Tamko la Rais Magufuli juu ya mimba za wanafunzi linapingana na sheria zilizopo

Wakati mwingine inabidi tu tuwe wakali na kuachana na huu upuuzi wa sheria,ifike pahala kila mzazi awe macho na mtoto wa mwenzake ma kuangalia jamii husika,ukali wa malezi na maadili ufike popote pale katika mazingira hatarishi ya mtoto wa kike na msababishaji pia,no way out naungana na kauli ya mheshimiwa Rais
 
Mmh. Umetembea duniani kiasi gani hadi kutoa kauli hii? Nenda tu hapo South Afrika utaona.
mkuu naona umequote,ukaedit ndipo ukakoment, sababu naona kwenye chapisho lake ameuliza raisi gani hapa tz, ila wewe umetaja south afrika, nadhani ulipaswa usome kwa umakini zaidi.
 
mkuu naona umequote,ukaedit ndipo ukakoment, sababu naona kwenye chapisho lake ameuliza raisi gani hapa tz, ila wewe umetaja south afrika, nadhani ulipaswa usome kwa umakini zaidi.
Yeye ame-edit baada ya mimi ku-comment. Kitu gani hakieleweki hapo? Mara ya kwanza haku-specify Tanzania
 
Kwa hiyo unataka kusema hiyo statutory rape ambayo hata hivyo hujacite ni ya sheria gani, inaprovide pia suala la kuendelea na darasa la sita kama kapata mimba akiwa darasa la Tano? au kuendelea form three kama kapata ujauzito kidato cha pili? ndugu yangu upo out of context kabisa, hujajenga hoja hapo hata kidogo.
Wewe usipoelewa thread sio warrant kuni-accuse mimi kuwa out of context, kwa sababu tu siku hizi unajua kuandika out of context, japo hujui maana yake.

In fact ni context ya Statutory rape law that makes what Magufuli says to be a contradiction. Kama statutory rape inatambua kwamba mtoto wa chini ya miaka 18 hana uwezo wa kiakili kujua kwamba kufanya ngono ni vibaya, na hivyo huyo anaefanya nae achukuliwe kambaka, sasa kwa nini umuhukumu mtoto asiye na akili ya kuelewa kwamba kufanya ngono ni vibaya kwa kumkatalia kurudi shule ukidai kachagua kuwa mzazi? Kama hajui kufanya ngono ni vibaya, basi usimhukumu kuwa kachagua kuwa mzazi, kwa kuwa hakujua ubaya wake. Na huenda hata hakujua akifanya ngono atapata mimba - kama vile tu statutory rape law inavyodai.

Sasa unajiona unavyohemuka huelewi "context" ya kisheria ya thread unakimbilia kusema niko out of context.
 
Kwanza kabisa kasome tena Sheria inaonekana ulikalili I'll ufahuru maana umeshindwa kabisa kujua maana ya Sheria hii,Pili katika maisha yako hapa Tanzania kuanzia kwa Mwl.Nyerere ulishawai kusikia binti kapewa mimba akaendelea na Shule?au kajifungua akaludi tena kusoma?

Wewe mtu wa kuhurumiwa sana. Kiwango chako cha elimu kiko wazi katika sehemu ya pili ya post yako, "katika maisha yako hapa Tanzania kuanzia kwa Mwl.Nyerere ulishawai kusikia binti kapewa mimba akaendelea na Shule? au kajifungua akaludi tena kusoma?"

Unaniambia nikasome tena sheria, wakati wewe hata elimu ya kati huonyeshi kama unayo. Ni wazi hauko kwenye ligi yaku kujadili suala hili lenye complexity ya kisheria. Na tunasema "akarudi" sio "akaludi", "ulikariri" sio "ulikalili". Na pia jifunze kutenganisha maneno unapoandika, na kujua wapi pa kutumia herufi kubwa na ndogo. Na pia hatusemi "ulishawai" angalau sema "ulishawahi".

Elimu haina mwisho. Jiendeleze ili uweze kujibu hoja za kisomi kama msomi.
 
Lakini mtoa mada naona na yeye anajichanganya , kwa kuzungumzia statutory rape halafu anazungumzia itungwe sheria ya kifungo cha maisha wakati sasa hivi tunayo sheria ya kifungo cha miaka 30 jela kwa issue ya rape. Mimi Naona ni kusisitizia hapo kwenye kufunga hiyo miaka 30 jela, lakini limekuwepo tatizo la victim kuwa upande wa mtuhumiwa kwa sababu ya Hiyo loophole ya yeye kuonekana Kama muathirika na si mkosa.
Sasa hili tamko la Raisi na la Mama Kikwete linajaribu ku elezea jukumu la Huyu mwanafunzi au mtoto kuelewa madhara ya mimba za utotoni hivyo kujilinda na wazazi na walezi pia kushiriki ktk kuwaeleza na kuwalinda watoto na hizi changamoto za chips, kurudi usiku, usafiri nk.

Mkuu, nashindwa kuelewa kwa nini watu msioelewa mambo ndio mnaokimbilia kuwasema wengine wanajichanganya.

Kwanza, "statutory rape" na "rape" ni vitu viwili tofauti kabisa. Statutory rape inakuwa rape hata kama msichana alikubali kufanya ngono kwa hiari, wakati rape unayoongelea hapa ni ile tu unapofanya ngono na mwanamke mtu mzima kinyume na utashi wake. Sasa hiyo rape ya kawaida kifungo chake ni miaka 30, mimi nilipendekeza kifungo cha maisha kwa statutory rape.

Pili, essence ya statutory rape ni kwamba huyo mwanafunzi au mtoto hawezi kuelewa madhara ya mimba za utoto na hivyo hawezi kujilinda - tofauti na maoni ya Mama Kikwete na wewe. Ndio maana nikasema huwezi kumhukumu asirudi shule wakati ulishasema kwenye statutory rape kwamba anafanya asilolijua - inakuwa contradiction, au kujipinga.

Wengi wa wachangiaji humu ndani hamjielewi kabisa mnachojibu kwenye thread yangu. Nyie mnang'ang'ania kujibu kama kauli ya Magufuli ni sawa au sio sawa. Mimi ninaichambua kauli ya Magufuli in the context of statutory rape.
 
Adhabu ya kukiuka taratibu ni ipi?
Adhabu ya kukiuka taratibu inategemea mandhari ya taratibu, na makubaliano yaliyofanywa na walioziweka. Lakini hakuna sheria inayotoa adhabu kwa kukiuka taratibu.

Kwa mfano, ukiwa mwanakijiji, kuna taratibu ambazo kijiji kitajiwekea ambazo mwana kijiji asipozifuata atatakiwa kupewa adhabu kulingana na makubaliano yaliyofanyika wakati wa kuweka taratibu hizo. Mwana kijiji anaweza kushitaki mahakamani kwa kuadhibiwa na akashinda kwa sababu taratibu sio sheria.

Katika ngazi ya kitaifa ukiukwaji wa taratibu hauwezi kuzuiwa kwa adhabu, bali kwa kumzuia mtu asikiuke taratibu. Lakini pia, kuzuia mtu asikiuke taratibu zipo njia mbili. Ikiwa katika kuvunja taratibu huyo mtu anavuruga amani, basi unaweza kum-arrest kwa kuleta uvunjaji wa amani - kwa sheria ya kuvunja amani. Njia ya pili ni kwenda tu na kumwambia unachofanya sio sahihi kwa hiyo acha.

Ikiwa nitavunja taratibu bila kuvunja amani basi huna msingi wa kisheria wa kuni-arrest baada ya tukio la kuvunja taratibu. Sasa hicho ndicho walifanya kina Sumaye.

Kwa hiyo ndio maana inakuwa ni ukihiyo sana, kutoa amri Sumaye akamatwe kwa kitendo cha kuvunja taratibu kilichokwisha fanyika wakati ambapo hapakuwa na uvunjaji amani.

Kwa mfano, kuna utaratibu wa kumwona na kuongea na raisi. Lakini mimi naweza kuongea na raisi kwa njia nyingine bila kufuata utaratibu uliowekwa - naweza kunyosha mkono wakati akitoa hotuba na kuomba anisikilize. Je, uta-niarrest kwa kuvunja taratibu ya kumwona na kuongea na raisi? Au nikimwandikia barua ya wazi?

Kuna utaratibu wa kuonana na Mkuu wa Wilaya na kumweleza matatizo. Je, nikimwona yuko baa anakunywa bia nikamfuata, kumnunulia bia na kumweleza matatizo, ninatakiwa kuwa arrested kwa kuvunja utaratibu wa kuwakilisha matatizo yangu kwa Mkuu wa Wilaya?
 
Mnaleta wehu. Mtu anamaliza form 6 unasema kabakwa? Mnakuwa kama wale wanawake wapuuzi ambao hawataki kushiriki na waume zao badala yake wanasema wanabakwa. Siku hizi uwezo wa akili za wanafunzi siyo kama zenu za vidumu na mfagio, sahivi wanafunzi wana uelewa mkubwa sana na wanafahamu karibu kila kitu. Itashangaza kwamba mwanafunzi anaweza kufanya paper gumu akatoka na 1/2 ila ssifahamu madhara ya ngono kwake, hii itakuwa ni sinema ya karne na inahitaji ushahidi wa neuropsycologists kutuelewesha kwanini mengine ayaelewe kwa wastani wa A na afeli kuelewa lile la kujamiiana

Wehu ni pale ambapo mtu anauliza mtu kamaliza form 6 unasema amebakwa, kama amekubali ngono kwa hiari na ana miaka zaidi ya 18. Kwa sabau huyo hayuko katika context ya kauli ya Magufuli. Sasa sijui anaingiaje hapa.

Pia, thread hii inajadili context ya Magufuli katika sheria tuliyonayo inayosema msichana yeyote chini ya miaka 18, mwanaume akifanya naye ngono anakuwa amembaka, iwe amekubali au la (statutory rape). Sasa hiyo sheria haisemi statutory rape ni kwa wale wasichana ambao hawana uelewa mkubwa wakati siku hizi wengi wana uelewa mkubwa. As long as sheria ipo inayosema msichana akiwa chini ya miaka 18 ukifanya naye ngono umembaka, sisi tutasema basi usiwahukumu wasichana wanaobakwa na kupata mimba.

Labda jiulize, ina Maana Magufuli ana maana msichana wa shule akibakwa na vibaka na kupata mimba, akatoe hiyo mimba ili aendelee na shule? Au ana maana hata huyo afukuzwe tu shule, ni shauri yake kwamba alibakwa, kiherehere chake?

Kiongozi ngazi ya raisi anatakiwa awe na uwezo wa kutafakari mambo kamba ya kutoa tamko.
 
Anaweza kujiendeleza mwenyewe kwa utaratibu mwingine ila sio mfumo rasmi wa Serikali wa darasa la kwanza hadi la kumi na mbili, kwa mfano kuna vyuo vya VETA, SIDO na hata Private kama atapata hao wafadhili (NGO) hasa wanaotetea hawa mabinti wazazi wapate elimu, njia nyingine pia wanaweza kusomeshwa na wazazi wao, walezi na hata familia ya hao waliombebesha hiyo mimba. Kwa hiyo Rais kafungia njia moja tu - lakini nyingine zote kaziachia wazi.

Kwa hiyo basi kupata mimba kutampotezea mama huyu mtarajiwa haki ya kupata elimu ya msingi na secondary hadi kidato cha nne kwa mfumo wa serikali ulio rasmi. ila hajafungiwa kujiendeleza mwenyewe popote atakapo.
Jamani Watanzania wenzangu, saa nyingine tuweke pembeni akili za facebook na whatsApp na tuiangalie nchi yetu kwa mapana yake. Tanzania haiishii Kibaha na VETA sio kanisa kusema kila mtu ataingia kwa kuwa tu anamkiri Yesu.

P7071514.jpg


Unaujua umbali kutoka hapa hadi ilipo VETA?

_68628291_5_tanzania.jpg


_68628185_03_201306-tza-05.jpg


130710104124_7_tanzanian_girl_pi.jpg


19503.jpg


Shida yetu tunapoyajadili haya tunakosa picha pana ya maisha ya mwanafunzi kwa kuwa tumezungukwa na St Magreth, St. Paukwa, St. Makinikia na kadhalika.

Huko vijijini hakuna VETA. VETA ikiwepo mkoani basi ni makao makuu ya mkoa au wilaya. Na sijui inaingiaje akilini VETA ikampokee mwanafunzi ambaye hajui kusoma wala kuandika.

Hapo hapo umezungumzia 'kugharamiwa masomo na wazazi wake'...labda nikuulize swali: Mpango wako wa kumnyima elimu huyu binti pichani akipata mimba, utamuwezesha kuwa mzazi mwenye uwezo wa kumlipia ada binti yake akipata mimba?

Haijawahi kupatikana faida yeyote hapa duniani kwa kundi fulani kunyimwa elimu. Tabaka hujizaa. Binti unayemnyima elimu kwa kuwa tu alijikuta 'victim of circumstance' na kupata mimba sio maandalizi ya jamii bora bali ni mwendelezo wa jamii jinga.

Ni elimu tu ndio itatutoa hapa. Tuondoe hiyo dhana kuwa tunapaswa kuwakomoa kwa kuwa walifaidi ngono. Huko vijijini watoto wa kike wana madhila makubwa sijapata mfano wake. Wamekeketwa na bado wanaingiliwa kwa nguvu na bado tunawahukumu kwa kuwanyima fursa ya kuwakomboa watakaowazaa.

Jambo hili linahitaji tafakari na sio kauli za kutafuta kick
 
Kwani sheria au kanuni/taratibu za Tanzania kama Taifa huru zinalingana na za huko South Africa?..

Nadhani huyo uliyemnukuu amezungumzia Marais waliotangulia wa Tanzania (Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete)...
hivi.....kama sheria ipo kwa nini rais atoe decree tena? mbona hao watangulizi wa JPM wao hawakutoa such a decree?

urais ni hekima, mkuu.
 
Elimu bure kwa pesa ya nani, kumbuka hizi ni kodi za wananchi na mkulu asifikiri ni zake alizouza ngo'mbe wa urithi. Tuwe na ubinadamu na tujue wengi wanaopata ujauzito wanatoka familia na mazingira magumu kidogo. So aende private school kwa support ya nani?au tunasahau kuwa hizi mimba ni matokeo ya mwingiliano wa sababu nyingi sana na inatupasa kutatua hizo sababu kabla ya kutoa hukumu hii ya maisha.
Mungu hulifurahia taifa la watu wenye haki na kuliinua.

Tunayasahau mengi yanayowapata hawa watoto tunakimbilia kuwahukumu. Wengi wao wanabeba ujauzito kabla hata hawajajua kuwa kuna raha kwenye ngono. Washabiki wengi hawajui kuwa tuna mazingira zaidi ya haya wanayoyaona mjini wanakoishi.

Mzazi hana elimu matokeo yake anashindwa kuisimamia familia, binti anapata mimba. Binti naye tunamnyima elimu, mwishowe anakuwa mama kama mama yake, na mtoto wake anaishia tena kupata mimba. Hili tabaka linaendelea kujizaa na kutanuka.

Wenzetu wanawekeza fedha zaidi kwenye tatizo, sisi tunakimbilia kuondoa kidogo zilizoelekezwa huko kwa kuwa tu tunataka KUKOMOA. Tutaangamia kwa kukosa maarifa.

ELIMU NI KWA WOTE.
 
Mkuu, nashindwa kuelewa kwa nini watu msioelewa mambo ndio mnaokimbilia kuwasema wengine wanajichanganya.

Kwanza, "statutory rape" na "rape" ni vitu viwili tofauti kabisa. Statutory rape inakuwa rape hata kama msichana alikubali kufanya ngono kwa hiari, wakati rape unayoongelea hapa ni ile tu unapofanya ngono na mwanamke mtu mzima kinyume na utashi wake. Sasa hiyo rape ya kawaida kifungo chake ni miaka 30, mimi nilipendekeza kifungo cha maisha kwa statutory rape.

Pili, essence ya statutory rape ni kwamba huyo mwanafunzi au mtoto hawezi kuelewa madhara ya mimba za utoto na hivyo hawezi kujilinda - tofauti na maoni ya Mama Kikwete na wewe. Ndio maana nikasema huwezi kumhukumu asirudi shule wakati ulishasema kwenye statutory rape kwamba anafanya asilolijua - inakuwa contradiction, au kujipinga.

Wengi wa wachangiaji humu ndani hamjielewi kabisa mnachojibu kwenye thread yangu. Nyie mnang'ang'ania kujibu kama kauli ya Magufuli ni sawa au sio sawa. Mimi ninaichambua kauli ya Magufuli in the context of statutory rape.
Ndugu yangu Synthesizer nashukuru kwa maelezo yako. Lakini kitu kinacho ni tatiza kwa Bongo kwenye suala la statutory rape ni mtendewa kutotoa ushirikiano hivyo kusababisha mtuhumiwa kutochukuliwa hatua ndio maana matendo hayo bado yanaendelea au kushamiri.
Tofauti na nchi zingine ambapo mtendaji anakuwa paedophile .
Sasa tukiweza kutoka ktk hii shida ya mtendewa kuwa upande wa serikali itasaidia. Jingine ni issue ua umri kwa mfano victim akisema mahakamani mimi nilimweleza A na 19 etc
 
asant
Ni agizo mkuu, halina nguvu ya kisheria. Kumbuka Raisi anaweza kutoa agizo linalopingana na sheria/katiba na hata ukaenda mahakamani kupinga utekelezaji wa agizo lake.

Lakini, japo nimesema agizo la Magufuli linapingana na sheria, hakuna sheria inayosema mwanafunzi akipata mimba arudi shule. Labda usahihi zaidi ingekuwa ni kwamba agizo la Magufuri linapingana na "interests" zinazokuwa implied na sheria ya statutory rape. Hivyo kwa namna hiyo unaweza kupinga agizo la Magufuli kwa interests (au nia nzuri) zilizopo katika sheria ya statutory rape.

Na wala sio sera katika really sense ya sera (policy), japo inaweza ikawa ni jambo la Ilani ya CCM.

Na by the way, watendaji wa Magufuli wengi ni vihiyo sana wa sheria. Kwa mfano hapa juzi tumeona mkuu mmoja wa wilaya akiagiza watu wakamatwe na kuwekwa ndani kwa kukiuka utaratibu wa kutembelea miradi. Sasa huwezi kumuweka mtu ndani kwa kukiuka utaratibu, kwa sababu unapomuweka mtu ndani ina maana kuna sheria ya kumshitakia na kumhukumu. Mtu anapokiuka utaratibu utamzuia kufanya anachotaka kufanya, sio kumuweka ndani (arrest), kwa sababu utaratibu uliowekwa unaweza kukiukwa/kuvunjwa katika mazingira fulani.

Kwa mfano, wabunge wanapotolewa nje ni zuio kwao kwa kukiuka utaratibu. Sasa alichofanya huyu Mkuu wa wilaya ungelinganisha na Spika kuamuru Mbunge awekwe ndani kwa kukiuka uratatibu wa Bunge - huo ni ukihiyo. Ila kumbuka kuna thin line kati ya kukiuka utaratibu na kusababisha fujo. Suala la kina Sumaye na ziara za miradi there is no way ungesema ni kuvunja sheria. Hivyo ilikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki kumuweka yule Meya ndani eti kwa kuwa alikiuka taratibu (kama kweli), wakati ambao ukiukwaji huo wa taratibu haukuleta vurugu/uvunjaji wa amani. Hakuna sheria ambayo yule meya ungeweza kumhukumia. Na ukihiyo zaidi ni pale ilipotolewa amri eti Sumaye akamatwe - kwa kosa gani, sheria ipi alivunja? Unatoa amri mtu akamatwe bila kuvunja sheria? Ni sawa na wewe meneja wako akuweke ndani kwa kufika kwenye mkutano saa tatu badala ya saa mbili mliyokubaliana.

By the way, mie sio mwanasheria.
mkuu hongera,alichosisitiza magufuli ni kuwa tukiwa na sheria inyosema alie pewa mimba aendele shule ile ya umma yaani tutakuwa na shule za wamama ,kuhusu kubakwa sheria iko wazi
hivyo basi kiwa kuwa shule binafsi hazijakatazwa,ni vema tukaendelea na sheria iliyopo inayotaka mwanafunzi alie pata mimba asisome shule za umma
 
asant

mkuu hongera,alichosisitiza magufuli ni kuwa tukiwa na sheria inyosema alie pewa mimba aendele shule ile ya umma yaani tutakuwa na shule za wamama ,kuhusu kubakwa sheria iko wazi
hivyo basi kiwa kuwa shule binafsi hazijakatazwa,ni vema tukaendelea na sheria iliyopo inayotaka mwanafunzi alie pata mimba asisome shule za umma

Bado hujaelewa MKuu. Sheria ya statutory rape inasema mtoto wa shule hafanyi ngono, anabakwa kama mtoto asiyejua lolote. Sasa kama tuna sheria inayosema mtoto wa shule hafanyi ngono bali anabakwa kama mtoto asiyejua lolote, kwa nini tumwadhibu mtoto aliyebakwa bila kujua lolote? Hilo ndio swali kwa Magufuli.

Ndio maana nkasema ni sawa na kumtandika viboko mtoto wako wa miaka miwili aliyeungua kwa kuchezea maji ya moto kwa kosa la kuchezea maji ya moto.
 
Bado hujaelewa MKuu. Sheria ya statutory rape inasema mtoto wa shule hafanyi ngono, anabakwa kama mtoto asiyejua lolote. Sasa kama tuna sheria inayosema mtoto wa shule hafanyi ngono bali anabakwa kama mtoto asiyejua lolote, kwa nini tumwadhibu mtoto aliyebakwa bila kujua lolote? Hilo ndio swali kwa Magufuli.

Ndio maana nkasema ni sawa na kumtandika viboko mtoto wako wa miaka miwili aliyeungua kwa kuchezea maji ya moto kwa kosa la kuchezea maji ya moto.
je kuna sheria ya elimu kwa sasa ambayo inataka mtt aliepewa mimba aendelee na shule?ili tujue magufuli kajitungia au sheria ipo tangu zamani
 
Kuna nyakati huwa nafikiria, hizi mbinu za uzazi wa mpango (kijiti, vidonge, etc) haviwezi kutumika kwa watoto wa shule ili kuwanusuru? Je zina madhara ya kiafya kwa kiasi gani? Je kuna madhara mengine ya kijamii ukiacha STDs na lile kuonekana kama "ruksa" kwa watoto hawa kufanya ngono?
 
Bado hujaelewa MKuu. Sheria ya statutory rape inasema mtoto wa shule hafanyi ngono, anabakwa kama mtoto asiyejua lolote. Sasa kama tuna sheria inayosema mtoto wa shule hafanyi ngono bali anabakwa kama mtoto asiyejua lolote, kwa nini tumwadhibu mtoto aliyebakwa bila kujua lolote? Hilo ndio swali kwa Magufuli.

Ndio maana nkasema ni sawa na kumtandika viboko mtoto wako wa miaka miwili aliyeungua kwa kuchezea maji ya moto kwa kosa la kuchezea maji ya moto.
Hakuna, ndio maana suala la kuruhusu waendelee na shule lilikuwa sio tatizo na halikuhitaji utungaji wa sheria kulitekeleza. Sasa hili la magufuli linakuja kama directive na hivyo kuondoa ile leeway iliyokuwapo ya kuwaacha waendelee au kutuwaruhusi waendelee.
 
nimeona na mimi nitoe mawazo yangu kama mwananchi wa kawaida,kwa nionavyo mimi kuwafukuza watoto wa kike shuleni kwa ajili ya kupata mimba ni kuwaonea sana,kwanza inatupasa kuelewa kwamba,hawa bado ni watoto hawajajua kufautisha baya na zuri kwa hiyo ni raisi kwao kudanganywa au kubakwa,mimi kwa upande wangu ningeona ni vizuri kuwafukuza watu wazima wanaopata mimba ambao awajaolewa waliopo vioni maana wao wanaelewa baya na zuri hivyo upataji mimba wao nikwa hiari yao badala ya hawa watoto wadogo. hiyo ni hoja yangu sina maana ya kupingana na mtu ila kama kuna mwenye mawazo au hoja tofauti na yangu anielimishe
 
Back
Top Bottom