TAMKO la UVCCM Arusha 25/5/2011 SOMA UJIONEE! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAMKO la UVCCM Arusha 25/5/2011 SOMA UJIONEE!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sitakuwafisadi, May 25, 2011.

 1. s

  sitakuwafisadi Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TAMKO LA VIJANA WA CCM MKOA WA ARUSHA
  Tarehe 25/05/2011

  Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumeona tuwaite hapa ili tuweze kutoa maoni yetu kuhusiana na mustakabali wa chama chetu cha Mapinduzi na Jumuiya yetu ya Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha.

  Tumewaita hapa kwa malengo makuu Sita:-

  1.
  Kuunga mkono Halimashauri kuu ya CCM Taifa kwa kuona umuhimu wa kuifanyia kazi kwa vitendo falsafa ya kujivua gamba. Tunaipongeza na kuiunga mkono Halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwamba mafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chama chetu mbele ya umma wa watanzania. Kwa mantiki hiyo tunatamka kwa kauli moja kwamba mapacha hao watatu wa kifisadi ambao ni Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge na vibaraka wao wafukuzwe mara moja kwa maslahi ya CCM na Watanzania. Pia tunasisitiza kuwa Andrew Chenge aondolewe kwenye kamati ya maadili ya CCM mara moja na wakati huohuo Edward afukuzwe kwenye kwenye ya uwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya umoja wa vijana wa CCM Taifa haraka iwezekanavyo.

  2.
  Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunamtaka kuwa James Millya ambaye ni kibaraka mkuu wa mafisadi mkoa wa Arusha ajiuzulu mara moja na tunatamka rasmi kumfukuza kwenye UVCCM mkoa wa Arusha ili apate fursa ya kwenda kuwa tumikia mafisadi. Tunamtaka James Millya aache kufikiria kwa kutumia tumbo na badala yake atumie kichwa. Pia tumeshaandika barua yenye kumbukumbu namba kumb. Ars/Malalamiko/01 kwenye Chama kuelezea namna alivyo mnafiki, mfitini,mwongo na namna asivyo jali maslahi ya vijana wa UVCCM mkoa wa Arusha. Vilevile tunapenda kuujulisha umma wa Tanzania kuwa Ally Bananga anaetumiwa na Millya pamoja na mafisadi hana nafasi yoyote ndani ya Umoja wa vijana wa CCM kuanzia kwenye tawi hadi Taifa. Kwa mantiki hiyo Ally Bananga aache mara moja kuganga njaa kwa kutumia jina la UVCCM. Pia tunampa onyo kali Catherine Magige aache mara moja kutumia fedha za mafisadi kuwagawa vijana wa Arusha kabla hatujatumia haki yetu ya kikanuni ya kumsimamisha Ubunge. Tunajua kuwa amepata ubunge kwa nguvu za kifisadi kupitia UVCCM.

  3.
  Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunakiomba chama cha cha mapinduzi kiwafukuze mara moja makatibu wa UVCCM kutoka wilaya za Monduli, Arumeru, Longido na Karatu kwa kushiriki mandalizi ya maandamo haramu na kwa kukataa wito wa chama wa kwenda kutoa ushahidi wa malamiko yao kuhusu mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa. Kitendo hicho cha kukataa wito wa Chama ni dharau na ukosefu wa maadili.

  4.
  Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka kwamba ili kulinda hadhi ya CCM mkoa wa Arusha tunamtaka Onesmo Nangole ajiuzulu mara moja kwa kuwa anafanya kazi ya Fisadi Edward Lowasa na si ya CCM. Kitendo chake yeye cha kufanya kazi ya mafisadi na si ya CCM kimetupelekea kupoteza majimbo mawili kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.

  5.
  Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka kwamba Mhe. Mary Chatanda (MB) ambaye ni katibu wa CCM Mkoa wa Arusha ni mpiganaji na ni lulu ya CCM mkoa wa Arusha. Amefanya mengi ya maana na wa-CCM makini, wazalendo na wanaojali maslahi ya chama chetu wanatambua hilo. Pia tunawaomba CCM Taifa waendelee kumwacha hapa Arusha ili aendelee kukijenga chama na kukomesha mafisadi pamoja na dagaa wao.

  6.
  Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka rasmi kumtambua Ndugu. Mrisho Gambo kuwa ni mjumbe halali wa baraza kuu la UVCCM Taifa kuwakilisha mkoa wa Arusha. Tunamuunga mkono kwa ujasiri wake, umahiri wake na uzalendo wake wa kupambana na ufisadi ndani ya chama na Tanzania kwa ujumla. Na huo ndiyo msimamo wetu kwa kuwa una tija kwa vijana wa Tanzania. Tunashauri CCM Taifa kuwaita rasmi mapacha watatu wa kifisadi (Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge) kwenye kamati ya maadili ya CCM Taifa na kisha kuwafukuza mara moja kama kweli tuna nia ya kuendelea kuwa chama tawala katika nchi hii.

  TUTASEMA KWELI DAIMA FITINA KWETU MWIKO
  KAULI YETU: KULINDA NA KUJENGA UJAMAA
  KITADUMU CHAMA CHAMAPINDUZI BILA MAFISADI
   

  Attached Files:

 2. V

  Vumbi Senior Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kweli mwaka huu tutaona mengi.Hivi CCM kila mtu au juimuia ina haki ya kujisemea jinsi inavyo jisikia? hakuna utaratibu wa kutoa matamko? kweli CCM imefilisika.
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  [​IMG][​IMG]
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  wamefikisha ujumbe walio ambiwa waufikishe na CCM Taifa,kwa wale msio juwa system ya chama inavyofanya kazi hivyo ndivyo,Vijana wamepewa bomu wajilipue na wamejilipuwa
  mwisho wana kuambia TUTASEMA KWELI DAIMA FITINA KWAO NI MWIKO

  UJUMBE HUO UMEFIKA KWA WAHUSIKA
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  haya mechi jumamosi Man U na Barc
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hawa nao eti ni kina huko kwenye CCM ? Nimesoma tamko lao kweli wanapoteza muda hawa
   
 9. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Well done UVCCM Arusha nawaomba BAVICHA waige mavitu adimu ya UVCCM sote twajenga TZ
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Cheap fake.
   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,589
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Hii nadhani itakuwa UVCMM- CHITANDA!!!!!

  Nape upoooooooo!!!!!!!!
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama kweli ccm ni kidume kama wanavyotaka tuamini kwa nini wasiwaite hao waliowabatiza MAPACHA na kuwatimua kimoja? kwa nini wanawatumia watoto kutangaza mambo ambayo kiungozi ni wao (viongozi wa juu ccm) wanatakiwa watoe? Why beat around the bush?

  Hivi si waliutangazia umma kuwa barua zinaandikwa? Sasa hizi kelele za hawa watoto zinatoka wapi au ndio AINA ya barua za ccm? Nijuavyo mimi na kwa context ya siasa za Tanzania fisadi ni mtu aliyeibia umma kwa kiwango cha juu sana (grand corruption) sasa kama ndivyo hawa vijana wanashauri mafisadi waondelewe kwenye kamati na sio ubunge, au uenyekiti wa kamati ya bunge!!! Maana yake mapacha hawa hawafai kuwa kwenye safu ya uongozi ndani ya ccm lakini wanafaa kuongoza umma?!! Haya si madharau kwa watanzania? Na fisadi si anatakiwa aende KEKO au?

  Kwa upande mwingine, nawasihi Lowasa, Chenge na Rostamu Azizi waende mahakamani ili hawa vijana walete ushahidi wao huko? Msipofanya hivyo basi watanzania tutaamini kuwa kweli ninyi ni mafisadi. Na kwa sheria mtuhumiwa is innocent until he/she is proven gulty. Vile vile mkiondoka ccm tutaamini kuwa ninyi ni mafisadi. Are you?
   
 13. h

  hans79 JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  bavicha waige upuuzi we vipi?hatungozwi na nyie vimeo nenden kuzimu barua za mapenz za nn?bure kabisa afadhal pofu
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  aiseee
   
 15. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  UVCCM are fighting a lonely battle. Hawawezi kushinda vita ya mapacha watatu. Mapacha watatu are well organized and focused katika mambo yao. Kama katibu mkuu wa CCM anawagwaya na kusema mambo tofauti na ya mwenzake Nnape, hao vijana wanategemea nini? Pengine hiyo vita hawaifahamu vizuri.
   
 16. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  mbona kama kijifeki tu?!
   
 17. mwakichi

  mwakichi JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2011
  Joined: May 14, 2011
  Messages: 420
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  na bado JK
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mbona hii ipo kama fake! Hawana headed paper!? official stationery jamani vipi hili?
   
 19. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa, tamthilia ya makundi bado inaendelea! Chitanda amebuni namna ya kutoka kivingine!
   
 20. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kama ndio wameamua kuuana itakuwa burudani.
  Ila kama ndio uandishi wao wa mambo ya kiofisi uko hivyo,CCM hakuna anayejua kuandika.
   
Loading...