Tamko la Madiwani na viongozi wa mila (Ilaigwanak) wa eneo la hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro (NCAA)

Bikis

Member
Feb 23, 2019
52
74
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAMKO LA MADIWANI NA VIONGOZI WA MILA (ILAIGWANAK) WA ENEO LA HIFADHI YA NGORONGORO (TARAFA YA NGORONGORO) JUU YA UHIFADHI NA JAMII

Sisi, Madiwani na Viongozi wa Mila (Ilaigwanak) wa Tarafa ya Ngorongoro (eneo la Hifadhi ya Ngorongoro), Wilaya Ngorongoro kwa niaba ya wenyeji waishio ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro kutoka Kata 11 na Vijiji 25, kwa pamoja tunatamka yafuatayo:

1. Tunaipongeza Serikali yetu inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake za kuleta maendeleo kwa wananchi wote hasa wanyonge. Wenyeji wa Ngorongoro wanaunga mkono jitihada hizi na wako mbele katika utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

2. Tunatambua kuwa eneo la hifadhi ya Ngorongoro ni la matumizi jumuishi ya Uhifadhi, Utalii na shughuli za Jamii ya wenyeji. Mfumo wa Matumizi Jumuishi ya Ardhi ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro hufanya eneo kuwa la kipekee ndani ya nchi ya yetu, Afrika na duniani. Mfumo huu umewezekana kwa sababu ya mfumo wa maisha ya jamii ya ufugaji wa asili wa jamii za wenyeji. Pamoja na shughuli zote kufanyika ndani ya eneo tangu hifadhi kuanzishwa mwaka 1959, kama ulivyo kwa maeneo mengine ya hifadhi, eneo la hifadhi ya Ngorongoro limekuwa na changamoto kadha wa kadha zinazojumuisha, ongezeko la idadi ya watu, mime vamizi, na kudorora kwa maendeleo ya jamii, n.k.

3. Kwa zaidi ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa eneo la Hifadhi, eneo limepata mafanikio ya kutambulika kwa hadhi mbalimbali ndani ya nchi yetu, Afrika na Dunia. Kimsingi, jamii ya asili (wenyeji) ya eneo ni sehemu ya mafanikio hayo kupitia desturi na tamaduni zao na kwa ujumla mfumo wao wa maisha uliyowezesha hifadhi kustawi kwa miongo yote.

4. Tunatambua pia kuwa shughuli za uhifadhi na za utalii zinachangia kwa sehemu kukuza uchumi wa nchi yetu na hivyo kupunguza umaskini.Wenyeji wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni wahifadhi wa asili na wameendelea kuisaidia Serikali katika kulinda, kutangaza na kushiriki kutatua changamoto zinazokumba sekta ya maliasili na utalii.
5. Tunakumbusha kuwa wenyeji wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, si wavamizi wa eneo la hifadhi bali ni wakaazi halali wenye haki za msingi na wanaotambulika na sheria iliyoanzisha eneo la hifadhi mwaka 1959. Jamii imeendelea kushauri kuwa mjadalala wowote kuhusu changamoto za eneo, ushirikishe wenyeji na usiwe wa kilaghai na shinikizo kama unavyotumika na uongozi wa sasa wa eneo la hifadhi

6. Tunasikitishwa na kufedheeshwa na jitihada za chuki za waziwazi za muda mrefu zinazoongozwa na Mamlaka ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, za kutaka kuimanisha Serikali yetu na umma wa watanzania kuwa idadi ya wenyeji na shughuli zao za ufugaji ni hatari kwa mazingira na hivyo tunapaswa kuondolewe mara moja. Kupitia vyombo vya habari, taasisi za uhifadhi za kimataifa kama vile UNESCO, watafiti toka taasisi za uhifadhi hasa TAWIRI, Mamlaka inayosimamia eneo umeendelea kuwalaumu na kuwatuhumu wenyeji kuwa chanzo cha changamoto za uhifadhi.

Kwa mfano, mwaka 2018-2019, Mamlaka imeshawishi Serikali kuunda timu ijulikanayo kama Taskforce to Review the Ngorongoro Conservation Area’s Multiple Land Use Model ili kutathmini ‘Mfumo wa Matumizi Mseto wa Ardhi’ na hasa iwapo wenyeji bado wanastahili kuwepo ndani ya eneo hili. Japo, mapendekezo ya timu yalikataliwa na wenyeji, Mamlaka ya wa eneo imeendelea kuimanisha Serikali kuwa jamii iliridhia maoni ya ripoti hiyo.

Ifahamike kuwa wenyeji, walikataa maoni ya ripoti kwa sababu: i. Ukusanyaji wa maoni uligubikwa na matisho na ubabe na pale wenyeji walipotoa maoni, maoni hayo hayakuzingatiwa katika ripoti hiyo. ii. Kamati ilikuwa na sura ya Wizara moja na haikuonekana kutenda haki hasa ya kusikiliza na kuzingatia maoni ya wananchi. iii. Eneo iliyopendekezwa kwa shughuli za maendeleo ya jamii ni asilimia 18 ya eneo lote na maeneo kame. iv. Kamati iliongozwa na Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Maliasili, kuratibiwa na Dr Manongi, Kamishna wa Uhifadhi na Katibu alikuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori. Kwa ushawishi wao, Kamati ilionyesha upendeleo na haikuwa tayari kusikiliza na kuzingatia maoni ya wananchi wenyeji.

7. Kwa muktadha wa mapungufu ya taarifa ya Tume tuliyoanisha hapa juu, kimsingi, jamii haipingi uwepo wa changamoto zilizoko katika eneo, bali ni mkakati wa kutatua changamoto hizo ambapo mamlaka inapendekeza na kuishawishi serikali kuwaondoa wenyeji au kuwahamishia maeneo kame yasiyofaa kwa ufugaji. Wenyeji wanaomba Serikali yetu ya Rais Mhe. Dkt. Magufuli isitumie maoni ya kamati hiyo kutekeleza uwagawaji wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro kwani kwa sehemu kubwa haijashirikishwa, haikuzingatia maoni ya jamii na kupendekeza eneo kubwa wenyeji kutwaliwa hivyo itaathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya jamii ya eneo.

8. Katika kuendeleza chuki dhidi ya jamii ya wenyeji, tarehe 28-30/12/2020, uongozi wa eneo uliitisha Warsha juu ya kukuza utalii na uwekezaji, kwa Wahariri na Waandishi Waandamizi wa vyombo vya habari wa ndani na nje ya nchi kueleza hali ya eneo la hifadhi na hasa kuwaomba kutangaza utalii wa eneo. Kamishna wa Uhifadhi wa eneo la uhifadhi, Dkt. Freddy Manongi alitumia fursa hiyo kutangaza kuwa Ngorongoro ‘inakufa’.

9. Tunakataa dhana inayojengwa na Mamlaka ya eneo kuwa eneo la hifadhi Ngorongoro ‘linakufa’. Huu ni upotoshaji na propaganda za uongozi kuishtua Serikali na umma wa watanzania ifanye maamuzi ya kuondoa wenyeji nje ya eneo hili. Ukweli ni kwamba, Mamlaka ya Ngorongoro inakwepa au imeshindwa kutekeleza jukumu lake la kisheria la uboreshaji wa ustawi wa jamii na hasa kutatua changamoto kwa mkakati uliyoshirikishi na jamii. Ili wasionekane wanakwepa au wanashindwa kutekeleza jukumu lao kuu, wameamua kulaumu na kutuhumu uwepo wa wenyeji ili waondolewe ndani ya ardhi yao.

10. Katika kuchambua na kubainisha changamoto zinazoikumba eneo la hifadhi kwa wanahabari, uongozi wa eneo ulikwepa;

i. Kuwakutanisha wanahabari na wenyeji. Kukosekana kwa wawakilishi wa jamii katika shughuli hiyo muhimu ni ishara kuwa uongozi wa sasa wa eneo hili hauthamini ushirikiano wa jamii katika usimamizi wa eneo la hifadhi.

ii. Kutaja uwepo wa watumishi wengi ukilinganisha na ukubwa wa eneo na shughuli za kufanyika. Hivi sasa Mamlaka inawatumishi takriba 800 wa kusimamia kilometa za mraba 8100 na ambao sehemu kubwa ya mapato ya shirika hutumika kuwalipa. Idadi hii ni kikubwa sana ukilinganisha na wanatumishi pungufu ya 2000 wa TAWA wanaosimamia kilometa za mraba 220,231.

iii. Kutaja malalamiko ya wadau wa sekta ya utalii juu ya uwepo wa utitiri wa mahoteli katika maeneo nyeti kiikolojia na wanyama, ambao unakwamisha hamahama na uzalishajia wa wanyama, mifumo mibovu ya maji taka ambayo hutitirisha maji ndani ya Kreta ya Ngorongoro, uchafu wa kambi za wageni zikiwepo vyoo.

iv. Kutaja malalamiko ya wafanyakazi juu ya mahusiano mbovu ya Mamlaka na watumishi.Tunaamini hili linatokana na kuwa asilimia kubwa ya watumishi wa Mamlaka hawana uelewa wa mfumo wa Matumizi Mseto wa Ardhi ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro tofauti na Hifadhi za Taifa.

v. Kutambua kuwa uwepo wa wenyeji ndani ya eneo umechangia kupatikana kwa mafanikio kama vile ulinzi na usalama wa wanyama na makazi yao, kuongezeka kwa idadi ya wageni wanaotembelea eneo na kuongezeka kwa mapato. Wenyeji wanafurahia kuwa tangu kuanzishwa kwake 1959, eneo limeendelea kupata medali za kimataifa, kama tulivyoelza hapa juu na ushirikiano baina ya wenyeji na uongozi wa eneo wa huko nyuma.

11. Jamii ya wenyeji iko tayari kushirikiana na Mamlaka katika kutatua changamoto zinazoikumba eneo la hifadhi ya Ngorongoro zikiwepo uvamizi wa mimea isiyo ya asili, ongezeko la idadi ya watu, maendeleo hafifu ya wenyeji lakini siyo kwa kupitia uongozi wa sasa, ambayo mara kadhaa imeonyesha hujuma za waziwazi kwa wenyeji.

12. Wananchi hawakubaliani na mchakato wa timu ya Ardhi Mseto (MLUM), timu ya Mpango wa Ujumla wa Usimamizi wa Eneo (GMP), na hivyo tunamuomba Mhe Rais asikubaliane na mapendekezo ambayo hayana ridhaa au Baraka za wenyeji. Wenyeji wapo tayari kutafuta suluhu ila ushirikishwaji uwe wa dhati na si wa chuki, kilaghai na mashinikizo kutoka uongozi wa eneo la hifadhi.

13. Hivyo, sisi Madiwani na Ilaigwanak, kwa niaba ya Wenyeji wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, kwa unyenyekevu mkubwa tunamuomba Mhe Rais utupie jicho eneo hili ili ikiwezekana abadilishe uongozi wa NCA na kufumua kabisa taasisi yote kwa sababu imeshindwa kusimamia eneo na ndio chanzo cha migogoro na kudorora kwa mahusiano kati ya jamii na wahifadhi. 14. Taarifa na tamko hili imetolewa hapa kata ya Endulen Tarafa ya Ngorongoro (eneo la Hifadhi ya Ngorongoro) tarehe 16 Januari, 2021.
 
Mna hoja na hongereni kwa kuwa sehemu muhimu ya utalii na mafanikio ya hifadhi.
Japo kiukweli ipo haja kuangalia namna bora kubakiza familia chache uwakilishi kwa awamu na msimu kwa lengo la utalii pekee na wote kupangiwa maeneo ya kudumu jirani na hifadhi pamoja na mifugo yao .
 
Naisihi sana serikali Chini ya Rais Dr. Magufuli kutowaondoa wafugaji wenye asili ya kimasai toka hifadhi ya Ngorongo.

Wamasai wamekua sehemu ya utalii wa Ngorongoro kwa muda mrefu Sana na sio tishio kwa hifadhi hiyo.

Kitendo cha kuwaondoa wafugaji hao itakua ni sawa na kuondoa sehemu ya vivutio vya asili vya hifadhi hiyo.

Naamini Serikali yangu sikivu haitafanya hivyo.
 
Jamaa wana point..."people centered development"...tufanye maamuz kwa hekma!
 
Ndio maana nchi inahitaji taasisi imara na zilizo independent,suala hili mahakama ingeamua sio no 1 manyumbu sisi.
 
Leo wapo wamasai kumi miaka 30 mbele wameongezeka wakawa 40 ardhi n ileile na Tabia ya binadamu ni kuharibu kuliko kujenga.
 
Back
Top Bottom