanachama viongozi watatu, wakiwamo Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na mwenzake wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Vijana hao pia walikishauri chama hicho kupitia kamati yake ya maadili kuwaita na kuwahoji makada hao maarufu na baadaye kuwachukulia hatua, zikiwamo za kuwafukuza kwa maslahi ya chama na taifa.

Tamko hilo lililosomwa na mjumbe wa baraza la umoja huo mkoani Arusha, Ali Babu lilitaka watuhumiwa hao waliowaita mapacha watatu, kuwa ndio chanzo cha kudhoofika kwa chama hicho tawala.

"Pia, tunasisitiza Andrew Chenge aondolewe kwenye Kamati ya Maadili ya CCM mara moja na kumtaka mtuhumiwa mwingine (jina tunalo) aondolewe pia kwenye uongozi wa ndani ya umoja wetu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Lakini, alipotafutwa jana kuzungumzia tuhuma hizo, Chenge alijibu kwa ufupi: "Kwa sasa sitaki kuzungumzia masuala hayo. Kila la heri."

Lowassa akaa kimya
Naye Lowassa alipotafutwa alisema kwa ufupi: ‘no comment’ akimaanisha kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo.
Hata hivyo, wakati makada hao wakigoma kuzungumzia suala hilo, mwenyekiti wa umoja huo Mkoa wa Arusha, James ole Milya anayeshinikizwa kujiuzulu wadhifa huo, jana aliibuka na kudai kuwa tamko hilo lilitolewa na kundi la vijana aliowaita wahuni wa mitaani na wasiokuwa na kazi.

“Wale ni wahuni, hawana chochote wala lolote, wanapenda kukaa vijiweni hawana kazi za kufanya, tuna taarifa kwamba walitumwa na baadhi ya viongozi hapa Arusha kupindisha na kuvuruga hoja za umoja wetu mkoani Arusha,” alisema Milya

Alisema kuwa vijana hao wakiongozwa na Ali Babu hawatambuliki ndani ya umoja huo, huku akisisitiza kwamba hoja na malalamiko yote hupitishwa katika ngazi husika ili ziweze kufanyiwa kazi na sio kuibuka na kutoa matamshi yasiyo na tija.

Millya aliendeleza msimamo wake wa kutaka Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu aondoke madarakani kwa madai ya kusababisha jimbo kwenda upinzani (Chadema), huku akimtaka katibu huyo asikilize kilio chao (UVCCM) cha kumtaka aondoke.

Alisema kuwa endapo kiongozi huyo ataendelea kung'ang'ania nafasi yake, basi atang’olewa kwa maandamano ya vijana yasiyokuwa na kikomo ambayo yatafanywa na wanachama wa umoja huo.

“Msimamo wetu uko pale pale, Chatanda ni lazima aondoke kwa kuwa amekivuruga chama chetu,ametuchonganisha na viongozi wa dini, lakini pia amesababisha Jimbo la Arusha Mjini liangukie upinzani kwa kukimbilia Tanga kusaka ubunge wa viti maalumu kipindi cha uchaguzi,”alisisitzia Milya.

Juzi, katika mkutano wao wenye malengo makuu sita, vijana hao wa Mkoa wa Arusha walisema wanaunga mkono falsafa ya CCM ya kujivua gamba."Tunaipongeza na kuiunga mkono Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwamba mafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chama chetu mbele ya umma wa Watanzania," ilisema taarifa hiyo na kuongeza:

"Kwa mantiki hiyo tunatamka kwa kauli moja kwamba mapacha hao watatu wa ufisadi (wakiwataja kwa majina) na vibaraka wao wafukuzwe mara moja kwa maslahi ya CCM na Watanzania."

Source; Mwananchi
 
Chanzo Gazeti la Mwananchi.
*Send to a friend

Friday, 27 May 2011 00:22

Waandishi Wetu
TAMKO la baadhi ya vijana wa UVCCM, Mkoa wa Arusha kutaka mafisadi wafukuzwe, limezidi kukivuruga chama hicho baada ya Katibu Mkuu, Wilson Mukama kusema hawezi kujiingiza 'kichwa kichwa' kuzungumzia suala hilo, huku baadhi ya watuhumiwa wakikataa kulizungumzia.Akizungumza na gazeti hili jana, Mukama alisema CCM inafuatilia kwa karibu mgogoro huo, lakini haiwezi kuuzungumzia sasa kwa kuwa hajapata taarifa rasmi kutoka umoja wa vijana.

Kwa mujibu wa Mukama, UVCCM ni jumuiya halali ya chama tawala yenye mamlaka kamili ya kuzungumzia matatizo yake, hivyo yeye kusema chochote itakuwa ni kuingilia kazi za jumuiya hiyo.

digg

“Chama chetu kina utaratibu wake, UVCCM ni jumuiya ndani yake, hayo yaliyotokea kule Arusha siwezi kuyazungumzia, ila kesho (leo) tuna kikao, hivyo wao vijana watatupa taarifa zao,” alisema Mukama, huku akisoma ujumbe mfupi wa simu (sms) alioandikiwa na katibu mkuu wa umoja huo, Martin Shigella kuwa watatoa taarifa ya yaliyotokea Arusha.

“Suala la Arusha tunalifuatilia kwa ukaribu sana, ila utendaji tunawaachia wao (UV-CCM), nasi tukishapata taarifa zao ndio tutaweza kulizungumzia suala hilo, ila kwa sasa mtafute Shigella,” alielekeza Mukama.
Alipotafutwa kwa simu jana kuzungumzia tuhuma hizo, Shigella alisema kuwa hawezi kutolea ufafanuzi kwa kuwa alikuwa nje ya nchi kikazi.

“Sikuwapo nchini, kwa hiyo sitaweza kuzungumza lolote, kuna mtu alikuwa akikaimu nafasi yangu, hivyo nikipata maelezo kutoka kwake nitakuwa tayari kuzungumza, nitafute kesho (leo),”alisema Shigella.

Beno Malisa asikitika
Naye makamu mwenyekiti wa umoja huo taifa, Benno Malisa alisema wamesikitishwa na kauli zilizotolewa na vijana wenzao wa Arusha, hivyo watatuma kamati ya maadili kwenda kuzungumza na makundi yanayolumbana.

“Hivi karibuni Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM itakaa na kutoa uamuzi, lakini ni baada ya Kamati ya Maadili itakayotumwa kuzungumza na wanachama wanaolumbana huko Arusha kuleta ripoti makao makuu ya umoja wetu,”Alisema Malisa.

Akizungumzia adhabu wanazoweza kupewa wanachama wa umoja huo, Malisa alisema adhabu hizo zitatokana na aina ya makosa watakayokutwa nayo.

“Suala hili liko ndani ya uwezo wetu na tutalifanyia kazi na kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni za UVCCM, kama kutakuwa na makosa makubwa zaidi yatapelekwa* ngazi za juu zaidi,”alisema Malisa.

Juzi, UVCCM Mkoa wa Arusha waliuomba uongozi wa juu wa chama tawala kuwafukuza uanachama viongozi watatu, wakiwamo Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na mwenzake wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Vijana hao pia walikishauri chama hicho kupitia kamati yake ya maadili kuwaita na kuwahoji makada hao maarufu na baadaye kuwachukulia hatua, zikiwamo za kuwafukuza kwa maslahi ya chama na taifa.

Tamko hilo lililosomwa na mjumbe wa baraza la umoja huo mkoani Arusha, Ali Babu lilitaka watuhumiwa hao waliowaita mapacha watatu, kuwa ndio chanzo cha kudhoofika kwa chama hicho tawala.

"Pia, tunasisitiza Andrew Chenge aondolewe kwenye Kamati ya Maadili ya CCM mara moja na kumtaka mtuhumiwa mwingine (jina tunalo) aondolewe pia kwenye uongozi wa ndani ya umoja wetu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Lakini, alipotafutwa jana kuzungumzia tuhuma hizo, Chenge alijibu kwa ufupi: "Kwa sasa sitaki kuzungumzia masuala hayo. Kila la heri."

Lowassa akaa kimya
Naye Lowassa alipotafutwa alisema kwa ufupi: ‘no comment’ akimaanisha kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo.
Hata hivyo, wakati makada hao wakigoma kuzungumzia suala hilo, mwenyekiti wa umoja huo Mkoa wa Arusha, James ole Milya anayeshinikizwa kujiuzulu wadhifa huo, jana aliibuka na kudai kuwa tamko hilo lilitolewa na kundi la vijana aliowaita wahuni wa mitaani na wasiokuwa na kazi.

“Wale ni wahuni, hawana chochote wala lolote, wanapenda kukaa vijiweni hawana kazi za kufanya, tuna taarifa kwamba walitumwa na baadhi ya viongozi hapa Arusha kupindisha na kuvuruga hoja za umoja wetu mkoani* Arusha,” alisema Milya

Alisema kuwa vijana hao wakiongozwa na Ali Babu hawatambuliki ndani ya umoja huo, huku akisisitiza* kwamba hoja na malalamiko yote hupitishwa katika ngazi husika ili ziweze kufanyiwa kazi na sio kuibuka na kutoa matamshi yasiyo na tija.

Millya aliendeleza msimamo wake wa kutaka Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu aondoke madarakani kwa madai ya kusababisha jimbo kwenda upinzani (Chadema), huku akimtaka katibu huyo asikilize kilio chao (UVCCM) cha kumtaka aondoke.

Alisema kuwa endapo kiongozi huyo ataendelea kung'ang'ania nafasi yake, basi atang’olewa kwa maandamano ya vijana yasiyokuwa na kikomo ambayo yatafanywa na wanachama wa umoja huo.

“Msimamo wetu uko pale pale, Chatanda ni lazima aondoke kwa kuwa amekivuruga chama chetu,ametuchonganisha na viongozi wa dini, lakini pia amesababisha Jimbo la Arusha Mjini liangukie upinzani kwa kukimbilia Tanga kusaka ubunge wa viti maalumu kipindi cha uchaguzi,”alisisitzia Milya.

Juzi,* katika mkutano wao wenye malengo makuu sita, vijana hao wa Mkoa wa Arusha walisema wanaunga mkono falsafa ya CCM ya kujivua gamba."Tunaipongeza na kuiunga mkono Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwamba mafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chama chetu mbele ya umma wa Watanzania," ilisema taarifa hiyo na kuongeza:

"Kwa mantiki hiyo tunatamka kwa kauli moja kwamba mapacha hao watatu wa ufisadi (wakiwataja kwa majina) na vibaraka wao wafukuzwe mara moja kwa maslahi ya CCM na Watanzania."

Habari hii imeandaliwa na Elias Msuya, Fidelis Butahe, Dar* na Moses Mashalla, Arusha
 
Hili chama nalo kwa makelele, wananchi tunalia na hali ngumu ya maisha wao wanagombania vyeo. Endeleeni kugombania hizo nyadhifa zenu sijui mtamwongoza nani watz tumejipanga kuwatosa kisawasawa.
 
kwanza napenda kuwasahihisha m/kiti uv ccm Arusha na James Millya, James Ole Millya ni mtu mwingine kabisa ni mkuu wa wilaya Longido. Back to the topic hayo makundi yanayohasimiana yote yanatumiwa na vigogo kwa maslahi yao so ni vigumu sana kuisha ngoja tu iko siku mambo yatawekwa hadharani nani na nani ndo wanawaekea hao vijana maneno mdomoni, ila yote ni sababu ya kuganga njaa
Pukudu @Ilkiding'a, Arusha
 
Eti kauli yao ni Kulinda na Kujenga Ujamaa!! Du, sijui ni ujamaa upi wanaouzungumzia hapa. Nimecheka mpaka mbavu zinaniuma.
 
MGOGORO ndani ya Umoja wa Vijana wa CCCM (UVCCM), mkoani Arusha umevuta kasi baada ya baadhi ya vijana wa umoja huo kutishia kufunga ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa, Mary Chatanda ili kushinikiza uondoke madarakani.

Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kwamba vijana hao walipanga kufunga ofisi hiyo jana, lakini baadaye walibadili uamuzi na kukubaliana kutekeleza azima hiyo wakati katibu huyo wa CCM akiwa bungeni mwezi ujao.

Mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya UVCCM, Ally Bananga alisema jana kuwa msimamo wa vijana ni kutolala mpaka Chatanda aondoke madarakani.

Kauli hiyo ya Bananga, imekuja siku moja baada ya Makamu Mwenyekiti wa moja huo, ngazi ya Taifa, Beno Malisa kudai kuwa anasikitishwa na kauli zilizotolewa na vijana wenzao mkoani Arusha.

Malisa alisema kutokana na hali hiyo atatuma kamati ya maadili ambayo itakutana na makundi yanayolumbana mkoani Arusha.

Bananga alisema ana unga mkono kamati hiyo ya maadili kwenda mkoani Arusha kuzungumza na makundi yote na aliitahadhirisha kamati hiyo kwamba suala la Chatanda kung ‘oka ni lazima.

“Sisi tuko tayari kuipa ushirikiano kamati hiyo ya maadili, lakini suala la Chatanda kuondoka Arusha liko pale pale tunaomba kuiambia tume hiyo kabla haijawasili kabisa,”alisema Bananga.

Alisema endapo kamati hiyo itaonekana kupendelea ili katibu huyo aendelee kushikilia nafasi yake ya ukatibu wa CCM mkoani hapa, kamwe hali ya hewa haitatulia na kwamba Chatanda atangolewa kwa gharama yoyote.

“Sikiliza endapo Chatanda asipong’ooka tutapambana mpaka kieleweke, hapa ni aluta continua na tunaitaka tume isimpendelee Chatanda kwani sisi tumebaini huyu mama hatufai,”alisema Bananga.

Alisisitiza kwamba vurugu za makundi ndani ya CCM zinazoendelea mkoani Arusha zinapoteza mvuto wa chama hicho.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha, James Ole Milya alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu madai ya vijana hao kwamba watafunga kwa makufuli ofisi katibu huyo alisema alipata taarifa hizo huku akisisitiza kwamba endapo kilio cha vijana hao hakitasikilizwa huenda wakaamua kutekeleza azma hiyo.

Alisisitiza kwamba ili hali ya hewa iweze kurejea ndani ya chama tawala mkoani hapa ni lazima Chantanda ang’ooke kwa madai kwamba amekuwa akikivuruga chama hicho tawala, kusababisha jimbo kuangukia upinzani sanjari na kuwachonganisha na viongozi wa dini mkoani Arusha.

Wakati vita ya kisiasa ikiendelea kwa kasi ndani ya UVCCM, mkoani Arusha, aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ally Bananga ameibuka na kutamka kwamba umoja wao uko tayari kuipa ushirikiano kamati ya maadili itakayowasili mkoani hapa kuzungumza na makundi yanayolumbana.

Alisema kamati hiyo lazima iwatambue kwamba Chatanda lazima andoke mkoani Arusha.

Source: Mwananchi Saturday 28 May 2011
 
Hivi CCM watapata hasara gani wakimwondoa Chitanda Arusha? Au tuseme ndio mnara wa Babeli umeshika kasi?
 
Endeleeni kulumbana tu,ugomvi ukiisha tayari mmeisha poteza wanachama kibao watakao amua kwenda Chadema kwani siku zote vita vya panzi furaha kwa kunguru.
 
Hao vijana si wanaCCM bali ni wafuasi wa CDM, P'se CDM msiivuruge CCM yetu, mungu ibariki CCM mungu mbariki Chatanda, japo aliwatukana watumishi wa mungu
 
Hao vijana si wanaCCM bali ni wafuasi wa CDM, P'se CDM msiivuruge CCM yetu, mungu ibariki CCM mungu mbariki Chatanda, japo aliwatukana watumishi wa mungu

Kama ni wafuasi wa CDM mbona wanaingia kwenye vikao vyenu halali na mnawalipa posho kama wajumbe halali?. Uwe unapiga mswaki unapoamka sio unakurupuka tu na kuanza ku comment thread za humu Jamvini!
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Kama ni wafuasi wa CDM mbona wanaingia kwenye vikao vyenu halali na mnawalipa posho kama wajumbe halali?. Uwe unapiga mswaki unapoamka sio unakurupuka tu na kuanza ku comment thread za humu Jamvini!

Wanatapatapa hao, gamba limewakwama shingoni, hawaoni na wanakaribia kukosa pumzi!
 
Hivi CCM watapata hasara gani wakimwondoa Chitanda Arusha? Au tuseme ndio mnara wa Babeli umeshika kasi?

kwa hili nalazimika kusema CCM taifa ni wapumbavu.... wanamng'ang'ania mtu simply because yuko kwenye mtanao fulani, wamesahau kabisa maslahi ya chama, wamesahahu kabisa ustawi wao, wamekomaliana wenyewe na makucha yao

acha wafu wazikane wenyewe
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom