Tamko la Rais Magufuli juu ya mimba za wanafunzi linapingana na sheria zilizopo

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,563
Tanzania tunayosheria inayoitwa "Statutory Rape"

Sasa hii sheria imewekwa kwa msingi kwamba ukifanya ngono na msichana chini ya miaka 18 - au mwanafunzi kwa ujumla, utakuwa umembaka. Utachukuliwa umembaka kwa kuwa inachukuliwa kwamba katika umri chini ya miaka 18 au kipindi cha uanafunzi, msichana bado ni mtoto na hana akili ya kutambua kwamba kukubali kufanya ngono sio jambo jema. Hivyo huwezi kujitetea kwamba hukumbaka bali mlikubaliana kufanya ngono.

Sasa basi, ikiwa Raisi Magufuli anasema mwanafunzi yeyote akipata mimba asipewe nafasi tena ya kuendelea na shule - kimsingi ni sawa na kusema hakubaliani na sheria ya Statutory Rape.

Kwa maneno mengine - utakuwaje na sheria ya statutory rape - na hapo hapo uamue kwamba mwanafunzi yeote kupata mimba akiwa shuleni ni uamuzi wake na hivyo moja wapo ya adhabu ni kutompa nafasi ya keundelea na masomo?

Na kumbuka kwamba, kauli ya Raisi Magufuli inadokeza kwamba kila mwanafunzi atakayepata mimba akiwa shuleni kajitakia - yale yale ya kiherehere ya Raisi Kikwete. Hapo hakuna kuangalia sababu wala mazingira ya mimba - awe alibakwa au vinginevyo, mimba ni mimba!

Kwa nini kama Taifa tusijikite katika kuongeza kampeni kuwasaidia hawa watoto kutojiingiza katika ngono za mapema badala ya kutoa adhabu za ujumla zisizoangalia mazingira?

Mie ningemwona Raisi Magufuli ana busara sana kama angesema tutawaruhusu wasome, ila sasa tutatunga sheria atakaempa mimba mwanafunzi afungwe jela maisha! Mimba za wanafunzi zingekoma. Sasa Raisi anaadhibu wanafunzi kuliko wanaowapa mimba!
 
inawezekana ni kweli kwa nyie mliosoma sheria ..sasa swali linakuja lile alilotamka rais ni sheria au agizo au sera?

Ni agizo mkuu, halina nguvu ya kisheria. Kumbuka Raisi anaweza kutoa agizo linalopingana na sheria/katiba na hata ukaenda mahakamani kupinga utekelezaji wa agizo lake.

Lakini, japo nimesema agizo la Magufuli linapingana na sheria, hakuna sheria inayosema mwanafunzi akipata mimba arudi shule. Labda usahihi zaidi ingekuwa ni kwamba agizo la Magufuri linapingana na "interests" zinazokuwa implied na sheria ya statutory rape. Hivyo kwa namna hiyo unaweza kupinga agizo la Magufuli kwa interests (au nia nzuri) zilizopo katika sheria ya statutory rape.

Na wala sio sera katika really sense ya sera (policy), japo inaweza ikawa ni jambo la Ilani ya CCM.

Na by the way, watendaji wa Magufuli wengi ni vihiyo sana wa sheria. Kwa mfano hapa juzi tumeona mkuu mmoja wa wilaya akiagiza watu wakamatwe na kuwekwa ndani kwa kukiuka utaratibu wa kutembelea miradi. Sasa huwezi kumuweka mtu ndani kwa kukiuka utaratibu, kwa sababu unapomuweka mtu ndani ina maana kuna sheria ya kumshitakia na kumhukumu. Mtu anapokiuka utaratibu utamzuia kufanya anachotaka kufanya, sio kumuweka ndani (arrest), kwa sababu utaratibu uliowekwa unaweza kukiukwa/kuvunjwa katika mazingira fulani.

Kwa mfano, wabunge wanapotolewa nje ni zuio kwao kwa kukiuka utaratibu. Sasa alichofanya huyu Mkuu wa wilaya ungelinganisha na Spika kuamuru Mbunge awekwe ndani kwa kukiuka uratatibu wa Bunge - huo ni ukihiyo. Ila kumbuka kuna thin line kati ya kukiuka utaratibu na kusababisha fujo. Suala la kina Sumaye na ziara za miradi there is no way ungesema ni kuvunja sheria. Hivyo ilikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki kumuweka yule Meya ndani eti kwa kuwa alikiuka taratibu (kama kweli), wakati ambao ukiukwaji huo wa taratibu haukuleta vurugu/uvunjaji wa amani. Hakuna sheria ambayo yule meya ungeweza kumhukumia. Na ukihiyo zaidi ni pale ilipotolewa amri eti Sumaye akamatwe - kwa kosa gani, sheria ipi alivunja? Unatoa amri mtu akamatwe bila kuvunja sheria? Ni sawa na wewe meneja wako akuweke ndani kwa kufika kwenye mkutano saa tatu badala ya saa mbili mliyokubaliana.

By the way, mie sio mwanasheria.
 
cjutegemea kama wengi wenu umu ndani mtasupport haya maneno aliyoongea uyu magu!!!kumbukeni c wte ni wazazi na kama sio mzazi utakuja pita tu kwenye uzazi!!tunayemzungumzia hapa mkae muelewe ni msichana wa kuanzia darasa la 5 na kuendelea hadi secondary!!wengi walio hapa ni chini ya miaka 18,kiujumla wengi wao bado hawajajitambua na vigumu sana kukwepa vishawishi kutokana na umri wao,wengi wao wanashawishiwa na kurubuniwa bila kujitambua!!!na ndio maana sheria inamkaba mwanaume sbb anakua kama amembaka!!sasa kma tunatambua hili ndio maana tukaeka adhabu kwa mwanaume!!why tuje tumuhukumu uyu aliyerubuniwa!!kumbuka ni mtoto au kasichana!!!tupambane na ujinga lakini si elimu!!
 
People will always have sex - religion or no religion, legal or illegal, underage, marital or extra marital - you name it. Girls/women will always get pregnant as adults or underage - we can't and shouldn't penalise them for that. When we deny girls education, they will not value it in the lives of their children too and we'll in turn create a generation that is illiterate and dependent. Having an illiterate generation has multiplier effects in areas such as poor health, malnutrition, high maternal and infant mortality, low accessibility to credit facilities etc. Jailing the men, or threatening them with 30 years jail term will not stop people from desiring to have sex, that's nature in control.
 
Sasa basi, ikiwa Raisi Magufuli anasema mwanafunzi yeyote akipata mimba asipewe nafasi tena ya kuendelea na shule - kimsingi ni sawa na kusema hakubaliani na sheria ya Statutory Rape.
Anaweza kujiendeleza mwenyewe kwa utaratibu mwingine ila sio mfumo rasmi wa Serikali wa darasa la kwanza hadi la kumi na mbili, kwa mfano kuna vyuo vya VETA, SIDO na hata Private kama atapata hao wafadhili (NGO) hasa wanaotetea hawa mabinti wazazi wapate elimu, njia nyingine pia wanaweza kusomeshwa na wazazi wao, walezi na hata familia ya hao waliombebesha hiyo mimba. Kwa hiyo Rais kafungia njia moja tu - lakini nyingine zote kaziachia wazi.

Kwa hiyo basi kupata mimba kutampotezea mama huyu mtarajiwa haki ya kupata elimu ya msingi na secondary hadi kidato cha nne kwa mfumo wa serikali ulio rasmi. ila hajafungiwa kujiendeleza mwenyewe popote atakapo.
 
cjutegemea kama wengi wenu umu ndani mtasupport haya maneno aliyoongea uyu magu!!!kumbukeni c wte ni wazazi na kama sio mzazi utakuja pita tu kwenye uzazi!!tunayemzungumzia hapa mkae muelewe ni msichana wa kuanzia darasa la 5 na kuendelea hadi secondary!!wengi walio hapa ni chini ya miaka 18,kiujumla wengi wao bado hawajajitambua na vigumu sana kukwepa vishawishi kutokana na umri wao,wengi wao wanashawishiwa na kurubuniwa bila kujitambua!!!na ndio maana sheria inamkaba mwanaume sbb anakua kama amembaka!!sasa kma tunatambua hili ndio maana tukaeka adhabu kwa mwanaume!!why tuje tumuhukumu uyu aliyerubuniwa!!kumbuka ni mtoto au kasichana!!!tupambane na ujinga lakini si elimu!!
Mzazi wake atakaelimisha kwa kadri atakavyoweza baada ya kulea mtoto wake ila siyo kwny hz elimu bure
 
Anaweza kujiendeleza mwenyewe kwa utaratibu mwingine ila sio mfumo rasmi wa Serikali wa darasa la kwanza hadi la kumi na mbili, kwa mfano kuna vyuo vya VETA, SIDO na hata Private kama atapata hao wafadhili (NGO's) wa kumsomesha ama mzazi wake.

Kwa hiyo basi kupata mimba kutampotezea mama huyu mtarajiwa haki ya kupata elimu ya msingi na secondary hadi kidato cha nne kwa mfumo wa serikali ulio rasmi. ila hajafungiwa kujiendeleza mwenyewe popote atakapo.

Basi kama ni hivyo Raisi Magufuli alipaswa kusema wanaopata mimba wakiwa shule za serikali na hizi yeboyebo za kata. In fact, mimi nikiwa nina private school naweza kumruhusu mwanafunzi aliyepata mimba na kuzaa arudi shule. Agizo la Magufuli sio sheria, na haliwezi kunibana mie kisheria nikiwa na private school nikaruhusu warudi shule.

Na ndio maana hata yeye akijua hili amesema NGO zinazowatetea zianzishe shule zao ili ziwaruhusu warudi.

Mie natoa mwito kwa private schools zimwambie wazi Raisi Magufuli sie tutawaruhusu warudi.
 
Mmh. Umetembea duniani kiasi gani hadi kutoa kauli hii? Nenda tu hapo South Afrika utaona.
Kwani sheria au kanuni/taratibu za Tanzania kama Taifa huru zinalingana na za huko South Africa?..

Nadhani huyo uliyemnukuu amezungumzia Marais waliotangulia wa Tanzania (Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete)...
 
Aaaha. Sawa Mkuu. Unajua watu huwa tunafikiria outside the box, kumbe wenzetu mawazo yao yote yanaishia ndani ya mipaka ya Tanzania.

Lakini suala hapa ni mtazamo wa kisheria, sio nini walifanya maraisi waliopita. Haya mambo ya kumwambia trafiki mbona Juma alipita hapa na spidi hamkumkamata ni kufikiri kuliko kufupi sana.
 
People will always have sex - religion or no religion, legal or illegal, underage, marital or extra marital - you name it. Girls/women will always get pregnant as adults or underage - we can't and shouldn't penalise them for that. When we deny girls education, they will not value it in the lives of their children too and we'll in turn create a generation that is illiterate and dependent. Having an illiterate generation has multiplier effects in areas such as poor health, malnutrition, high maternal and infant mortality, low accessibility to credit facilities etc. Jailing the men, or threatening them with 30 years jail term will not stop people from desiring to have sex, that's nature in control.

Good point Mkuu. I posted this comment somewhere, very much in line with what you say;

Mimba linaweza kuwa tokeo la ngono moja tu, na haimanishi mwanafunzi aliyepata mimba ni mhuni au fuska. Mara nyingi ni suala la mazingira. Wale wanafunzi mafuska sio rahisi kupata mimba - ni wazoefu na wanajua jinsi ya kuzuia. Kwa hiyo tusitafsiri kwa ujumla mimba za wanafunzi na ufuska. Anaepinga kwamba wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni wasirudi shule - wanaume na wanawake, watuambie wao walifanya ngono kwa mara ya kwanza (kupoteza ubikira) wakiwa wapi. Imagine kwamba katika ngono ile uliyofanya kwa mara ya kwanza ungeshika mimba (wanaume wajifikirie ni wanawake), leo ungekuwa wapi kama usingepewa nafasi ya kuendelea na shule? Wengi wetu hata darasa la saba tusingemaliza, achilia mbali form three, four au six. Jambo la msingi na busara kufanya ni kuongeza kampeni za kuelimisha watoto wasijiingize kwenye ngono mapema.
 
Ni Rais yupi aliruhusu waliozaa wasome?!

Mnamshambulia JPM kwa issue binafsi.
Ukiwa mkuu wa kaya inabidi uchunge sana kauli, hili ni tatizo kubwa sana la mkulu wetu, kushindwa kujua wapi pa kuongea nini na aongeeje. Hizi kauli zinawakwaza wengi na inabidi abadilike, sio lazima uongee kila kitu vitu vingine unamalizia chini ya kapeti kwa maagizo tu au kwa kutumia kauli nzuri. Ndo maana mfalme Suleimani aliomba hekima above kila kitu. Ndo maana wengine wanamuita mzee wa kiki (Sikuleta tetemeko, nyie fyatueni nitasomesha tu, serikali haina shamba,mnataka niwapikie chakula, badilisha debe la mahindi kwa ngo'mbe watatu, unakaa unaangalia mpaka ngo'ombe anakufa si ukauze n.k)
 
Mzazi wake atakaelimisha kwa kadri atakavyoweza baada ya kulea mtoto wake ila siyo kwny hz elimu bure
Elimu bure kwa pesa ya nani, kumbuka hizi ni kodi za wananchi na mkulu asifikiri ni zake alizouza ngo'mbe wa urithi. Tuwe na ubinadamu na tujue wengi wanaopata ujauzito wanatoka familia na mazingira magumu kidogo. So aende private school kwa support ya nani?au tunasahau kuwa hizi mimba ni matokeo ya mwingiliano wa sababu nyingi sana na inatupasa kutatua hizo sababu kabla ya kutoa hukumu hii ya maisha.
 
Rais yupo sahihi,mkanye mwanao asikimbilie ngono badala yake azingatie masomo

Kwa namna ya Raisi Magufuli anavyofikiria, ni sawa na kusema madereva wote wanaopata ajali kwa kuendesha kwa mwendo kasi wasipelekwe hospitali kupata matibabu ili wakipona waendelee kuwa madereva.

Sasa na wewe ukaja na kauli kwamba Magufuli yuko sawa, wakanyeni madereva wenu wasiendeshe kwa mwendo kasi.

Sasa unaona tatizo la lojiki yenu?
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom