Tamko la Tanzania Social Support Foundation (TSSF) juu ya kutokutambuliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

white hat

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
3,323
2,487
Kufuatia kauli ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako aliwa Bungeni leo na baadae Wizara kutoa tamko rasmi kuwa haiitambui taasis ya Tanzania Social Support Foundation (TSSF) ambayo ilikuwa inatoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu

Rejea hapa; Serikali: Hatuitambui Taasisi ya Tanzania Social Support Foundation (TSSF) iliyojigamba kutoa mikopo kwa wanafunzi

Shirika hilo limetoa tamko lake juu ya kauli hiyo na kusema linakiri kupokea tamko hilo ya Wizara ya Elimu. Lakini pia Shirika la TSSF limeshtushwa na kusikitishwa kutokana na namna ambavyo juhudi zake za kuwasaidia watoto masikini wa kitanzania kupata elimu ya juu ambayo ni haki yao ya kimsingi na ya kikatiba zinavyominywa na kuzodolewa kila kona ya nchi hii kutokana na hisia hasi za kitapeli

Aidha Shirika hilolimefafanua mambo sita muhimu;
  1. Uhalali wa Kisheria
  2. Utoaji wa Mikopo Nafuu ya Elimu kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu chini ya Mfuko wa Elimu ya Juu Shirika la TSSF
  3. Uhalali wa TSSF kutoza Gharama za Huduma zake
  4. Majibu ya TSSF Dhidi ya Tamko la Mhe. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako
  5. Taarifa ya Wizara kwa Umma kuhusu TSSF
  6. Msimamo wa TSSF dhidi ya Huduma zake kwa Umma

Soma nyaraka zifuatazo ambazo ndio tamko zima la Shirika hilo la TSSF

1.PNG

2.PNG

3.PNG

4.PNG

5.PNG

6.PNG
 
  • Thanks
Reactions: ELX
Mmmh kimantiki na maelezo yanaonekana yanaeleweka, ila sijajua nini kilifanya Waziri atoe matamko vile na kuleta sintofahamu hii kwa wanufaika wa hiyo fursa. Na tena Kumbe kuna maafisa toka ofisi ya waziri wamefika na kujiridhisha nyaraka za uhalali wao.

Ila naona hakukuwa na mawasiliano ya kina. Hili ni ombwe kwa sekta nyingi nchini kwa sasa, viongozi kisiasa huwa wanatoa majibu haraka bila kuwasiliana na watendaji wao wa chini. Hivi kulikuwa na kosa gani angejibu suala hilo watalifanyia kazi then wajiridhishe bila shaka uhalali wao hawa ndo watoke na tamko?

Je, ni kosa watu kutoa misaada kwa vijana wanaokosa mikopo?

Je, ni kweli vijana wote waliochaguliwa vyuo wamepata mkopo wa serikali hivyo hakuna haja ya wengine kuonekana kusaidia?

Kwa mantiki tu, kilichotakiwa kufanywa na serikali/wizara husika ni kuona hiyo mikataba na wanufaika kweli ni nafuu au itawaumiza mbele ili wawabane wairekebishe tu.

Oooh my Country, utawahurumia sana vijana wenye nia ya kusoma ila wamekosa mkopo, maisha wanayoishi na alikotoka Mungu ndo anajua.

Ni mtazamo wangu tu, pia naweza kuwa sipo sahihi, muda tu utaweka ukweli.
 
jamaa wanapiga mpunga sana hakuna riba nafuu hapo hata taratibu za mkopo ukikamilisha lazima utaombwa hela ili ufanikishe,ndiyo maana ndalichako kapanyoshea kidole hapo
 
Kuna kila dalili ya hawa watu kujiendesha kwa registration fee, imagine applicants wawe 10,000 ina maana watakuwa wamekusanya 300,000,000/= kwenye registration forms tu. Kama kwa mwaka mwanafunzi anahitaji 4m, wataishia support wanafunzi 50, like 200m, still huo ni mkopo. Inshort kuna possibility kubwa sana hakuna funds zozote toka nje ya nchi kama wanavyodai.
 
Hio serikal waisaidie wao wenyewe basi hizo hela za mikopo kwa wanachuo mana mpaka vijana wanaandamana for what sasa
 
Ni kweli ninanusa harufu ya upigaji hapa, kitu kinachotakiwa ni maximum transparency. NGO hairuhusiwi kufanya biashara kwa sababu hazilipi kodi. Hawa jamaa walipaswa kujisajili Brela kama Micro finance Organisation na kupata vibali vya BOT kuendesha fundraising ili ndipo wakopeshe. NGO haiwezi kutoa mikopo ya riba bali inapaswa kutoa grants au revolving funds. Kuna NGO ya Heifer inatoa mkopo wa ng'ombe jike na mbuzi wa maziwa, mkopaji anatakiwa kulipa ng'ombe jike au mbuzi jike ili akopeshwe mwingine.

Sasa hawa jamaa kama gharama ya fomu tuu ni 30,000 wakiomba wanafunzi 100,000, jamaa wanakusanya 3,000,000,000 tax free kama ada ya mkopo!. Wakitenga bilioni 2.5 na kutoa mkopo wa milioni 10 kwa kila mwanafunzi, watakopesha wanafunzi 250!. This is pure business unless we
aonyeshe source of fund na proof of payment, vinginevyo this is a revolving funds kuwaibia masikini wa Tanzania kwa kuwachangisha.

Paskali
 
hakuna mtu yeyote atakayepata mkopo TSSF zaid ya utapeli tu,, ,,watz bhanaa
 
Pascal, there is no free lunch! Hawa ni matapeli walio registered! Nakubaliana na wewe!
 
kher hawa kuliko heslb , heslb unagharimika zaid ya elfu arubaini na bado unakosa.... matapeli wa kwanza heslb
 
Kuna kila dalili ya hawa watu kujiendesha kwa registration fee, imagine applicants wawe 10,000 ina maana watakuwa wamekusanya 300,000,000/= kwenye registration forms tu. Kama kwa mwaka mwanafunzi anahitaji 4m, wataishia support wanafunzi 50, like 200m, still huo ni mkopo. Inshort kuna possibility kubwa sana hakuna funds zozote toka nje ya nchi kama wanavyodai.
Una akili nyingi mno
 
Ommy mkopo wa HESLB, hauna dhamana, hauna riba, hauna tracing kama hujaajiriwa hauwajibiki kulipa na walioajiriwa kulikuwa hakuna enforcement mechanism. Find out utaratibu wa hawa jamaa.
P
Unajaribu wabeba hao jamaa ila so far sioni kama wanabebeka. Wakubebeka wangemjibu waziri kwa kuweka proof of where their funds originates and number of students they are going to sponsor. I repeat, kuna kila dalili za hao jamaa kujiendesha kwa registration fee.
 
Back
Top Bottom