Tamko la Jukwaa la Wahariri kuhusu "Bunge Live"

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,100
114,680
Bodi ya Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF) iliyokaa Ijumaa Aprili 22, 2016 jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine ilijadili hali ya mwenendo wa tasnia ya habari nchini hasa juu ya haki ya wananchi kupata habari.

Katika kujadili hali hiyo, TEF imeguswa kwa namna ya kipekee kabisa na mwenendo mzima wa urushaji wa bahari za Bunge kwa njia ya redio na luninga, hususan katika mkutano wa tatu wa Bunge la 11 unaoendelea mjini Dodoma kwa sasa.

Itakumbukwa kwamba Muhimili wa Bunge kupitia Kitengo chake cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Aprili 15 2016 ulitoa taarifa kwa umma ikieleza utaratibu mpya ambao sasa umeanza kutumika katika kurusha matangazo ya redio na luninga kutoka Bungeni.

Katika taarifa hiyo, Ofisi ya Bunge ilisema kuwa imeamua kuboresha mfumo wa urushaji wa Matangazo ya Bunge kwa Bunge lenyewe kurusha Matangazo ya Vikao vyake pamoja na Vipindi mbalimbali vyenye Maudhui kuhusu Shughuli za Bunge ambazo hazijapata fursa ya kufahamika vyema kwa umma kuanzia katika Mkutano wa Bunge la Bajeti unaoendelea sasa.

Ofisi hiyo ilisema kuwa mfumo huo mpya ni Utamaduni wa kawaida kwa kila Bunge hususani Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kuwa na Studio zake kwa lengo la kurusha Matangazo ili yawafikie wadau kwa lengo la kurusha kupitia vituo vyao.

Kwa maana hiyo, Bunge lilisisitiza kuwa chini ya utaratibu huo mpya, jukumu la kurusha Matangzo ya Vikao vya Bunge litafanywa na Bunge lenyewe kupitia FEED MAALUM ili kurahisisha kila Kituo cha Radio na Televisheni kupata Matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga Mitambo yao Bungeni Dodoma.

Katika kutekeleza uamuzi huo na mfumo huo mpya, kila kituo cha Televisheni na Redio sasa watatumia Masafa ya Matangazo ya Bunge (Frequencies) bure kupitia FEED MAALUM itakayorushwa na Satellite ya INTELSAT 17 ambayo iko nyuzi 66 Mashariki kwa masafa maalum ambayo pia yaliwekwa wazi.

Kwa mantiki hiyo, Bunge sasa limezuia vituo vyote vya televisheni nchini kupeleka kamera zake ndani ya Bunge kwa kuwa habari hizo zitapatikana kwenye feed maalum ambayo ni ya Bunge ambayo inasimamiwa na waandishi wa Bunge ambao pia ndio wanaamua nini kionyeshwe kwa utashi wao.

================

Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) watoa tamko juu ya matangazo ya Bunge

Baada ya kutafakari hatua hizi mpya za Bunge na baada ya kufuatilia kile kinachorushwa, mambo kadhaa yamethibitika:-

Mosi, habari kutoka ndani ya Bunge sasa zinachujwa mno kupitia mfumo huu mpya wa feed maalum;

Pili, ubora za picha zinazorushwa kupitia feed hii nao ni wa kiwango cha chini pia;

Tatu, kwa mantiki ya kawaida kabisa, hatua hizi zote zimepunguza na kukwaza haki ya wanahabari kufanya kazi yao kwa uhuru, lakini pia inawanyima wananchi haki ya kupata kwa uhakika na bila kuchujwa kile kinachofanywa na wawakilishi wao.

Kwa kuzingatia haya yote, TEF inasema bayana kwamba:

  1. Hatua hizi mpya za kuzuia kamera za televisheni kuingia Bungeni ni hatua za dhahiri kabisa za kukwaza uhuru wa habari nchini na kukuza censorship nchini. Hali hii haisaidii siyo Bunge tu, bali hata wabunge, wananchi na taifa kwa ujumla katika kupiga hatua za kweli katika kujenga demokrasia na kulinda haki za kupata habari na uhuru wa kujieleza nchini;
  2. TEF imeanza kuingiwa na hofu kwamba sababu za awali zilizokuwa zimetolewa za kuzuia utangazaji wa moja kwa moja wa Bunge kupitia TBC kwa sababu ya gharama, huenda hazikuwa za dhati. Hali hii imejionyesha hasa baada ya vituo binafsi vya televisheni kujitokeza na kuendelea kuonyesha vikao vya bunge moja moja, lakini navyo sasa vimenyimwa fursa hiyo kwa utaratibu huu mpya wa feed maalum.
  • Ni dhahiri sasa, ushiriki wa wananchi katika kufuatilia mwenendo wa Bunge na wabunge wao umekwazwa sana kwa hatua hizi mpya na kwa maana hiyo, kupunguza ushiriki wa wananchi katika mfumo wa utawala wa nchi yao.
Kwa kuzingatia haya yote, TEF inatoa rai kwa uongozi wa Bunge kufikiria upya hatua hizi za kuzidi kufunika shughuli za Bunge kwenye blanketi zito la usiri na censorship, hivyo uruhusu kituo chochote cha televisheni chenye nia, uwezo na utayari wa kurusha matangazo ya Bunge moja moja bila kulazimika kujiunga na feed maalum iliyoanzishwa.

Tunaamini kwamba kama hali hii ya kutumia feed maalum itaachwa iendelee hakika Tanzania kama taifa tunapiga hatua nyuma kwa yale mazuri machache tuliyokuwa tumeyafikia, mojawapo, uhuru wa Bunge kuendesha mambo yake kwa uhuru na uwazi mkubwa hivyo kuwa mfano mojawapo wa taasisi za umma zinazojiendesha kwa uwazi.

Imetolewa leo, Jumapili Aprili 24 2016 jijijni Dar es Salaam na Jukwaa la Wahariri Tanzania.

Theophil Makunga Neville Meena

Mwenyekiti Katibu

DSC_1579.jpg

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concept, Theophil Makunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) kushoto akitoa tamko hilo mapema leo Aprili 24 jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti JAMHURI, Deodatus Balile ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakati wa mkutano huo.
maxresdefault-4.jpg

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concept, Theophil Makunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) akitoa tamko hilo mapema leo Aprili 24 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti JAMHURI, Deodatus Balile ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakati wa mkutano huo.
DSC_1582.jpg

Baadhi ya vyombo vya habari vikifuatilia tamko hilo mapema leo Aprili 24.2016
DSC_1584.jpg

Mmoja wa wanahabari akiulzia swali kwa viongozi wa jukwaa la Wahariri (hawapo pichani)
DSC_1590.jpg

Viongozi wa jukwaa la Wahariri wakisikiliza maswali kwa umakini wakati wa mkutano huo
DSC_1592.jpg

Wanahabari wakiuliza swali kwa viongozi wa jukwaa la wahariri
DSC_1607.jpg

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concept, Theophil Makunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) akijibu baadhi ya maswali juu ya tamko lao hilo leo Aprili 24 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti JAMHURI, Deodatus Balile ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakati wa mkutano huo.

(Picha zote na Andrew Chale)

Sijao tatizo hapo wala haki iliyokiukwa ikiwa habari zinapatikana, sio lazima kila chombo kikaweke vifaa vyake pale wakati wamerahisishiwa.
 
Mbona hilo tangazo nakumbuka lilisema waandishi wataruhusiwa kuendelea na shuguli zao,
Kweli bongo full mkorogo, leo taarifa hii kesho vice versa
 
Wabunifu..
Watu wa chache walikaa wakaja na ubunifu mpya "SELFIE"
Wabunifu wanajua muhula huu kuna mizigo, hata ile ya JK afadhali..

Kwahili JK pekee ndie alikua jasiri asiye ogopa/kuteswa na Uhuru/Uwazi..
 
Kuna harufu ta ufisadi inanukia bungeni....nadhani akina kangi wanafurahia sana hii issue.naishangaa serikali ya magu ina uwoga kuliko ya mstaafu yule wa msoga.
 
Hivi nyie waandishi maslahi mbona hatusikii mkitoa matamko kama haya kupinga posho ya makalio?
 
Sijao tatizo hapo wala haki iliyokiukwa ikiwa habari zinapatikana, sio lazima kila chombo kikaweke vifaa vyake pale wakati wamerahisishiwa.
weeeeeh hebu nyamaza...imekuwa movie hiyo hadi ikaeditiwe ndipo ioneshwe..hilo ni bunge na wabunge tumewachagua sisi tunataka kujua pumba na almasi zao bungeni...wanaosinzia tuwaone...hatutaki kueditiwa waondoe madudu yao.
 
Back
Top Bottom