YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,908
- 51,904
Mkurugenzi wa mamlaka ya anga TCAA Amesikika vyombo vya habari akisema kuwa ni marufuku watu kutengeneza ndege kienyeji linaua ubunifu wa watu na kwenda kinyume na sera ya viwanda Ya Magufuli.Yeye kama mkurugenzi wa Anga hakutakiwa kutoa Tamko koko kama lile alitakiwa awaalike watu ofisini kwake wote wanaotaka kuunda ndege awasaidie namna wanavyoweza kufanikisha azima yao au awatembelee ajue namna ya kuwasaidia.
Yupo pale kuwasaidia watu wafikie ndoto zao sio tu kusema ni marufuku.Anaua ubunifu na vipaji vyao.Yeye anatakiwa awabaini na atafute mbinu zipi za kuwasaidia hadi ikiwezekana wawe na viwanda vyao vya kuunda ndege au helikopta.Wakurugenzi mamangi meza kama hawa hawawezi isaidia nchi kufikia kuwa ya viwanda.
Kila mkurugenzi anatakiwa ajipange ajue atafanyaje kuiwezesha nchi kuwa ya viwanda katika eneo lake siyo ashinde anaota atafanyaje kuikwamisha nchi kufikia kuwa ya viwanda
Angalia huyu Mkenya alivyojitengenezea ndege kienyeji