TAMKO la UVCCM Arusha 25/5/2011 SOMA UJIONEE!

Haya hayana budi kutokea ili kuijenga nchi na demokrasia imara. Hongereni UVCCM. kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi''.
 
Tunashauri CCM Taifa kuwaita rasmi mapacha watatu wa kifisadi (Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge) kwenye kamati ya maadili ya CCM Taifa na kisha kuwafukuza mara moja kama kweli tuna nia ya kuendelea kuwa chama tawala katika nchi hii
.
:dance:
 
Yule FaizaFoxy sijui yuko wapi......twamtaka tuhangaike nae hapa kwenye hili:pound::pound::pound:
 
Dhambi ya ubaguzi mkishakuitenda haifi, itaendelea tu ni sawasawa na kula nyama ya mtu... J. K. Nyerere
 
Duh! hawa ndio viongozi wa CCM ya kesho? kwani mwenyekiti wa CCM Taifa yupo au hayupo, kwanini wasifunkuzwe watu tukajua kweli imeamua kujisafisha?
 
jambo usilolijua sawa na usiku wa giza.......ushabuki wa wote nyie ni kwasababu mpo side b ya chama tawala.....tamko limetulia...kidumu chama tawala...viva uvccm arusha
 
TAMKO LA VIJANA WA CCM MKOA WA ARUSHA
Tarehe 25/05/2011

Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumeona tuwaite hapa ili tuweze kutoa maoni yetu kuhusiana na mustakabali wa chama chetu cha Mapinduzi na Jumuiya yetu ya Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha.

Tumewaita hapa kwa malengo makuu Sita:-

1.
Kuunga mkono Halimashauri kuu ya CCM Taifa kwa kuona umuhimu wa kuifanyia kazi kwa vitendo falsafa ya kujivua gamba. Tunaipongeza na kuiunga mkono Halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwamba mafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chama chetu mbele ya umma wa watanzania. Kwa mantiki hiyo tunatamka kwa kauli moja kwamba mapacha hao watatu wa kifisadi ambao ni Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge na vibaraka wao wafukuzwe mara moja kwa maslahi ya CCM na Watanzania. Pia tunasisitiza kuwa Andrew Chenge aondolewe kwenye kamati ya maadili ya CCM mara moja na wakati huohuo Edward afukuzwe kwenye kwenye ya uwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya umoja wa vijana wa CCM Taifa haraka iwezekanavyo.

2.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunamtaka kuwa James Millya ambaye ni kibaraka mkuu wa mafisadi mkoa wa Arusha ajiuzulu mara moja na tunatamka rasmi kumfukuza kwenye UVCCM mkoa wa Arusha ili apate fursa ya kwenda kuwa tumikia mafisadi. Tunamtaka James Millya aache kufikiria kwa kutumia tumbo na badala yake atumie kichwa. Pia tumeshaandika barua yenye kumbukumbu namba kumb. Ars/Malalamiko/01 kwenye Chama kuelezea namna alivyo mnafiki, mfitini,mwongo na namna asivyo jali maslahi ya vijana wa UVCCM mkoa wa Arusha. Vilevile tunapenda kuujulisha umma wa Tanzania kuwa Ally Bananga anaetumiwa na Millya pamoja na mafisadi hana nafasi yoyote ndani ya Umoja wa vijana wa CCM kuanzia kwenye tawi hadi Taifa. Kwa mantiki hiyo Ally Bananga aache mara moja kuganga njaa kwa kutumia jina la UVCCM. Pia tunampa onyo kali Catherine Magige aache mara moja kutumia fedha za mafisadi kuwagawa vijana wa Arusha kabla hatujatumia haki yetu ya kikanuni ya kumsimamisha Ubunge. Tunajua kuwa amepata ubunge kwa nguvu za kifisadi kupitia UVCCM.

3.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunakiomba chama cha cha mapinduzi kiwafukuze mara moja makatibu wa UVCCM kutoka wilaya za Monduli, Arumeru, Longido na Karatu kwa kushiriki mandalizi ya maandamo haramu na kwa kukataa wito wa chama wa kwenda kutoa ushahidi wa malamiko yao kuhusu mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa. Kitendo hicho cha kukataa wito wa Chama ni dharau na ukosefu wa maadili.

4.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka kwamba ili kulinda hadhi ya CCM mkoa wa Arusha tunamtaka Onesmo Nangole ajiuzulu mara moja kwa kuwa anafanya kazi ya Fisadi Edward Lowasa na si ya CCM. Kitendo chake yeye cha kufanya kazi ya mafisadi na si ya CCM kimetupelekea kupoteza majimbo mawili kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.

5.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka kwamba Mhe. Mary Chatanda (MB) ambaye ni katibu wa CCM Mkoa wa Arusha ni mpiganaji na ni lulu ya CCM mkoa wa Arusha. Amefanya mengi ya maana na wa-CCM makini, wazalendo na wanaojali maslahi ya chama chetu wanatambua hilo. Pia tunawaomba CCM Taifa waendelee kumwacha hapa Arusha ili aendelee kukijenga chama na kukomesha mafisadi pamoja na dagaa wao.

6.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka rasmi kumtambua Ndugu. Mrisho Gambo kuwa ni mjumbe halali wa baraza kuu la UVCCM Taifa kuwakilisha mkoa wa Arusha. Tunamuunga mkono kwa ujasiri wake, umahiri wake na uzalendo wake wa kupambana na ufisadi ndani ya chama na Tanzania kwa ujumla. Na huo ndiyo msimamo wetu kwa kuwa una tija kwa vijana wa Tanzania. Tunashauri CCM Taifa kuwaita rasmi mapacha watatu wa kifisadi (Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge) kwenye kamati ya maadili ya CCM Taifa na kisha kuwafukuza mara moja kama kweli tuna nia ya kuendelea kuwa chama tawala katika nchi hii.

TUTASEMA KWELI DAIMA FITINA KWETU MWIKO
KAULI YETU: KULINDA NA KUJENGA UJAMAA
KITADUMU CHAMA CHAMAPINDUZI BILA MAFISADI
Yalaaaaaaaaaaaah, full burani mwaka huu. Uiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Hizi sarakasi za UV CCM Arusha ni matokeo ya unafiki na siasa chafu zilizokithiri. Hii vita mliyoianzisha Ally Babu na wenzako though inaweza ikawa ina nia nzuri haitafanikiwa kwa sababu zifuatazo:-
1. Hiyo kambi mnayopigana nayo ina stratergy kubwa na haikurupuki ka nyie mnavyofanya kwa sasa nyie mmechelewa saana, kumbukeni hawa jamaa walijipanga muda mrefu saana na kwa njaa zenu pia mlishiriki kumbuka uongozi wa UV-CCM katika wilaya za Longido, Karatu, Monduli, Arumeru, na Ngorongoro ni product ya hawa mafisadi walihakikisha wanashinda uchaguzi na wakashinda baadhi yao wamepewa scolarship na wengine wamesaidiwa hata gharama za arusi, kwa hiyo mjue kwa hilo mnalopinga kwa nguvu zote ni wa wilaya ya Arusha kwa hiyo tayari nyie mko out numbered, na sio tu uongozi wa Vijana pia viongozi wengine wengi tu wa CCM Arusha ni vibaraka wao refer kwenye sarakasi za uchaguzi wa uongozi CCM jinsi mzee Elisa Mollel na Lekule Laizer walivyofanywa simply because hawaelewani na EL. Na bbadhi yenu mlishiriki nawashangaa sana leo eti mnageuka unafiki wa hali ya juu.
2. Ally Babu na wenzenu mnatumika tu na mtaachwa baadae suala la Mrisho Gambo kusimamishwa ktk mkutano wa Longido ambao maamuzi yalipitishwa Impala ktk kikao kilichosimamiwa na mtoto wa EL na nyie mlikuwepo na mlibugi kumpa barua kabla hata kikao hakijakaa. Na sasa tunajua nani yuko nyuma yenu si bure kwanza Ally Babu and etal na vijana wengi ni wa hapo kata ya kati na tunajua Riz1 anawapump, though kuna tetesi ambazo hazithibitishwa kuwa na Mrisho Gambo anatumika na kina Elisa Mollel na wenzake kulipiza kisasi. Siasa gani mnafanya machalii zangu? acheni hiyo mambo mnapingana sababu tu mnawekewa maneno mdomono na baadhi ya watu? hebu acheni hiyo mambo ur better than that.
Suala lingine ambalo lina liuzungumkuti ni hili la James Millya, Jamani leo mnakimbia kivuli chenu kwani mmejua Jemuuu anatumika na mafisadi leo? acheni unafiki. James tuliwambia habari zake tangia wakati wa uchaguzi tuliomfahamu tulisema tukawapa habari zake jinsi alivyoshinda urais wa serikali ya Wanafunzi (TUSO- IUCO) Tumaini Iringa na jinsi alivyoshinda uenyekiti TAHLISO na jinsi alivyoshindwa kuperfom hadi yakataka kutokea mapinduzi ambayo aliyasuppress kwa nguvu ya pesa, hamkutusikia mkaanza kutuona wanafiki na ka tunawazibia kula, ndo maana tulikaa pembeni na mwishowe tulihama chama, mlituona maduwanzi kukimbia ''hela za boya'' ka zilivyokuwa zinaitwa sasa nani kawa boya? Hiyo hamkuona ikaja ile kesi ya uzushi kati ya Millya na Ole Sendeka na jinsi Millya alivyokuwa anatumika na EL hadi akawa anakimbia upatinishi wa wazee wa ukoo dhidi ya Ole Sendeka ambaye ni ndugu wa mama yake, hilo pia hamkuliona kwenye kura ya maoni jinsi jamaa alivyokuwa anacheza rafu dhidi ya Ole Sendeka nako hamkujua kuwa anatumiwa na mafisadi? Kweli? je mlikuwa hamuoni au mliamua kutokuona? wenye akili tunajiuliza why now? Ni kwanini sasa ndo mmeoona Milya a.k.a Jemuuu anatumika au kwa sababu na nyie sasa mna Buster nyingine inayowapa nguvu yule kijana wa mjini mjini.
MNACHOKIFANYA KINAWEZA KIKAWA KIZURI KABISA ILA JE NI KWA NIA IPI? NI KWELI MNATAKA KUSAFISHA AU KUFANIKISHA MASLAHI YA WATU? COZ NAJUA UKWELI MLIKUWA MNAUJUA LONG TIME KINYAMA, HAIWEZEKANI KUPINGA UBAYA KWA NJIA YA FITINA HAMTAFANIKIWA MUWE OPEN KABISA NA MSEME YOTE. SUALA LA CHATANDA TENA LIMEN AMAZE TENA KIDOGO SIO NYIE KIPINDI KILE BAADA YA UCHAGUZI PAMOJA NA KINA RAMA(raha promotions) MLIKUWA MSTARI WA MBELE MKITAKA CHATANDA NA MZEE KILEO WAWAJIBISHWE KWA KUSHINDWA KUMSAIDIA DR.Buriani. NAWAMBIA TENA VIJANA WENZANGU HUYO ANAEWAPUMP HAWASAIDII ANAWATUMIA TU. ACHANENI NAE FANYENI MBISHE ZENU TUSOGEZE MBELE GURUDUMU LA MAENDELEO

Pukudu @Ilkiding'a, Arusha
 
tamko la vijana wa ccm mkoa wa arusha
tarehe 25/05/2011

ndugu zangu waandishi wa habari leo tumeona tuwaite hapa ili tuweze kutoa maoni yetu kuhusiana na mustakabali wa chama chetu cha mapinduzi na jumuiya yetu ya umoja wa vijana wa ccm mkoa wa arusha.


6.
sisi vijana wa ccm kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa arusha tunatamka rasmi kumtambua ndugu. Mrisho gambo kuwa ni mjumbe halali wa baraza kuu la uvccm taifa kuwakilisha mkoa wa arusha. Tunamuunga mkono kwa ujasiri wake, umahiri wake na uzalendo wake wa kupambana na ufisadi ndani ya chama na tanzania kwa ujumla. Na huo ndiyo msimamo wetu kwa kuwa una tija kwa vijana wa tanzania. Tunashauri ccm taifa kuwaita rasmi mapacha watatu wa kifisadi (edward lowasa, rostam azizi na andrew chenge) kwenye kamati ya maadili ya ccm taifa na kisha kuwafukuza mara moja kama kweli tuna nia ya kuendelea kuwa chama tawala katika nchi hii.

tutasema kweli daima fitina kwetu mwiko
kauli yetu: Kulinda na kujenga ujamaa
kitadumu chama chamapinduzi bila mafisadi
naamini chama kama kawaida yake kitakaa kimya tena juu ya hii hoja-
 
Huyu mrisho Gambo ni nani? Hili ni gamba lenye ngozi ya kenge huyu jamaa alikua anapiga mbonji kwenye vibanda vya watu hadi alipoachiwa nyumba na mwanamke mmoja inasemekana alikua hawara yake (shemzigo) tangu hapo akaanza kuishi hapo leo hii anajiona wamaana anakaa manispaa arusha anamtukana kamanda wetu lema matusi yanguoni akidai nitapeli sasa wana jf huyu anatuhuma zakuwasaliti wenzake {magamba wenzake} nahapohapo anataka kukubalika magambani akiwa nahuyo gamba kubwa chatanda aliyesababisha damu zawanamapinduzi wetu zimwagike Arusha. jana kapost taarifa yakinafiki wana jf peoples powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr hatumuhitaji yeye nigamba anashindana na usingizi hiyo tabia yako ya unafki nihatari kuliko hao unaowaita mafisadi usicheze na nguvu ya umma wewe nikibaraka wa RIZ1 .huwezi kujifananisha na kamanda lema mtetezi wawanyonge unafiki hukohuko magambani
 
Hiyo ni dalili ya mafua na bila shaka HOMA haiko mbali "KUVUJA KWA PAKACHA NAFUU KWA MCHUKUZI",bado 2tatwanga kotekote! NI WAKATI WA UKOMBOZI NA KAMA SI SASA BASI NI KESHO.
 
Huyu mrisho Gambo ni nani? Hili ni gamba lenye ngozi ya kenge huyu jamaa alikua anapiga mbonji kwenye vibanda vya watu hadi alipoachiwa kijichumba akalipiwa kodi yamwaka mmoja na mwanamke mmoja inasemekana alikua hawara yake (shemzigo) tangu hapo akaanza kuishi hapo leo hii anajiona wamaana anakaa manispaa arusha anamtukana kamanda wetu lema matusi yanguoni akidai nitapeli sasa wana jf huyu anatuhuma zakuwasaliti wenzake {magamba wenzake} nahapohapo anataka kukubalika magambani akiwa nahuyo gamba kubwa chatanda aliyesababisha damu zawanamapinduzi wetu zimwagike Arusha. jana kapost taarifa yakinafiki wana jf peoples powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr hatumuhitaji yeye nigamba anashindana na usingizi hiyo tabia yako ya unafki nihatari kuliko hao unaowaita mafisadi usicheze na nguvu ya umma wewe nikibaraka wa RIZ1 .huwezi kujifananisha na kamanda lema mtetezi wawanyonge unafiki hukohuko magambani
 
Huyu mrisho Gambo ni nani? Hili ni gamba lenye ngozi ya kenge huyu jamaa alikua anapiga mbonji kwenye vibanda vya watu hadi alipoachiwa nyumba na mwanamke mmoja inasemekana alikua hawara yake (shemzigo) tangu hapo akaanza kuishi hapo leo hii anajiona wamaana anakaa manispaa arusha anamtukana kamanda wetu lema matusi yanguoni akidai nitapeli sasa wana jf huyu anatuhuma zakuwasaliti wenzake {magamba wenzake} nahapohapo anataka kukubalika magambani akiwa nahuyo gamba kubwa chatanda aliyesababisha damu zawanamapinduzi wetu zimwagike Arusha. jana kapost taarifa yakinafiki wana jf peoples powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr hatumuhitaji yeye nigamba anashindana na usingizi hiyo tabia yako ya unafki nihatari kuliko hao unaowaita mafisadi usicheze na nguvu ya umma wewe nikibaraka wa RIZ1 .huwezi kujifananisha na kamanda lema mtetezi wawanyonge unafiki hukohuko magambani
Tafadhali usihusishe vurugu zenu huko UVCCM na kamanda Lema nyie mvurugane kivyenu.
 
CCM now is like a house with a dark heavy smoke rising to the sky,hope you know what that means!!CCM will soon burn and we will fail even to gather the ashes!!
 
Hivi jamani mpaka watoto hawa wanakuwa na uwezo wa kutaja majina ya mapacha watatu,wakati mwenyekiti wa CCM kakaa tu kimya na ameshindwa kuchukua hatua za maana zaidi ya kufumbia macho kweli hii ni aibu kwa chama na serikali
 
Back
Top Bottom