Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
inawezekana ni kweli kwa nyie mliosoma sheria ..sasa swali linakuja lile alilotamka rais ni sheria au agizo au sera?
Anaweza kujiendeleza mwenyewe kwa utaratibu mwingine ila sio mfumo rasmi wa Serikali wa darasa la kwanza hadi la kumi na mbili, kwa mfano kuna vyuo vya VETA, SIDO na hata Private kama atapata hao wafadhili (NGO) hasa wanaotetea hawa mabinti wazazi wapate elimu, njia nyingine pia wanaweza kusomeshwa na wazazi wao, walezi na hata familia ya hao waliombebesha hiyo mimba. Kwa hiyo Rais kafungia njia moja tu - lakini nyingine zote kaziachia wazi.Sasa basi, ikiwa Raisi Magufuli anasema mwanafunzi yeyote akipata mimba asipewe nafasi tena ya kuendelea na shule - kimsingi ni sawa na kusema hakubaliani na sheria ya Statutory Rape.
Ni Rais yupi aliruhusu waliozaa wasome?!
Mnamshambulia JPM kwa issue binafsi.
Mzazi wake atakaelimisha kwa kadri atakavyoweza baada ya kulea mtoto wake ila siyo kwny hz elimu burecjutegemea kama wengi wenu umu ndani mtasupport haya maneno aliyoongea uyu magu!!!kumbukeni c wte ni wazazi na kama sio mzazi utakuja pita tu kwenye uzazi!!tunayemzungumzia hapa mkae muelewe ni msichana wa kuanzia darasa la 5 na kuendelea hadi secondary!!wengi walio hapa ni chini ya miaka 18,kiujumla wengi wao bado hawajajitambua na vigumu sana kukwepa vishawishi kutokana na umri wao,wengi wao wanashawishiwa na kurubuniwa bila kujitambua!!!na ndio maana sheria inamkaba mwanaume sbb anakua kama amembaka!!sasa kma tunatambua hili ndio maana tukaeka adhabu kwa mwanaume!!why tuje tumuhukumu uyu aliyerubuniwa!!kumbuka ni mtoto au kasichana!!!tupambane na ujinga lakini si elimu!!
Anaweza kujiendeleza mwenyewe kwa utaratibu mwingine ila sio mfumo rasmi wa Serikali wa darasa la kwanza hadi la kumi na mbili, kwa mfano kuna vyuo vya VETA, SIDO na hata Private kama atapata hao wafadhili (NGO's) wa kumsomesha ama mzazi wake.
Kwa hiyo basi kupata mimba kutampotezea mama huyu mtarajiwa haki ya kupata elimu ya msingi na secondary hadi kidato cha nne kwa mfumo wa serikali ulio rasmi. ila hajafungiwa kujiendeleza mwenyewe popote atakapo.
Kwani sheria au kanuni/taratibu za Tanzania kama Taifa huru zinalingana na za huko South Africa?..Mmh. Umetembea duniani kiasi gani hadi kutoa kauli hii? Nenda tu hapo South Afrika utaona.
Kwani sheria au kanuni/taratibu za Tanzania kama Taifa huru zinalingana na za huko South Africa?..
Nadhani huyo uliyemnukuu amezungumzia Marais waliotangulia wa Tanzania (Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete)...
People will always have sex - religion or no religion, legal or illegal, underage, marital or extra marital - you name it. Girls/women will always get pregnant as adults or underage - we can't and shouldn't penalise them for that. When we deny girls education, they will not value it in the lives of their children too and we'll in turn create a generation that is illiterate and dependent. Having an illiterate generation has multiplier effects in areas such as poor health, malnutrition, high maternal and infant mortality, low accessibility to credit facilities etc. Jailing the men, or threatening them with 30 years jail term will not stop people from desiring to have sex, that's nature in control.
Mimba linaweza kuwa tokeo la ngono moja tu, na haimanishi mwanafunzi aliyepata mimba ni mhuni au fuska. Mara nyingi ni suala la mazingira. Wale wanafunzi mafuska sio rahisi kupata mimba - ni wazoefu na wanajua jinsi ya kuzuia. Kwa hiyo tusitafsiri kwa ujumla mimba za wanafunzi na ufuska. Anaepinga kwamba wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni wasirudi shule - wanaume na wanawake, watuambie wao walifanya ngono kwa mara ya kwanza (kupoteza ubikira) wakiwa wapi. Imagine kwamba katika ngono ile uliyofanya kwa mara ya kwanza ungeshika mimba (wanaume wajifikirie ni wanawake), leo ungekuwa wapi kama usingepewa nafasi ya kuendelea na shule? Wengi wetu hata darasa la saba tusingemaliza, achilia mbali form three, four au six. Jambo la msingi na busara kufanya ni kuongeza kampeni za kuelimisha watoto wasijiingize kwenye ngono mapema.
Ni Rais yupi aliruhusu waliozaa wasome?! Mnamshambulia JPM kwa issue binafsi.
Ukiwa mkuu wa kaya inabidi uchunge sana kauli, hili ni tatizo kubwa sana la mkulu wetu, kushindwa kujua wapi pa kuongea nini na aongeeje. Hizi kauli zinawakwaza wengi na inabidi abadilike, sio lazima uongee kila kitu vitu vingine unamalizia chini ya kapeti kwa maagizo tu au kwa kutumia kauli nzuri. Ndo maana mfalme Suleimani aliomba hekima above kila kitu. Ndo maana wengine wanamuita mzee wa kiki (Sikuleta tetemeko, nyie fyatueni nitasomesha tu, serikali haina shamba,mnataka niwapikie chakula, badilisha debe la mahindi kwa ngo'mbe watatu, unakaa unaangalia mpaka ngo'ombe anakufa si ukauze n.k)Ni Rais yupi aliruhusu waliozaa wasome?!
Mnamshambulia JPM kwa issue binafsi.
Naongelea hapa kwetu mkuu.Mmh. Umetembea duniani kiasi gani hadi kutoa kauli hii? Nenda tu hapo South Afrika utaona.
Elimu bure kwa pesa ya nani, kumbuka hizi ni kodi za wananchi na mkulu asifikiri ni zake alizouza ngo'mbe wa urithi. Tuwe na ubinadamu na tujue wengi wanaopata ujauzito wanatoka familia na mazingira magumu kidogo. So aende private school kwa support ya nani?au tunasahau kuwa hizi mimba ni matokeo ya mwingiliano wa sababu nyingi sana na inatupasa kutatua hizo sababu kabla ya kutoa hukumu hii ya maisha.Mzazi wake atakaelimisha kwa kadri atakavyoweza baada ya kulea mtoto wake ila siyo kwny hz elimu bure
Ni sawa. Kwenye hili ningependa tu nimuunge mkono, hakuna namna!Kwa sababu kila mara Magufuli anafanya issue za kitaifa kuwa zake binafsi. So anaji-expose kushambuliwa na kila mtu mwenye akili na kuona mbali.
Rais yupo sahihi,mkanye mwanao asikimbilie ngono badala yake azingatie masomo