Tamko la polisi kuhusu bomu la arusha mkutano wa chadema

Hii ina maana polisi itafanyia kazi kaili ya Nchemba! Mi kweli yeye ndo alotoa ksuli hiyo ys viyisho. Hebu tungoje tuone jinsi polisisiem watakavyo mshughulikia kada huyu maarufu wa CCM. ninasuubiri kwa hamu nione polisisiem wanavyo shughulikia suala hili!

Division 0 zinaendelea
 
attachment.php
 
Inspekta Jenerali wa Polisi nchini, ametoa taarifa kwa vyombo vya habari, kisha amejibu maswali kadhaa, vitu vya msingi kwa sasa ni kuwa Taarifa Muhimu zitatolewa na Jeshi kwa wakati muafaka tena kwa usahihi, ila kwa leo amesema hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa na jeshi kutokana na tuhuma za tukio hilo ingawa Ushirikiano umepatikana wa kutosha kutambua wajihi wa anayesadikiwa ndiye mtuhumiwa, lakini pili, Jeshi la Polisi litaifanyia kazi kauli ya Kiongozi mmoja wa Chama cha siasa aliyesema watu wasipochagua chama chao watakufa, watakufa kabisa

Tutabishana humu ndani lakini napenda mujue kuwa Serikali inaweza kuandaa matukio kama iliwaweze kupata sympathy kutoka kwa wananchi. Someni sana mambo ya Organised Crime, the State and the Legitimate Economy. Mtaalamu mmoja wa mambo ya makosa ya jinai aliwahi kusema "The American criminologist William Chambliss coined the phrase "State-Organized Crime" which he defined as "acts committed by state or government officials in the pursuit of their job as representatives of the government" (Chambliss, 1989). In Chambliss' view governments often engage in such activities as arms or drugs smuggling, assassinations and even terrorist acts, in furtherance of their foreign policy objectives. Covert collaboration may be established with organised crime or even terrorist groups for these purposes"
Let us think big.


 
Kama hadi sasa hawajamuweka Mwingulu Nchemba chini ya ulinzi, upelelezi wao ni wa mashaka
 
Hivi yule aliochorwa,na yule dereva bodaboda aliyekamatwa ile picha inaendeleaje!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kauli za polisi hazina la maana,jana RPC na NAPE arusha alikua anajitamba eti wamejipanga,hapo hapo tukio la bomu linatokea
 
Hii ina maana polisi itafanyia kazi kaili ya Nchemba! Mi kweli yeye ndo alotoa ksuli hiyo ys viyisho. Hebu tungoje tuone jinsi polisisiem watakavyo mshughulikia kada huyu maarufu wa CCM. ninasuubiri kwa hamu nione polisisiem wanavyo shughulikia suala hili!

polisisiem imshughulikie savimbi? Haiwezekani maana savimbi ni mtume wa fastjet
 
Kauli kama hizi zimetolewa na Mamri, Nape na mwigulu kwa maneno tofauti

Mwanri alisema mkongoto utatembea
Nape alisema" Watawashughulikia watu kwa vijana wao kwa masaa 3 ndipo wamkabidhi Polisi kwani polisi hawajui kuwashughulikia watu kama wao
Mwigulu" Msipoichagua CCCM mtakufa.

Nilikuwepo na nilisikia ila nilifanikiwa kumrekodi Nape na Mwanri na video ninazo
waropokaji wajiandae kweli
 
Bomu linalipuka watu wanataharuki wanakimbia kuokoa maisha yao.......askari wanapga mabomu ya machozi na risasi hewani..........kumtawanya nani? kumdhibiti nani? Kumlinda nani?

Kijana aliye rusha bomu alionekana...........lakini mabomu ya machozi, risasi hewani, nani angemfuatilia kumkamata?.........was it a tactic.....kwamba we lipua then sisi puuuuuuuuuu..........paaaaaaaa aaaaaaaa...........kabouuuuuuu uuuuuuuuuum? Hapa chenga tu kwakweli, cjui hao askari walipotoka maofsini kwao kuja kulinda amani walipata muda wa kujadili na kupeana mawazo juu ya aina za matukio yanayoweza kutokea na namna ya kuyakabili? hii inatisha sana........
 
Polisi walisema haitatokea tena bomu kulipuka kwamba, Polisi wamejipanga sana pamoja na vyombo vingine vya usalama hii riport aliisoma Nchimbi bungeni sasa nawauliza vipi mbona mpango wa magaidi unazidi kunawiri?
 
Iwapo viongozi waliopewa mamlaka wataendelea kulinda vyama badala ya kulinda nchi, nadhani tutegemee makubwa zaidi huko mbeleni. Vyama hivi vitapita lakini nchi itaendelea kuwepo na athari zinazotokea hazitafutika.
Mambo haya yalianza Igunga, watu walikufa, pia tulisikia kauli nyingi kutoka kwa wanasiasa; wengine wakitangaza hadharani kuwa kuna vikundi vya kigaidi vimeletwa nchini. Arumeru nako watu wakauawa. Kinachoonekana kwa mamlaka husika ni kama vile funika kombe, katika matukio mazito kama haya. Nadhani ifike mahali kuwe na nia ya dhati kuthibiti haya kwa kuwahoji na kuwachukulia hatua stahiki wahusika bila kujali nyadhifa zao au vyeo vyao katika vyama.
 
Huu uchaguzi wameona ccm wanazidiwa sasa wanadiriki kumwaga damu za watu bure umesikia tena na kule makuyuni mambo imekuwa sio vurugu kila mahali jamani kwa nini wasiache wananchi wachague viongozi wanaowataka?
 
Mkuu katoa neno, natarajia uchunguzi utafanywa haraka na taarifa zitoke, hawa ni Watanzania wenzetu wanakufa, familia zinapoteza watoto, wazazi, nk. kama sio leo basi kesho inaweza kuwa wewe. je utajisikiaje kumpoteza kaka, dada au mzazi wako sababu tu ya mtu au kikundi cha watu kisichopenda uhuru wa demokrasia nchni? wanaokufa ni nguvukazi ya Taifa letu... tunahitaji majibu sahihi na hukumu ya haki kwa kila anayehusika.
 
kesi ya ngedere unapeleka kwa nyani,tz kuna vituko.
polisiccm wamkamate nchemba?labda sio tz hii!!
 
Back
Top Bottom