TAMKO la UVCCM Arusha 25/5/2011 SOMA UJIONEE!

Hii nadhani itakuwa UVCMM- CHITANDA!!!!!

Nape upoooooooo!!!!!!!!

Hii ni Chatanda original, Ni habari za nani tutakazoziamini?
VITA VYA PANZI HIVYO KWA HIYO CHADEMA KAENI MKAO WA KUWADAKA NA KUWAKAANGA TUPATE MLO BILA KUTUMIA NGUVU!!!!!

CCM Arusha CDM iliwakata vichwa sasa jimalizieni kwa kukatana miguu. Naomba hii vita ipambe moto hadi 2016
 
vijana wameanza kumuumbua CHATANDA teteteh magamba hayo damu za umma zilimwagika bure Arusha sasa zinamrudia chatanda...................wana jf kwahabari zakuaminika chatanda kaonekana jioni hii akiwa na gamba nape nakahakikishiwa nagamba nape kesho lazima aongee na press so msishangae kesho kumuona gamba nape akiongea hana jipya.... nimipango yake yajioni hii nachatanda....sasa je yule meya wao wakichina anahali gani kama vijana wamemkataa aliyekua anamkingia kifua,.... cdm tukiitisha uchaguzi wa meya Arusha vijana wamagambani watakua wakwanza kumkubali meya wetu nahuyu Riz1 katokea wapi Arusha? wana jf nikweli kafungua kampuni yakukodi magari Arusha heeee mwenzetu anamijihelaaaaaaaaaaa nakampa usimamizi mwenyekiti wa UVCCM ARUSHA MJINI(mwalusamba) chanzo cha habari kimedai tumbo jamani tumbo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! yeye ninani akajiingize mambo ya Arusha?? jamani hawa magamba wache waendelee tusubiri 2015..peoplesssssssssssssssssssssspower
 
Ukiangalia lengo 5 & 6.
Huulizi ni nani au ni kwanini waraka huu umeandikwa.
Ni ukweli kwa usemi usemao, mfa maji .......
 
Kama wao wanatumiwa na mapacha watatu...na nyie mnatumiwa na nani? kweli mfa maji haachi..............pa! cheap and insane politics. Wote nyie lenu moja period!
 
UVCCM a.k.a MAVUVUZELA njaa zitawaua mjini mnakubalije kutumiwa hovyohovyo wa*h*n*i nyie! @&¥§%*
 
Sidhani kama kuna mwanachama serious kabisa anayeweza kuwanyoshea vidole akina chenge, rostam na edwar! Thubutu!
 
Kikwete, Je unaona raha ya makundi? Uliyatengeneza, ukawaumiza wapinzani wako ndani ya CCM ili upate Urais, Ulipopata Urais ukanzisha kundi lingine kupitia Richmond, Hatimae umeanzisha Mapacha watatu (RA, AC, EL). Kabla hamjakaa vizuri, CDM wakawazalia mapacha wengine watatu (Six, Mwakyembe, Nape).

Sijui utatashughulikia lipi na uache lipi!!
Huku moto kule moto!!
Utatutumikia saa ngapi Tuliokuweka madarakani?
Je,kwa Staili hii utafika 2015?
 
vijana wameanza kumuumbua CHATANDA teteteh magamba hayo damu za umma zilimwagika bure Arusha sasa zinamrudia chatanda...................wana jf kwahabari zakuaminika chatanda kaonekana jioni hii akiwa na gamba nape nakahakikishiwa nagamba nape kesho lazima aongee na press so msishangae kesho kumuona gamba nape akiongea hana jipya.... nimipango yake yajioni hii nachatanda....sasa je yule meya wao wakichina anahali gani kama vijana wamemkataa aliyekua anamkingia kifua,.... cdm tukiitisha uchaguzi wa meya Arusha vijana wamagambani watakua wakwanza kumkubali meya wetu nahuyu Riz1 katokea wapi Arusha? wana jf nikweli kafungua kampuni yakukodi magari Arusha heeee mwenzetu anamijihelaaaaaaaaaaa nakampa usimamizi mwenyekiti wa UVCCM ARUSHA MJINI(mwalusamba) chanzo cha habari kimedai tumbo jamani tumbo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! yeye ninani akajiingize mambo ya Arusha?? jamani hawa magamba wache waendelee tusubiri 2015..peoplesssssssssssssssssssssspower

Kama ni kweli na kesho akipanda meza moja na KITANDA basi NAPE kwishneeeeeeee atakuwa NEPI.
 
kweli mwaka huu tutaona mengi.Hivi CCM kila mtu au juimuia ina haki ya kujisemea jinsi inavyo jisikia? hakuna utaratibu wa kutoa matamko? kweli CCM imefilisika.

Afu angalia maudhui ya lugha waliyotumia! Lol...KIBOKO!!!!!!!...Tehe tehe tehe tehe tehe tehe
 
haaaah haaah haaaah magamba bwana duh haaaah kweli huku ni kufulia jaman yani chama shaghalabaghala kila mtu anatoa tu tamko kwa jinsi atakavyo yeye! Damu za wazalendo zitakuwa juu yenu milele! Malizaneni tu!
 
Kikwete, Je unaona raha ya makundi? Uliyatengeneza, ukawaumiza wapinzani wako ndani ya CCM ili upate Urais, Ulipopata Urais ukanzisha kundi lingine kupitia Richmond, Hatimae umeanzisha Mapacha watatu (RA, AC, EL). Kabla hamjakaa vizuri, CDM wakawazalia mapacha wengine watatu (Six, Mwakyembe, Nape).

Sijui utatashughulikia lipi na uache lipi!!
Huku moto kule moto!!

Utatutumikia saa ngapi Tuliokuweka madarakani?
Je,kwa Staili hii utafika 2015?

Unashangaa ya Kikwete, ya Slaa Je? Ana operesheni Sangara, operesheni ondoa Zitto, Operesheni susia Shibuda, Operesheni CCJ c/o Kubenea na mapacha watatu, Operesheni mke mdogo (Josephine) n.k.
 
Huu ni uchantanda utaahira! Hamna uongozi wa maneno ya matusi kama kwenye ripoti hii. Kweli uvccm ni genge la wauni na majambaka!
 
Wanatudanganya hawa majoka wadogo hawana jipya. Ufisadi ndani ya chama chao si wa watu watatu tu...ni mfumo wa utendaji kazi. Kuondoa ufisadi ccm ni kuiondoa ccm yenyewe

TAMKO LA VIJANA WA CCM MKOA WA ARUSHA

Tarehe 25/05/2011

Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumeona tuwaite hapa ili tuweze kutoa maoni yetu kuhusiana na mustakabali wa chama chetu cha Mapinduzi na Jumuiya yetu ya Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha.

Tumewaita hapa kwa malengo makuu Sita:-

1.
Kuunga mkono Halimashauri kuu ya CCM Taifa kwa kuona umuhimu wa kuifanyia kazi kwa vitendo falsafa ya kujivua gamba. Tunaipongeza na kuiunga mkono Halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwamba mafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chama chetu mbele ya umma wa watanzania. Kwa mantiki hiyo tunatamka kwa kauli moja kwamba mapacha hao watatu wa kifisadi ambao ni Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge na vibaraka wao wafukuzwe mara moja kwa maslahi ya CCM na Watanzania. Pia tunasisitiza kuwa Andrew Chenge aondolewe kwenye kamati ya maadili ya CCM mara moja na wakati huohuo Edward afukuzwe kwenye kwenye ya uwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya umoja wa vijana wa CCM Taifa haraka iwezekanavyo.

2.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunamtaka kuwa James Millya ambaye ni kibaraka mkuu wa mafisadi mkoa wa Arusha ajiuzulu mara moja na tunatamka rasmi kumfukuza kwenye UVCCM mkoa wa Arusha ili apate fursa ya kwenda kuwa tumikia mafisadi. Tunamtaka James Millya aache kufikiria kwa kutumia tumbo na badala yake atumie kichwa. Pia tumeshaandika barua yenye kumbukumbu namba kumb. Ars/Malalamiko/01 kwenye Chama kuelezea namna alivyo mnafiki, mfitini,mwongo na namna asivyo jali maslahi ya vijana wa UVCCM mkoa wa Arusha. Vilevile tunapenda kuujulisha umma wa Tanzania kuwa Ally Bananga anaetumiwa na Millya pamoja na mafisadi hana nafasi yoyote ndani ya Umoja wa vijana wa CCM kuanzia kwenye tawi hadi Taifa. Kwa mantiki hiyo Ally Bananga aache mara moja kuganga njaa kwa kutumia jina la UVCCM. Pia tunampa onyo kali Catherine Magige aache mara moja kutumia fedha za mafisadi kuwagawa vijana wa Arusha kabla hatujatumia haki yetu ya kikanuni ya kumsimamisha Ubunge. Tunajua kuwa amepata ubunge kwa nguvu za kifisadi kupitia UVCCM.

3.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunakiomba chama cha cha mapinduzi kiwafukuze mara moja makatibu wa UVCCM kutoka wilaya za Monduli, Arumeru, Longido na Karatu kwa kushiriki mandalizi ya maandamo haramu na kwa kukataa wito wa chama wa kwenda kutoa ushahidi wa malamiko yao kuhusu mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa. Kitendo hicho cha kukataa wito wa Chama ni dharau na ukosefu wa maadili.

4.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka kwamba ili kulinda hadhi ya CCM mkoa wa Arusha tunamtaka Onesmo Nangole ajiuzulu mara moja kwa kuwa anafanya kazi ya Fisadi Edward Lowasa na si ya CCM. Kitendo chake yeye cha kufanya kazi ya mafisadi na si ya CCM kimetupelekea kupoteza majimbo mawili kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.

5.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka kwamba Mhe. Mary Chatanda (MB) ambaye ni katibu wa CCM Mkoa wa Arusha ni mpiganaji na ni lulu ya CCM mkoa wa Arusha. Amefanya mengi ya maana na wa-CCM makini, wazalendo na wanaojali maslahi ya chama chetu wanatambua hilo. Pia tunawaomba CCM Taifa waendelee kumwacha hapa Arusha ili aendelee kukijenga chama na kukomesha mafisadi pamoja na dagaa wao.

6.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka rasmi kumtambua Ndugu. Mrisho Gambo kuwa ni mjumbe halali wa baraza kuu la UVCCM Taifa kuwakilisha mkoa wa Arusha. Tunamuunga mkono kwa ujasiri wake, umahiri wake na uzalendo wake wa kupambana na ufisadi ndani ya chama na Tanzania kwa ujumla. Na huo ndiyo msimamo wetu kwa kuwa una tija kwa vijana wa Tanzania. Tunashauri CCM Taifa kuwaita rasmi mapacha watatu wa kifisadi (Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge) kwenye kamati ya maadili ya CCM Taifa na kisha kuwafukuza mara moja kama kweli tuna nia ya kuendelea kuwa chama tawala katika nchi hii.

TUTASEMA KWELI DAIMA FITINA KWETU MWIKO

KAULI YETU: KULINDA NA KUJENGA UJAMAA

KITADUMU CHAMA CHAMAPINDUZI BILA MAFISADI
 
Back
Top Bottom