Wanafunzi wa kike ngono imekuwa jambo la kawaida kwao, Walezi "wamelala"

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
222
529
Kama kuna jambo linatishia uhai wa Taifa basi ni swala la vijana hasa wa kike kuchukulia swala la ngono jambo la kawaida sana

Zamani mvulana kugusa mwili wa msichana (hata mkono tu) ilikuwa mvulana anaweza kuota mwezi mzima na atawasimulia washikaji zake kijiweni. Hiyo ilikuwa kugusana tu na mtoto wa kike kwasababu walikuwa na staha na adabu na waliheshimu miili yao

Mambo yamebadilika sana siku hizi! Watoto wadogo hasa wanafunzi wa sekondari na vyuo kwao swala sio kuguswa tena, ngono kwao imekuwa kama jambo la kawaida sana! Yaani sio swala la aibu wala kujitafakari, wanaona fahari kutembea na wanaume

Watoto wa kike kuanzia miaka 16+ kutembea na wanaume wenye miaka 30+ sio aibu kwao ni fahari

Wasichana wadogo miaka 20+ kutembea na wanaume miaka 40+ kwao sio aibu tena ni jambo la kawaida sana

Ukiangalia umri huo ni wa uanafunzi bado.

Walimu mashuleni kazi wanayo hasa kwa hawa watoto wa uswahilini maana wamekua wakiona dada zao, shangazi zao, mama zao wadogo wakifanya hivyo. Hawana wa kuwashauri kitu kinachofanya walimu nao waonekane wanatwanga maji kwenye kinu wanapokemea maswala hayo

Nimeshuhudia mtoto wa kidato cha kwanza (miaka 13) amejenga mahusiano "sugu" na jamaa ana familia yake (mke na watoto wawili) kiasi cha kupata ujasiri wa kutoroka kwao kila ifikapo usiku wa manane kwenda kwa jamaa huyo na anavizia alfajiri ndio anarudi kwao. Binti haoni hata aibu anakiri kabisa kuwa anampenda!!

Ukiona shule ya sheria pale mawasiliano wanafaulu wanafunzi 17 kati ya maelufu sio swala la kuwalaumu watunga mitihani, tuangalie chanzo

Ukiona wanafunzi wa udaktari Muhimbili wanagomea baadhi ya mitihani tutafute chanzo sio kulaumu utaratibu

Watoto siku hizi hawasomi, "standardization" inayofanywa na NECTA huku madarasa ya chini kwa malengo ya kisiasa inaharibu sana elimu yetu

Zamani kuvuka kidato cha pili kwenda cha tatu ilikuwa "avarage" ya alama 30, yaani mwanafunzi afaulu masomo saba si chini ya alama 30. Lakini siku hizi akifaulu masomo mawili tu kwa alama 30 anavuka (yaani D mbili) na bado wanafeli wengi sana tu

Mmomonyoko wa maadili kwenye Taifa letu unaua vipaji vya watoto na sasa kipaji kinachoibukia kwa kasi kubwa sana ni kipaji cha Ngono! Hiki watoto wanajua kukitumikia vizuri sana

Kumbi za starehe na hizi night clubs siku hizi kuwakuta watoto wadogo wa kike kwa wa kiume ni kawaida sana kana kwamba hakuna serikali wala sheria zinazoongoza maeneo hayo

Mtoto wa sekondari anakesha club akichezewa chezewa maungo yake na kulewa kila aina ya kilevi halafu utegemee aheshimu Wazazi na Walimu na kuelewa darasani?
 
Sasa kama mtot anafundishwa kutumia kondomu, anafundishwa na uzazi wa mpango unategemea nini.

Hiyo si sababu kuu ila ina mchangi wake katika haya yanayoendelea.
Jamii ambayo zinaa sio jambo la kustaajabu, miziki mpaka movie zinahamasisha ngono.
Kwakweli inasikitisha sana.
Enzi za ukuaji wetu tulikuwa tukifundishwa elimu juu ya magonjwa ambukizi kwa njia ya ngono kwa mifano ambayo ni rafiki kwa umri wetu wa utoto.

Lakini siku hizi imekuwa tofauti sana, watoto wanaanza mahusiano mapema sana na wanafahamu hata mbinu za kuzuia/kutoa ujauzito.
Kuna vingi vinachochea zinaa aidha bika kujua au kwa makusudi (wanajua)

Kwenye tv niliona tangazo la binti wa shule na mpenzi wake wameenda zahanati ya mbali huko kuoata elimu ya uzazi wa mpango, wakakutwa na shangazi yao wakaona aibu akawaambia wamefanya jambo sahihi.
Sasa like tangazo linamfundisha nini binti mdogo!?
Nao wapo kwenye umri wa ujana wa mwanzo kabisa wanatamani kujaribu kila kitu ukijumlisha na mihemko ya mwilini ndio tabu tupu.

Kila mzazi ana wajibu kuzuia haya.
 
Sasa kama mtot anafundishwa kutumia kondomu, anafundishwa na uzazi wa mpango unategemea nini.
Hiyo si sababu kuu ila ina mchangi wake katika haya yanayoendelea.
Jamii ambayo zinaa sio jambo la kustaajabu, miziki mpaka movie zinahamasisha ngono.
Nao wapo kwenye umri wa ujana wa mwanzo kabisa wanatamani kujaribu kila kitu ukijumlisha na mihemko ya mwilini ndio tabu tupu.

Kila mzazi ana wajibu kuzuia haya.
Huwa natamani sana watokee watu hasa hao haki elimu na watetezi wa haki za watoto washuke huku uswahili waone watoto wanavyo"pigania" haki yao ya kushiriki ngono katika umri mdogo.

Watoto hasa wa kike wanaona kama ni kawaida na hawatakiwi kuzuiliwa. Wanaona kama ni haki yao kiasi wengine wanafikia hatua ya kugombana na wazazi wao
 
Bongo fleva inamchango mkubwa sana kutufikisha hapa tulipo. Ngono imeimbwa na kutukuzwa haswa na wasanii wetu wa bongo fleva.
Tabia za ovyo zinabadilishwa majina na kusifiwa kwenye nyimbo mfano ulawiti wanaita kwa mpalange, mara wanasafisha mitaro n.k. Na wimbo sio moja ni nyingi tu matokea yake jamii inazoea na kuona usafishaji mitaro ni jambo la kawaida kabisa.
Sasa hivi wasanii wamehamia kusifia ulevi. Miaka ya nyuma kidogo kuitwa mlevi lilikua ni jambo la aibu sana lakini leo tunapiga masanga huku tunaimba sisi ni walevi, tunapenda kamnyweso.
 
malizia hapa, watetezi wa haki za watoto wa kike

ambao ndiyo walewale watetezi wa wanawake, wanaharakati, wenye mlengo wa kumkomoa mwanaume na kumpigania KE awe na haki na nguvu sawa na mwanaume ikiwemo kokojoa kwa kusimama na kuvuta mkokoteni kifua wazi

shenzi zao
Hawa nao kabla ya kuanza na kutetea walitakiwa waanze na kuwafundisha namna ya kujilinda. Wanawapa ujasiri usio wao kiasi cha kuhisi wanaweza kufanya lolote popote bila kujua hawa wanaopiga kelele wapo kwa malengo maalumu na kushibisha matumbo yao
 
Mambo yamebadilika sana siku hizi! Watoto wadogo hasa wanafunzi wa sekondari na vyuo kwao swala sio kuguswa tena, ngono kwao imekuwa kama jambo la kawaida sana! Yaani sio swala la aibu wala kujitafakari, wanaona fahari kutembea na wanaume

Watoto wa kike kuanzia miaka 16+ kutembea na wanaume wenye miaka 30+ sio aibu kwao ni fahari

Wasichana wadogo miaka 20+ kutembea na wanaume miaka 40+ kwao sio aibu tena ni jambo la kawaida sana

Ukiangalia umri huo ni wa uanafunzi bado.
Usemalo ni kweli imekuwa kama basic need kwao
 
Back
Top Bottom